Duru za Siasa Special: Mgogoro kambi ya Upinzani (CHADEMA)

Duru za Siasa Special: Mgogoro kambi ya Upinzani (CHADEMA)

Nilikuwa nazirejea nyuzi na kukumbana na maoni mengi. Moja ya hoja zinazosemwa sasa hivi ni kumuondoa Zitto katika mkakati wa waraka na kumwacha Kitila mwenyewe. Ndugu yangu The big show amesema zito hahusiki. Nasema inawezekana hahusiki lakini katajwa. Kutajwa si kuhusika sasa swali linakuja, ni lini waraka huo umeandikwa? Kuna tarehe inayoonyesha hapo?

Ushahidi wa kimazingira unaonyesha waraka ni muda mrefu kidogo.
Ukiusoma kuna sehemu inasema
tunayemtaka....apunguzeukaribu na viongozi wa serikali na wa chama tawala na awe crical zaidi nautendaji wa serikali nje na ndani ya bunge
Nadhani siku za karibuni Zitto amekuwa critical kwa mambo kama pesa za Uswiss na kule Bungeni
Ashirikikikamilifu katika shughuli za taasisi yetu zikiwamo vikao vyote vinavyomhusu,operesheni mbalimbali, chaguzi ndogo, nk.
Ni siku za karibuni Zitto ameshiriki sana katika kampeni za kanda magharibi. Historia inaonyesha ni muda mrefu tangu afanye hivyo
Sina shaka mawasiliano yalishafanyika na kilichokuwa kinaendelea ni utekelezaji.

Kuna hoja kuwa Zitto ameundiwa Zengwe.
Kwakuhusishwa na waraka huu kama mhusika mkuu na ushahidi wa kimazingira ni wazi alishiriki.
Hata hivyo watetezi wake pamoja na yeye mwenyewe hawajaeleza ushiriki wake katika kundi la Kafulila, Sakata la M7 na wala hakukanusha kuhusika na waraka.

Katika kujenga hoja hafifu watetezi wa Zitto wanasema Mzee Edwin Mtei ndiye tatizo, wengine wakifumba macho na kusema hakuhusika na waraka.

Wanachoshindwa kukisoma katika utetezi wake mwenye (Zitto) ni hiki
Kama mwanasiasa kijana niliyekaa katika siasa kwa muda sasa yapo mengi mazuri nimeyafanya.
Lakini kuna maeneo nilipojikwaa na yapo makosa niliyofanya kisiasa katika maisha yangu ya siasa

Wapo wanaodai kuwa suala la ukaguzi wa fedha ndicho chanzo na wameligeuza kama ndio hoja.
Wamesahau kuwa waraka uliopo unamtia Zitto matatani.

Tatizo walililofanya akina Zitto na Mkumbo si kuandika waraka. Waraka unaweza kuandikwa na mtu yoyote yule.
Tatizo ni aina gani ya waraka, ulikusudia nini ili kuleta nini na kwa akina nani.

Waraka ulikusudia kuleta mapinduzi (coup d'etat). Nisingeona ajabu kama hilo lingetokea TLP.
Kwa chama kinachojinasibu ni cha kidemokrasia hilo halifai kutamka achilia mbali kuliandika.

Huwezi ukahamasisha demokrasia kwa njia zisizo za kidemokrasia.
Huwezi ukachohochea maasi vichochoroni ukijidai unalinda demokrasia.
Huwezi kukaa na kundi la watu wasiozidi 4 mkawa na mkakati wa kumweka kiongozi wenu kwa njia za kificho mkilaghai watu mkadai mnatekeleza demokrasia.

Hawawezi kunyooshea CCM mkono kwa kukandamiza demokrasia nchini ili hali wao wapo tayari kwenda nchi za jirani kufanya mikutano ya kuhamasisha mapinduzi. Hapa kuna demokrasia gani?

Narudia, kuna hoja zao zenye mantiki kwa kuziangalia kwa haraka.
Mathalani Mbowe kukopesha chama kuna element za conflict of interest.
Kunapokuwa hakuna nyaraka ni mbaya zaidi. Mbowe anaposhindwa kutetea hali hiyo ni mbaya kuliko.

Tatizo linakuja pale Zitto na Mkumbo wakiwa hawajawahi kusimama na kusema watajiuzulu kwasababu ya matumizi mabaya ya fedha. Wanachokifanya ni kwenda nchi jirani kwa mikutano baada ya kuhudhuria mikutano ya kamati kuu bila kuonyesha pingamizi.

Kutetea kalenda ya chama kuna mantiki na hapo Dr Slaa anaulizwa utaratibu wa uchaguzi ukoje?
Kama akina Zitto wangefukuzwa kwa hilo ningesema wameonewa.
Ningesema kama nilivyowahi kusema kuhusu kauli za kumpaka matope Zitto.

Niliwahi kusema kuhusu Muungano CDM haijui nini inakitaka isipokuwa Zitto aliyeandika kwa uwazi kuhusu serikali tatu.
Nilismama na kumsema Mbowe na ziara ya Togwa Ikulu na kufikia mahali nilimwita mnafiki.
Nilisimama na kumsema Dr Slaa kwa suala la Rwanda na kauli zake zilizokosa maono.

Kinachotokea mitandaoni kwa mashabiki wa vyama vya siasa ni ushabiki na si kuangalia mambo kwa mantiki.
Hakuna sababu za kuendelea kulea viongozi wasio na maadili.
Lazima vijana wabadilike na wafanye siasa za maendeleo.Muda wa siasa za tunampenda umekwisha.

Leo tukiuliza CDM kinafuata model gani ya uongozi hatuna jibu, lakini ni wepesi kusimama na kutafuta flimsy reasons za kuficha ukweli. Mtei anaingiaje katika waraka ambao haumhusu na washiriki wamekiri wameuandika na makosa?
Leo mada si waraka mada ni Mtei!

Nilitegemea vijana wangekuwa wanatafuta ukweli na kulumbana kuhusu ukweli, naona siasa za mitaani bado hazijawatoka.

Huu si muda wa kupenda maneno ni muda wa ukweli na sera, mission na vision

Amkeni Watanzania
 
Well said Bongolander
Katika bandiko 3 nimezungumzia hili la ushindani nikasema ni jambo zuri sana katika kuimarisha demokrasia.
Ninachokiona ndani ya cdm ni upinzani na wala si ushindani. Upinzani hauwezi kutokea ndani ya chama kimoja lakini upinzani unatokea miongoni mwa vyama.

Chadema kama insitution ambayo imebeba matarajio ya sehemu ya jamii inapaswa kuoneysha utayari wa kushughulikia migogoro ndani ya chama kwanza ili kuonyesha utayari wa kushughulikia migogoro katika dola.

Kwa viashirio, maoni, maonyo n.k. haikuonekana kama insitution inayoweza kufanyia kazi habari. Ndio maana nilieleza kuwa tatizo halikuanza juzi Arusha, lilianza kuanzia wakati wa Kafulila, Juliana na Masalia kwa ujumla.
Kwanini tatizo lenye miaka zaidi ya 5 liendelee kuitafuna institution kubwa kama hiyo? Kuna utayari kwa hilo.

Ni kweli lazima tuiangalie kama institution lakini pia ikumbukwe kuwa institution inatangenezwa na watu na hakuna institution inayoishi bila watu. Ni watu wanaojenga au kubomoa na hao ndio wanaangaliwa.
CDM kama chama sioni kama kuna tatizo, lakini CDM kama uongozi naona lipo tatizo.
Je, hilo lifumbiwe macho tukitumaini kuwa institution itajirekebisha yenyewe?

Ni kweli kuwa kuna mbinu za kuihujumu kutoka kwa CCM. Hii ni baada ya CCM kukosa nguvu za hoja kama insstitution iliyotokana na watu kuacha misingi yake ya awali, kuruhusu watu kuingilia institution n.k.
Lakini pia majaribio kama ya kuwagawa watu kwa kutumia ukabila na udini yalionekana kugonga mwamba na pengine kuirudi CCM kwa namna moja au nyingine.

Kinachoonekana sasa hivi ndani ya cdm ni kuruhusu au kutoa udhaifu ambao CCM wanautumia kuimaliza.
CCM sidhani kama ina makosa kwasababu ndicho inachotaka, makosa yapo CDM kwa kuruhusu udhaifu unaowezesha CCM kutimiza matakwa yake.

Nakubaliana kabisa na wewe kuwa CCM haina kosa, tena naweza kusema ni strategy nzuri sana kisiasa. Chama chochote makini kinaweza kutumia njia kama hiyo.

Nadhani so far, hatua zilizochukuliwa na Chadema kama chama ni sahihi. As a party it should have shock absorbing mechanism, and when members of the party misbehave there should be official ways of dealing with them.

Ni kweli mbali na chama kuwa institution yenye collective ambition, kuna members ndani ya chama nao wanakuwa na ambitions zao. As long as ambitions zao zinaendana na matakwa ya chama, na as long as hazivurugi uimara na mwelekeo wa chama hilo ni jambo jema kabisa. Lakini kama members wanatumia charisma yao kama njia ya ku-attain political goals, na kutumia illegal channels ku-address matatizo ndani ya chama, hilo ni tatizo ambalo kama halishughulikiwa ni cancer ndani ya chama.

By the way CCM imekuwa na issues kubwa kuliko hii, tunaweza kukumbuka kina Kolimba, Hizza Tambwe, Dr Wilborad Slaa, na wengine wengi tu, baadhi waliitatua kwa njia ya kistaarabu na mengine kwa njia mbaya.

Nakubaliana na wewe kuwa utaratbu wa Chadema kusubiri vikao vikuu kushughulikia mambo ya chama labda sio mechanism nzuri, kusibiri issue ifukute kwa miaka mitano ni jambo baya madhara yako ndio kama haya tunayoona sasa.
 

Tunaendelea kupata undani wa sakata.

Ukisoma utetezi wa Zitto ni tofauti na tuhuma zinazomkabili.
Alichokifanya Zitto ni spinning na nazidi kupata wasi wasi kwa email hizo tukizingatia kuwa waraka ulikamatwa katika kompyuta na wamekubali .

Kumetokea kundi la vijana wa CDM ambao kwa kutojua au mapenzi kwa Zitto wameamua kuingilia agenda isiyohusika agenda isiyohusiana na waraka ambayo ni tuhuma dhidi ya Mtei.

Hili linashangaliwa sana na vijana wa CCM akiwemo Mwigulu.

Nasema haya kuweka uwazi na kupata ukweli.

Demokrasia haiwezekani kufanikiwa katika mazingira tunayo yaona.


Kuhusu Zitto kuja na madai ya kikao kutokuwa halali, bado ana nafasi ya kukata rufaa.
Hivyo sioni hilo kama big deal zaidi ya utetezi wa tuhuma za waraka.


Nawasihi wananchi waache siasa za hisia, wasimame katika ukweli.

Wapo
wananachi bila kujadli itikadi zao wanapoteza maisha, wanateswa na wanaumia kutafuta haki na ukweli.
Kukana ukweli ni kuwasaliti watu hao wawe CCM, CDM, TLP au CUF.


Ukimsoma Kitila Mkumbo yeye ni kama amekubali makosa.

Tatizo linalomkabili Zitto ni kuendelea na spinning na kukwepa ukweli wa kuhusika na waraka na tuhuma zingine.

Tumeonyesha kuwa alishaanza kutekeleza mkakati huo kwa ushahidi wa mazingira.


Duru za siasa tunamsihi Zitto akubali makosa kama mwanadamu.

Zitto bado ana future kisiasa na wala si mwanasiasa wa kwanza kufanya makosa.

Anachokifanya kuendeleza majadiliano kwa mbinu za kutumia watu na spinning zinammaliza kabisa kisiasa.


Na ninyi vijana wa CDM, acheni ushabiki na simameni katika ukweli.
Mnakimaliza chama kwasababu ‘you have been drawn in' kufuata kile kisichowahusu.


Mathalan, mnamjadili Mtei badala ya waraka ulio mbele yenu.
Mnajadili uchaga badala ya usaliti unaotafuna chama chenu.

'Mumeitwa na wasiowatakia mema na mnaitika knowing or unknowingly'


Hebu jiulizeni, CDM inapita katika kipindi gani cha kisiasa. Is it a political movement or a political party.

Na katika kipindi hicho nini mnatarajia kitokee na mnata kiwe handled vipi.

Je, kuna umuhimu wa kufanya uchaguzi ili kuchuja na kupata safu ya uongozi kwa mwelekeo mpya?



Hamjiulizi kwanini kampeni zenu zimezorota na badala yake mnaingia katika majadiliano ya Mtei.


Kuna tatizo la weledi katika siasa za nchi yetu across the board


 
KUVUNJIKA KWA MAKUNDI

Mkirejea majadiliano duru za siasa na uzi huu tuliyataja makundi yanayoisumbua Chadema
1. ''Power struggle'' ambalo linamiliki waraka
2. Kundi neutral
3. Chadema wahafidhina
4. Chadema wasaliti.

Kundi la power struggle linaonekana kuathirika sana kukamatwa kwa waraka.
Tumeeleza hapo juu mkakati ulishaanza kutekelezwa na Zitto, mfano kuwa mwiba kwa serikali ndani na nje ya Bunge na kuendeleza kampeni kanda ya magaharibi.

Watu wasichokifahamu ni kuwa katika waraka Kitila na Zitto waliponda sana kuanzishwa kwa kanda na kusema mkakati huo ulikufa kabla ya kuanza.

Ukisoma katika mkakati wao sehemu ya mwisho, wao walipanga kanda zaidi ya 15 kuanzishwa.
Hivyo kulikuwa na hujuma kuhusu utengenezaji wa kanda ulioafikiwa na uongozi wa sasa kwa kuogopa kuvunja nguvu ya kanda zao wanazoziunda nyuma ya ukumbi.

Kanda zao zimeshaanza kutayarishwa ndio maana unaona kuna resistance kuhusu tuhuma hata kama inajulikana ni kosa na wahusika wamekiri. Maana ya hilo ni kuwa kitaifa mpango umekufa kikanda bado upo.

Namshangaa Mnyika akisema shughuli za kanda zinaendelea, well zinaendelea lakini kama ilivyotarajiwa hadi pale muafaka na hatima ya wahusika waliosuka kanda zao itakapofikiwa.
Na wala nisingemshauri aendelee na shughuli hizo hadi bahari itakapokuwa shwari. Sasa hivi hali ni tete.

Tuliwaasa kuhusu ukubwa wa mgogoro na sasa tunawaasa kuwa the dust must settle before they forge ahead.
Make sure you arrest the situation which is spiralling uncontrolled.

Kujifariji kuhusu Kaboru na Wangwe ni kujidanganya, hizi figure mbili 'have the force to be reckonned with and every precaution should be taken before they take the building down'

Kundi Neutral
Hili liliwahusisha watu wasiosikika katika mijadala na malumbano ndani ya chama
Mchambuzi ameliita borderline na sasa nakubaliana naye kwani limechukua upande na sasa neutral hakuna.

Kundi la Wahafidhina
Hili linapata nguvu kutokana na kundi la struggle kuwa katika wakati mgumu.
Tatizo la wahafidhina ni kufanya mambo nusu nusu.
Taarifa yao haikuwa wazi kwanini wanamuondoa Zitto katika uongozi.

Hilo limefanya Zitto apate upenyo wa kukana kuhusika kuandika(si kushiriki) waraka na hivyo kuonekana kama anaonewaLakini pia limempa nafasi Zitto kuchagua hoja zinazosimama au anazoweza kucheza nazo.

Hoja mojawapo ni ya PAC ambayo Zitto anasema yeye ni kiongozi wa taifa na si chama.
Nasema hilo ni kweli kwasababu anafanya kazi kama mwenyekiti wa kamati ya bunge.

Kwa upande mwingine Zitto ni mtendaji msaidizi na hakuna rekodi kuwa alishawahi kulifanyia kazi katika nyadhifa yake ndani ya Chama. Alipaswa kulielewa hilo. Makinda ni mjumbe wa CC na wala usidhani yupo kwa bahati mbaya!

Hili linaacha loopohole kwa wahafidhina kuuliza
Kama katibu mkuu mtendaji wapi au lini alizungumzia suala hilo.
Lini aliibua hata katika OAB na kukataliwa

Lakini pia ni baada ya taarifa ya Zitto na hata kabla habari hizi zilikuwa mitandaoni ukiwa ni ushahidi kuwa alifanya hivyo si kama kiongozi wa umma bali kutumia nafasi ya uongozi wa umma kutaka kujenga mazingira ya manufaa yake binafsi akiwa tayari ameshaanda mazingira mitandaoni kama sehemu ya mkakati.

Whafidhina sasa hivi wanalazimika kuwa on defence badala ya kuwa on offense
Hivi kwanini hawaweki tuhuma zilizomuondoa Zitto wazi ili aweze kuzijibu kwa uwazi kuliko vipande vipande vinavyompa nafasi ya kuchagua kipi ili acheze nacho?

Kundi la Wasaliti
Habari zaidi zinaonyesha kuna mengi yasiyosemwa yatajitokeza kila muda
Kundi la wasalaiti litajulikana tu kwasababu halina kiongozi na linaongozwa kwa ushirikiano na kundi la power struggle na watu nje ya CDM. Suala la masilahi litazua sintofahamu na kitakachofuata ni wewe mwaga ugali mimi namwaga mboga.

Kitendo cha Kitila kujilipua ili kumnusuru Zitto hakijasaidia kwasababu huko katika kanda kuna 'waathirika' na hao ndio watakaomwaga mtama. Ni suala la muda utasikia mengi na mengine yakusikitisha zaidi.

CDM watambue huu ni mwanzo wa wakati mgumu, wapo watu ndani na nje watapigana kuhakikisha ima wanalinda watuhumiwa wa waraka au wanakwenda chini na jengo zima.
 
Mkuu Nguruvi3

Hongera sana kwa kuja na mada ambayo uwasisilishaji wake upo "considerably balanced". Kuna maeneo kadhaa ambayo kidogo unajenga hoja zinazoegemea upande mmoja (but without losing objectivity) lakini nikisoma kwa umakini, nahisi pengine ni kutokana na kusononeka kwako na na ‘unnecessary interference' zinazojitokeza katika harakati za kuwapatia wananchi chama kikubwa cha pili nchini ambacho kinazidi kuimarika na kuonyesha uwezo mkubwa wa kupambana na chama tawala (CCM) kwa maslahi ya umma na demokrasia nchini kwa ujumla. Iwapo nipo sahihi, then I share similar sentiments kwani kwa afya ya demokrasia ndani ya taifa letu, Chadema ilitakiwa iwe imeshafika mbali sana na harakati zake za kufika kila kona ya nchi kwa nia ya kujijenga kuelekea 2015, kama inavyofanya CCM hivi sasa chini ya watendaji wake wakuu ambao wanazunguka nchi nzima.

Maoni na mchango wangu unaweza kutoka nje kidogo ya mada from time to time, lakini ningependa nieleweke kwamba i come from a background yenye imani kwamba: Bila Ya Chadema Madhubuti, CCM Makini Haiwezekani.

Moja ya mapungufu makubwa ya CCM ambayo hata Mwalimu aliyajadili wakati Fulani ni kwamba CCM kama chama kilichokuwa kinaminiwa na wananchi walio wengi wakati ule kilikuwa kinazidi kukaa mbali na wananchi. Tofauti na CCM, hivi karibuni, Chadema ilijipanga vyema ambapo tuliona chama kikiwa mstari wa mbele kuzunguka nchi nzima kujijenga na kupelekea CCM kuchanganyikiwa na kubakia kuendesha ‘Desk Politics' - siasa za kujihami na kutatua migogoro ya ndani (kujivua gamba) kutokea ofisini - Lumumba. Lakini kilichoshangaza wengi ni jinsi gani, tena kwa kasi ya ajabu, hivi karibuni, CCM imefanikiwa kuchukua nafasi ya awali ya Chadema ambapo sasa – ni CCM ndio ipo katika mzunguko nchi nzima kujijenga, huku Chadema sasa ikihamia kwenye "Desk Politics" za kujihami na pia kutatua migogoro ndani ya chama.

Nadhani moja ya maswali muhimu ni kwamba je:
· Maamuzi ya Kamati Kuu yameleta madhara gani kwa wananchama wa Chadema na Wananchi kwa ujumla?

Kwa mtazamo wangu, suala la ZZK lilikuwa ni Pandora's Box ambalo wananchi wengi walikuwa na hamu lifunguliwe ili wawaze kukidhi curiosity yao kubaini all the evils and miseries contained in the box. Swali linalofuatia ni je:
· Have all the evils being exposed? What about the miseries?

Pengine ni mapema mno kupata majibu ya uhakika, lakini kwa maoni ya yasiyo na utafiti wa kina ni kwamba uamuzi wa Kamati Kuu umezaa ‘mixed feelings in the electorate'. Lakini mbaya Zaidi ni kwamba, pande zote zinajadili Zaidi suala husika kwa vigezo vya personalities kuliko issues. Tukianza na upande unaounga mkono uamuzi wa kamati kuu, upande huu una amini kwamba Chadema bado ina hazina kubwa ya Viongozi Vijana (sio imani, sera au itikadi bora) ambao bado wanaleta matumaini ya kuwakomboa wananchi. Na kwa upande mwingine unaopinga maamuzi ya kamati kuu umechukizwa na kitendo cha kuondolewa kwa shujaa wao (ZZK) for reasons ranging from ukanda, ujana, na masuala mengine yasiyokuwa na uhusiano wa moja kwa moja na imani, sera au itikadi za Chadema. Kundi hili linahisi kwamba harakati za chadema kuikomboa nchi kwa maslahi ya wanyonge walio wengi (Vijana) zimeingia dosari na kwamba kukosekana kwa ZZK 2015 and his style of leadership and articulation kutaleta ugumu mkubwa wa kushawishi wananchi (hasa Vijana) kukipigia kura Chadema katika uchaguzi wa 2015.

Vinginevyo, kwa ujumla wake, ukweli unabakia kwamba Chadema kimefanikiwa sana kugeuka kuwa tumaini jipya la wanyonge na kwamba - kwamba angalau sasa kuna chama kinachosikiliza vilio vyao, kwa maana ya kwamba - hata kama chadema haitafanikiwa kuingia Ikulu hivi karibuni, lakini uwepo wa viongozi wake makini kumesaidia sana kukiamsha chama tawala ambacho sasa nacho kimeanza kuendesha siasa za kujali kero za wananchi kwa vitendo. Kwa mfano, ziara za watendaji wakuu wa CCM nchi nzima kwa scale ya sasa ni kitu ambacho hakijawahi kutokea kwa Zaidi ya miaka thelathini. Credit katika hili inastahili kwenda kwa Chadema na sio kwingineko.

Baada ya kusema hayo, naomba sasa nijadili baadhi ya hoja zako kadhaa kama ifuatavyo:

Kwanza ni juu ya makosa ya waraka husika. Naungana na wewe katika hoja yako kwamba kosa la msingi lipo kwenye ‘intention, content and context'. Hili halina mjadala hata litetewe vipi kwani kama ulivyojadili, kulikuwa na njia nyingine mbadala kwa mujibu wa sheria, kanuni na utaratibu kufanyia kazi au kuwasilisha hoja husika. Na iwapo mbadala huo ungekwama, hapo ndio kungekuwa na hoja yenye mashiko kwamba 'nia ya mabadiliko na demokrasia ndani ya chama vinahujumiwa'. Vinginevyo, wanachama huchagua viongozi ndani ya vyama vyao ambao wanafanya kazi ya KUWATETEA na KUWAUNGANISHA, Sio KUWACHOCHEA na KUWAGAWANISHA. Kwa mantiki hiyo, Chadema imefanya uamuzi wa maana, lakini muhimu zaidi ni kwamba:

· Chadema kama Chama kimeonyesha jinsi gani kinaweza kukabiliana na Migogoro ya ndani, kwani hii ni ishara nzuri kwamba kitakuwa na uwezo wa kukabiliana na migogoro nje ya chama (ndani ya taifa) iwapo utakiamini na kukipeleka ikulu.

· Katika harakati za Ujenzi wa TANU, Mwalimu Nyerere (rejea chapisho la TANU na Raia, 1962), alipata kusema kwamba:
Chama ni Watu, Chama Sio Viongozi
. Uamuzi wa Chadema umeonyesha ukomavu kwa kukubaliana na ukweli huu, na umeijadili hoja hii vyema pale unaposema kwamba
tatizo la chadema sio chama bali uongozi
.

Hoja ya pili ni ile unasema kwamba – "hakuna umuhimu wa Chadema kuwa karibu au kupendwa na watawala". Katika hili, pia naungana na wewe kwani katika mazingira ya ambayo nchi inakabiliwa na ombwe kubwa la dira ya taifa, itikadi za vyama vya siasa, na utawala wa sheria, sioni mantiki yoyote ya viongozi wa chama kikuu cha upinzani kujiweka karibu na watawala, ili iweje? hasa ikizingatiwa kwamba tangia mapendekezo ya tume ya nyalali (1990s), wanachofanya watawala imekuwa ni kuhodhi mchakato mzima wa political reforms in Tanzania (wanazuoni – Hyden na Shivji wameandika sana juu ya tatizo hili la top – down democratization process in Tanzania). Suala hili limeathiri sana kasi ya ukuaji wa demokrasia na utawala wa sheria nchini. Lakini hapa sina maana kwamba kuna umuhimu wa Chadema kuwa na ‘confrontational relationship with the status quo'. Kwa mtazamo wangu ambao pengine ni finyu, tatizo lililopo katika siasa za nchi yetu ni kwamba:

Tumeshindwa kubaini masuala yanayohitaji ‘bipartisan politics', kama msimamo wa pamoja juu ya umuhimu wa masuala kama ‘good economic governance' (rasilimali za nchi kwa manufaa ya wananchi), ‘national values and ethos', ‘uadilifu', ‘uzalendo', ‘national security' (kwa manufaa ya wananchi), ‘strengthening of democracy', n.k, masuala ambayo yangepelekea uwepo wa ‘win-win situations' kwa pande zote mbili. Binafsi, sioni tatizo kwa viongozi wa vyama kuwa na ukaribu katika masuala kama haya, lakini kwa vile siasa zetu ni za matukio na za kutafuta power, wealth and popularity through politics, viongozi wengi hutumia muda wao mwingi to create tensions ndani ya vyama vyao, na pia kujenga alliance with the corridors of power nje ya vyama, kwa lengo la kujijenga in terms of power, wealth, popularity; Hali hii inanikumbusha maneno ya Issa Shivji katika kitabu chake cha "Let the people speak: Tanzania Down the Road to Neo Liberalism (2005, pp.134) " ambapo anasema hivi:

Opposition parties, news papers and some intellectual commentators have capitalized on CCM's transformation by sensationalizing scandals and the apparent association of the party with a particular set of tycoons. What matters to the opposition and the commentators is not the tycoonisation of CCM. In fact, the mouths of some opposition leaders water when they hear of pouring of funds by the tycoons into CCM's coffers or the pockets of CCM leaders. How much they wish they were recipients instead of CCM. After all, they too have ambitions to enter the state house and build palaces in Manzese .

Hoja yako ya nne ni inahusiana na umuhimu wa Chadema kufanya mabadiliko (reforms) za haraka. Katika hili, nakubaliana na wewe pia , hasa juu ya umuhimu wa Chadema kufanya uchaguzi ndani ya Chama. Nadhani hii ni moja ya njia chache zilizobakia kwa Chadema ‘to effectively manage the crisis following the sacking of ZZK et al'. Na kama ulivyojadili, Chadema walipoteza fursa ‘to manage' vizuri sakata husika kwa kutoteua ‘a neutral organ' kushughulikia suala husika na badaa yake, chama kutumia mfumo ule ule uliojadiliwa kwa kina katika waraka husika. Hata wakati wa mfumo wa chama kimoja, Mwalimu Nyerere hakuwa anafanya maamuzi yanayohusiana na haya ‘single handedly', badala yale alishirikisha vyombo mbalimbali na kujiridhisha kwanza kabla ya kufikia maamuzi (mfano rejea mchakato wa Mzee Jumbe kuvuliwa madaraka ndani ya CCM na Serikali, na baadae Seif, Hamad Rashid na wengineo).

Hoja yako nyingine kwamba uamuzi wa kuwavua madaraka wahusika ni uamuzi sahihi. Naungana na wewe katika hili, hasa kwanza – kupitia hoja zangu za awali kwamba waraka husika unakabiliwa na matatizo makuu matatu kama ifuatavyo:
· Wrong on Context
· Wrong on Content
· Wrong on Intent;

Pili, naungana na hoja yako juu ya hili kwa kuzingatia hoja zangu za awali kwamba Chadema imeonyesha kwamba:
· Inaweza kukabiliana na migogoro ndani ya chama, hivyo kuwapa wananchi fursa ya kukipima chama hiki iwapo kitakuwa na uwezo wa kukabiliana na migogoro kitaifa.
· Uamuzi husika unaendana na dhana ya Mwalimu kwamba Chama Ni WATU, Sio VIONGOZI.

Swali linalofuatia ni Je:

Ø Chadema itafikia uamuzi wa kuwafukuza wahusika uanachama? Nini madhara ya kuwafukuza? Kutowafukuza

Itaendelea…
 
Katika hili ukweli unaokuja waziwazi ni kuwa Zitto ana tatizo la kutaka kuwa juu ya kila kitu, hasa kiuongozi. Hilo ni tatizo linalonifanya niwe na mashaka na uwezo pamoja na lengo lake. Kuna mifano mingi sana ya kihistoria kuonyesha kuwa viongozi wenye tabia hiyo huwa wanageuka kuwa majanga kwa nchi zao inapotokea wakafanikiwa kupata madaraka; mifano minngine tunayo leo kwetu hapa hapa nyumbani.

Wakati wa Uchaguzi wa mwaka 2010, wakati CDM inatakiwa ivute raslimali zake zote na kuimarisha mshikamano ndani ya chama kuelekea uchaguzi mkuu, Zitto akaibuka na mtafuruku wa kugawanya wanachama wake kwa kupigania madaraka ya kuongoza chama jambo ambalo angekuwa amelifanyia tathmini ndani ya chama hicho alichokuwa akishiriki kuongoza kabla hata halijafika kwenye vyombo vya habari. Mara tu baada ya uchaguzi akabandika picha moja akiwa na Kikwete na kutangaza kuwa Kikwete amemsifia kuwa yeye ndiye anayefaa kuwa Rais wa kumrithi Kikwete.

Kuna mambo mengi sana ambayo amewahi kuwa anaandika na kuyafanya ama unconsciously au consciously yote yakiwa yanaonyesha mwelekeo mmoja wa tamaa ya madaraka. Inapofikia kuwa hata viongozi wenzake anaofanya nao wamemshindwa basi ujue kuna tatizo; uongozi ni institution siyo one man business. Iwapo hawezi kuishi vizuri ndani ya institution hii basi hata akipewa insitution gani atakuwa na matatizo yale yale unless iwe ni institution ya familia yake tu isiyokuwa na watu wengi. Siku chache zilizopita aliripotiwa akiwa anatafuta misaada huko Ujerumani kwa ajili ya malengo yake binafsi ya kisiasa. Wengi wetu hatujui ukweli wa ripoti hizo lakini inapotokea mlundikano wa hahithi zenye kufanana kutokea vyanzo mbalimbali zikiwa zinamhusu mtu mmoja basi inakuwa ni vigumu kuendelea kuzitilia mashaka taarifa hizo.

Jinsi gani Zitto atakavyo-handle situation hii in the long run ndiyo itakatuyosaidia sana kumwelewa yeye ni mtu wa namna gani.
 
Inaendelea kutoka Bandiko #30

Katika bandiko langu la wali (#30) nilimalizia kwa swali kwamba je:
· Chadema itafikia uamuzi wa kuwafukuza wahusika uanachama? Nini madhara ya kuwafukuza? Kutowafukuza

Ni vigumu kuja na jibu lililojitosheleza, kwahiyo nitachofanya hapa ni kutoa tu maoni yangu binafsi juu ya suala hili.

Kuna umuhimu wa kukubaliana kwamba pamoja na waraka husika kuwa na makosa ya content, context na intent, yapo masuala kadhaa ndani ya waraka ambayo yamekuwa yanajadiliwa kwa mudda mrefu na watanzania kutoka katika kada mbalimbali ndani ya jamii. Licha ya ukweli huu, lakini bado sehemu kubwa ya wananchi hawa wameendelea kuwa na imani kubwa na uongozi ulipo pamoja na mikakati iliyopo ya kuimarisha chama na kujenga mazingira ya ushindi kwa ajili ya chaguzi kuu zijazo. Lakini nirudie tena kwamba pamoja na haya, zipo hoja kadhaa za msingi ndani ya waraka husika, tatizo likibakia kuwa kwenye intent, context & content. Ni kwa muktadha huu, wengi (ikiwa ni pamoja na Nguruvi3 nadhani) wanaona kwamba kuna umuhimu wa Chadema kufanyia kazi masuala kadhaa, moja wapo likiwa ni reforms kama vile kuitisha uchaguzi wa ndani na mengineyo.

Nikirudi kwenye swali la msingi hapo juu kuhusiana na kuwafukuza au kutowafukuza uanachama wahusika na nini inaweza kuwa ni madhara ya either decision, mtazamo wangu ni kama ifuatavyo:

Kama nilivyojadili awali, the end (kuwasimamisha uongozi wahusika) was justified, kama lipo tatizo, basi ni kwenye means, na Nguruvi3 kalijadili vizuri kwamba mchakato husika ungefanyika kupitia ‘a neutral organ'. That said and done, baada ya siku kumi na nne ambazo wahusika wamepewa muda kujieleza kwanini wasifukuzwe, kuna scenario kuu tatu ambazo zinaweza kutokea:

1. Scenario ya KWANZA: Wahusika HAWATAFUKUZWA UANACHAMA, na badala yake wataandikiwa barua za ONYO KALI kwa makosa waliyotenda na kuagizwa kwamba ‘within a certain PROBATION PERIOD', shughuli zao zitakuwa closely monitored ikiwa ni pamoja na kutakiwa kuvunja mara moja makundi yao na iwapo watashindwa kufanya hivyo, uamuzi wa kuwafukuza uanachama ndio utafuatia.

2. Scenario ya PILI: Wahusika HAWATAFUKUZWA UANACHAMA. Badala yake, wataandikiwa barua za ONYO KALI kwa makosa waliyotenda, ONYO ambalo litaambatana na ADHABU ya kuzuiwa wasishiriki shughuli zote za kisiasa ndani ya chama, hasa kutoruhusiwa kugombea nafasi za uongozi ndani ya chama kwa kipindi Fulani, na pia kutoruhusiwa kujihusisha na kampeni za aina yoyote katika chaguzi za ndani ya chama kwa kipindi fulani. Iwapo watakiuka haya, uamuzi wa kuwafukuza uanachama ndio utafuatia.

3. Scenario ya TATU: Wahusika WATAFUKUZWA UANACHAMA, baada ya barua zao za maelezo juu ya kwanini wasifukuzwa uanachama, kupokelewa ndani ya siku kumi na nne. Chini ya scenario hii, uamuzi wa kuwafukuza umeshachukuliwa, hizo barua ndani ya siku na nne zinasubiriwa ili kukamilisha formality.


Kila Scenario ina implications zake kwa siasa za Chadema na Taifa kwa ujumla kuelekea 2015. Kwa mfano:
· Kutowafukuza uanachama huku pia kuwaacha bila ya adhabu maana yake ni kwamba wahusika watakuwa na fursa ya kutumia haki zao za kikatiba za ‘kuchaguliwa katika nafasi za uongozi', hivyo kufanikisha malengo yao kwa mujibu wa waraka husika. Sina uhakika kama Kamati Kuu ya Chadema ingependa kwenda huko.

· Kutowafukuza na badala yake kuwapa adhabu, hasa ya kutogombea nafasi za uongozi itakuwa ni kuahirisha tu tatizo husika. Vile vile kauli ya Tundu Lissu wakati akisoma maamuzi ya kamati kuu kwamba "wahusika walikataliwa kujiuzulu kwa sababu wangeondoka na heshima wasiostahili" itaingia doa kwani kwa kutowafukuza na badala yake kuwapa tu adhabu maana yake nikwamba kuna ‘a fraction' ya heshima watakayobakia nayo ndani ya chama. Na ingawa kufanya kosa sio kosa, ila kosa ni kurudia kosa, ukipitia maelezo ya wahusika mbele ya vyombo vya Habari (hasa Dr. kitila Mkumbo), ni dhahiri kwamba wakibakia ndani ya chama, harakati walizolenga kufanikisha zitaendelea, ila safari hii kosa ambalo halitarudiwa ni lile la kupelekea mkakati wao kugundulika na uongozi wa Chama. Sina uhakika kwamba Kamati Kuu ya Chadema pia ingependa sakata hili liende huko.

· Kuwafukuza wahusika ni dhahiri kwamba kutaleta madhara makubwa kwa chama, hasa kwa wapenzi na wafuasi wa ZZK wa ndani na nje ya Chadema ambao kwa namna moja au nyingine, wataleta athari kwenye idadi ya kura 2015 – hasa ngazi ya Urais. Ni dhahiri kwamba zitakuwepo kura za hasira, na pia wapo wengine ambao hawataenda kupiga kura kwa sababu ya kuzira, mambo ambayo yataipunguzia chadema kura nyingi ngazi ya Urais, ingawa sioni madhara sana kwenye ngazi ya ubunge. Katika hili, sina uhakika kwamba Kamati Kuu ya Chadema imejiandaa kukabiliana na outcome hii.

Kwa ujumla wake, kila scenario itakitikisa chama, hivyo cha msingi ni kwa Chama kuangalia mtikisiko gani utakuwa ni wa muda mfupi na ambao utakuwa ni rahisi kukabiliana nao kuelekea 2015. Je, whats the way forward for kamati kuu ya Chadema?

Itaendelea......
 
Last edited by a moderator:
Inaendelea kutoka bandiko #32

Katika bandiko #32 nilihitimisha na swali kwamba je: whats the way forward for kamati kuu ya Chadema?

Yafuatayo ni maoni yangu:

· Kwanza, kwa vile waraka husika una makosa yaliyo wazi (intent, content na context), kuna haja ya Chadema kuwafukuza wahusika lakini pia iwape fursa ya kuomba upya uanachama. In the time being, Chadema ije na marekebisho kadhaa ya katiba, hasa juu ya masharti ya uanachama, viapo vya wanachama n.k. Uamuzi wa kuamua kuomba tena uanachama au kutoomba uanachama utarudishwa tena mikononi kwa wahusika, once and for all.

· Pili, Chadema itangaze kitu kama hali ya hatari au uwepo wa hali chafu ya kisiasa ndani ya Chama. Chama kijenge hoja nzuri na ya kueleweka mbele ya umma. Suala muhimu hapa ni kwa Chadema kueleza kwamba kinaahirisha uchaguzi wa ndani ambao kikatiba ulikuwa ufanyike 2014, hadi pale itakapotangazwa baadae. Chama kiweke wazi kwamba pamoja na kuelewa umuhimu wa suala zima la demokrasia ndani ya vyama, suala ambalo chama kimekuwa kikizingatia pengine (I insist pengine, sina uhakika) kuliko vyama vyote vya siasa nchini, kukiingiza chama kwenye uchaguzi katika mazingira ya hali hewa chafu ya kisiasa kutakiweka chama vulnerable na maadui wa ndani na nje ya chama. Isitoshe, it has been argued in the literature on democracy and party politics several times kwamba:
intra-party democracy sio mwarubaini wa matatizo ndani ya vyama vya siasa na kwamba there are stable democracies with parties that lack guarantees or regular processes of internal party democracy."
.

Baada ya kufanya maamuzi haya, kitengo cha ELIMU NA UTAFITI cha chadema (kama kipo) kianze kazi ya utafiti nchi nzima mara moja kubaini iwapo wanachama wa chadema lakini hasa wapenzi wa chadema ambao ni independent voters wanasemaje juu ya umuhimu wa uchaguzi wa ndani wa chama kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015; Je, kama uchaguzi wa ndani ni muhimu, kwa sababu zipi? Na kama sio muhimu, nini kifanyike kama mbadala. Iwapo utafiti utaleta majibu kwamba uchaguzi ni muhimu, basi Chadema watekeleze hilo lakini with a ‘grand slam' in terms of timing, strategy, and candidates, ili impact iwe positive kuelekea 2015. In the process, kitengo cha Elimu na Utafiti kielimishe umma kwamba hata kwa chama tawala, wagombea na wateule wa nafasi za utendaji hawapatikani barabarani, bali wanatengenezwa, na mara nyingi huwa ni confidants wa uongozi wa juu wa chama. Umuhimu wa hili ufafanuliwe vyema.

Katika hili, hoja ya Nguruvi3 inakuwa na uzito sana – kwamba uongozi wa chama kujaza nafasi zilizoachwa wazi baada ya wahusika kufukuzwa ulikuwa ni uamuzi wa kukurupuka. Hapa, Chadema ilitakiwa ionyeshe kwamba ipo makini sana katika suala zima la recruitment and selection ya viongozi.

Tatu, Chadema ijitahidi kuhakikisha inawekeza katika mikakati ya kuondokana na politics of personalities na badala yake kuelekea katika "politics of issues"; Hii ni kwa sababu, hofu kubwa ya Chadema hivi sasa ni uwezekano wa wanachama na viongozi wengi ‘to defect' kutokana na personality yao (ZZK), kupata dhoruba ya kisiasa; Politics of issues zitawezekana kwa Chadema kuanza kuwa serious na suala zima la ‘ideology', kwani pamoja na chama hiki (pamoja na watetezi wake) kuendelea kudai kwamba kina itikadi iliyo wazi, uwazi na uelewa wa itikadi hii hauja trickle down to the mass, lakini muhimu Zaidi, itikadi husika ina elements za soko huria na ubepari ambao umechangia sana kuangamiza maisha ya watanzania walio wengi kiafya, kielimu, vipato bila ya maelezo ya uhakika kwamba hali hii itaisha liji chini ya mfumo uliopo. Impracticability ya itikadi husika kwa wananchi wa kawaida will continue to bedevil the party, kwani siasa za personalities kuendelea ku gain prominence.

Nne, Chadema irudi uwanja wa mapambano (vijijini) kwani kwa sasa CCM is back in the lead. Uwepo wa CCM kwenye front line chini ya viongozi wake waandamizi maana yake ni kwamba wamefanya utafiti na kugundua kwamba mkakati wa awali wa Chadema unafanya kazi. Ni muhimu kwa Chadema pia kufanye maamuzi magumu haraka kwani haina muda wala rasilimali za kutosha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 – Chadema ifanye uamuzi juu ya uwiano sahihi wa time and resources Chadema as a Political Party Vis a Vis Political Movement; Kwa mfano, kuelekea 2015, masuala gani yaendeshwe chini ya Chadema as a political party na masuala gani chini ya political movement.

Tano, kama nilivyogusia kidogo awali, Chadema ije au iboreshe kitengo chake cha utafiti na elimu kwa umma (kama kipo). Chama kinafanya makosa makubwa kupima its political mileage kwa kuangalia mahudhurio ya mikutano yake ya hadhara peke yake. Kitengo cha elimu na utafiti kinaweza kuja na focus group discussions vijijini – kijiji kwa kijiji, mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba, chumba kwa chumba, shuka kwa shuka, kubaini mapungufu ya chama kwa mtazamo wa wananchi, matarajio ya umma, kero zao, vipaumbele kubaini iwapo vinaendana na vipaumbele vya serikali/bungeni n.k. Baada ya zoezi hili, Chadema itoe elimu kwa umma juu ya uhalisia wa mambo – nini kinaweza fanyika, lini; kipi hakiwezekani, kwa nini n.k.

Sita, hivi karibuni Chadema ilifanikiwa kushawishi vyama vingine vya siasa kuungana na Chadema katika kudai mchakato wa katiba wenye maslahi kwa wananchi. Chadema kisiache moto huu uzimike kwani hali hii ilizua hofu kubwa sana kwa chama tawala. Chadema ikumbuke kwamba it scored a lot of mileage katika hili, lakini muhimu Zaidi, chama kikumbuke kwamba vyama vingine vya siasa havitakuwa na interest ya kuungana na chama chenye migogoro isiyokwisha, hivyo ni muhimu kwa Chadema kumaliza mgogoro uliopo sasa mapema iwezekanavyo na kujikitika katika masuala mengine muhimu ya ujenzi wa chama kuelekea 2015 and beyond.

Saba ni Suala la Fedha za chama - kuna haja ya Chadema kuanza kuwa transparent katika hili kwani hili ni tatizo. Vile vile kuna haja ya Chadema kuanza kubuni vitega uchumi vipya vya kuingizia chama fedha. Suala hili limejadiliwa katika waraka, na ni moja ya maeneo machache ambayo binafsi nadhani yana hoja zenye mashiko. Vinginevyo, bila ya uangalifu, Chadema kitajikuta ni kinakuwa kinaongozwa na PLUTOCRACY (exercise power by virtue of wealth) & KLEPOCRACY (Rule by thieves).

Mwisho, ni suala la kutafakari, na linahusiana na suala zima la "FACTIONS" ndani ya vyama vya siasa. Ningependa kumalizia na nukuu kutoka kwa 'Jonas Ewald och Lennart Wohlgemuth', titled: "Challenges for the opposition and democratization in Tanzania – a view from the opposition"

In 2000 CCM was divided in three major factions. The basis for the factions was not strongly related to different political vision, policy or ideology, but rather to the power struggle involving three charismatic leaders and their factions. All three had been among the major presidential candidates since the election 1995. The first, Benjamin Mkapa the ruling President, chairman of the party and Nyerere's man in the 1995 election; The second was Jakaya Kikwete, the Minister of Foreign Affairs, representing a new generation and pragmatic polices, considered by Nyerere to be too young (45 years) and inexperienced in the 1995 election; The third challenger was John Malacela (Vice-chairman of CCM, former Prime Minister and not favoured by Nyerere in 1995 and regarded to represent the "old hardliners" and elders in the party). Some political differences were ascribed to the candidates, related to the views on the reforms, where the Malacela fraction criticised the neo-liberal aspects of the reform policies implemented by the Mkapa government and claimed to represent a more socialistic tradition. But in practice the competition between the factions within the party turned out to be limited, as could be expected in an election in-between the first and the second of the two presidential periods allowed by the constitution. In CCM's internal nomination to the presidential election 2000, Mkapa in the end was the only candidate presented to the party's national congress for election. The nomination of a new presidential candidate and MPs in 2005 was a much more open, unpredictable and competitive process, even if the three major factions describe above remained. This time the Kikwete factions presented itself as standing for a new era and a representative for the youth.

Je, nukuu hii inatufunza lolote kuhusiana na factions in political parties and political competition in Tanzania?
 
Last edited by a moderator:
Ndugu Mchambuzi, kwa vile unakwenda haraka sana, mimi nitasoma tena posts zako baadaye pole pole.

Ila swali lako moja zuri sana uliloluiza kuhusu Chadema kuwafukuza wanachama nitalichangia kwa vile hili swali la kufukuza wanachama huwa linanikera sana. Mimi nachukulia chama kama taasisi ya umma ambayo inawakutanisha watu wenye itikadi moja. Huwa hainiingii akilini kwa vyama vya kisiasa kufukuza wanachama wake ambao wana itikadi moja hata kama wanatofautiana njia za kufikia malengo ya itikadi hiyo. Ni kama Taifa kufuta uraia wa watu waiozaliwa nchini mle ambao pia baba zao na babu zao pia walizaliwa nchini mle mle. Iwapo mtu anakubaliana na itikadi ya chama chenu, hata kama ni mhalifu, basi mshughulikieni kama mhalifu ila mkijua kuwa huyo ni mwenzenu kiitikadi.

Inawezana kabisa uhalifu wake ni pamoja na kuuza siri za chama chenu, bado msimfukuze. Mpeni adhabu ndani ya chama asiweza kuuza siri hizo tena au hadi akiamua mwenyewe kuondoka kwenye itikadi yenu. Sasa leo mimi nikiuza siri za nchi kwa adui wetu kweli nitafukuzwa utanzania wangu au nitafungwa miaka mingi nikibakia kuwa mtanzania mafungwa tu?
 
In 2000 CCM was divided in three major factions. The basis for the factions was not strongly related to different political vision, policy or ideology, but rather to the power struggle involving three charismatic leaders and their factions. All three had been among the major presidential candidates since the election 1995. The first, Benjamin Mkapa the ruling President, chairman of the party and Nyerere's man in the 1995 election; The second was Jakaya Kikwete, the Minister of Foreign Affairs, representing a new generation and pragmatic polices, considered by Nyerere to be too young (45 years) and inexperienced in the 1995 election; The third challenger was John Malacela (Vice-chairman of CCM, former Prime Minister and not favoured by Nyerere in 1995 and regarded to represent the "old hardliners" and elders in the party). Some political differences were ascribed to the candidates, related to the views on the reforms, where the Malacela fraction criticised the neo-liberal aspects of the reform policies implemented by the Mkapa government and claimed to represent a more socialistic tradition. But in practice the competition between the factions within the party turned out to be limited, as could be expected in an election in-between the first and the second of the two presidential periods allowed by the constitution. In CCM's internal nomination to the presidential election 2000, Mkapa in the end was the only candidate presented to the party's national congress for election. The nomination of a new presidential candidate and MPs in 2005 was a much more open, unpredictable and competitive process, even if the three major factions describe above remained. This time the Kikwete factions presented itself as standing for a new era and a representative for the youth.
Je, nukuu hii inatufunza lolote kuhusiana na factions in political parties and political competition in Tanzania?

Nukuu hiyo ni fundisho kubwa sana kwetu kuwa msuguano wa kichini kuhusu madaraka katika siasa za kitaifa zina madhara makubwa sana kwa taifa lengwa. Tungekuwa na Civil Service Commision imara inayotofautiisha siasa na utendaji wa serikali isingekuwa tatizo, lakini kwa Tanzania hayo ni majanga makubwa
 
Mchambuzi, Kichuguu, Nguruv3 and others;

Kwa maoni yangu binafsi matatizo yaliopo ndani ya CDM yapo ndani ya vyama vingine na ya kujitakia. Hivyo hakuna wa kumlaumu ingawaje wale walioweka matumaini yao kwa CDM wanaweza kuona kuwa ni mkono wa CCM.

Kimuundo na kiundeshaji, CDM wameiga vitu vingi kutoka CCM. Hivyo matatizo yanayotokana na muundo au utendaji yanayotokea au yaliotokea ndani ya CCM yatayokea ndani CDM pia.

Mtego mkubwa waliotegewa CDM na vyama vingine vya upinzani ni mgawo wa ruzuku. Nadhani mfumo mzuri wa vyama ungetokea kama vyama vingezuka kwa juhudi za wananchi wenyewe na sio kutegemea road map na ruzuku iliyopangwa na CCM.

Pamoja na kuwa CDM ina katiba, lazima katiba ya nchi ifuatwe kwanza na baadaye ya chama. Katiba ya nchi inatoa uhuru ya watu kutoa mawazo yao na kushiriki katika maamuzi ya kisiasa. Hivyo Zitto ana haki za kiraia kusema kuwa atagombea urais 2015. Kitu ambacho hana haki nacho ni kuwalazimisha wa CDM kuwa mgombea wa chama chao. Tamaa ya madaraka yakiwa yanafuata sheria ya nchi na katiba za vyama sio kitu kibaya kama wengi tunavyofikiri.

Vilevile katika kipindi hiki cha mabadiliko, CDM ilitakiwa kutokuwa na muundo wa kichama cha kudumu milele. Kilitakiwa kuwa na muundo shirikisho la mabadiliko (movement or coalition). Kwa mfano matatizo yaliopo sasa ni ya kikatiba. Hivyo priority ingekuwa kwenye katiba na sio madaraka.
 
Katika hili ukweli unaokuja waziwazi ni kuwa Zitto ana tatizo la kutaka kuwa juu ya kila kitu, hasa kiuongozi. Hilo ni tatizo linalonifanya niwa na mashaka na uwezo pamoja na lengo lake.

Kuna mifano mingi sana ya kihistoria kuonyesha kuwa viongozi wenye tabia hiyo huwa wanageuka kuwa majanga kwa nchi zao inapotokea wakafanikiwa madaraka; mifano mininge tunayo leo kwetu hapa hapa nyumbani.

Wakati wa Uchaguzi wa mwaka 2010, wakati CDM inatakiwa ivute reaslimali zoake zote na kuimarisha mshikamano ndani ya chama kuelekea uchaguzi mkuu, Zito akaibuka na mtafuruku wa kugawanya wanacama wake kwa kupigania madaraka ya kuongoza chama jambo ambalo angekuwa amelifanyia tathmini ndani ya chama hicho alichokuwa akishiriki kuongoza kabla hata halijafika kwenye vyombo vya habari.

Mara tu baada ya uchaguzi akabandika picha moja akiwa na Kikwete na kutangaza kuwa Kikwete amemsifia kuwa yeye ndiye anayefaa kuwa Rais wa kumrithi Kikwete. Kuna mambo mengi sana ambayo amewahi kuwa anaandika na kuyafanya ama unconsciously au consciously yote yakiwa yanayonyesha mwelekeo mmojawa tamaa ya madaraka. Inapofikia kuwa hata viongozi wenzake anaofanya nao wamemshindwa basi ujue kuna tatizzo; uongozi ni institutions siyo one mana business. Iwapo hawezi kuishi vizuri ndani ya institution hii basi hata akipEwa insitution gani atakuwa na matatizo yale yale unless iwe ni insitution ya familia yake tu isyokuwa na watu wengi.

Siku chache zilizopita aliripotiwa akiwa anatafuta misaada huko Ujerumani kwa ajili ya malengo yake binafsi ya kisiasa. Wengi wetu hatujui ukweli wa ripoti hizo lakini inapotokea mlundikano wa hahithi zenye kufanana kutokea vyanzo mbalimbali zikiwa zinamhusu mtu mmoja basi inakuwa ni vigumu kuendelea kuzitilia mashaka taarifa hizo.

Jinsi gani Zito atakavyo handle situation hii in the longe run ndiyo itakatuyosaidia sana kumwelewa yeye ni mtu wa namna gani.
Mkuu Kichuguu, hadithi za Zitto hazina shaka tena. Watu wamempa benefit of doubt za kutosha. Waraka umemsifia kama mtu anayeweza kubomoa hoja, kwasasa hiyo ni hadithi.

Kuhusu migogoro, mmoja ni huo uliosema wa uchaguzi. Sioni tatizo Zitto kuwania nafasi ya uongozi.
Niliwahi kuhoji viongozi wa CDM kulikuwa na kosa gani Zitto kupambana na Mbowe.
Nilisimama na hoja hiyo mpaka mwisho.

Tatizo ZZK hakuongozwa na busara za wapi pa kusema na athari zake ni nini.
Alitaka kufanya pre preemptive strategy kuongea na vyombo vya habari,angeliongelea kichama halafu vyombo vya habari.

Mgogoro mwingine ni ule wa Kafulila ambao alidai ameumia sana na damu yake kwa CDM. Alitengeneza mtafaruku uliohusisha vijana wenzake kwa sababu rahisi tu, kutaka kupata wadhifa

Mgogoro mwingine ni wa masalia ambao laiti Ben Saa nane asingejilipua ulikuwa unaelekea kubaya.
katika mgogoro huo Kitila alijitokeza kusema 'vijana waachwe wabalehe' kwasababu tu kuna watu wanawatumia

Mgogoro wa Mwigamba ndio umedhihirisha kuwa Zitto ni tatizo. Huu ulipangwa kama jaribio la mapinduzi katika chama cha kidemokrasia.

Tatizo la Zitto
1. Zitto anafahamu kuwa yeye ni maarufu katika chama na anaona anauwezo mkubwa kuliko watu wengine

2. Kukosa busara:
ZZK amekosa busara katika mambo mengi. Majaribio yote hapo juu alitajwa wazi na ushahidi yalitosha kumkumbusha busara. Kwa vile ana tabia niliyoisema hapo namba 1, ZZK anadhani usomi au umaarufu vinaweza ku compliment busara.

3.Uvumilivu:
Ingawa wanasema ni mvumilivu, uvumilivu wa Zitto ni katika mipango yake.
Si uvumilivu ndani ya institution laiti angekuwa mvumilivu leo angebebwa na wafuasi wa CDM kuwa kiongozi wao. Lakini pia ukisoma majibu na tambo zake hasa anapojibishana na public ni rahisi kubaini hana uvumilivu.

4. Charisma na courage.
Courage ndio imekuwa msingi mkubwa wa umaaurufu wake bahati mbaya hana charisma.
Siasa ni kitu aha ajabu sana, hakizingatia principles za ukurugenzi au umeneja.
Wilson Mukama wa CCM hakukubalika kwasababu hana Charisma, lakini ni mtu makini sana.
Thabiti Kombo Jecha wa ZNZ alikuwa na charisma kisiasa na kuonekana kama opinion leader visiwani.


Charisma tu ni sehemu kubwa sana ya siasa. Kwavile Zitto hana Charisma, mbadala wake ulikuwa ni busara.
Laiti angechanganya courage na wisdom zote zingeficha udhaifu wa charisma.

Jinsi gani ata handle situation?

1.Handling ya situation ni mbaya to begin with.
ZZK alifahamu kikao kilikusudia kujadili nini.Akaondoka kwenda ziarani jambo lililoleta hasira miongoni mwa wenzake.
Ni kukosa busara ninako kusema.

Leo anasimama katika vipaza sauti na kusema ''ni mwanasiasa na katika maisha yake amejikwaa na amefanya makosa'

Hayo angeyasema katika katika kikao ingesaidia zaidi kuliko vyombo vya habari.
Lakini pia asingesafiri hata kama asingehudhuria.

2. Zitto amekimbilia katika vyombo vya habari na mkutano mkubwa.
Angetoa taarifa fupi tu ya yeye kubaki kuwa mwanachama mtiifu .

Alichokifanya ni spinning ili kupata public sympathy kuwa amehukumiwa kwa kusimamia masilahi ya umma.
Sasa hivi inaonekana wazi kuwa hakuwa na mpango huo.
Waraka unaonyesha alikuwa mkali nje na ndani ya bunge kwa masilahi yake kama alivyoelekezwa.

zzk ana expose weakness zake kwa flimpsy excuse na kuwa vulnerable zaidi.
Watu hawakujua mambo 11 yaliyomfukuzisha. Kutokana na kufanya spinning za PAC n.k. yale 11 yatawekwa hadharani na atajikuta pabaya zaidi. PR yake kuhusu suala hili ni mbovu sana.

Ukiniuliza wakati huu afanye nini, jibu langu, Zitto anatakiwa kuwa na busara basi.
Kila analosema, analotenda ahakikishe lina busara, asitegemee akili za vitabuni.

Pili aache spinning kwasababu anajiweka katika mazingira magumu.
Tatu asitumie vijana kumsafisha, jina lake lijisafishe lenyewe. Itachukua muda lakini hakuna short cut.
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi, Kichuguu, Nguruv3 and others;

Kwa maoni yangu binafsi matatizo yaliopo ndani ya CDM yapo ndani ya vyama vingine na ya kujitakia.
Hivyo hakuna wa kumlaumu ingawaje wale walioweka matumaini yao kwa CDM wanaweza kuona kuwa ni mkono wa CCM.

Kimuundo na kiundeshaji, CDM wameiga vitu vingi kutoka CCM. Hivyo matatizo yanayotokana na muundo au utendaji yanayotokea au yaliotokea ndani ya CCM yatayokea ndani CDM pia.

Mtego mkubwa waliotegewa CDM na vyama vingine vya upinzani ni mgawo wa ruzuku. Nadhani mfumo mzuri wa vyama ungetokea kama vyama vingezuka kwa juhudi za wananchi wenyewe na sio kutegemea road map na ruzuku iliyopangwa na CCM.

Pamoja na kuwa CDM ina katiba, lazima katiba ya nchi ifuatwe kwanza na baadaye ya chama. Katiba ya nchi inatoa uhuru ya watu kutoa mawazo yao na kushiriki katika maamuzi ya kisiasa. Hivyo Zitto ana haki za kiraia kusema kuwa atagombea urais 2015. Kitu ambacho hana haki nacho ni kuwalazimisha wa CDM kuwa mgombea wa chama chao. Tamaa ya madaraka yakiwa yanafuata sheria ya nchi na katiba za vyama sio kitu kibaya kama wengi tunavyofikiri.

Vilevile katika kipindi hiki cha mabadiliko, CDM ilitakiwa kutokuwa na muundo wa kichama cha kudumu milele. Kilitakiwa kuwa na muundo shirikisho la mabadiliko (movement or coalition). Kwa mfano matatizo yaliopo sasa ni ya kikatiba. Hivyo priority ingekuwa kwenye katiba na sio madaraka.
Zakumi
Hoja ya 1:
Watu kudhani kuna mkono wa CCM,naafiki.
Mashabiki wa CDM wamelewa ushabiki kiasi unaweza kuwaambia anayehujumu CDM ni Raila Odinga wakaamini.
Kuna viashirio vingi uliwawekea wazi hamkani si shwari. Wakapuuzia na kuelekeza nguvu zao kutafuta mchawi CCM.
Ni kweli kuna element za CCM na vyombo dola kufanya hivyo lakini udhaifu wa wao kuingia CDM unatoka ndani ya CDM.

Kwa mfano harakati zao kuelekea vijijini kama Mchambuzi alivyosema zimesimama kushughulikia mgogoro ulioletwa na naibu katibu mkuu na mshauri wa chama ambao ni wajumbe wa kamati kuu.
Hata kama wametumiwa bado udhaifu huo ni wa CDM na waukubali kwanza.

Hoja ya 2: Naafiki 100%
Tulishawaambia kule duru za siasa waache kufanya mambo kwa template ya CCM.
Hawa ni wasomi wabuni mifumo inayokidhi haja za vyama vyao na hakuna template standard.
Mfano, leo kungekuwa na senate ya CDM ambayo ni independent mzozo kama huu ungeshakwisha siku nyingi.

Na hapa lazima tuseme wahafidhina hawakubali mabadiliko na hilo ni tatizo kubwa.
Wahafidhina lazima waangalie mambo mbali zaidi na kwa mtazamo wa kona tatu.

Hoja ya 3: Ruzuku
Huu ni mtego ambao CDM wameshindwa. Kuna tatizo la mgao ambao hauhusiani na shughuli za chama unaoleta taabu. Uongozi umeshindwa kuridhisha watu kuwa matumizi na mapato yanawiana.

Sioni kwanini katibu mkuu na mwenyekiti wajihusishe na mambo haya badala ya wataalam.
Kisha walianza vizuri sana kwasababu kila jambo walikuwa wanafanya consultations, sijui hili la ruzuku lina tatizo gani.
Uwazi hakuna na hilo ni donda litakalobaki hata kama asprin itatolewa.

Hoja 4: Katiba na madaraka
Absolutely !! Nilidhani wangejifunza kutoka vyama vingine. Kulikuwa na mgogoro NCCR, TLP, UDP na CUF.
Migogoro yote ilihusisha katiba. Na hata CDM walikuwa na mgogoro wa wabunge wa viti maalum, sijui imekuwaje hawakujifunza kutokana na hilo. Lakini twende mbele turudi nyuma siku zote 'Chadema Wahafidhina' hawakubali mabadiliko na hilo ni tatizo.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu Mchambuzi, kwa vile unakwenda haraka sana, mimi nitasoma tena posts zako baadaye pole pole.

Ila swali lako moja zuri sana uliloluiza kuhusu Chadema kuwafukuza wanachama nitalichangia kwa vile hili swali la kufukuza wanachama huwa linanikera sana. Mimi nachukulia chama kama taasisi ya umma ambayo inawakutanisha watu wenye itikadi moja. Huwa hainiingii akilini kwa vyama vya kisiasa kufukuza wanachama wake ambao wana itikadi moja hata kama wanatofautiana njia za kufikia malengo ya itikadi hiyo. Ni kama Taifa kufuta uraia wa watu waiozaliwa nchini mle ambao pia baba zao na babu zao pia walizaliwa nchini mle mle. Iwapo mtu anakubaliana na itikadi ya chama chenu, hata kama ni mhalifu, basi mshughulikieni kama mhalifu ila mkijua kuwa huyo ni mwenzenu kiitikadi. Inawezana kabisa uhalifu wake ni pamoja na kuuza siri za chama chenu, bado msimfukuze. Mpeni adhabu ndani ya chama asiweza kuuza siri hizo tena au hadi akiamua mwenyewe kuondoka kwenye itikadi yenu. Sasa leo mimi nikiuza siri za nchi kwa adui wetu kweli nitafukuzwa utanzania wangu au nitafungwa miaka mingi nikibakia kuwa mtanzania mafungwa tu?
Mkuu Kichuguu na Mchambuzi , suala la kufukuza au kutofukuza linapaswa liangaliwe kwa upana wake
1. Aina ya kosa na kama adhabu hiyo vinawiana
2. Risks ya wahusika kubaki katika chama
3. Ramifications zinazoweza kutokea kutoka maeneo mbali mbali ya kijamii
4. Haki ya watuhumiwa katika kufikia maamuzi.

Nipo katika rekodi nikiwaambia CDM wazi kuwa mgogoro wa Arusha walikosa uthubutu.
Niliwaambi ni bora wakapoteza viti vyote 7 kuliko kuwa na madiwani 7 wanao paralyze shughuli zao.
Wakachukua maamuzi magumu na imelipa, mgogoro hakuna na shughuli za Arusha jijini zinaendelea

Dr Slaa akajaribu kufanya usuluhishi kule Mwanza na kuogopa kuchukua hatua ili asipoteze umaarufu kanda ya ziwa.
Gogoro la Jiji la Mwanza linaendelea na lina watesa.

Kuhusu hili la akina Zitto kuna hitajika busara za kulishughulikia kwa kuangalia risk za wao kubaki ndani ya chama.
Kama hawana madhara baada ya kuvuliwa uongozi na wanapenda kubaki ndani ya chama waachwe.

Endapo kubaki kwao kuta paralyze shughuli za chama bora waondoshwe.
Kinacho matter hapa ni ushahidi walio nao uongozi na kutumia vigezo nilivyosema wanaweza kufikia maamuzi sahihi.`

Sijui kama jazba itadhibitiwa katika kutenda haki, ndiyo maana nilisema uongozi ulipaswa utafute chombo neutral.
Amin alimkosa kosa Obote mara ya kwanza, mara ya pili Obote akafanya kosa likamgharimu aliporudi katika uongozi akwafanyizia wabaya wake. Ilikuwa series of vengeance

The bottom line ni calculation za risks kutokana na ushahidi walio nao dhidi ya watuhumiwa.
Kiwango cha adhabu waliopewa na factors zingine zinazoweza kuwafanya CDM vulnerable kwa maamuzi hayo.

Ni suala la busara
 
Last edited by a moderator:
Kuna namna rahisi sana ya kushughulikia suala la Zitto ndani ya CDM. Avuliwe uanachama, aende mahakamani, kesi iendelee, kwa kipindi hicho atakuwa "kibogoyo", uchaguzi wa chama ufanyike, mchakato wa katika ya nchi usimamiwe sawasawa (maana kuna hisia kuwa huu mgogoro utaiondolea CDM concentration kwenye katiba), baadae ashinde kesi, nina uhakika hataendelea kuwa CDM wakati wa uchaguzi mkuu ujao...

Hii mbinu imefanya kazi kwa Kafulila NCCR na Hamad Rashid CUF... probably itafanya kazi kwa Zitto CDM...
 
Mkuu Kichuguu na Mchambuzi , suala la kufukuza au kutofukuza linapaswa liangaliwe kwa upana wake
1. Aina ya kosa na kama adhabu hiyo vinawiana
2. Risks ya wahusika kubaki katika chama
3. Ramifications zinazoweza kutokea kutoka maeneo mbali mbali ya kijamii
4. Haki ya watuhumiwa katika kufikia maamuzi.

Nipo katika rekodi nikiwaambia CDM wazi kuwa mgogoro wa Arusha walikosa uthubutu.
Niliwaambi ni bora wakapoteza viti vyote 7 kuliko kuwa na madiwani 7 wanao paralyze shughuli zao.
Wakachukua maamuzi magumu na imelipa, mgogoro hakuna na shughuli za Arusha jijini zinaendelea

Dr Slaa akajaribu kufanya usuluhishi kule Mwanza na kuogopa kuchukua hatua ili asipoteze umaarufu kanda ya ziwa.
Gogoro la Jiji la Mwanza linaendelea na lina watesa.

Kuhusu hili la akina Zitto kuna hitajika busara za kulishughulikia kwa kuangalia risk za wao kubaki ndani ya chama.
Kama hawana madhara baada ya kuvuliwa uongozi na wanapenda kubaki ndani ya chama waachwe.

Endapo kubaki kwao kuta paralyze shughuli za chama bora waondoshwe.
Kinacho matter hapa ni ushahidi walio nao uongozi na kutumia vigezo nilivyosema wanaweza kufikia maamuzi sahihi.`

Sijui kama jazba itadhibitiwa katika kutenda haki, ndiyo maana nilisema uongozi ulipaswa utafute chombo neutral.
Amin alimkosa kosa Obote mara ya kwanza, mara ya pili Obote akafanya kosa likamgharimu aliporudi katika uongozi akwafanyizia wabaya wake. Ilikuwa series of vengeance

The bottom line ni calculation za risks kutokana na ushahidi walio nao dhidi ya watuhumiwa.
Kiwango cha adhabu waliopewa na factors zingine zinazoweza kuwafanya CDM vulnerable kwa maamuzi hayo.

Ni suala la busara

Madhara watakuwa nayo sana ndugu yangu, maana hawakukubali kushindwa, na tayari wana mtandao wao kuanzia makao makuu hadi mikoani.

Njia ni moja tu nayo ni kuwavua uanachama, waende mahakamani... Wakati kesi inaendelea hawatakuwana nguvu ya kuendeleza mapambano chamni, maana hata wanaowaamini sasa watakuwa na hofu kuwa itakuwaje endapo hawatashinda kesi...
 
Kuna namna rahisi sana ya kushughulikia suala la Zitto ndani ya CDM. Avuliwe uanachama, aende mahakamani, kesi iendelee, kwa kipindi hicho atakuwa "kibogoyo", uchaguzi wa chama ufanyike, mchakato wa katika ya nchi usimamiwe sawasawa (maana kuna hisia kuwa huu mgogoro utaiondolea CDM concentration kwenye katiba), baadae ashinde kesi, nina uhakika hataendelea kuwa CDM wakati wa uchaguzi mkuu ujao...

Hii mbinu imefanya kazi kwa Kafulila NCCR na Hamad Rashid CUF... probably itafanya kazi kwa Zitto CDM...
Nadhani CDM hawahitaji temporary solution, wanachohitaji ni suluhu ya kudumu.
The bottomline, unatibu malaria kwa dawa zake au unachagua kutumia asprin kupunguza homa?

Watuhumiwa kama Zitto anaweza kwenda mahakamani kutetea kiti chake cha ubunge.
Mkakati huo unaweza kufanikiwa kwa muda.

Bado atakuwa amepoteza nguvu za kisiasa hata kama atajaribu kuzijenga kupitia michango yake bungeni.
Suala la kuvuliwa uanachama linategemea ukubwa wa kosa na ushahidi uliopo.

Endapo ushahidi hautajitosheleza hilo laweza kuwa shubiri kwa uongozi uliopo.
Kutakuwa na hoja ya uonevu ambayo inaweza kujengewe mazingira mazito na kushinda nguvu ya tuhuma. Kwa mfano suala la PAC limevaliwa njuga kuliko tuhuma nyingine kwa jicho la Kengeza.
Hakuna anayeongelea kuhusu 'Kafulila, Juliana, M7 masalia' kama sehemu na mchango wa Zitto.

Yes, Zitto ni kiongozi wa bunge, wakati huo huo ni naibu katibu mkuu.
Hana rekodi ya kutenda alichokisema ndani ya chama chake.

Hapa tukubaliane kuwa alichokifanya ilikuwa kutupa kombora kwa wadhifa wake.
Hilo halimfanyi awe amekosea kusema kwa niaba ya PAC lakini the motive behind was not on national interest.

Kuna suala linajitokeza kuwa Mkumbo amekiri kosa na hivyo Zitto ingawa ametajwa lakini hakuhusika.
Hapa kuna hoja moja kuu watu wanashindwa kuielewa. Je, wanajua tarehe waraka huo ulipoandaliwa?

Inawezekana uliandaliwa mwaka 2012 au January na sasa ilikuwa utekelezaji baada ya makubaliano.
Ushahidi wa kimazingira wa maandishi ya waraka unaonyesha wazi mkakati ulishaanza, tumeonyesha hilo.

 
Zakumi
Hoja ya 1:
Watu kudhani kuna mkono wa CCM,naafiki.
Mashabiki wa CDM wamelewa ushabiki kiasi unaweza kuwaambia anayehujumu CDM ni Raila Odinga wakaamini.
Kuna viashirio vingi uliwawekea wazi hamkani si shwari. Wakapuuzia na kuelekeza nguvu zao kutafuta mchawi CCM.
Ni kweli kuna element za CCM na vyombo dola kufanya hivyo lakini udhaifu wa wao kuingia CDM unatoka ndani ya CDM.

Kwa mfano harakati zao kuelekea vijijini kama Mchambuzi alivyosema zimesimama kushughulikia mgogoro ulioletwa na naibu katibu mkuu na mshauri wa chama ambao ni wajumbe wa kamati kuu.
Hata kama wametumiwa bado udhaifu huo ni wa CDM na waukubali kwanza.

Hoja ya 2: Naafiki 100%
Tulishawaambia kule duru za siasa waache kufanya mambo kwa template ya CCM.
Hawa ni wasomi wabuni mifumo inayokidhi haja za vyama vyao na hakuna template standard.
Mfano, leo kungekuwa na senate ya CDM ambayo ni independent mzozo kama huu ungeshakwisha siku nyingi.

Na hapa lazima tuseme wahafidhina hawakubali mabadiliko na hilo ni tatizo kubwa.
Wahafidhina lazima waangalie mambo mbali zaidi na kwa mtazamo wa kona tatu.

Hoja ya 3: Ruzuku
Huu ni mtego ambao CDM wameshindwa. Kuna tatizo la mgao ambao hauhusiani na shughuli za chama unaoleta taabu. Uongozi umeshindwa kuridhisha watu kuwa matumizi na mapato yanawiana.

Sioni kwanini katibu mkuu na mwenyekiti wajihusishe na mambo haya badala ya wataalam.
Kisha walianza vizuri sana kwasababu kila jambo walikuwa wanafanya consultations, sijui hili la ruzuku lina tatizo gani.
Uwazi hakuna na hilo ni donda litakalobaki hata kama asprin itatolewa.

Hoja 4: Katiba na madaraka
Absolutely !! Nilidhani wangejifunza kutoka vyama vingine. Kulikuwa na mgogoro NCCR, TLP, UDP na CUF.
Migogoro yote ilihusisha katiba. Na hata CDM walikuwa na mgogoro wa wabunge wa viti maalum, sijui imekuwaje hawakujifunza kutokana na hilo. Lakini twende mbele turudi nyuma siku zote 'Chadema Wahafidhina' hawakubali mabadiliko na hilo ni tatizo.

Thanks Nguruv3:

Hivi walaka wa kuonyesha hili kundi ulipatikana vipi?
 
Mkuu Nguruvi3

Hongera sana kwa kuja na mada ambayo uwasisilishaji wake upo “considerably balanced”.
Kuna maeneo kadhaa ambayo kidogo unajenga hoja zinazoegemea upande mmoja (but without losing objectivity) lakini nikisoma kwa umakini, nahisi pengine ni kutokana na kusononeka kwako na na ‘unnecessary interference’ zinazojitokeza katika harakati za kuwapatia wananchi chama kikubwa cha pili nchini ambacho kinazidi kuimarika na kuonyesha uwezo mkubwa wa kupambana na chama tawala (CCM) kwa maslahi ya umma na demokrasia nchini kwa ujumla. Iwapo nipo sahihi, then I share similar sentiments kwani kwa afya ya demokrasia ndani ya taifa letu, Chadema ilitakiwa iwe imeshafika mbali sana na harakati zake za kufika kila kona ya nchi kwa nia ya kujijenga kuelekea 2015, kama inavyofanya CCM hivi sasa chini ya watendaji wake wakuu ambao wanazunguka nchi nzima.

Nadhani moja ya maswali muhimu ni kwamba je:
· Maamuzi ya Kamati Kuu yameleta madhara gani kwa wananchama wa Chadema na Wananchi kwa ujumla?

Kwa mtazamo wangu, suala la ZZK lilikuwa ni Pandora’s Box ambalo wananchi wengi walikuwa na hamu lifunguliwe ili wawaze kukidhi curiosity yao kubaini all the evils and miseries contained in the box. Swali linalofuatia ni je:
· Have all the evils being exposed? What about the miseries?

Pengine ni mapema mno kupata majibu ya uhakika, lakini kwa maoni ya yasiyo na utafiti wa kina ni kwamba uamuzi wa Kamati Kuu umezaa ‘mixed feelings in the electorate’. Lakini mbaya Zaidi ni kwamba, pande zote zinajadili Zaidi suala husika kwa vigezo vya personalities kuliko issues. Tukianza na upande unaounga mkono uamuzi wa kamati kuu, upande huu una amini kwamba Chadema bado ina hazina kubwa ya Viongozi Vijana (sio imani, sera au itikadi bora) ambao bado wanaleta matumaini ya kuwakomboa wananchi. Na kwa upande mwingine unaopinga maamuzi ya kamati kuu umechukizwa na kitendo cha kuondolewa kwa shujaa wao (ZZK) for reasons ranging from ukanda, ujana, na masuala mengine yasiyokuwa na uhusiano wa moja kwa moja na imani, sera au itikadi za Chadema.

Kundi hili linahisi kwamba harakati za chadema kuikomboa nchi kwa maslahi ya wanyonge walio wengi (Vijana) zimeingia dosari na kwamba kukosekana kwa ZZK 2015 and his style of leadership and articulation kutaleta ugumu mkubwa wa kushawishi wananchi (hasa Vijana) kukipigia kura Chadema katika uchaguzi wa 2015.

Vinginevyo, kwa ujumla wake, ukweli unabakia kwamba Chadema kimefanikiwa sana kugeuka kuwa tumaini jipya la wanyonge na kwamba - kwamba angalau sasa kuna chama kinachosikiliza vilio vyao, kwa maana ya kwamba - hata kama chadema haitafanikiwa kuingia Ikulu hivi karibuni, lakini uwepo wa viongozi wake makini kumesaidia sana kukiamsha chama tawala ambacho sasa nacho kimeanza kuendesha siasa za kujali kero za wananchi kwa vitendo. Kwa mfano, ziara za watendaji wakuu wa CCM nchi nzima kwa scale ya sasa ni kitu ambacho hakijawahi kutokea kwa Zaidi ya miaka thelathini. Credit katika hili inastahili kwenda kwa Chadema na sio kwingineko.

Baada ya kusema hayo, naomba sasa nijadili baadhi ya hoja zako kadhaa kama ifuatavyo:

Kwanza ni juu ya makosa ya waraka husika. Naungana na wewe katika hoja yako kwamba kosa la msingi lipo kwenye ‘intention, content and context’. Hili halina mjadala hata litetewe vipi kwani kama ulivyojadili, kulikuwa na njia nyingine mbadala kwa mujibu wa sheria, kanuni na utaratibu kufanyia kazi au kuwasilisha hoja husika. Na iwapo mbadala huo ungekwama, hapo ndio kungekuwa na hoja yenye mashiko kwamba ‘nia ya mabadiliko na demokrasia ndani ya chama vinahujumiwa’. Vinginevyo, wanachama huchagua viongozi ndani ya vyama vyao ambao wanafanya kazi ya KUWATETEA na KUWAUNGANISHA, Sio KUWACHOCHEA na KUWAGAWANISHA. Kwa mantiki hiyo, Chadema imefanya uamuzi wa maana, lakini muhimu zaidi ni kwamba:

· Chadema kama Chama kimeonyesha jinsi gani kinaweza kukabiliana na Migogoro ya ndani, kwani hii ni ishara nzuri kwamba kitakuwa na uwezo wa kukabiliana na migogoro nje ya chama (ndani ya taifa) iwapo utakiamini na kukipeleka ikulu.

· Katika harakati za Ujenzi wa TANU, Mwalimu Nyerere (rejea chapisho la TANU na Raia, 1962), alipata kusema kwamba: . Uamuzi wa Chadema umeonyesha ukomavu kwa kukubaliana na ukweli huu, na umeijadili hoja hii vyema pale unaposema kwamba .

Hoja ya pili ni ile unasema kwamba – “hakuna umuhimu wa Chadema kuwa karibu au kupendwa na watawala”. Katika hili, pia naungana na wewe kwani katika mazingira ya ambayo nchi inakabiliwa na ombwe kubwa la dira ya taifa, itikadi za vyama vya siasa, na utawala wa sheria, sioni mantiki yoyote ya viongozi wa chama kikuu cha upinzani kujiweka karibu na watawala, ili iweje? hasa ikizingatiwa kwamba tangia mapendekezo ya tume ya nyalali (1990s), wanachofanya watawala imekuwa ni kuhodhi mchakato mzima wa political reforms in Tanzania (wanazuoni – Hyden na Shivji wameandika sana juu ya tatizo hili la top – down democratization process in Tanzania). Suala hili limeathiri sana kasi ya ukuaji wa demokrasia na utawala wa sheria nchini. Lakini hapa sina maana kwamba kuna umuhimu wa Chadema kuwa na ‘confrontational relationship with the status quo’. Kwa mtazamo wangu ambao pengine ni finyu, tatizo lililopo katika siasa za nchi yetu ni kwamba:

Tumeshindwa kubaini masuala yanayohitaji ‘bipartisan politics’, kama msimamo wa pamoja juu ya umuhimu wa masuala kama ‘good economic governance’ (rasilimali za nchi kwa manufaa ya wananchi), ‘national values and ethos’, ‘uadilifu’, ‘uzalendo’, ‘national security’ (kwa manufaa ya wananchi), ‘strengthening of democracy’, n.k, masuala ambayo yangepelekea uwepo wa ‘win-win situations’ kwa pande zote mbili.

Binafsi, sioni tatizo kwa viongozi wa vyama kuwa na ukaribu katika masuala kama haya, lakini kwa vile siasa zetu ni za matukio na za kutafuta power, wealth and popularity through politics, viongozi wengi hutumia muda wao mwingi to create tensions ndani ya vyama vyao, na pia kujenga alliance with the corridors of power nje ya vyama, kwa lengo la kujijenga in terms of power, wealth, popularity; Hali hii inanikumbusha maneno ya Issa Shivji katika kitabu chake cha “Let the people speak: Tanzania Down the Road to Neo Liberalism (2005, pp.134) ” ambapo anasema hivi:

Hoja yako ya nne ni inahusiana na umuhimu wa Chadema kufanya mabadiliko (reforms) za haraka. Katika hili, nakubaliana na wewe pia , hasa juu ya umuhimu wa Chadema kufanya uchaguzi ndani ya Chama. Nadhani hii ni moja ya njia chache zilizobakia kwa Chadema ‘to effectively manage the crisis following the sacking of ZZK et al’. Na kama ulivyojadili, Chadema walipoteza fursa ‘to manage’ vizuri sakata husika kwa kutoteua ‘a neutral organ’ kushughulikia suala husika na badaa yake, chama kutumia mfumo ule ule uliojadiliwa kwa kina katika waraka husika. Hata wakati wa mfumo wa chama kimoja, Mwalimu Nyerere hakuwa anafanya maamuzi yanayohusiana na haya ‘single handedly’, badala yale alishirikisha vyombo mbalimbali na kujiridhisha kwanza kabla ya kufikia maamuzi (mfano rejea mchakato wa Mzee Jumbe kuvuliwa madaraka ndani ya CCM na Serikali, na baadae Seif, Hamad Rashid na wengineo).

Hoja yako nyingine kwamba uamuzi wa kuwavua madaraka wahusika ni uamuzi sahihi. Naungana na wewe katika hili, hasa kwanza – kupitia hoja zangu za awali kwamba waraka husika unakabiliwa na matatizo makuu matatu kama ifuatavyo:
· Wrong on Context
· Wrong on Content
· Wrong on Intent;

Pili, naungana na hoja yako juu ya hili kwa kuzingatia hoja zangu za awali kwamba Chadema imeonyesha kwamba:
· Inaweza kukabiliana na migogoro ndani ya chama, hivyo kuwapa wananchi fursa ya kukipima chama hiki iwapo kitakuwa na uwezo wa kukabiliana na migogoro kitaifa.
· Uamuzi husika unaendana na dhana ya Mwalimu kwamba Chama Ni WATU, Sio VIONGOZI.

Swali linalofuatia ni Je:
Ø Chadema itafikia uamuzi wa kuwafukuza wahusika uanachama? Nini madhara ya kuwafukuza? Kutowafukuza
Mkuu Mchambuzi , niseme kuwa kwa hali yoyote kuujadili waraka lazima itaonekana kama kuegemea upande mmoja.

Hilo nalifahamu vema, tatizo ni kuwa waraka umeandikwa na watuhumiwa wamekiri.
Jambo lililopo mbele yetu ilikuwa kwanza kuujadili waraka ili tupate mahali pa kuanzia.

Sehemu kubwa ya waraka ina makosa kama ulivyo ya fupisha.
Hata pale penye substance lugha iliyotumika haikuwa sahihi.
Na mbaya zaidi imeandikwa na watu wenye viwango vya juu katika weledi.

Baada ya kuujadili waraka hatutaishia hapo tumeuliza maswali kuhusu mambo yaliyoibuliwa na waraka.
Mfano, nimeuliza hivi Mbowe kutoa mkopo kwa chama akiwa mwenyekiti hakuna conflict of interest hapo?
Na je anakumbu kumbu zozote kuhusu mikopo anyotoa? n.k.

Bila upinzani imara hakuna utawala imara nakubaliana nawe.
Siku za karibuni tumeshuhudia wabunge wa CCM wakisita na hata kukikosoa serikali yao kwa kuamini kuwa yupo atakayepeleka kesi katika mahakama ya juu ya wananchi na consequences zake ni kubwa.

Ndiko kumezaa akina Fikunjombe, Lugora n.k. na ni kwa mwendo huo serikali imekuwa na uangalifu wa 'business as usual' inapotokea kuna wasomi wa waraka hawalioni hilo nadhani inajenga sentiment fulani.

Kuhusu maswali yako
Have all the evils being exposed? What about the miseries?
Naweza kusema No, bado kuna maeneo mengi ya kufanyiwa kazi ambayo yamejificha.
Kazi hiyo ilitakiwa ifanywe na wasomi, kwabahati mbaya wameangukia pua kuandika madudu ya waraka.
Lakini ukweli unabaki kuwa kama taasisi bado kuna maeneo mengi ya kufanyiwa kazi.

Kwanza kuna mapungufu kwa CDM kutojiendesha kama taasisi bali mkusanyiko wa watu fulani.
Kwa hapa ilipo CDM lazima iwe taasisi inayojitegemea bila kujali personality.

Mgogoro huu si mkubwa, ukubwa wake umeegemea katika personality.
Kuna haja ya CDM kufumua mfumo wao na kuunda mfumo usiotegemea uwepo wa mtu au watu taasisi.
Kwa mfano, mfumo wa fedha unaolalamikiwa usingemhusu katibu au mwenyekiti kama ingekuwa taasisi yenye vitengo kamili na huru. Kwa sasa haiweleweki !

Nyakati za Mtei na Makani si za sasa. CDM kimekua naumiliki uwe wa wanachama, wengine ni watumishi tu.
Ownership ya chama irudishwe kwa wananchi.

Hivi niulize ni chombo gani kinaweza kumwadhibu mwenyekiti au katibu panapotokea matatizo.
Mwanachama wa CDM ana haki gani ya kusema na kusikilizwa.
Kazi ya naibu katibu mkuu ni ipi kama hajui nini kinaendelea katika chama chake!

Hoja hapa ni kuwa hii template ya CCM ambayo inaisumbua CCM yenyewe miaka 50 haifai kufuatwa.

Kuhusu Bipartisan na ushirikiano wa viongozi hilo sioni kama ni tatizo.
Tatizo ni pale ukaribu huo unapo compromize integrity ya mhusika.

Kwa mfano, mpinzania anapokuwa na mtu wa chama tawala badala ya kuongelea maendeleo au ushirika wa kutafuta suluhu za matatizo anatumika kisiasa hilo si jambo jema hata kidogo.

Kwa bahati mbaya Bipartisan inafanya kazi kukiwa na weledi pande zote, kwa CCM bipartisan ni kujiunga katika kufukia uhalifu na kuficha maovu. Ni bora pengine isiwepo kwasababu' it takes two to tango'

Swali la pili
Nini madhara ya mgogoro huu kwa wanachadema na wananchi?

Madhara ni makubwa. Wananchi wanashindwa kuelewa mbadala, wanaona kile kinachohubiriwa si kile wanachotaraji.

Wananchi wanakata tamaa kujiona wapo mayatima kumbe wenzao katika ukombozi ni hawa wanaotaka madaraka na wala si ukombozi.

Madaraka sawa lakini yawe kwa njia za kidemokrasia na si coup d'etat ya Kitila na Zitto.
Wakati huu kukiwa na uhaba wa demokrasia wananchi wanajiuliza wakimbilie wapi?

Kuna mambo mengi yanayohitaji uwakilishi wa upinzani katika kusimamia matatizo ya nchi.
Mgogoro kama huu unawaacha wajiulize hivi nani atasimamia suala la Simcard linalowatesa ikiwa suala hilo lililoletwa na CCM na Serikali yake litaachwa kwa hao hao.
I mean wanauliza where is check and balance. Nani atasimama upande wao! wanakata tamaa.

Katika CDM madhara ni makubwa, electoral college yao imegawanyika, political base ipo paralyzed.
Chama kikitaka kushindwa malengo njia rahisi ni ku paralyze political base kitu kinachotokea sasa hivi.
Wanachama wamechanganyikiwa hawajui mbivu na mbichi. Wanajiuliza kulikoni na nani wamwamwini tena?

Mgogoro huu unatoa mwanya kwa maadui wa nje wa CDM kufanyia kazi agenda zao.
Mathalan, CCM wameshikilia bango kufukuzwa kwa Zitto ni kutokana na kutoitonya CDM kuhusu ukaguzi.

Sijui kama kuna kauli ya CDM kuhusu kutonywa lakini aliyemwaga mtama huo hadharani ni Zitto na CCM wana uhalali kabisa wa kuzungumzia hili.
Si limesemwa na aliyekuwa naibu katibu mkuu na mjumbe wa kamati kuu? Nini cha kubisha hapo.

Wapinzani wa nje swanatafuta sababu za kuendelea kuwagawa CDM.
Wanachukua fursa za mtafaruku kuleta mtafaruku zaidi.

Utashangaa hawaongelei waraka na kifungu kinachochoea udini lakini wanaongelea udini as as general.
Nani alifungua pandora box ni Kitila na Zitto na CDM wakaingia na sasa ni mtafaruku tu.

Kiini cha yote haya ni kutokuwa na taasisi imara bali taasisi yenye personality. Hatari sana.


 
Last edited by a moderator:
Thanks Nguruv3:

Hivi walaka wa kuonyesha hili kundi ulipatikana vipi?
Sijui kama nitakuwa nimelielewa veama swali lako, nitajaribu kufafanua kadri nijuavyo. Insider kama Tuko anaweza ku chip in

Waraka ulikamatwa kutoka katika lap top ya Mwigamba. Mwigamba ndiye mchapaji aliyetajwa kama M3. Ni huyu bwana alikuwa anatumia ID ya mkulima masikini. Nadhani walifuatiliwa kwa ukaribu na mtu wao ambaye alikuwa mshirika wa kundi la waandika waraka. Huyu ndiye alivujisha habari zote kwasababu kukamatwa kwa waraka kulikuwa na precision ya hali ya juu sana.

Kundi. Uwepo wa kundi haujulikani. Kama ulivyosoma waraka ni watu wachache sana waliojua mpango huo.
Kwa bahati mbaya wengi wa vijana waliotumika hawakujua nini kipo nyuma yake. Walipewa maelekezo na ahadi kem kem mambo yakishakamilika. Leo wengi wanatazama nyuma na kuona walivyolishwa hujuma dhidi ya chama chao.

Kwahiyo hili si kundi lenye kadi ni elite wachache sana waliofanya mazingaombwe na kubeba wengi bila kujijua.
Hata hivyo ikumbukwe kuwa uwepo wa kundi hili haukuanza leo.

Kiongozi wao ni Zitto ambaye ametajwa kuhusika na tuhuma kubwa tatu
1. Wakati wa Kafulika alikuwemo
2. Wakati wa Juliana alikuwepo
3. Masalia M7 alikuwepo.

Baada ya kugundua kuwa kuwatumia vijana kuna madhara kwasababu ya kutokuwa na simile au subra ndipo wakaamua na mwenziwe waanzishe kitu kukiwa na watu wachache kama waraka unavyoonyesha.

Utakumbuka wakati wa sakata la kufukuzwa kwa Juliana, Kitila Mkumbo aliandika makala raia mwema si kulaani uhalifu bali akiwataka viongozi wa CDM wawasamehe 'hawa ni vijana waachwe wabalehe'. Leo tunajua kubalehe ilikuwa kuwalinda kwasababu ni watu wao.

Sijui kama nimeeleweka kutokana na swali lako, kama kuna mapungufu wengine wachangie kwa kadri yao.

Kundi la waandika waraka naomba lijulikane kama 'ZIKI' (Zito & Kitila)

 
Back
Top Bottom