Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #101
Ndugu yangu umechukua maneno ukapandikiza ya kwako halafu ukahitimisha kuwa Nguruvi3 kasema.Kwa mtazamo wangu naona ni udhaifu wa kihoja kudhani watu fulani ni bora sana kwakuwa eti wameifikisha CDM hapa ilipo leo na hawakustahili kuandaliwa waraka kama ule
Hoja kama Mbowe amemlea Zitto, amefanikisha idadi ya wabunge kuongezeka, na kuifanya CDM chama kikuu cha upinzani nk nk hakumaanishi chochote iwapo kuna viti haviendi sawa
Mimi ninaweza kona ilitakiwa CDM wawe wamechuka nchi kitambo lakini wana wabunge kidogo sana, Mbowe alitakiwa kuwa amela akina Zitto kama 1000 hivi lakini yupo mmoja nk nk
Sehemu yoyote kwenye demokrasia upinzani ni swala la zima, makundi ya watu wenye mtazamo mmoja ni lazima, pengine kinacho tushinda sisi ni namna tu ya kufanya kazi pamoja kama chama baada ya chaguzi
Tunaweza kuona madhambi mengi sana ya Zitto kama mkuu Nguruvi3 na Mchambuzi wanavyojaribu kuyadadafua ambayo kimsingi inaonekana ni kama CDM walishindwa kuyathibitisha miaka nenda rudi lakini sasa kwa waraka ule wakaona sasa hapa hapa tummalize
Pamoja na tuhuma za Zitto lakini wakosoaji wa Zitto hawataki kufikiri zaidi kiasi kwamba pia hawataki kuamini CDM kuna ombwe la uongozi
CDM hawataki demokrasia ndani ya chama kwa kisingizio cha "kugawa" chama........Ni ajabu sana
Leo hii hata ukitangaza nitagombea cheo fulani ndani ya chama utaambiwa unakiherere, unaharaka nk nk
Uoga umewajaa viongozi wa CDM kumbuka nguvu kubwa iliyotumika kumlazimisha Zitto atoe jina wakati ule
Binafsi sitaki kuamini waraka ule it worth kuwavua uongozi Zitto na Kitila uongozi, Kitila alipoomba kujiuzulu alijua wenzake hawawezi kuwa na imani naye tena lakini hakusema ilikuwa ni kosa
Tafadhali simama katika ukweli utakuwa huru zaidi.
Waraka umesema uongozi wa sasa hauna lolote la maana ukisifia enzi za watangulizi Makani na Mtei kwa kuacha wabunge 3. Mimi nikasema waraka ungeeleza nani amefikisha CDM kuwa cha upinzani rasmi?
Takwimu zinasemaje kuhusu hilo.
Nilikusudia kuwa takwimu zisitumike nusu nusu, ima ni kamili au hakuna.
Waraka umesema mbowe ana akili ndogo sana na elimu yake ya magumashi.
Nimeuliza hivi huyu si ndiye alifanya recruitment ya Zitto na Kumlea hadi alipo? Akili ndogo imeweza kutoa 'shujaa' ambaye anatetewa hata kama ametenda ouvu.Nimeuliza tu akili ndogo haijafanya hivyo?
Hao vijana 1000 unaosema, pengine wapo zaidi, tatizo ni kuwa hawaoni kama wapo kwasababu wamefunikwa katika kivuli .
Ndio maana tunasema kama kuna kivuli kwanini kiweke giza chini ya mwamvuli tukijua kuna 1000 wanasubiri fursa hiyo?
Watu wanosema kuna ombwe la uongozi nakubaliana nao kwa hoja, lakini basi onyesheni wapi omwe lilipo. Hakuna ombwe la kujenga hoja za kumtetea mtu . Elezeni ombwe lipo wapi.
Nilishawahi kueleza tena kwa kina kuhusu ombwe bila kusukumwa na Zittoism, sasa ninyi mnaojenga ngao kwa Zitto onyesheni wapi ombwe lilipo na je namna ya kuziba ombwe ni njia haram, za kitoto za waraka.
Tulidhani Zitto angetangaza ili tuone hiyo demokrasia ya CDM inafanya kazi vipi.
Hakuwahi, alichokifanya ni kutumia mitandao na vijana kuchafua wenzake, je huko ndiko kutangaza nia?
Na mwisho hutaki kuamini waraka una makosa, au hutaki kuamini zitto kuvuliwa madaraka kufuatia waraka?