Mkuu Nguruvu3, kwanza asante, wewe kutumia bandiko langu ni heshima kubwa kwangu.
Mwaliko wako wa PSI niliupata jana ulipomwaga tuu thanks kwenye bandiko langu, ila pia kwenye zile powers from within, Mkuu Nguruvi3, you are very powerful!, you have the powers to make things happen kwenye political atmosphare, nakuomba sana make you wish now!, ili 2015 mambo ya change!, play more active role kwa kusema tuu kunatosha!, sio lazima mpaka uingie kwenye ngoma kuicheza!, vivyo hivyo Mzee Mwanakujiji a very powerful man inside, keeps playing "hide and seek", saidieni!, jahazi ndio hili linakwenda marama!. 2015 tutakuja tuu kutoa pole na kusema tuliwaambia!.
Nakutafutia muda nikujibu rasmi posti yako, ila kuna jambo nimeanza kulinote, nikilithibitisha, nitakuambia!, in short kuna ma great thinkers wako blindfolded na mapenzi ya Chadema!, wametake sides! ukiwemo wewe Mkuu Nguruvi3!.
Nilimwambia Mzee Mwanakijiji mahali, kuwa "mchelea mwana kulia, hulia yeye!", Mkuu Nguruvi, 2015 mtalia..!.
Kwa vile huu uzi uko page zaidi ya 100, mambo ya "powers" yalinitinga nikapoteza a bit of my political focus, nitakurudia tangu mwanzo, nitakueleza ya kwangu!.
Tangu alipoanza Tumtemeke, wakaja kina Shonza, waraka wa Mngamba, waraka wa Kitila, nyaraka zote hizo zina hoja za msingi sana ambazo kamwe hazijibiwi!, inachofanya Chadema ni kuwatimua watoa nyaraka, kisha kufunika kombe mwanaharamu apite!, wanachofanya ndio ile ile ya mbuni kujificha ndani ya mchanga kwa kufunika kichwa!.
Nitakujibu!.Pasco.
Mkuu
Pasco wakati tunasubiri udurusu kurasa ili uje na yako, ningependa nizungumzie kidogo kuhusu aya ya mwisho.
Awali ya yote nieleze kuwa ukiwa huru utaongea bila hofu. Nia kubwa ya baadhi yetu si ushabiki bali kuona tunafikia demokrasia ya wenzetu ambayo si uchama bali kanuni, misingi, taratibu na nidhamu.
Tony Blair aliondolewa na Labour baada ya kubaini anakipeleka chama kusiko.
Ndivyo ilivyokuwa kwa Margareth Thatcher na wengine.
India imeweza kubaki bila waziri mkuu kwa miezi 3 na nchi haikuathirika.
Ndivyo ilivyokuwa kwa Uingereza baada ya GB kutoweza kuundwa seikali ya minority kwa wiki tatu.
Yote yametokea na nchi zimeendelea kuwepo. Ndipo wenzetu walipo katika demokrasia.
Tunainyooshea kidole CCM kwa kushindwa kuchukua hatua au kuwawajibisha viongozi wake.
Inapofika waziri mhusika anakutwa na majnga 2 ya vifo vya raia bila hatia kwa mabomu na bado yupo ofisini inatupaswa tisikitike.CCM ni 'old dog you can't teach new tricks'.
Hivi vyama vingine vinavyowania madaraka lazima vijifunze taratibu, nidhamu na sheria.
Tutake tusitake inaweza kutokea siku vikachukua dola. Je, tuendelee kuishi katika mazingira tuliyo nayo sasa hadi lini?
Kama umeusoma waraka na mjadala hatukatai uwepo wa matatizo. Tunachojadiliana ni jinsi gani watu wanashughulikia matatizo hayo. Njia zilizotumika katika waraka hazionyeshi political maturity ya aina yoyote.
Njia za kuwa kiongozi na kuchukua siri ili kuzifanyia kazi embe kiburugwa ni za kizamani, kishamba na kihuni zisizopaswa kufumbiwa macho
Tumeeleza Kitila na Zitto walipaswa wajiuzulu nafasi zao kama hatua ya kwanza ya kupinga mambo yalivyo ndani ya chama chao. Hatua ya kwanza ilikuwa kuongea katika vikao na kama hawakupewa nafasi katika agenda wangeweka katika OAB. Hawakufanya chochote zaidi ya espionage na kwenda embe kiburugwa.
Hao akina Kafulila, Juliana Shonzo, Masalia ni sehemu ya mtandano wa watu hawa.
Soma bandiko la nyuma nimeeleza kwa undani ilianza vipi kwa Kafulila, ikahamia kwa akina Juliana.
Sakata la Juliana halikuwa kuhusu uongozi bali kauli ya Heche kwa Shibuda.
Ilikuwa timing ili kumuondoa Heche na Juliana ambaye ni 'mtu wao' achukue nafasi katika kujenga mtandao.
Sakata la Masalia lilikuwa na lengo la kumweka Zitto kama lilivyokuwa la Kafulila.
Masakata yote Zitto ametajwa. Huu mtandao wa waraka ilikuwa ni hatua nyingine ya kudhibiti habari kuvuja.
Ukisoma utaona wanasema 'watu waaminifu' wachache. Ni kwa bahati mbaya Mwigamba kauza silaha.
Hakuna kupuuza malalamiko yao lakini basi yaelezwe kwa lugha ya kidplomasia, yawe na maono na mipango,nidhamu, hekima,taratibu na si matusi na kejeli kama unavyousoma waraka.
Ni kutokana na kukosa mashiko wenyewe wameshindwa kuutetea waraka na kukimbilia kujiuzulu.
Soma waraka na utetezi wao uone kama kuna hoja.
Ndugu yangu Pasco, unafahamu kuanzia duru ilipoanza na ukweli upi nasimamia.
Wakati namkaanga Mbowe kuhusu Togwa na chaguzi ndogo, au Dr Slaa na msimamo wa Rwanda pamoja na ulege ulege nilionekana mwema, leo nasema ukweli kuhusu waraka nashutumiwa.
Uhuru unaniweka huru sana na nafurahia hilo.
Labda tukusikilize uje na habari nyingine mpya kwasababu tuhuma, shutuma na lawama tumezieleza vema tu.
Tumeuangalia waraka upside down na tunaendelea kuuangalia nukta hadi nyingine.
Mkuu Pasco kwani mwenzetu una lipi jipya utuhabarishe wanajamvi wenzako kuhusu timbwili hili? Karibu uwanjani