Mkuu
Mkandara
Katika bandiko lako hapo nyuma umeonyesha wazi madai ya waraka yana uhalali
Mimi sijasema hayana uhalali au vinginevyo.
Ninachosema yamekosa nguzo muhimu ya uhalali kama alivosema Mchambuzi.
Waraka una makosa katika maudhui, uandishi na hoja. Hapo ndipo tatizo lilipo.
Umesema pia watu wasisusie suala la kutajwa watu watatu.
Huko nyuma nimewahi kuandika kuhusu udhaifu wa Mbowe, udhaifu wa Slaa, udhaifu wa Zitto na upotoshaji wa Kitila.
Nilionya sana kuhusu tatizo la masali na Kafulila. Nilisema uongozi wa CDM unalea personality na kushindwa kuchukua hatua. Hata pale unapochukua hatua kuna double standard.
Nilikumbusha mgogoro utalipuka ndani ya miezi 18 nikiandika June 2012.
Kuna mapungufu kama taasisi hilo, lazima walikiri.
Hata hivyo ni wazi mapungufu ni kutokana na kutoaminiana au kuhujumiana.
Sidhani kama ni vema tukijisahaulisha ya nyuma ili tutee waraka au tusiseme wahusika au kutoa excuse kwa Zitto. Waraka ni mwendelezo wa tatizo la muda mrefu. Tatizo lililopo ni njia zilizotumika kufikisha ujumbe kwa taasisi.
Ni kwa msingi huo Zitto ambaye ni kiini cha mgogoro ataangaliwa kwa ukubwa na mapana yake.
Hakuna asiyejua kuwa public ilianza kupoteza imani naye siku nyingi aliposhiriki sakata la Kafulila, Masalia na Juliana.
Katika waraka huu ametekeleza mambo muhimu yaliyosemwa kama kulipua bomu la ukaguzi wa fedha ambalo waraka umetamka wazi litawamaliza viongozi wa sasa.
Nia haikuwa kutetea fedha za umma, ilikuwa kutumia nyadhifa na ofisi za umma kuungamiza uongozi ambao yeye ni mshiriki. Hivi kitendo hicho kinatofauti gani na usaliti wa umma na chama chake.
Anausaliti umma kwa kujivika ngozi ya ushujaa, anasaliti chama chake kama katibu mkuu kwa kutumia umma.
Tunaelewa Kitila alikimbilia kusema Zitto hakushiriki ili kumokoa. Alichosema ni Zitto kutoshiriki kuandika, lakini ukweli usio na chembe ya shaka Zitto ameshiriki kuutekeleza waraka katika hatua za awali.
1. Ameshiriki katika kulipua bomu la ukagauzi lililoandikwa vema katika waraka.
2. Ameanza kushiriki kampeni za chama baada ya kususia miaka mingi kama ilivyoandikwa katika waraka
3. Alianza kujenga mtandao ambao leo utasikia matamko ya kulaani tu kufukuzwa si upuuzi wa waraka kama ilivyoandikwa katika waraka.
Pamoja na hayo, Zitto amendelea kuughilibu umma. Leo alikuwa na Fina Mango ambaye ukisoma interview ni kama pre prepared lakini tunaipa benefit of doubt.
Zitto ameeleza jinsi gani ameshiriki mambo ya kitaifa na kimataifa, akitaka kuundoa umma katika hoja za msingi kabisa za jinsi anavyowasumbua CDM kwa makundi, kiu ya madaraka na usaliti na ushiriki katika waraka ambao Kitila amekiri ni makosa na Zitto mshiriki na mtekelezaji anajiondoa.
Mkakati huu wa kueleza mazuri na si kuomba radhi kwa uchafu waliowahi kuufanya ni ishara njema ya kukosa hekima na uaminifu kwa Zitto.
Ni Zitto huyu anayezungumzia ufisadi wakati tunafahamu wazi kuwa aliisema sana Barrick na kisha kwenda Kigoma kupokea milioni 10 kwa mlango wa halamshauri.
Baada ya hapo ni Kimya hadi leo.
Ufisadi gani atauongelea huyu kijana na kughilibu umma wote. Yes, anaweza lakini ni kwa baadhi.
Hatuhitaji kusikia Zitto alishirikiana na kiongozi gani wa nje, tunamtaka ajibu tuhuma zinazo mkabili ikiwa ni pamoja na usaliti wa wenzake mara nyingi sana akipewa benefit of doubt.
Mkuu Mkandara, kuna tatizo ndani ya CDM. Wakati watu wanaliona leo sisi tumeliongelea miezi 14 iliyopita na wewe ulikuwa sehemu ya mjadala.
Tuliwasaidia CDM kuwashauri kwa nia njema kabisa wakaamua ku entertain personality.
Mimi nipo katika rekodi ya kusema Juliana alikuwa anatumiwa na watu wakubwa sana, nikamtaja Kitila Mkumbo hasa kwa kauli yake ya 'waachwe wabalehe'.
Niliwaambia CDM, Juliana kwa umri wake, kielimu, kisiasa na kijamii hawezi kuleta timbwili kama lile kulikuwa na vigogo. Leo waraka umefumua kila jambo.
Sidhani kama taifa hili lina upungufu wa viongozi iwe CCM au CDM.
Wapo watu wazuri na vichwa vya maana kutoka kila chama.
Taifa hili haliwezi kuendelea kama tutakemea ulaghai wa CCM na kuficha ulaghai wa CDM.
Sioni tofauti ya mhalifu wa CCM na mhalifu wa CDM ndio maana tunasema wazi tukiwa huru.
CDM kama wanachama hawana tatizo to be honest with you.
Matatizo yaliyopo ni ya kitaasisi tena inayokua hivyo kuna nafasi ya kujirekebisha.
Tatizo la CDM ni hizi personality zinazodhani kuwa zenyewe ndio CDM hasa viongozi.
Hizi ndizo zitaitafuna CDM hadi mwisho. Nilidhani Zitto angechukua ushauri wa kukaa kimya ili japo aonekane amejifunza.
Ukosefu wake wa busara unazidi kutamalaki kwa kudhani kuwa anaweza kufanya spinning dunia yote ikaingia katika ghiliba zake kama alivyozoea na kama waraka ulivyotaja kuwa ni moja ya strength zake.
Kwa mwendo wa Zitto wa sasa na ukosefu wa uaminifu, busara, hekima na uwezo wa kupima nadhani CDM wanacheza na kaa la moto.