gfsonwin
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 18,272
- 20,692
Zakumi ndugu yangu umesema yote.gfsonwin;
Jinga la Falsafa ana hoja zilizotulia sana. Ukisoma katiba ya Marekani, hakuna sehemu yoyote inayotaja vyama vya siasa. Inavyotaja ni haki ya wananchi kushiriki katika shughuli za kisiasa, haki ya kujikusanya kufanya majadiliano, na haki ya watu kuwakilishwa.
Mfumo wa vyama umekuja baadaye sana baada ya watu kutumia haki zao za kiraia zilizomo kwenye katiba. Hivyo vyama vya Republican na Democrat vipo kutimiza haki za kiraia. Na kiongozi wa chama, jukumu lake la kwanza ni kuhakikisha haki za kikatiba za wanachama zinatimizwa kwa sababu haki hizo ndizo zinazofanya chama kisimame. Katiba inaposema kuwa watu wana haki ya kukusanyika ina maana wanaweza kuanzisha makundi ambayo utaita chama au upinzani ndani ya chama.
Katiba ya Marekani haisemi Marekani iwe nchi ya kijamaa au kibepari. Wala haisemi Marekani liwe taifa tajiri au lenye nguvu duniani. Katiba inatoa muundo wa kijamii ambao unatoa haki za kisiasa. Kwa kifupi haya ndio malengo ya katiba ambayo yanapatikana katika jamii zote zilizoendelea na zenye taratibu.
Kwa upande wetu, tumeanza na matokeo (vyama vya kisiasa) bila kuwa na haki za kimsingi ambazo zingekuwa ni misingi ya kuwepo kwa vyama. Ukiwauliza wana CCM na CDM kwanini ni wanachama wa vyama hivyo, watakwambia ndio vyama pekee vyenye uwezo wa kuleta maendeleo. Na hili walete maendeleo na kufanya mabadiliko ni lazima waende Ikulu.
Ukweli wa mambo, hili kuleta mabadiliko ya kweli sio lazima CDM, CCM, au CUF iende Ikulu. Na matatizo ndani ya vyama vya kisiasa yangepungua kama viongozi wake wa juu wangeacha kutumia muda wao mwingi kutafuta njia ya kwenda Ikulu.
kiukweli sasa ifike mahali tuone tanzania inaweza kuwepo hata nje ya vyama vya siasa, na kwamba sio lazima sana migogoro inayosumbua vyama hivi ikatufanya sisi tuwe na wasiwasi kwamba eti nchi itayumba, itayumbia wapi?? je watumish wote wanaofanya kazi ni wana vyama vya siasa?? mbona wengi wao sio lkn bado wanatenda kwaajili ya nchi??
huu ujinga wa kuka n kila siku nkujadili migogoro ya vyama vya siasa ndio unaotuponza tunaacha kuwaza yaloe ya maana kabisa.
Last edited by a moderator:
