Duru za Siasa Special: Mgogoro kambi ya Upinzani (CHADEMA)

Duru za Siasa Special: Mgogoro kambi ya Upinzani (CHADEMA)

Mkuu nguvuri i got the feeling this will be going into circles unless we agree on one thing kuhusu huu waraka and move forward or we agree to disagree and call it quits
Kutojua mkkati hakuna maana kuwa siwezi kujali kilicho wazi kama waraka huo.
Ninachokisema ni kuwa mikakati ndani ya CDM siijui, lakini mkakati uliowekwa wa waraka si mkakati.
Lakini jiulize mkakati huo ni CDM au ni wa kundi la watu, na kama baadhi ya watu ukiwemo mnaujua je hiyo inafanya uwe mkakati wa CDM? Nitakupa mfano, hivi kujadili mapenzi ya Dr Slaa ni sehemu ya mkakati wa CDM?
hapa naposema Mkakati simaanishi wa kichama ni mbimu or preparation in early stages za kuuva uongozi uliopo, Huko pia unahitaji mkakati/mpango jinsi ya kumvaa mpinzani au unadhani na yeye hana mbinu za ushindi. Kumbuka huu waraka aukuandikwa kwa ajili ya public it was a private plan ya watu ndani ya chama hivyo wanasababu za kutaka kujiuliza utendaji wa viongozi wao ukoje na kujiba legitimate reasons za kwanini watoke na kwanini wamekuwa vikwazo kimaoni yao. Unagombea nafasi ya juu udai mabadiliko kama huna sababu hizo why bother hivyo wanajiaminisha ya kwa nini hao watu hawafai (mbona kawaida sana mkuu).

Pili, hujajibu hoja nilizoweka, ulianza katikati na sasa unarudi nyuma.
Hukunitendea haki kwasababu ulitakiwa upitie uzi kwa undani ujiridhidhe kuwa unachokisema kina ushahidi na mantiki.
Kipi sasa hapa tunazungumzia, kama swala la wewe kuhitimisha waraka unamatatizo na hilo ndilo nililo kua accuse nalo si hata hapa unarudia, kuna haja kweli ya mimi kurudi nyuma zaidi, ntarudi tu kwa sababu ya kuangalia angle zingine lakini kwa hapa msimamo wako hupo wazi.

Tatu, tafadhali sana onyesha mkakati ndani ya waraka kipengele kimoja hadi kingine.
Nimeonyesha makosa kipengele kimoja hadi kingine.
Nini mantiki ya SWOT analysis ukishaifanya ikusaidie nini mbele.

Nne, pitia vipengele nilivyoainisha uonyeshe wapi unadhani kulikuwa na matatizo.
Matatizo yepi unayoyaongelea hapa? wakati nimekuwekea kwenye quote yangu ya kwanza kwako vipengele ambavyo sikubaliani mfano wewe kusema wananchi hawatowaamini CDM wakishindwa kutoa adhabu stahiki kwa makosa ya waraka, si tayari umeshakili waraka ni tatizo linalo stahili adhabu ama?

Tano, Kumuondoa kiongozi hatujasema ni kosa, kosa ni njia zinazotumika kumuondoa.
Kuandaa mapinduzi katika chama chenye nembo ya demokrasia si vision au mission ni treason.
Mkakati ni tendo, hata mapinduzi ni sehemu ya mkakati. Sijui unaongelea ni huu wa mapinduzi au wa kuendeleza CDM?
Labda unadhani wangemtoaje, maana nilivyoelewa mimi wanajipanga kwa uchaguzi ujao that requires a mission.

Sita, bado hujajibu swali,je unadhani waraka huo ni sahihi?
Hapa tunataka tuelewe position yako ili tujue tunajadiliana katika muktadha upi.
Mimi nasema tena waraka una makosa.
Yap i see nothing wrong with it is just a plan in its early stages and the author seemed troubled with the emotions wakawa wanajipa sababu za kwanini hawa hawafai, lakini kupanga kuwania uongozi si dhambi au kutaka kuona kiongozi aliyepo yupo nje uamuzi ujao is matter of taste.

saba; Ukipitia nyuzi yangu nimesema si kila kitu ni trash kuna sehemu hoja zina mantiki ya kuzihoji nakiziorodhesha kwa kutoa nafasi uongozi ujibu(pitia nyuzi), lakini sehemu kubwa ya waraka haina mantiki.
Na namalizia hapa kwa kurudia kusema ule si waraka wa wasomi na nipo tayari kukuonyesha kwanini si wa kisomi.
Mkuu si hata mimi nimekwambia ulikuwa na hoja za msingi isipokuwa sikubaliani na hitimisho lako ya kuwa waraka unamakosa.

Nane, hebu tuonyeshe mission, objective and strtategies katika waraka kipengele kimoja hadi kingine.
[Long ting. ndio maana hata siku hizi wengine tumeacha kuchangia mada za economic humu ndani maana comparison are no longer based on facts and the readiness of changes zilizokuwepo mpaka tunao jilinganisha wakatoka haraka, me out. Ohh this is a very simple strategy everything is there so i wont go point simpe plans, politicians dont use SWOT much they prefer 'game theory' imekaa kinafiki kama proffesion yenyewe ya siasa me out, trust me wangekuwa waangalifu zaidi na kuto mu-underestimate mpinzani.

me out for now. Ntapitia huko nyuma baadae.
 
For one second, kama CCM kweli waliwatumia wenye uchu ndani ya CDM, naipongeza sana CCM.

Siku zote ukitaka kumshinda adui yako ni lazima uangalie mbinu zake na udhaifu wake. Kama CCM waliona udhaifu wa Chadema hauko kwenye sera, ila upo kwenye muundo na kwa baadhi ya wajumbe wake wa kamati kuu, hatua walizochukua ku-deal nao kisiasa ni legitimate. Kwa hili kama kuna atakayeilaumu CCM atakuwa anakosea kabisa.

Unapokuwa vitani unachoangalia ni ushindi kwanza, sio silaha unayotumia, unatumia silaha yoyote itakayokusaidia ushinde.
 
For one second, kama CCM kweli waliwatumia wenye uchu ndani ya CDM, naipongeza sana CCM. Siku zote ukitaka kumshinda adui yako ni lazima uangalie mbinu zake na udhaifu wake. Kama CCM waliona udhaifu wa Chadema hauko kwenye sera, ila upo kwenye muundo na kwa baadhi ya wajumbe wake wa kamati kuu, hatua walizochukua ku-deal nao kisiasa ni legitimate. Kwa hili kama kuna atakayeilaumu CCM atakuwa anakosea kabisa. Unapokuwa vitani unachoangalia ni ushindi kwanza, sio silaha unayotumia, unatumia silaha yoyote itakayokusaidia ushinde.

Kama Chadema inanasa kwenye mitego midogo namna hii, je inaweza kujimili mikiki na vishawishi toka kila pembe ya Dunia ikipewa nchi?
 
Eric Cartman,
umeuliza how is everybody today? Mimi nasema everybody Bukheri

Katika bandiko #60 umetetea mkakati wa kufika kileleni kwa mh Zitto.
Kwanza nikueleze kuwa walichotaka kukifanya ni uhaini kama nilivyosema. Ni uhani katika ngazi ya chama na si nchi kwa analogy ile ile. Kwanini nasem hivyo

1. Zitto/Kitila ni viongozi wajuu CDM. Hakuna kumbu kumbu za kuonyesha
a) Waliwahi kueleza masikitiko yao juu ya uongozi wazi wazi.

Upo ushahidi walieleza kwa kutumia watu
i) Sakata la Kfulila, Zitto alitajwa ii)Skata la Juliana shonzo Zitto alikuwa kiongozi wa Masalia(M7)
iii)Sakata la Mwigamba ambalo ni waraka Zitto na Kitila wamekiri kuhusika.

b)Njia nzuri ya kidemokrasia kuonyesha kutoridhika na uongozi ilikuwa kujiuzulu.
Hilo lingewapa nafasi ya kueleweka na kutengeneza mkakati kuelekea katika uongozi.

Mkakati uwe wa ushindani na si upinzani kama waraka unavyosema.
Huwezi kuwa na upinzani ndani ya chama, unakuwa na ushindani. Hizo tofauti unapaswa kuzielewa.
Hawakufanya hivyo.

c)Waraka umetamka kuwang'oa waliopo madarakani. Ukizingatia hoja 1 (a)(i) hapo juu, kuwang'oa kulikusudia kutekelezwa na makundi yote ya nyuma ambayo Zitto na kitila walishiriki kikamilifu.
Katika utawala wa kidemkrasia kama ilivyo jina la CDM huo si utawala ni uhaini usio na shaka kwa mwenye macho mawili.

d)Vurugu zilizotokea CDM wanahusika kwa ushiriki wao katika makundi.
Sijui kama mkakati wa kupanda ngazi unaozungumzia unahusu kuiangusha CDM kwanza ili waje kujenga CDM yenye maono?

Hilo halikuwezekana NCCR na CUF na it is likely walikusudia kuvuruga kwa ushahidi wao wenyewe. Uhaini.

e)Wamechomeka data nusu na kuficha baadhi ili kuwapumbuza watu wasiojua kutafsiri data kwa njia za ulaghai wa kisomi. Hilo ni usaliti wa imani ya waliowachagua na ni uhaini kimantiki.

2. Waraka pamoja na wewe mumetetea uhalali wake kwa kusema huo ni mkakati wenye mission na vision.
Hebu soma hapa halafu ujiulize kama kuna mkakati au ilikuwa kuweka rehani chama chao na pengine taifa

''Kwa kuwa ni mwislamu. Hii ni fursa katika kupata kuungwa mkono na wanachama waislamu ambao wamekuwa na kigugumizi wakidhani waislamu hawatakiwi katika uongozi wa taasisi yetu''

Kama kuna mambo hatari katika taifa ni kupata viongozi kwa njia za ukabila na udini.
Sifa ya kiongozi ni kuwaunganisha watu kwa sera, mission na vision kama 'unit'
Taifa halihitaji Maaskofu au Masheikh kwasababu wapo wa kutosha.
Taifa linahitaji viongozi wa kuliweka pamoja na kuongoza.

Huu mkakati kama unadhani si hatari basi tuna hatari kubwa mbele yetu zaidi ya waraka.
Kama umesoma hukuliona hili ujue kuna tatizo.

Katika maandishi yangu yaliyopita nimejjaribu sana kutoliongelea kwasababu miongoni mwa mambo yanayonikera na kuniudhi ni udini na ukabila.

Hapa nimelezimika kuyasema kwa kutambua kuwa ipo haja.
Eric, umasikini wa Watanzania hauletwi na dini au kabila bali maono ya viongozi.
Ufisadi, wizi, uzembe na ufujaji ndio chanzo.
Tena hayo yanafanywa na viongozi ambao wewe, Kitila na Zitto mnaita mkakati.
Wanaiba na kutoa sadaka, ninyi mnafanya sehemu ya mkakati.

Mkirudi bungeni mnamsifia mtu kwa kuibua ufisadi wakati kwenye nyaraka zenu za siri mnatengeneza mazingira ya kifisadi. Kuongoza kwa kutumia dini ni ufisadi uliotamalaki unaohitaji makakati kutoka kwa wapuuzi tu.

Hivi kweli katika SWOT kipengele cha dini unaweza kukisema ni sehemu yake?
Hivi akitokea kiongozi mzuri sana ambaye hana dini huyo hataweza kuongoza taifa hili.

Nionyesha SWOT ya Kitila na Zitto ilivyo na matatizo

Inaendelea
 
Mkuu nguvuri i got the feeling this will be going into circles unless we agree on one thing kuhusu huu waraka and move forward or we agree to disagree and call it quits
hapa naposema Mkakati simaanishi wa kichama ni mbimu or preparation in early stages za kuuva uongozi uliopo, Huko pia unahitaji mkakati/mpango jinsi ya kumvaa mpinzani au unadhani na yeye hana mbinu za ushindi.

Kumbuka huu waraka aukuandikwa kwa ajili ya public it was a private plan ya watu ndani ya chama hivyo wanasababu za kutaka kujiuliza utendaji wa viongozi wao ukoje na kujiba legitimate reasons za kwanini watoke na kwanini wamekuwa vikwazo kimaoni yao.

Unagombea nafasi ya juu udai mabadiliko kama huna sababu hizo why bother hivyo wanajiaminisha ya kwa nini hao watu hawafai (mbona kawaida sana mkuu).
Soma nukuu hizi ujiridhishe mwenyewe
''Hakuna mtu anayejua hivi sasa fedha za chama zinatumikaje zaidi ya kakikundi ka watu watatu yaani mkuu kabisa, mtendaji mkuu na mkuu wa fedha kwenye taasisi yetu.

Mpinzani wetu.... Si tuelimu yake ya darasani ni ya magumashi bali pia vipaji na akili ya kuzaliwa havijaonekana katika maisha yake.

Hoja ya uongozi uliopo kushindwa kabisa kusoma taarifa za fedha tokea 2010 ikifahamika kwa wapiga kura inaweza kuwa machinjio kabisa ya uongozi uliopo na kumpa fursa kubwa tunayemtaka.

Mpinzani wanawake humwona kama malaya anayependa kutumia miili yao kujistarehesha wakati wazee humwona kama mtu anayedhalilisha hata nafasi aliyopewa kwa kufanya uhuni waziwazi hata kuvunja ndoa si ya kwake tu bali hata za watu wengine.

Elimu ndogo na duni aliyenayo mpinzani wetu ambaye ndiye mkuu wa taasisi yetu kwa sasa.
Kimsingi tumekubali kuongozwa na mtu mwenye akili ndogo.

Ni dhahiri kwamba pale mpinzani wetu anaporushiwa kombora la kashfa anakuwa mzito kujieleza hata kama anapewa nafasi ya kufanya hivyo na hii ni fursa muhimu kwa tunayemtaka''
Eric Cartaman: Nini mantiki ya SWOT analysis ukishaifanya ikusaidie nini mbele.Matatizo yepi unayoyaongelea hapa?
''Mtendaji mkuu msaidizi n
i kiongozi anayeweza kuongoza taasisi bila kujenga makundi akijali zaidi kazi ya taasisi kuliko maslahi binafsi''

Zitto ana makundi tena yaliyowahi kuleta vurugu.
Kundi la waraka ni ubinafsi, kundi la Kafulila na Masalia aliyaanzisha kwasababu ya ubinafsi. Hawezi kuwa kiongozi katika chama akiwa na makundi pembeni.
SWOT inasema hiyo ni strength wakati ushahidi wa kuanzisha makundi upo hauna shaka
.

''Ni msomi wa kiwango cha juu na mwenye uwezo mkubwa katika kuchanganua mambo ya kiuchumi, kisiasa, kijamii, kimichezo''

Hakuna ukweli kuwa ana uwezo wa kuchanganua mambo. Waraka umethibitisha hilo
''
Maneno yake mara nyingine hayazingatii anayazungumza katika mazingira gani na hivyo kuwasha masikio ya wanataasisi jambo linalompunguzia kukubalika kwake taratibu.

Kama ilivyo kwa maneno, kuna matendo pia ambayo mara nyingine huyafanya bila kuzingatia mazingira na wasikilizaji wake na hivyo kupunguza imani ya wana taasisi kwake

Kwa kifupi kuna wakati tunayemtaka huonekana kufanya maamuzi kwaemotion zaidi badala ya kutulia kwanza na kutafakari kwa kina ikiwa ni pamoja na kutafuta ushauri kwa wenzake kabla ya kurespond''
Hapa unaona jinsi wanavyoandika mambo bila kutafakari. Kujichanganya ni dalili kuwa huu haukuwa mkakati wa kuisadia CDM bali wao wenyewe kwa faida zao wenyewe.
Angalia jinsi wanavyojichaganya, hivi hapo unasema kuna mission na vision kwa chama cha kisiasa!!
''Kuna mambo ambayo ni haki ya mtu mfano mahusiano binafsi ya kimapenzi, kuwa na marafiki wa damu kutoka upande mwingine wa utawala, nk. Lakini mambo hayo ni muhimu wakati mwingine ama kwa kiwango fulani yakafanywa kwa siri kuepuka mitazamo potofu kwa unaowaongoza''

halafu soma hapa
''
Mpinzani wanawake humwona kama malaya anayependa kutumia miili yao kujistarehesha wakati wazee humwona kama mtu anayedhalilisha hata nafasi aliyopewa kwa kufanya uhuni waziwazi hata kuvunja ndoa si ya kwake tu bali hata za watu wengine''

Niambie kuna chochote kama mkakati wa kisiasa hapo.
Ni majungu tu kwamba Zitto akifanya uzinifu basi iwe kwa siri, akifanya Mbowe au Slaa wanadhalilisha chama.

Hapo kuna mtu anatushawishi kuwa kundi hili lilikaa kwa nia njema ya kutoa maono na mtazamo kwa CDM.
Kwamba waraka wao ulikuwa safi sana katika hatua za awali na unakubalika. Real

Eric umeridhika japo kidogo kuwa hakukuwa na mission au vision kilichokuwepo ni majungu katika lugha njema sana. Hakukuwepo na jambo lolote la kusaidia CDM ni mambo ya kuwasaidia wao wenyewe.

SWOT analysis inalenga kumshauri Zitto afanye mapenzi kwa siri. My God!
 
Mkuu Nguvuri,

Ni vigumu sana kwa wanasiasa kutoonekana wanafiki au kushiriki katika mikakati inayoweza onekana ina element hizo kwenye malengo yao ya kupanda ngazi. Wanasiasa mara nyingi hawaanzi juu, ni watu ambao wapo kwenye mfumo wa kupanda daraja and as you climb the hierarchy ladder the less chances are available. Na mfumo wa kusogea mbele umejengwa kwa namna za kupigiwa kura au kuteuliwa na kiongozi wa juu. Therefore groups and power struggles are inevitable inside political parties, fighting for control.

Hivyo basi wanasiasa wenye ndoto za kusogea mbele wanamajukumu ya kujiwekea au kujiweka kwenye mazingira halisi ya kisiasa hili kufikia malengo yao, ikiwa kujipangia muda, kuangalia namna za kufika huko, kunahitajika mbinu zipi, kuelewa structure ya chama chao, utamaduni wa ndani ya chama, uhuru wao upoje ndani ya chama kutokana na structure zilizopo, where power lies and how is maintained. Hivyo basi kwakuwa mimi si CDM siwezi jua hali halisi ya ndani along those lines, isipokuwa Kitila, Zitto na Mwigamba (or something), wanajua ndio maana pengine wameona muhimu kulizungumzia hilo Tatizo.

Ntachokwambia mimi na hili ni own interpretition, ule waraka umeandikwa na wasomi na kwa fikra za kisomi kivipi? Mosi ni wanachama wa aina gani walikuwa watu wa mwanzo kujiunga na CDM na kwa sababu zipi, Kwa mtazamo wangu mimi watu wa kwanza kujiunga na mzee Mtei watakuwa ni marafiki zake, watu wa karibu yake na wachache waliokuwa wameichoka CCM, kwakuwa akikuanza au ni zao la vuguvugu kama mapinduzi/ukombozi/independence purposes; bali kwa sababu za ku-fill gap in the democratic deficit hivyo ni commonsense wanachama wa mwanzo ni watu ambao waliokuwa wapenzi wa demokrasia ya ushindani na wengi ni watu wa karibu yake including mwenyekiti wa sasa that is understandable na kulikuwa na base yao na mpaka leo ndio kwanza CDM bado hipo kwenye juhudi za kujiweka nationally (in terms of establishing permanent bases elsewhere nationally).

Kwa hivyo it is more likely kutakuwa kulikuwa na utamaduni ambao ulikidhi wanachama wa mwanzo kwa kuwa kulikuwa na little variety among them. Mara nyingi changamoto za demokrasia zinaanza pale makundi mengi yanapokuwa ndani hapo utamaduni inabidi ubadilike, sasa hayo maswala ya udini na ukabila siwezi yaongelea hila walio ndani wanaona huo utamaduni lazima uvunjwe na chama kilenge kwenye 'catch all party' ideologues. Sababu zao ni earlier forged loyalties do not fit a national party and they do not wish to see their party being identified that way or else why would they mention it in their weakness of the party.

Again unapozungumzia swala la kwanini hawa jamaa hawakufuata taratibu za grievance procedure, wakati wewe ni mtu wa nje kama mimi umejiuliza how do they handle criticism inside their party ama unalazimisha tu bila kujua matokeo ya the aggrieved after complaining, unajua ni nani anae handle malalamiko na fairness inapatikana vipi. Kama huwezi jibu kwa ufasaha jinsi CDM inavyo handle complaints then unasababu ya kushabikia kanuni ambazo ujui kama zinaheshimiwa, si hata CCM wanadai viongozi wao wanatakiwa wawe waaminifu ki kanuni je wanaheshimu hilo na kuna njia za kutoa adhabu kuna anaejali ndani kwa sasa. Sasa wewe unatumia evidence hipi kulazimisha ufuataji wa kanuni ilihali ujui zinafanya kazi vipi ndani ya chama.

Pengine ndio sababu ya waraka kuongelea yale ambayo wanaona hayafai kutokana na utendaji wa kiongozi wao ambae amekosa vision na kuelewa ukuaji wa demokrasia unafanana vipi mwisho wa siku wanataka kuvunja the 'iron law of oligarchy' ambayo kwa sasa practitioners ni wale waliokuwa viongozi wa awali na sasa chama kimekuwa inabidi ki-reflect its members diversity moja wapo kunanikisha malengo hayo including kuvunja vile ambavyo wewe unaona taboo kuviongelea.

itaendelea jioni.

By the way mimi si kiongozi wala sijawahi kufika bungeni as yet.
 
Mkuu Nguvuri,

Ni vigumu sana kwa wanasiasa kutoonekana wanafiki au kushiriki katika mikakati inayoweza onekana ina element hizo kwenye malengo yao ya kupanda ngazi. Wanasiasa mara nyingi hawaanzi juu, ni watu ambao wapo kwenye mfumo wa kupanda daraja and as you climb the hierarchy ladder the less chances are available. Na mfumo wa kusogea mbele umejengwa kwa namna za kupigiwa kura au kuteuliwa na kiongozi wa juu. Therefore groups and power struggles are inevitable inside political parties, fighting for control.

Hivyo basi wanasiasa wenye ndoto za kusogea mbele wanamajukumu ya kujiwekea au kujiweka kwenye mazingira halisi ya kisiasa hili kufikia malengo yao, ikiwa kujipangia muda, kuangalia namna za kufika huko, kunahitajika mbinu zipi, kuelewa structure ya chama chao, utamaduni wa ndani ya chama, uhuru wao upoje ndani ya chama kutokana na structure zilizopo, where power lies and how is maintained. Hivyo basi kwakuwa mimi si CDM siwezi jua hali halisi ya ndani along those lines, isipokuwa Kitila, Zitto na Mwigamba (or something), wanajua ndio maana pengine wameona muhimu kulizungumzia hilo Tatizo.

Watuhumiwa ni sehemu ya uongozi wa juu katika chama na ninaamini wamefika hapo walipofika kwa njia za kidemokrasia na si vinginevyo. Iweje leo ionekane kuwa hakuna demokrasia ndani ya chama kiasi cha kuwasukuma wanasiasa hawa kutumia njia mbadala? Kulikuwa na umuhimu wowote mkakati huu kuhusisha personal attacks kama elimu ya mwenyekiti?

Mkuu Nguruvi3 amejitahidi kwa kiasi kikubwa kuuchambua waraka huu na mapungufu yake kifungu kimoja baada ya kingine. Pengine ingekuwa vema na wewe basi uchambuzi wako ujikite kwenye waraka wenyewe hatua kwa hatua.
 
Last edited by a moderator:

Mwalimu;

Kwanini Cartman auchambue waraka? Na kwanini awe na mtazamo sawa na Nguruvi3. Ukisoma posti utaona kuwa Nguruv3 amejitahidi kuchambua waraka na agenda zingine. Lakini utaona kuwa Nguruv3 ana mapenzi fulani na CHADEMA. Na uchambuzi wake ni wa kufanya CHADEMA kujirekebisha hili siku moja kiwe chama tawala.

Kwa upande mwingine Cartman anachambua flaws ambazo wana CHADEMA wamehamua kuzifumbia macho kwa ajili umoja wa chama au kwa kuwa na nia ya kuonyesha kuwa wananguvu za kuondoa CCM.

Hizi flaws zilizokuwepo ndio chanzo cha waraka na migogoro mingine. Hivyo mtu anaweza kuchambua kwa kuangalia flaws.

Kabla ya 2005 CDM kilikuwa ni chama kidogo tu cha kisiasa kilichoridhika na ruzuku za serikali na kuwa na wabunge wawili watatu. Kashfa za Richmond, Buzwagi, EPA na matatizo mengine ilibadilisha fortunes za chama hicho. Kimuundo na kiutendaji chadema haikujiandaa na hizi fortunes mpya.
 
Mwalimu;

Kwanini Cartman auchambue waraka? Na kwanini awe na mtazamo sawa na Nguruvi3. Ukisoma posti utaona kuwa Nguruv3 amejitahidi kuchambua waraka na agenda zingine. Lakini utaona kuwa Nguruv3 ana mapenzi fulani na CHADEMA. Na uchambuzi wake ni wa kufanya CHADEMA kujirekebisha hili siku moja kiwe chama tawala.

Kwa upande mwingine Cartman anachambua flaws ambazo wana CHADEMA wamehamua kuzifumbia macho kwa ajili umoja wa chama au kwa kuwa na nia ya kuonyesha kuwa wananguvu za kuondoa CCM.

Hizi flaws zilizokuwepo ndio chanzo cha waraka na migogoro mingine.
Hivyo mtu anaweza kuchambua kwa kuangalia flaws.

Kabla ya 2005 CDM kilikuwa ni chama kidogo tu cha kisiasa kilichoridhika na ruzuku za serikali na kuwa na wabunge wawili watatu. Kashfa za Richmond, Buzwagi, EPA na matatizo mengine ilibadilisha fortunes za chama hicho.

Kimuundo na kiutendaji chadema haikujiandaa na hizi fortunes mpya.
Nafahamu si rahisi kuongelea jambo bila kuongelea CCM mtu akaeleweka. Waraka ni wa CDM na mada imeeleza wazi toka mwanz kuwa tuutendee haki.

Nitakuwa kama wale mashabiki wa CDM wanaodhani kuwa mchawi wao ni CCM peke yake. Nimeandika katika bandiko kuwa CCM wanachokifanya ni sahihi kwasababu
1. Hawana sera nyingine za kuushawishi umma kwanini miaka 50 tu masikini
2. Wanataka kubaki madarakani na mbinu mojawapo ni kuondoa vikwazo.

Ninachokionyesha kwa maoni yangu ni jinsi gani mzozo wa CDM ulianza, ukalelewa na kfika ulipo.
Na muhimu zaidi ni kuweka sawa suala hili ambalo limepoteza mwelekeo kwa nyuzi za kumtuhumu Mtei, kumtetea Zitto bila mashiko, kutafuta mchawi CCM hata kama genge la wachawi lipo ndani ya CDM yenyewe.

Katika kufanya hivyo kunatokea mambo mawili
1. Kwakosoa CDM kama tulivyowahi kuikosoa CCM kuhusu mambo mengi sana
2. Kuangalia mustakabali wa taifa kwa kutokuwa na upinzani imara. Matokeo ya hili yana impact katika taifa
a) NCCR ilipomeguka CCM wakabaki wenyewe bungeni, serikali na kwingineko. Ndilo chanzo cha Kagoda,meremeta .k.
b)CUF ilipoingia Nyongo kukabaki ombwe la upinzani, tukano ung'oaji reli kama chuma chakavu, Jersy, BoT, Uswiss n.k.
c) Kuyumba kwa CDM, tunaona katiba ya CCM ikiandaliwa na makando kando mengine mengi sana.

Ndipo ninapokubaliana na Mchambuzi kuwa bila Upinzani imara hakuna CCM imara wala serikali imara.
Yes kama wanakoselewa ili wajirekebishe hilo ni sawa na sijui tatizo ni kitu gani.
Tulishawahi kuwakosoa CCM wajirerekebishe lakini ni sikio la kufa halisikii dawa, sasa hili linaloanza maumivu tuliache tu hata kujaribu dawa?

Lakini dhidi ya yote wengine tunataka viongozi waadilifu,waaminifu, wakweli na wenye kuaminiwa.
CCM wameridhika kuwa Chenge anaweza kuwatengenezea bajeti, magamba ni sehemu yao na wanaweza kuishi nayo salama salimin. Hatuna namna ya kuwasaidia ila kuwatakia kheri kama hiyo ndio njia waliyoamua kuwafuata UNIP na KANU mapunzikoni.

Hawa waliokuja na kujenga matumaini tunaona ni wanafiki wakubwa.
Kwa mfano, Zitto aliposema hesabu za vyama zikaguliwe kila mmoja alimuona mzalendo na mwenye uchungu.

Walimuona huyu anafaa kupewa uongozi hata wa nchi.
Ni mkweli, mwadilifu na mwaminifu kwa kile anachokisema.
Guess what, deadly wrong! soma hapa maoni ya waraka uliomkabidhi kadhi

''Hoja ya uongozi uliopo kushindwa kabisa kusoma taarifa za fedha tokea 2010 ikifahamika kwa wapiga kura inaweza kuwa machinjio kabisa ya uongozi uliopo na kumpa fursa kubwa tunayemtaka''

Hivi tutaendelea kuwa taifa na watu kama hawa hadi lini?
Huyu anayeweza kuughilibu umma ili apande ngazi akifika huko juu itakuwaje.
Kama ndivyo tunawalumu CCM kwa lipi?

Halafu huyu Zitto mtaalam wa spinning anakuja na kusema tatizo ni kutoa kauli ya ukaguzi wa fedha ndicho kimemuondoa madarakani. Sasa tunajua alikuwa na haki ya kufanya hivyo kama mwenyekiti wa PAC lakini nia na dhamira yake haikuwa kama inavyoonekana, alikuwa anatafuta mahali pa kupandia ngazi tena kwa mapinduzi
.

Nisichoafiki ni kunyoosha CCM vidole na kuvkunja kunapokuwepo na akina 'Chenge' upande mwingine.
Tuwe wakweli na tusimame katika ukweli, spade ni spade tu siyo kijiko kikubwa. Let us take'em on equ
ally
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3

Turudishe kumbukumbu nyuma. Ben Saanane alinekana shujaa kwa kufanya uspy na kuvumbua wasaliti ndani ya Bavicha.

Kazi hiyo Ben Saanane aliifanya kwa muda mrefu na haijawahi kujadiliwa kwenye kikao chochote halali cha chama.

Katika kikao cha Bavicha kujadili sakata hilo Ben Saanane alihukumiwa kwa kumchafua Zitto kwenye mitandao na sio kwa kuwa na mikakati ya siri. Ben alipewa adhabu ya kutokugombea uongozi kwa mwaka mmoja, mwaka ambao hakuna uchaguzi wowote ndani ya chama.

Je, uhalali wa Ben Saanane kufanya kazi ya upelelezi wa viongozi bila Kamati Kuu kujua inatoka wapi?

Je, Ben Saanane alikuwa anapeleka ripoti yake ya upelelezi kwa nani?

Ben Saanane alipata wapi fursa ya kuaminiwa zaidi kuliko wajumbe wa Kamati Kuu? What special did he or does he offer?

Haya ndio mambo yanyoleta mgogoro.

Ben sio kiongozi hata wa ngazi ya tawi lakini anachokisema kinapewa imani kubwa kuliko viongozi wa kamati kuu ya chama taifa. Why?

Katika mazingira kama haya, kuamini kwamba unaweza kufuata nyia za uwazi kuutoa uongozi madarakani kidemokrasia ni kujidanganya kulikopindukia. Uamuzi wa Kitila wa kuandaa mkakati wa siri ni sahihi na ulilenga kukinusuru chama na kukipa chama sura ya chama cha siasa kinachotaka kuongoza nchi.

Soma waraka pale unaposema kwamba "Mida Eight" yaani Ben Saanane anatumiwa na Dr. Slaa kwa kazi ya uspy na fitina mitandaoni. Hili linajulikana lakini hakuna hatua yoyote inayochukuliwa!!!

Vilevile nadhani unakumbuka Josephine Mushumbusi alivyokuwa anazunguka mikoani kutengeneza mtandao wa Dr. Slaa. Hili lilimalizwa kwa kumwambia Dr. Slaa aache kumtumia Josephine kwa shughuli hiyo, lakini Slaa hajapewa adhabu yoyote.

Yaani ni bayana kuwa ndani ya Chadema kuna misaafu ya aina mbili ya kutoa hukumu kutegemeana na nani anayeshutumiwa. Kitila was right.
Nianze ulipomaliza, Kitila was not right, amekubali haikuwa sahihi na ameomba radhi.
Kiongozi anayeomba radhi kwa kile anachodhani ni sahihi huyo si kiongozi kwa maana ya kiongozi.

Nelson Mandela alipotoka jela vijana wa Umkhonto Wesizwe waliumuomba awape silaha ili walipize kisasi.
Mandela aliwaambi silaha hawatatoa kwasababu hilo si lengo la kupinga ubaguzi, kama vijana wanadhani atakuwa amewasaliti yupo radhi kurejea magereza au kutoongoza ANC.
Huyu ndiye kiongozi anayesimamia kile anachokiona ni sahihi.

Pili, tumesema mara nyingi sana kuwa kuunda mkakati ni sehemu ya siasa, kuunda ushindani ni afya kwa chama. Lakini basi hayo yafanyike kwa kushindinisha sera bila kuwagawa wanachama katika misingi ya chuki, fitna n.k

Waraka siyo tatizo, tatizo ni maudhui, kauli, na kilichomo ndani ya waraka.
Hauna sura ya kujenga CDM unasura ya kuleta mapinduzi.

Hakuna tatizo kama Kitila na Zitto wangejiuzulu nyadhifa zao na kuomba wanachama uchaguzi uutishwe.
Lakini hili la kusema 'ukimtupia kombora hawezi kujibu' kisha Zitto akatumia nafasi ya PAC kuchomeka mambo yake akiaminisha ni ya kitaifa' ni ulaghai wa kiwango cha kimataifa. Ni dharau kwetu wananchi na taifa.

Wakati huo huo zitto anatumia Public office kulaani mabilioni ya Uswiss kwa kutumia ofisi za umma.
Na wakati huo huo anatumia ofisi ya umma kutafuta masilahi yake kama ambavyo akina Cheng walivyotumia ofisi hizo kuweka mapesa Uswiss. Hapa fisi ni yupi na mwanakondoo ni yupi.

Kuhusu kukinusuru chama hilo sidhani kama lilikuwa lengo lao.
Hawa watu wanaondaa mkakati wa kubomoa chama kwanza sijui walikuwa na nia ya kujenga kingine, sijui!

Ninachoweza kusema ni kuwa huo mkakati umemuonya Zitto kufanya mambo 'kama ya mapenzi kwa siri'
Hapo taswira ya chama inakuaje? Kwamba kuna wakati mapenzi ni haramu na wakati ni halali kwa kumlinganisha na mpinzani wao.

Pili, ukisoma waraka hakuna mahali waliposema wachague viongozi wa kukinusuru chama.
Mada yote ilikuwa kumchagua Zitto kwa njia za siri halafu kuleta mapinduzi.

Sina tatizo na mapinduzi kama ndio utamaduni wao, hata Mrema aliwahi kupigwa ngwara.
Tatizo ni kuwa hiki si chama cha kidemokrasia, sasa demokrasia gani wanataka kuleta huku wao wakiwa na falsafa za Smauel Doe, Bokasa, Amin, Yahaya Jamey n.k.!!

Tatizo si u-spy, tatizo ni maudhui yaliyokamatwa kwa u-spy. Nakubali hakuna timu isiyokuwa na u-spy hiyo ni sehemu ya research and development . Hilo silo tunalojadili, hapa unaungalia waraka wa kihaini kwa undani kabisa ili tujiridhishe kama hawa mabwana wana nia njema na taifa hili.

Katika kulijadili mada kama ilivyoletwa, mimi naanza kwa kukiri kwamba kwa muda mfupi nilikuwa mpenzi mkubwa wa Mh. Zitto lakini kwa muda mfupi sana. Kwa nini ilikuwa hivyo? Naanza kwa kuthubutu kusema kuwa waraka kama ulivyotolewa naamini ni muendelezo tu katika kufanikisha malengo maalum yaliyoandaliwa toka awali na kwa muda mrefu.

Hata hivyo mambo yameweza kufikia yalipofikiwa kwa sababu moja tu; udhaifu wa uongozi wa Chadema kusita kuchukua hatua mapema dhidi ya vitendo vya utovu wa nidhamu ambavyo dalili zake zilianza kuonekana tangu mapema sana. Nawaachia wasomaji wenyewe waamue kufuatia mtiririko wa matukio kama nitakavyoyaorodhesha hapa chini.

Septemba 2007 said:
Baada ya kuibua kashfa ya mkataba wa Buzwagi, Mh. Zitto aliibuka kuwa mbunge mashuhuri zaidi kuliko wengine. Kashfa hiyo, ilisababisha asimamishwe ubunge na aliyekuwa Spika wa wakati huo, Samwel Sitta. Hata hivyo bila kutafakari kwa kina Mh. Zitto yaonekana akaamini anaungwa mkono kwa sababu ya ushawishi wake binafsi.

Mara Mh. Zitto, kama vile anapima uzito wake kisiasa kwa Watanzania, aliibuka na hoja kwamba kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, hakuwa na uhakika wa jimbo gani angegombea kati ya matano aliyotangaza; majimbo hayo ni Kigoma Magharibi, Kigoma Mashariki, Kahama, Geita na Ubungo Dar es Salaam.
Hii tabia ya Mh.Zitto kukurupuka ilimfadhaisha hata na Dr. Kitila Mkumbo mwenyewe kama alivyonukuliwa humu jamvini JF na kumfananisha Mh. Zitto na Lyatonga Agostino Mrema!
Kitila Mkumbo said:
Well, inawezekana nje ya CHADEMA inaonekana hivyo kwamba chama ni personalities za watu. Of course, yes in politics, you cannot dissociate personalities and a party but this is far from saying that the absence of one popular individual would mean the end of the road. No way.

Ndio maana umeona kuna watu wanampinga ndani ya chama. Ina maana Zitto angekuwa kama Mrema enzi zile za NCCR hakuna mtu angethubutu kunyanyua mdomo against him.
Mara Dr. Slaa akatangaza orodha ya mafisadi Mwembeyanga na kuteka nyoyo za wanamageuzi walio wengi na habari za Buzwagi kuanza kuchukua nafasi ya pili. Kuona hivyo Mh. Zitto hakukubali kuachwa nyuma...
Novemba 2008 said:
Mh. Zitto atangaza kutogombea Ubunge mwaka 2010, "mpango wangu ni kutogombea Ubunge tena mwaka 2010 ili niweze kusoma na kupata PhD niweze kuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu. Ninapenda zaidi kufundisha kuliko siasa.

Kuna shinikizo kubwa nigombee tena lakini nafsi yangu ni nzito sana kurudi bungeni Bunge la 10. Nadhani nitafurahi zaidi nikiongoza chama changu kupata wabunge wengi zaidi na mimi nikae nje ya siasa kwa muda kidogo. Niliweka nia yangu hii kutoka mwaka 2006 lakini watu hawataki kulielewa hili"

Ghafla bin vuu, Mh. Zitto huyo kaamua kugombea Ubunge mwaka 2010!
Juni 2010 said:
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe alishangaza wengi pale alipochukua fomu za kugombea ubunge kupitia jimbo hilo ambalo kwa sasa ndiye anayeliongoza. Zitto alichukua fomu hizo katika Mkutano wa hadhara jana uliofanyika kijijini Mwandiga Kigoma Vijijini kisha Mh. Zito Kabwe CHADEMA akahutubia wakazi wa kijiji hicho.
Ni kweli aligombea na akashinda lakini hata mwezi haukupita tayari akaibua mengine baada ya kuwasaliti Wabunge wenzake walioamua kususia hotuba ya Kikwete bungeni...akazua mengine akidai kuna mbinu za kummaliza!
Desemba 2010 said:
KADRI siku zinavyozidi kusogea mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe yuko kwenye wimbi la wasiwasi wa kuuliwa kutokana na kupata ujumbe mfupi wa maneno wa simu ulioashiria kutishiwa uhai wake.

Imedaiwa kuwa, baadhi ya viongozi wa chama hicho wanaandaa mkakati wa kummaliza Zitto ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho kwa kile kinachodaiwa ni kukisaliti chama.

Awali kabla ya migogoro ndani ya chamda hicho, Wabunge wa CHADEMA walitia mgomo bungeni na kutoka nje ya ukumbi wa bunge kwa kudai kuwa hawamtambui Rais Jakaya Kikwete na kususia hotuba zake na badhi ya shughuli za serikali hiyo.
Wakati chama chake kinaendesha kampeni kikijiandaa kwa uchaguzi Arumeru mara kajitokeza Mh. Zitto na kama kawaida katoa nyingine kali!
September 2012 said:
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema hana mpango wa kugombea ubunge mwaka 2015 badala yake anajipanga kuwania urais kupitia chama chake cha Chadema.

“Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha. Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola,” alisema Zitto.
Akaamua kuwaaga wapiga kura wake wa Kigoma kwa mara ya pili!
Februari 2013 said:
Mh. Zitto amewaaga wapiga kura wake wa Kigoma Kaskazini kwa kutangaza rasmi kutowania tena nafasi ya ubunge kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2015.

“Ninachokifanya ndugu zangu ninaomba mjiandae kisaikolojia katika hili, ninatamka wazi kuwa mwaka 2015 sitagombea ubunge tena katika jimbo letu hili la Kigoma Kaskazini na lengo la kufanya hivi ni kutoa fursa kwa watu wengine kutoka ndani ya Chadema nao waonyeshe uwezo wao wa kuwahudumia wananchi", asema Mh. Zitto.
Wakati bado wananchi wamepigwa butwaa, akatokea naye mama mzazi wa Zitto...majambazi yamenivamia!
Aprili 2013 said:
SHIDA Salum ambaye ni mama mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ameuambia mtandao huu leo kuwa hana mpango wa kugombea ubunge katika jimbo lolote nchini. Alisema hayo wakati akisimulia kuhusu taarifa ya kuvamiwa kwake na majambazi kama ilivyotolewa na Gazeti la Uwazi.

“Mimi ni mwanachama wa Chadema nitabaki kuwa mwanachama lakini sitagombea ubunge. Nitaendelea kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Taifa (Chawata),” alisema Shida.
Kama hiyo haitoshi Mh. Zitto akamua historia ni lazima itimie, lazima ijirudie!
August 2013 said:
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), amesema hafikirii kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho wala ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015. Alisema mwaka 2015, ndio mwaka wa mwisho kujihusisha na siasa ambapo dhamira yake ni kutafuta chuo ambacho ataweza kufundisha masomo ya uchumi na maliasili.

"Hiki ni kipindi cha mwisho kwangu kujihusisha na siasa kwani nimechoka nazo, nitatafuta chuo nikafundishe na kama nitakosa ni bora nikalime michikichi... sihitaji urais," alisema.
Yale yalee! Mara ngapi tumesikia hadithi hii? Si mara moja ama mbili! Huyo ndiye Mh. Zitto Kabwe, Mbunge na Raisi mtarajiwa na hivi sasa kafungua mashtaka polisi akidai katishiwa maisha yake na tayari polisi wanafanya uchunguzi.

Wana JF, hapa mimi natoa taarifa mapema kwamba kutokana na mtiririko huu, Mh. Zitto sina imani naye na naamini Chadema wamechelewa sana kuchukua hatua waliochukua; hata hivyo nawapongeza kwa kuthubutu. Nimesita sana kuchangia hii mada kwa sababu humu JF mimi ni moja katika watu wasoweza kuficha msimamo wao katika swala lolote lile, sina unafiki na siko tayari kuita koleo kijiko. Huu ni mchango pekee nitakaoutoa kwenye huu mjadala na naomba radhi kwa yeyote atakayekwazwa na msimamo wangu huo. Nitabaki msomaji tuu...mjadala mwema.
 
Katika kulijadili mada kama ilivyoletwa, mimi naanza kwa kukiri kwamba kwa muda mfupi nilikuwa mpenzi mkubwa wa Mh. Zitto lakini kwa muda mfupi sana. Kwa nini ilikuwa hivyo? Naanza kwa kuthubutu kusema kuwa waraka kama ulivyotolewa naamini ni muendelezo tu katika kufanikisha malengo maalum yaliyoandaliwa toka awali na kwa muda mrefu.

Hata hivyo mambo yameweza kufikia yalipofikiwa kwa sababu moja tu; udhaifu wa uongozi wa Chadema kusita kuchukua hatua mapema dhidi ya vitendo vya utovu wa nidhamu ambavyo dalili zake zilianza kuonekana tangu mapema sana. Nawaachia wasomaji wenyewe waamue kufuatia mtiririko wa matukio kama nitakavyoyaorodhesha hapa chini.

Hii tabia ya Mh.Zitto kukurupuka ilimfadhaisha hata na Dr. Kitila Mkumbo mwenyewe kama alivyonukuliwa humu jamvini JF na kumfananisha Mh. Zitto na Lyatonga Agostino Mrema!

Mara Dr. Slaa akatangaza orodha ya mafisadi Mwembeyanga na kuteka nyoyo za wanamageuzi walio wengi na habari za Buzwagi kuanza kuchukua nafasi ya pili. Kuona hivyo Mh. Zitto hakukubali kuachwa nyuma...

Ghafla bin vuu, Mh. Zitto huyo kaamua kugombea Ubunge mwaka 2010!

Ni kweli aligombea na akashinda lakini hata mwezi haukupita tayari akaibua mengine baada ya kuwasaliti Wabunge wenzake walioamua kususia hotuba ya Kikwete bungeni...akazua mengine akidai kuna mbinu za kummaliza!

Wakati chama chake kinaendesha kampeni kikijiandaa kwa uchaguzi Arumeru mara kajitokeza Mh. Zitto na kama kawaida katoa nyingine kali!

Akaamua kuwaaga wapiga kura wake wa Kigoma kwa mara ya pili!

Wakati bado wananchi wamepigwa butwaa, akatokea naye mama mzazi wa Zitto...majambazi yamenivamia!

Kama hiyo haitoshi Mh. Zitto akamua historia ni lazima itimie, lazima ijirudie!

Yale yalee! Mara ngapi tumesikia hadithi hii? Si mara moja ama mbili! Huyo ndiye Mh. Zitto Kabwe, Mbunge na Raisi mtarajiwa na hivi sasa kafungua mashtaka polisi akidai katishiwa maisha yake na tayari polisi wanafanya uchunguzi.

Wana JF, hapa mimi natoa taarifa mapema kwamba kutokana na mtiririko huu, Mh. Zitto sina imani naye na naamini Chadema wamechelewa sana kuchukua hatua waliochukua; hata hivyo nawapongeza kwa kuthubutu. Nimesita sana kuchangia hii mada kwa sababu humu JF mimi ni moja katika watu wasoweza kuficha msimamo wao katika swala lolote lile, sina unafiki na siko tayari kuita koleo kijiko. Huu ni mchango pekee nitakaoutoa kwenye huu mjadala na naomba radhi kwa yeyote atakayekwazwa na msimamo wangu huo. Nitabaki msomaji tuu...mjadala mwema.

Mag3:

Pamoja na elimu yangu ndogo, nimesoma posti yako na sioni utovu wa nidhamu wa Zitto. Hajavunja katiba ya CDM au ya nchi. Vilevile hajavunja sheria ya nchi. Hivyo kulikuwa hakuna sababu yoyote ya kumchukulia hatua wakati alitumia uhuru wake wa kikatiba.

CDM ina utaratibu wa kumpata mgombeaji wa urais na viti vingine. Katika kipindi cha sasa CDM itoe ruhusa ya watu kusema nia zao. Utakapofika wakati wa uchaguzi wanaotaka watachukua fomu na utaratibu utafuatwa.
 
Nafahamu si rahisi kuongelea jambo bila kuongelea CCM mtu akaeleweka. Waraka ni wa CDM na mada imeeleza wazi toka mwanz kuwa tuutendee haki.

Nitakuwa kama wale mashabiki wa CDM wanaodhani kuwa mchawi wao ni CCM peke yake. Nimeandika katika bandiko kuwa CCM wanachokifanya ni sahihi kwasababu
1. Hawana sera nyingine za kuushawishi umma kwanini miaka 50 tu masikini
2. Wanataka kubaki madarakani na mbinu mojawapo ni kuondoa vikwazo.

Ninachokionyesha kwa maoni yangu ni jinsi gani mzozo wa CDM ulianza, ukalelewa na kfika ulipo.
Na muhimu zaidi ni kuweka sawa suala hili ambalo limepoteza mwelekeo kwa nyuzi za kumtuhumu Mtei, kumtetea Zitto bila mashiko, kutafuta mchawi CCM hata kama genge la wachawi lipo ndani ya CDM yenyewe.

Katika kufanya hivyo kunatokea mambo mawili
1. Kwakosoa CDM kama tulivyowahi kuikosoa CCM kuhusu mambo mengi sana
2. Kuangalia mustakabali wa taifa kwa kutokuwa na upinzani imara. Matokeo ya hili yana impact katika taifa
a) NCCR ilipomeguka CCM wakabaki wenyewe bungeni, serikali na kwingineko. Ndilo chanzo cha Kagoda,meremeta .k.
b)CUF ilipoingia Nyongo kukabaki ombwe la upinzani, tukano ung'oaji reli kama chuma chakavu, Jersy, BoT, Uswiss n.k.
c) Kuyumba kwa CDM, tunaona katiba ya CCM ikiandaliwa na makando kando mengine mengi sana.

Ndipo ninapokubaliana na Mchambuzi kuwa bila Upinzani imara hakuna CCM imara wala serikali imara.
Yes kama wanakoselewa ili wajirekebishe hilo ni sawa na sijui tatizo ni kitu gani.
Tulishawahi kuwakosoa CCM wajirerekebishe lakini ni sikio la kufa halisikii dawa, sasa hili linaloanza maumivu tuliache tu hata kujaribu dawa?

Lakini dhidi ya yote wengine tunataka viongozi waadilifu,waaminifu, wakweli na wenye kuaminiwa.
CCM wameridhika kuwa Chenge anaweza kuwatengenezea bajeti, magamba ni sehemu yao na wanaweza kuishi nayo salama salimin. Hatuna namna ya kuwasaidia ila kuwatakia kheri kama hiyo ndio njia waliyoamua kuwafuata UNIP na KANU mapunzikoni.

Hawa waliokuja na kujenga matumaini tunaona ni wanafiki wakubwa.
Kwa mfano, Zitto aliposema hesabu za vyama zikaguliwe kila mmoja alimuona mzalendo na mwenye uchungu.

Walimuona huyu anafaa kupewa uongozi hata wa nchi.
Ni mkweli, mwadilifu na mwaminifu kwa kile anachokisema.
Guess what, deadly wrong! soma hapa maoni ya waraka uliomkabidhi kadhi

''Hoja ya uongozi uliopo kushindwa kabisa kusoma taarifa za fedha tokea 2010 ikifahamika kwa wapiga kura inaweza kuwa machinjio kabisa ya uongozi uliopo na kumpa fursa kubwa tunayemtaka''

Hivi tutaendelea kuwa taifa na watu kama hawa hadi lini?
Huyu anayeweza kuughilibu umma ili apande ngazi akifika huko juu itakuwaje.
Kama ndivyo tunawalumu CCM kwa lipi?

Halafu huyu Zitto mtaalam wa spinning anakuja na kusema tatizo ni kutoa kauli ya ukaguzi wa fedha ndicho kimemuondoa madarakani. Sasa tunajua alikuwa na haki ya kufanya hivyo kama mwenyekiti wa PAC lakini nia na dhamira yake haikuwa kama inavyoonekana, alikuwa anatafuta mahali pa kupandia ngazi tena kwa mapinduzi
.

Nisichoafiki ni kunyoosha CCM vidole na kuvkunja kunapokuwepo na akina 'Chenge' upande mwingine.
Tuwe wakweli na tusimame katika ukweli, spade ni spade tu siyo kijiko kikubwa. Let us take'em on equ
ally

Nguruv3;

Yalipotokea matatizo ya EPA, Richmond, etc watanzania walitakiwa kufanya vile walivyofanya watu wa Tunisia. Wangeandamana na kuishinikiza serikali kujitoa madarakani au kuleta mabadiliko. Kilichofanyika ni kuipa nguvu cha CDM na kusubiri uchaguzi. That was a mistake.

Kwa sasa hivi watanzania wasubiri katiba. Katiba mpya ikitoa nafasi kwa wagombea huru, watanzania wataanza upya bila CDM au CCM.
 
Kwa vile muundo wa sasa umeshagubikwa na makundi, katika uchaguzi ujao, CHADEMA itafute viongozi wa nje kabisa ambao wana uwezo wa kuongoza lakini hawajahi kuwa viongozi wakubwa ndani ya chama. Hawa watu neutral ndio watakonusuru chama chao. Nadhani mtu kama Mnyika (kijana mwenye akili sana ya kujenga hoja), Lissu (mwanasheria anayejua sana kutetea hoja zake), ni baadhi tu ya majina ambayo nayaona kuwa yanaweza kuwa na nafasi nzuri sana kuingoza chadema bila makundi. Most likely wapo wengine ambao hawavumi lakini wanaweza. Chadema iwatafute hao ambao hawavumi lakini wanaweza.

SWOT Analysis aliyotoa Kitila inaonyesha kuwa wote; yaani yeye mwenyewe Kitila, Zitto, Slaa, na Mbowe wana matatizo ya kuongoza kutokana na hali ilivyo hata kama wana vipaji na elimu za juu. After-all kutumia elimu kama kipimo cha uongozi na udhaifu mkubwa sana kwenye hiyo single sided SWOT analysis.

Kitu kingine ni kuhusu nafasi ya wazee ndani ya CHADEMA. Kama hamtaki ushauri wao kwa vile ni wachagga, ni afadhali mziondoe nafasi zao kwenye katiba kuliko kuwa nazo lakini hamtaki kuziheshimu.
 
Mag3:

Pamoja na elimu yangu ndogo, nimesoma posti yako na sioni utovu wa nidhamu wa Zitto. Hajavunja katiba ya CDM au ya nchi. Vilevile hajavunja sheria ya nchi. Hivyo kulikuwa hakuna sababu yoyote ya kumchukulia hatua wakati alitumia uhuru wake wa kikatiba.

CDM ina utaratibu wa kumpata mgombeaji wa urais na viti vingine. Katika kipindi cha sasa CDM itoe ruhusa ya watu kusema nia zao. Utakapofika wakati wa uchaguzi wanaotaka watachukua fomu na utaratibu utafuatwa.
Mkuu Zakumi , kumbuka jambo lililopelekea Zitto kuchukuliwa hatua si moja, yapo 11 kwa mujibu wa Mnyika.
Ni mmapema mno kusema alichukuliwa hatua kwa waraka tu.

Pili,zito hajavunja sheria yoyote ya nchi. Katika chama Zitto amekiuka miiko ya uongozi ambayo ni uwajibikaji wa pamoja
Zitto aliingia katika vikao vyote vya chama lakini amejitoa katika maamuzi aliyokuwa mshirika kama waraka ulivyogusia.

Zitto akiwa mtendaji mkuu msaidizi ameshindwa kuisaidia CDM na badala yake ametumia mwanya huo si kuweka ukweli bali kama silaha ya kukishambulia chama ambacho yeye ni kiongozi.

Waraka umeonyesha kuwa kombora la matumizi ya fedha litawamaliza CDM na yeye alifanya hivyo.
Kwa umma hilo ni sahihi ingawa pia motive behind ni mbaya kwasababu halikudhaniria kuusadia umma bali yeye.
Kichama ni kujiondoa katika uwajibikaji, kutumia nafasi hiyo pengine kukihujumu chama katika mambo aliyoweza kusaidia

Zitto hajatumia uhuru wa katiba ya nchi au ya CDM kueleza alichikusudia.
1. Hakuna kumbu kumbu kwamba aliwahi kuleta madai kama hayo.
Zipo kumbu kumbu za kutosha kuhusu madai yake yakiwa katika mitandao kwa kupitia watu wengine.

2. Alipaswa kutumia uhuru wake kujiuzulu ili aweze kuongea kama mwanachama asiyeridhishwa na maendeleo.
Zitto hakufanya hivyo.

3. Kwa kushindwa kutumia uhuru wake kama 1 na 2 hapo juu, Zitto ameshiriki kikamilifu katika kuandaa makundi yaliyotishia uhai wa CDM.
i) Ametajwa katika sakata la Masalia 7 tena na ID yake. Kwanini asitumie uhuru wake hadi ajifiche katika ID
2) Ametajwa katika mzozo wa Kafulila kikamilifu
3)Ameshiriki katika mzozo wa waraka, kikamilifu

Hayo ni baadhi tu ya yale aliyoyasababisha akiwa kiongozi mwenye dhamana ya CDM.
Sijui kwa hayo kunahitajika nini kubaini kuwa alichokifanya ni utovu wa nidhamu.

Hebu tuangalie kwa uchache sana sana, watu wanavyotumia uhuru wao kikatiba
- Seneta Liebaman alimuunga mkono John Mcain na kuamua kuwa mgombea binafsi nje ya chama cha Democrat
- Seneta Mcain amepinga uwepo wa tea party kwasababu Republican wanahitaji kuwa moderate kwa maoni yake
- Secretary Collin Powell alijiuzulu kwasababu hakukubaliana na sera mbaya za vita za akina Dickey Chen
-Collin Powell alimuunga mkono Obama hadharani akiwa Republican.
- John Major alimpinga Thatcher hadharani na akafanya kampeni ya kumuondoa hadharani
- Linda Choker alimpinga Blair ndani ya house of common hadharani na kujiuzulu
- Godon Brown alimpinga Blair na kuendesha kampeni ya kumuondoa kupitia chama chake
- Malema alipinga sera za ANC hadharani kuhusu wafanyakazi, kilichomuondoa ni mtamshi ya ubaguzi.
-Zitto Kabwe alipinga msimamo wa wabunge wa CDM kuhusu JK bungeni. Hakuchukuliwa hatu kwa uamuzi huru
- Kigwangalla amempinga spika wa CCM hadharani , hajachukuliwa hatua. Pengine amewekwa kiporo! sina uhakika
-Kitila alipinga Juliana Shonzo kufukuzwa. hakuchukuliwa hatua kwasababu yalikuwa maoni huru
- Sumaye anaipinga CCM hadharani na anaendelea, hajachukuliwa hatua kwa maoni yake

Ni mifano rahisi michache sana, orodha inaweza kufika kurasa 99.75

Ukiangalia, uhuru unatumika hadharani, kuchochea vurugu si uhuru. Uhuru wa kusema haukupi uhuru wa kwenda kupiga gita mwaisela au Sewahaji. Uhuru una limitations, una ethics na una boundaries.

Kama Zitto anaona hana uhuru kwanini asitafute eneo atakalokuwa huru?
Kwani ni lazima apate uhuru kule anakoamini hakuna uhuru. Kufanya hivyo ni kujinyima uhuru kabla hajanyimwa uhuru.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu zangu nawapigia hodi humu kunyumba..

Hili swala nadhani tunalijadili vibaya sana maana kama kweli sababu ya hawa viongozi kunyang'anywa madaraka ni huu waraka basi ni vizuri sana tuuzungumzie WARAKA badala ya kurudi nyuma na kutazama maisha ya mtu yasohusika. Swala hapa ni waraka huu, tuhuma zake na kashfa zake. Je, unapousoma unakupa picha gani na hata kama hatukubaliani nadhani ni vizuri kila mmoja wetu azungumzie kile kilichomfanya akubaliane na hukumu ama kutokubaliana.

Kwanza kabisa mimi nimeusoma na sehemu hizi ndizo zilizonivuruga kabisa na zinahitaji majibu kwani kuwaadhibu Zitto na Kitila haiwezi kukisaidia chama hata kidogo isipokuwa kuwasaidia baadhi ya watu kuendeleza kile kinachodaiwa. Kinachonishinda mimi zaidi kuelewa ni hizi shutuma ambazo zimewekwa kwa uongozi uliopo na maajabu Zitto kama naibu katibu wa Chama inaonyesha hayumo ktk maamuzi yoyote isipokuwa kundi la watu watatu.. Nawaomba sana mjiulize haya! Inakuwaje watu hapa JF wanamlaumu Zitto ikiwa huyu Zitto hakushirikishwa ktk maamuzi makubwa kama haya ili hizi lawama zote kuhusu Uongozi wa Chadema na yeye awe mmoja wao?... Inakuwaje Zitto alitengwa tuache wajumbe wengine nje kwanza! Mkuu wangu Nguruvi3 kama unayo majibu nayaomba uyaanike hapa. Tuanze na tuhuma hizo, huu waraka unasema nini kuhusu uongozi uliopo..

1. Ni kwa msingi huo waliamua kuandika kabisa katika mwongozo wetu kwamba kiongozi yeyote katika ngazi yoyote ya kuchaguliwa atakapogombea na kushinda ataongoza kwa kipindi kimoja cha miaka mitano na kisha ataweza kugombea na kuongoza kwa kipindi cha pili cha miaka mitano baada yapo hawezi kugombea tena katika nafasi ile ile aliyoitumikia kwa vipindi viwili).
Je, kuna ukweli ktk swala hili maana sidhani kama kina Kitila amelizua tu, na kama sikosei Mnyika aliwahi kulikana ktk mitandano hata kabla ya huu waraka haijatoka. Kama kipengele hiki kiliondolewa kinyemela lengo lake lilikuwa nini? na kwa bahati mbaya sana majibu yote tunayapata against ni viongozi waliopo madarakani sasa hivi na hii inaweza kuwa ktk kutetea nafasi zao pasipo kujua. Kwa nini hakuna mjumbe nje ya uongozi anayeweza kusema ukweli kuhusu kipengele hiki kama kilikuwepo na kikaondolea.
2. Mfano mwaka 2008 uongozi ulianzisha mkakati wa operesheni samaki mkubwa (maarufu kama Oparesheni Sangara).
Huo ulifanyiwa kazi katika mikoa kadhaa na hatimaye ikafa kimya kimya. Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kulianzishwa matembezi ya maandamano ambayo nayo yalikuwa yakipeleka ujumbe kwa watu na yalipangwa kufanyika mikoa yote na wilaya zote.

Kumbukumbu zetu zinaonyesha kwamba yalikuwa yakianzia makao makuu ya mkoa na kwenda kwenye wilaya zote.
Lakini kumbukumbu hizo zinaonyesha kwamba yalifanyika Mwanza, Musoma, Shinyanga, Kagera na mikoa ya Nyanda za Juu kusini (Mbeya, Iringa, Njombe na Rukwa) kisha nayo yakafa kifo cha mende.

Kisha mwaka 2012 ikaanzishwa operation ya mabadiliko maarufu kama Movement for Change (M4C).
Hiyo ilikuwa inakwenda kwenye mikoa na timu kama nne hivi ambazo kwa ujumla zilitathmini hali ya mtandao na uongozi wa taasisi, kuhamasisha umma kwa njia ya mikutano ya hadhara, kuingiza wanachama na kusimika uongozi na hatimaye kufanya mafunzo kwa viongozi.

Hiyo ikafanyika Mtwara na Lindi, Morogoro na kisha ikaenda kufia Iringa. Mwaka huu viongozi wetu wamekuja na ugatuaji madaraka kutoka makao makuu ya taasisi na kupeleka madaraka kwenye kanda mbalimbali.

Mkakati huu ulikufa kabla ya kuanza pale viongozi wakuu walipobadilisha maazimio ya kikao kikuu na kutekeleza matakwa yao ikiwa ni pamoja na kuleta suala la viongozi wa muda kwa muda mrefu badala ya kuajiri maofisa na wakahakikisha wanaweka watu wao kwenye uongozi wa muda.

Katika hili uongozi uliopo unaweza kutupa jibu ama kukana yalotokea na maamuzi hayakufanywa na wao pekee pasipo kuwajumuisha viongozi wengine.

3. Performance yetu kwenye chaguzi ndogo nayo ni ishara kwamba mabadiliko yanahitajika.
Tangu uongozi huu uingie madarakani, kumefanyika chaguzi ndogo 8 za wawakilishi kwenye chombo kikuu, kati ya hizo tumeshinda 2 tu sawa na asilimia 25. Aidha baada ya mwaka 2010 kumefanyika chaguzi kadhaa za wawakilishi kwenye halmashauri. Mwezi Oktoba 2011, mwezi wa4 2012, mwezi Septemba 2012 na mwezi Juni 2013. Kote performance yetu imekuwa poor kupindukia. Mfano mwezi wa Juni 2013 tumepata viti 6 kati ya 22 (27%) na mwezi Septemba 2012 tulipata viti 7 kati ya 29 (24%).
Hizi takwimu hazikuundwa ni takwimu ambazo pekee nadhani hata sisi tunazijua japo wakati wote wa chaguzi hizi Chadema ilikuwa juu ya CCM ktk mapendekezo. Je, ni kweli tulishindwa kihalali na uongozi wa Chadema umegundua sababu zipi zilizowakosesha ushindi. Na ukizisoma vizuri hizi takwimu utaona kwamba Chadema inazidi kudidimia ktk ushindi na sidhani kama uongozi uliopo wanajua sababu zaidi ya kuendeleza yale yale yalowakosesha ushindi toka mwaka 2010. Tupeni sababu na kwa nini uongozi uliopo haukubali kupwaya!

4. Matumizi ya fedha za taasisi.
Hakuna mtu anayejua hivi sasa fedha za chama zinatumikaje zaidi ya kakikundi ka watu watatu yaani mkuu kabisa, mtendaji mkuu na mkuu wa fedha kwenye taasisi yetu. Maamuzi ya vikao hayaheshimiki tena na mabwana hawa.

Baada ya uchaguzi wa 2010 vikao halali vilielekeza kiasi na aina ya fedha ambazo hazitaguswa bali zitunzwe kwenye akaunti maalum kwa ajili ya uchaguzi wa 2015. Lakini leo si tu akaunti hiyo haina fedha bali hakuna akaunti yoyote yenye fedha.

Watu watatu ndo wanaamua fedha zitumikeje. Mfano mwingine ni maamuzi ya kikao cha juu mno cha hivi karibuni kilichoamua kwamba kiasi cha fedha inayotoka serikalini kipelekwe kwenye mikoa na wilaya na kiasi kingine kipelekwe kwenye kanda.

Leo ni mwezi wa tano maamuzi hayo hayajatekelezwa.
Lakini kuna michango ya watu binafsi kama yule mtanzania mwenye asili ya kihindi, hizo nazo hazijulikani zimechukuliwa lini kwa mfumo gani, zikatunzwa wapi na hatimaye zimetumikaje. Hapo hatujataja fedha zinazopatikana kutoka kwenye fundraising events mbalimbali kama ile ya Dar es salaam na Mwanza. Hizo nazo hazijawahi kuonekana na walioendesha hizo fundraising, uaminifu wao kwenye masuala ya fedha ni questionable.

Taarifa za fedha. Tokea baada ya uchaguzi wa 2010 mpaka leo, hakuna kikao chochote kilichowahi kupokea na kujadili hadi mwisho ripoti ya mapato na matumizi ya fedha za taasisi. Kila kikao agenda hiyo inarushwa kiaina.

Wanaojua mchezo huo ni watu watatu tu tuliowataja hapo juu na malengo ya kurusha hiyo agenda kila wakati na kukwepesha isijadiliwe pia wanayajua wao.
- Taarifa za fedha. Tokea baada ya uchaguzi wa 2010 mpaka leo, hakuna kikao chochote kilichowahi kupokea na kujadili hadi mwisho ripoti ya mapato na matumizi ya fedha za taasisi. Kila kikao agenda hiyo inarushwa kiaina.

Swala hili ni zito sana kuliko mengine yote. Binafsi yangu sijawahi kuona wala kusikia taasisi yoyote inayoweza kutumia fedha za wananchi pasipo kufanya kikao kila mwaka kuonyesha report ya mapato na matumizi! sijawahi. Ebu tufikirie tu kwamba mwaka mmoja upite pasipo waziri wa fedha kuja bungeni kuzungumzia bajeti ijayo pasipo kuonyesha mapato na matumizi ya mwaka ulopita. Hiyo bajeti kweli itakuwa bajeti ama vumbi la macho?.

5. Njia haramu za kubaki madarakani!

Kipengele hiki ndicho kilichonifanya mimi niamini kwa nini kundi hili walifanya Usiri ktk jambo hili. Na ukiweza kusoma kwa makini kipengele hiki utaogopa hata kunywa maji, yaani inatisha kuona viongozi ndani ya ndani ya chama wameweza kuandaa mazingira haya. Ni rahisi sana kulaumu nje lakini kama kweli haya ndio mazingira wanayofanya kazi kina Zitto sijui kama kuna mmoja wetu humu angeweza stahimili akiwa nje ya kundi hili..

Binafsi yangu kinachoniaminisha zaidi kuhusu waraka huu ni ktk kuelewa kwamba Zitto ndiye kiongozi pekee ktk uongozi wa juu wa Chadema mwenye shahada ya Uchumi, lakini hashirikishwi ktk mipango yoyote ya fedha wala mikakati ya chama inayohusu matumizi ya fedha. jamani, huyu ni NAIBU KATIBU MKUU wa chama inakuwaje tunamuuliza kwa nini asishirikiane na wenzake ilihali ni yeye alotengwa?..Ikiwa toka mwaka 2010, haya yote yaloandikwa ktk waraka huu yanamweka Zitto nje ya uongozi uliopo tunashindwa vipi kujiuliza maswali magumu kama vile kwa nini imetiokea hivyo?

Jamani hizi lawama za makao makuu zimezidi sana, Na wala si Zitto aloandika waraka huu isipokuwa Kitila na wenzake ambao wanaonyesha kuchoshwa na mfumo uliopo. Binafsi yangu sijui ningefanya nini tofauti kama ningekuwa nafasi ya Zitto ama Kitila. Ila tu kwa kuongezea ni kwamba najua fika Zitto hakuaminiwa kutokana na mapandikizi walowekwa maalum kuwavuruga kati yake na Mbowe. Na bahati mbaya Mbowe kauvaa mkenge wa kutomuamini Zitto japo walipokuwa pamoja Chadema ilikuwa na nguvu kubwa hadi kuwavuta kina Mnyika. Na Kutoaminika kwa Zitto kulimfanya aamini pia kuna siri kubwa nyuma ya Mbowe ambayo anaikinga maana ndivyo alivyo aminishwa.

Kwa hiyo Zitto anamtazama Mbowe kama kiongozi mwenye kuficha machafu yake wakati huo huo Mbowe akidhani anachokifanya ni kuficha siri za chama dhidi ya pandikizi. Yote yalosemwa hapo juu ni nguvu ya CCM kuwagawa CDM ktk makundi ili kupinguza nguvu yao na naweza sema toka swala la kwanza hadi la mwisho ni kutokana na utengano wa viongozi wa CDM ndio ulosababuisha kushindwa ktk chaguzi mabli mbali na hata matumizi ya fedha kuwekwa siri ambayo hata naibu katibu wa chama anafichwa.

Umoja Chadema umeshavunjwa na hakika utawagharimu uchaguzi ujao maana hukumu hii imedhihirisha kile CCM ilikusudia. CCM wamesimaa kama Utawala wa Marekani ambao kwa uhasidi wake wameweza kuwagombanisha waarabu wa dini moja wakatengana kwa sababu ya madhehebu tu na wote wakiuana wao kwa wao kwa jina la Mwenyezi Mungu!... Wamarekani leo wameweza kuwagombanisha hadi Wasomali, kitu ambacho kilishindikana toka enzi na enzi maana wasomali walijulikana ktk UMOJA wao. watagombana wao kwa maneno mtu yeyote akiingilia kati na kuchukua upande basi humgeukia wote wakampiga mande, hii ni historia yao toka mababu zao lakini kwa Mmarekani wamekwama..
 
Ahsante sama Mkuu Mkandara kwa mchango wako
Kabla sijachangia hoja zako ningeomba unisaidie jibu moja kwanza ambalo litajenga msingi wa majadiliano kwetu sote.

Je, unajua waraka huo uliandikwa lini?
 
Last edited by a moderator:
'MWANA CCM ALIANDIKA MANENO YA WARAKA HAPA JF KABLA YA WARAKA KKAMATWA'

Ndugu wana duru, wakati nasubiri Mkuu Mkandara anisaidie swali hapo juu ili tuendelee na majadiliano nimefanya kautafiti kadogo hapa mtandaoni kufuatilia instincts zangu za siku nyingi.

Nimebaini kuna mtu anajiita 'mwana CCM' ambaye ameandika maneno kama ya waraka mistari na mantiki neno kwa neno.
Sina shaka kuwa katika waaandika waraka MM, M1,M2,M3,M4 ni mmoja wapo.

Nina posts zote tayari ili kuwadhihirishia kuwa baadhi ya tuhuma dhidi ya CCM zinapikwa na wana CDM walioandika waraka huu ili kuwafarakanisha.

Naomba muongozo wenu, je, niweke post zenyewe au niweke na jina na muda ilipopostiwa hapa jamvini.
Sijui taratibu za jamvi zinasemaje kuhusu kumnukuu mtu.

Anyways mkinifungua macho nitaweka hapa zote nikilinganisha mstari kwa mstari na waraka ili muone wenyewe.

Hizo zitatupa picha nyingine kuhusu lini waraka umeanza kufanyiwa kazi.

Naomba ushauri wenu.
 
Wakuu zangu nawapigia hodi humu kunyumba..

Hili swala nadhani tunalijadili vibaya sana maana kama kweli sababu ya hawa viongozi kunyang'anywa madaraka ni huu waraka basi ni vizuri sana tuuzungumzie WARAKA badala ya kurudi nyuma na kutazama maisha ya mtu yasohusika. Swala hapa ni waraka huu, tuhuma zake na kashfa zake. Je, unapousoma unakupa picha gani na hata kama hatukubaliani nadhani ni vizuri kila mmoja wetu azungumzie kile kilichomfanya akubaliane na hukumu ama kutokubaliana.

Kwanza kabisa mimi nimeusoma na sehemu hizi ndizo zilizonivuruga kabisa na zinahitaji majibu kwani kuwaadhibu Zitto na Kitila haiwezi kukisaidia chama hata kidogo isipokuwa kuwasaidia baadhi ya watu kuendeleza kile kinachodaiwa. Kinachonishinda mimi zaidi kuelewa ni hizi shutuma ambazo zimewekwa kwa uongozi uliopo na maajabu Zitto kama naibu katibu wa Chama inaonyesha hayumo ktk maamuzi yoyote isipokuwa kundi la watu watatu.. Nawaomba sana mjiulize haya! Inakuwaje watu hapa JF wanamlaumu Zitto ikiwa huyu Zitto hakushirikishwa ktk maamuzi makubwa kama haya ili hizi lawama zote kuhusu Uongozi wa Chadema na yeye awe mmoja wao?... Inakuwaje Zitto alitengwa tuache wajumbe wengine nje kwanza! Mkuu wangu Nguruvi3 kama unayo majibu nayaomba uyaanike hapa. Tuanze na tuhuma hizo, huu waraka unasema nini kuhusu uongozi uliopo..

Mkandara;

Mimi ni Neutral kwanini nipoteze muda wangu kusoma waraka? Nadhani hiyo ni kazi yenu wanaCDM. Jinsi waraka ulivyopatikana kwa kutumia njia za kijasusi inaonyesha hata bila waraka mambo yalikuwa sio swari.

Hili kukipa maendeleo chama, sio lazima Zitto na Mbowe wapendane. Na sio lazima viongozi wote wawe na sauti moja. Wanachotakiwa ni kuwa profressional katika majukumu yao. Kinachoonyesha ni kuwa viongozi wa CDM sio professional.
 
Ahsante sama Mkuu Mkandara kwa mchango wako
Kabla sijachangia hoja zako ningeomba unisaidie jibu moja kwanza ambalo litajenga msingi wa majadiliano kwetu sote.

Je, unajua waraka huo uliandikwa lini?
Mkuu wangu sijui huu waraka umeandikwa lini lakini kulingana na events zilizoorodheshwa hapo juu inaonekana kuwa waraka huu umeandikwa sii muda mrefu sana laa sivyo hoja ya uchaguzi mdogo za wawakilishi kwenye Halmashauri ya June 2013 isingekuwepo..

Ukweli utabakia tu kwamba swala langu la namba TANO (5) ndilo wengi wetu wameshindwa kulipa uzito ama kuliona maana kama kweli kuna kundi hili ndani ya CDM sioni sababu kwa nini Zitto analaumiwa kuunda makundi wakati tayari kuna kundi hili ambalo kiutawala Zitto alitakiwa kuwa moja wao. Hawa watu watatu ni kina nani na wameaniwa kiasi gani kuwatenga kina Zitto na imeanza lini huku kutoaminiana ndani ya chama.

Je, kuna ukweli wowote kuhusu tuhuma hizi?...Tumeyasikia malalamiko kama ya waraka huu toka enzi za marehemu Chacha Wangwe, na tumeyasoma humu humu JF - haiwezekani iwe kila siku Makao makuu inasingiziwa na jambo lisilokuwepo.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom