Duru za Siasa Special: Mgogoro kambi ya Upinzani (CHADEMA)

Duru za Siasa Special: Mgogoro kambi ya Upinzani (CHADEMA)

gfsonwin;

Jinga la Falsafa ana hoja zilizotulia sana. Ukisoma katiba ya Marekani, hakuna sehemu yoyote inayotaja vyama vya siasa. Inavyotaja ni haki ya wananchi kushiriki katika shughuli za kisiasa, haki ya kujikusanya kufanya majadiliano, na haki ya watu kuwakilishwa.

Mfumo wa vyama umekuja baadaye sana baada ya watu kutumia haki zao za kiraia zilizomo kwenye katiba. Hivyo vyama vya Republican na Democrat vipo kutimiza haki za kiraia. Na kiongozi wa chama, jukumu lake la kwanza ni kuhakikisha haki za kikatiba za wanachama zinatimizwa kwa sababu haki hizo ndizo zinazofanya chama kisimame. Katiba inaposema kuwa watu wana haki ya kukusanyika ina maana wanaweza kuanzisha makundi ambayo utaita chama au upinzani ndani ya chama.

Katiba ya Marekani haisemi Marekani iwe nchi ya kijamaa au kibepari. Wala haisemi Marekani liwe taifa tajiri au lenye nguvu duniani. Katiba inatoa muundo wa kijamii ambao unatoa haki za kisiasa. Kwa kifupi haya ndio malengo ya katiba ambayo yanapatikana katika jamii zote zilizoendelea na zenye taratibu.

Kwa upande wetu, tumeanza na matokeo (vyama vya kisiasa) bila kuwa na haki za kimsingi ambazo zingekuwa ni misingi ya kuwepo kwa vyama. Ukiwauliza wana CCM na CDM kwanini ni wanachama wa vyama hivyo, watakwambia ndio vyama pekee vyenye uwezo wa kuleta maendeleo. Na hili walete maendeleo na kufanya mabadiliko ni lazima waende Ikulu.

Ukweli wa mambo, hili kuleta mabadiliko ya kweli sio lazima CDM, CCM, au CUF iende Ikulu. Na matatizo ndani ya vyama vya kisiasa yangepungua kama viongozi wake wa juu wangeacha kutumia muda wao mwingi kutafuta njia ya kwenda Ikulu.
Zakumi ndugu yangu umesema yote.
kiukweli sasa ifike mahali tuone tanzania inaweza kuwepo hata nje ya vyama vya siasa, na kwamba sio lazima sana migogoro inayosumbua vyama hivi ikatufanya sisi tuwe na wasiwasi kwamba eti nchi itayumba, itayumbia wapi?? je watumish wote wanaofanya kazi ni wana vyama vya siasa?? mbona wengi wao sio lkn bado wanatenda kwaajili ya nchi??

huu ujinga wa kuka n kila siku nkujadili migogoro ya vyama vya siasa ndio unaotuponza tunaacha kuwaza yaloe ya maana kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3 rejea bandiko lakon #157 .................
sawa ZZK anatafuta huruma ya wananchi/raia na hii imjketokana na ukweli kwamba anajua anayo nguvu ya watu nyuma yake yaani anao uwezo mkubwa wa kushawish na kupata sympathy ya watu kuliko ambavyo baadhi ya wanategemea.

lakin najiuliza swali la msingi sana hivi CDM ni chama cha siasa, ama taasisi isiyo ya kiserikali ama ni kikundi cha wahuni tu ambao hujiendesha pasina taratibu zinazoeleweka ama nini??

Hivi kama ishu ni kugombea uongozi kwann basi wasiache kura ikawa mwamuzi?? na ishu ni ZZK kuongopa hivi CDM inaona tabu gani kumuwajibisha hadi wafanya media ndio hakimu na msikiliza mashtaka wao??

Tuliona mfano ambao Lowassa alituonyesha kiukweli kitendo cha yeye kukubali kuresign hata kwa mambo ambayo mengine yalikuwa ni tuhumu ama yalikuwa ya kweli halikusambaratisha ccm wala haikufanya ccm kushindwa kuendelea na harakati zake za kuongoza nchi.

mfano huu ungetosha kuifunza cdm kwamba hata kama zzk kakosea na yy haoni kuwa kakosea basi wao waendelee kujenga chama na warekebishe baadhi ya makosa ambayo kwa namna moja ama nyingine ndio chanzo cha haya.

hakuna haja ya kunyenyekea watu kama miungu watu lkn pia hakuna haja ya kunyima taifa zima Usingizi kisa mgogoro ndani ya CDM.
gfsonwin na wengine, ningependa kuweka hoja zinazofanana ambazo kwa namna moja zinaonekana ''kama kuna mada ya mgogoro wa CDM unavyotishia amani ya nchi''

Nina hakika neno lililotumika na baadhi yetu kama zidane, Mchambuzi na mimi ni 'kwa mustakabali' linawapa wasi wasi. Neno mustakabali hlina maana ya hatima.

Mgogoro wa CDM (chama cha upinzani) ambacho kinacho ungwa mkono kwa wingi zaidi ya vyama vingine vya upinzani kwa sasa haumaanishia hatima ya taifa bali mustakabali wa demokrasia siku za baadaye.

Hakuna anayependa turudi katika communist party system au vanguard party.
Tumejaribu na kuona madhara yake kwa miaka 30 iliyopita.

Tunahitaji demokrasia ya watu kuamua namna ya kushiriki au kutoshiriki katika siasa kwa namna yoyote.
Gogoro la CDM ni dalili za demokrasia kutokomaa licha ya miongo miatatu ya uwepo wake.
Tunayoyaona ilivyokuwa NCCR na CUF.

Tumejadili siku za nyuma role of civil societies katika kujenga taifa.
Hatuna Civili societies zinazoweza kusimama mbadala wa vyama vya siasa kwa sasa.

Tuliuliza civili socities zetu kwanini hazipo na zile zilizopo kwanini ni function less?
Na je zinaundwaje, from top-bottom au bottom top?
Labda baadhi yetu mnaweza kutusaidia ili watu waachane na hoja za siasa na tujikite katika hoja za utaifa zaidi.

Nimeuliza swali ambalo sijajibiwa. Nikasema CCM wanchukua bilioni 8 , Chadema bilioni 1 na wengine si chini ya milioni 10 kwa mwezi kama ruzuku.

Ni kiasi gani kinapelekwa Muhimbili kama ruzuku?
Kwanini kama taifa tusisimame na kuhoji? Kitu gani vyama vya siasa vinatushinda?
Ni sahihi kuviacha tu kwasababu havina athari kwa mustakabali na hatima ya taifa?

Juzi wameongeza division 5 na kupunguza namna ya kupata A.
Watakaoathirika ni watoto, wadogo na ndugu zetu.
Wapi tunasimama kama taifa kusema hilo hapana?
Wapi role ya civil societies mnazosema zituunganishe?

Kumbekeni maagizo yalitolewa na wanasiasa, waliojadili ni wanasiasa na walioleta maagizo ni wansiasa, hivi hatuoni kuwa siasa ina athari kubwa katika maisha yetu ya kila siku.
Kwanini tusiongelee mwiba uliochoma mguuni tunaongelea homa iliyosababishwa na mwiba?

Hoja yangu ni kuwa hatuna civil societies za kuweza kusimamia sisi kama taifa.
Kilichopo ni vyama vya kisiasa.

Civil societies zimeshindwa kuzuia uchakachuaji wa uandikaji wa katiba.
Lililpoingiliwa na wanasiasa at least likaishtua serikali. Nguvu ya vyama ya vyama vya siasa si ya kudharau

Hadi tutakapokuwa na strong civil scoieties, umuhimu wa vyama vya siasa hauwezi kudharauliwa.
Ni sehemu muhimu ya jamii yetu hata kama hatutaki.

Mjadala kuhusu mzozo wa chedema ni mjadala unaohusu migogoro ndani ya kambi za kisiasa na dalili kuwa demokrasia yetu inadumaa badala ya kukua.

Ni dalili kuwa huko twendako wananchi watakaa pembeni kwasababu hawana chaguo.
Ni hatari ya kuachia Polituburo iamue mustakabali wetu tupende tusipende.
Ni dalili kuwa tumekata tamaa katika kujisimamia na kusimamia vyombo vyetu.

Na ni dalili kuwa ile stigma ya wasomi kukaa pembeni kwa mambo yasiyowahusu lakini yanayowaathiri bado ipo.
Siasa ni sehemu muhimu ya maamuzi yanayotuhusu. Tutaikwepa kwa maneno lakini kwa uhalisia inatutahiri na njia muhimu ni kutokaa pembeni.
 
Nguruvi3 umenena vyema sana na nisingependa kuongelea tena swala lka civil societies manake hili tuliliongelea kwa mapana sana.

turudi kwenye hoja ya msingi kwamba kwann siasa zetu zimejikita katima uchama zaid kuliko katika utaifa??
kwann ruzuku ya chama iwe 8billion kutoka kwenye pesa za walipa kodi ilihali MUHIMBILI ama AMANA hakuna vitanda vya wagonjwa kulalia??

ipi mantiki ya kuwapa watu 8bil wakaekee mdundiko na mipasho badala ya kuipa ruzuku iyo shule ambayo hata dawati haina??

siasa inapaswa kuachwa iwe kama chombo cha kuratibu tu lakin kwenye utendaji na maamauzi iachwe raia ndio wafanye. sasa utakuta eti chama cha siasa kinakuja na mpango sijui kilimo kwanza nauliza hivi ccm wao ndio wa kutupa sisis dira za tuishije?? kwann dira hizi wananchi wasiamue wenyewe hivi vyama vikabakli kama chomkbo cha kuratibu tu??

tuache ubwanyenye wa kuachia siasa ituamulie mambo, tuanze sisi wenyewe kama kweli tuna nia ya dhati, na hili lianzie kwenye ngazi ya kijiji kwamba sasa hatutaki siasa bali tunataka kufanya mambo yaendelee, siasa kwanza zisihusike katika kutuamulia yaani ziwe kama vile ni kiranja tu anayesimamia lkn mwanafunzi husika anajua nafagia na nikimaliza nitazoa taka
 
Last edited by a moderator:
Zakumi ndugu yangu umesema yote.
kiukweli sasa ifike mahali tuone tanzania inaweza kuwepo hata nje ya vyama vya siasa, na kwamba sio lazima sana migogoro inayosumbua vyama hivi ikatufanya sisi tuwe na wasiwasi kwamba eti nchi itayumba, itayumbia wapi?? je watumish wote wanaofanya kazi ni wana vyama vya siasa?? mbona wengi wao sio lkn bado wanatenda kwaajili ya nchi??

huu ujinga wa kuka n kila siku nkujadili migogoro ya vyama vya siasa ndio unaotuponza tunaacha kuwaza yaloe ya maana kabisa.
Migogoro ya kisiasa ina masilahi nasi.
Narudia tena kama haiyumbishi nchi, kwanini CCM wapewe bilioni 8 kwa mwezi zaidi kuliko Muhimbi?

Je, kazi yetu ni kukatwa kodi za mishahara iende tu tusikokujua kwasababu ni sehemu isiyoathiri maisha yetu?
Ni wapi mpaka wa maisha ya kisiasa na kijamii?

Kama nchi haiyumbi migogoro inayotokea ya migomo inasababishwa na akina nani, nani wanalalamikiwa na nani wenye final say kuhusu malalamiko hayo?

Hata kama wapo watu milioni moja wanaotenda kwa ajili ya taifa bado wana uhusiano na siasa.

Rafiki yangu aliwahi kuniuliza kwanini nazungumzia na kusoma magazeti kuhusu siasa. Nilimjibu ni interest tu.
Miezi 12 baadaye akaja kuniambia ameacha kazi serikali na kujiunga na private sector.
Nikamuuliza kwanini?

Alinijibu mshahara wa serikali ni mateso tu, sisi wanatupa chini ya milioni wao wanachukua milioni 11.
Nikamuuliza akina nani? Akasema si hao wabunge Dodoma.
Nikamuuliza wao ni wanasiasa hawapangi mshahara, akasema ndio wanapitisha makadirio na ndio wanaopaswa kusikiliza vilio vya wananchi.

Nilimuuliza huko kwenye shirika lisilo la serikali anapata nini? Akanijibu anapewa health insurance katika hospitali nzuri zaidi ya Muhimbili, anapewa vijisafari na hivyo kumsaidia katika kujazia n.k.

Huyu bwana aliyeniona mjinga kwa kuzungumzia siasa, baada ya maumivu alikuja kuzungumzia siasa bila kupenda.
Halafu akaonyesha siasa ilivyomuumiza kimaisha.

Badala ya kupigana ili kuwe na health insurance nzuri na mshahara mzuri usiotegemea allowance za safari yeye akakimbia. Akatafuta suluhu ya muda mfupi private sector na ile ya kudumu kamwachia mtoto wake naye aje ahangaike nayo.

Ndio maana nasema siasa haikwepeki, ni sehemu ya maisha yetu bila kujali upo wapi.

Unapolipa kodi za ruzuku za vyama vya siasa halafu ukasema umetimiza wajibu, kule kijijini kituo cha afya hakina 500,000 za kutengeneza solar kwasababu wanasiasa hawajafikiria kutoa pesa walizochukua kutoka kwako, utakuwa unajiumiza kwa kudhani siasa haina athari.
 
Mkuu JingalaFalsafa
Kama utakumbuka tiliwahi kujadili kuhusu Tanzania kutokuwa na strong civil societies. Tukasema nchi ijenge vipi society hizo, from-top ot bottom-top.Tukazungumzia kuhusu umuhimu wa civil society zaidi ya vyama vya siasa.
.
Ninakumbuka wazi Mkuu wangu. Lakini kutokuwepo kwake hakuwezi kututhibitishia kwamba vyama vya siasa vinaweza kucheza nafasi yake. HAPANA! Ninyi wachambuzi wa siasa kama mnatambua na kuamini umuhimu wa kuwepo kwa hizo Civil Societies katika ukombozi wetu, badala ya vyama vya siasa, mnapaswa kuwaambia hayo wananchi. Lakini kinachofanyika sasa ni ku-praise vyama ili hali tunaona wazi kutuangusha kwao. Kuna kitu kibaya tunakisiliba katika Fikra zetu, na ni sumu ya ustawi wetu. Kuna watu leo wa wanaamini CDM ikishika nchi, ataishi kwenye gorofa na kama CDM ikifa, naye ni mfu tayari. Nani wa kumuokoa kama si aina ya uchambuzi wetu? Kwanini tusianze kuvunja fikra hizi mfu kwa watu kwanza? Tukiweza, ni wao wenyewe watakaounda Strong Civil Societies.

Hatuwezi kukataa umuhimu wa vyama vya siasa hata kama ni uchwara.
CCM kinachukua bilioni 8 kwa mwezi kama ruzuku. Ni kiasi gani kinapelekwa Muhimbili hospitali kama ruzuku.

Rasimu nzima ya katiba imeondoka mikononi mwetu, inashughulikiwa na wabunge wa vyama ‘uchwara’ .
Mwisho wa siku katiba hiyo itakuja kutuathiri sote.Pamoja na uchwara wake bado vinaathari katika maisha yetu.

Wanapokaa bungeni na kupitisha maamuzi mazito kama ya kodi, mishahara na miradi hizo ni fedha zetu.
Athari zake ni katika mfuko wako, je, hapo uchwara haujakuathiri.

.
Hiki unachosema hapa Mkuu wangu sijakikataa. Labda hujanielewa vizuri. Nilichohoji ni hiki, Ni kwanini tumeruhusu Taasisi hizi Uchwara kushikilia mustakbali wa Uhai na Ustawi wa Taifa letu? Natambua wazi kabisa kwamba vyama vya siasa leo hii vinaweza kuyumbisha taifa, sasa kwanini tumeruhusu hili? Mkuu wangu gfsonwin anasema kwamba hawa wanasiasa ni waratibu tu si watendaji.
.

Hakuna haja ya kuiona nchi kama haita piga hatua simply kwasababu ya vyama vya siasa ambavyo tunavipa nafasi tu ya kuratibu lkn sio watendaji.
Ni hakika kabisa kazi ya siasa ilipaswa kuwa ni kuratibu Uchumi na Tamaduni za watu, namna gani UCHUMI na UTAMADUNI vihusiane kuleta ustawi wa Taifa, wanasiasa si watendeji hawakupaswa kuwa watendaji.
Lakini ukweli ni kwamba hili kwetu lipo kinyume, Wanasiasa wetu ndio watendaji wakuu. Ndio maana nahoji ni kwanini Tumeruhusu hili kutokea? Ni wazi Mkuu Nguruvi3 maranyingi umekemea hili. Wapo wanasiasa wanao-act directly kama watendaji na vile vile wapo wanao-act indirectly kama watendaji. Kwa maana kwamba wapo watendaji wanaofanya kazi kwa kushinikizwa, mahaba, ulimbukeni na ujuha wao juu ya vyama fulani au mwanasiasa fulani. Hili ni janga.

Ninachokubaliana nawe ni kuwa agenda za nchi zichukuliwe na wananchi kwa kupitia civil society.
Swali ni je tunazo hizo society? Na je, hapo hatujaingia katika uchwara wa vyama
? Au alternative ni ipi.

.
Asante! Alternative ya kuondoa mustakbali wa taifa letu toka mikononi mwa vitasisi uchwara ni kuwa na Strong Civil Societies. Kama hazipo ni lazima tutaangukia huku kwenye vyama uchwara. Tumeishia wapi katika kuunda Strong Civil Societies? Nani anawajibika kuziunda? Muhimu hapa ni nini tunawaambia wananchi. Mahubiri yetu humu majukwaani yanaonesha vyama ndio wakombozi wetu, huku ni kuwadanganya wananchi. Ni lazima kuwahubiria ukweli wananchi sio kuwalaghai na vyama vya siasa.
Kama tunaamini katika Civil Societies, kushindwa kwetu kuziunda hakuhalalishi upuuzi wa vyama uchwara.

Kuhusu Zitto, unaposema waliomwachia waadhibiwe nakubaliana nawe kwa msingi wa kuacha kufuata taratibu hadi hali inakuwa kama ilivyo. Lakini utamwadhibu mtu vipi wakati amekuwa anayafanyavichakani? Je, hapo si uonevu.

Hakuna aliyejua ushiriki wa ZZK katika maalia hadi ‘Ben Saanane’ alipojifunga mabomu.
Labda niseme wuongozi ulipaswa kuchukua hatua za awali kabisa bila kuogopa personality.
Swali, ni je, hiyo inaondoa tuhuma zinazomkabili ZZK.Je,makosa mawili yanaweza kusahihisha kosa?
.
Hujanipata nadhani Mkuu wangu. Nilichosema ni kuwa katika kufuata misingi na kanuni za demokrasia, Zitto ni Mkosaji na misingi hiyo inawajibu wa kumuadhibu vile inavyostahili. Nimesema tena hivi, Pili, Kwa mazingira yanayosemwa yapo ndani ya chama CDM (ambayo hakuna hoja ya wazi iliyotolewa na watuhumiwa kuyakanusha -turejee baadhi ya madai ya waraka), basi Zitto na wenzake walioandaa waraka huu wapo sahihi kabisa. Kwani mazingira hayo hayakutokana na utekelezaji wa kanuni bali ukiukwaji wa kanuni. Sasa kwanini hawa waliokiuka kanuni tuwaunge mkono kutoa adhabu? Je, wewe hutotokea dirishani kama mateka?

Umedai waraka wa Zitto et al ni sahihi. Tumeuliza usahihi wake upo wapi?
Ndicho tunahitaji kujua kutoka upande mwingine na labda utusaidie kwa hilo.
.

Hapana Mkuu wangu, sikusema hivyo. Nilichosema kama mazingira yanayodaiwa yapo CHDM, tumeyasikia muda mrefu sana nami sijawahi ona utetezi wa maana, Mazingira haya kama yapo ndiyo yahalalishayo waraka. Kutokea dirishani ni kosa lakini si kizuizini. Wanachodai Zitto na Kitila ni kuwekwa kizuizini kisiasa, huko ndiko kurikofanya kuvunja dirisha. Kwangu si kosa kwa maana wangepita mlangoni wangekutana na rungu la kichwa. Na kwa mujibu wao, walishajaribu kukatisha mlangoni, walichotoka nacho ni majeraha. Kwa mazingira hayo hata mimi ningefanya sawa au zaidi kabisa.

Kinachoshangaza humu ni kwanini hatutaki kuchunguza mazingira hayo, badala yake tunatoa hukumu tu ya andiko. Kwanini sasa tusitafute ushahidi huu na kuwawajibisha mateka kama wapo kweli? Ukisema ni kufuata kanuni utakuwa ni uongo kwani hakuna anayezifuata CDM, sasa nani anastahili kuvunja kanuni pasi na kuwajibika?
Suala la kutoa malalamiko au kutotoa hakuhalalishi watu kuvunja kanuni. Halafu ni kwanini utake Zitto aseme mwenyewe wakati kwenye kumuhukumu tunatumia madai ya tuwaitao Team Zitto? Je, hao hawakuwahi kusema madai hayo? Huku ni kuegemea upande mmoja.

Mwishoni zote hizo mimi ninaziita contradictions za Demokrasia kujaribu kuishi mahali pasipostahili. HATUTOKI.

Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani. Anaita sasa!

.
 
Last edited by a moderator:
Ninakumbuka wazi Mkuu wangu. Lakini kutokuwepo kwake hakuwezi kututhibitishia kwamba vyama vya siasa vinaweza kucheza nafasi yake. HAPANA! Ninyi wachambuzi wa siasa kama mnatambua na kuamini umuhimu wa kuwepo kwa hizo Civil Societies katika ukombozi wetu, badala ya vyama vya siasa, mnapaswa kuwaambia hayo wananchi. Lakini kinachofanyika sasa ni ku-praise vyama ili hali tunaona wazi kutuangusha kwao. Kuna kitu kibaya tunakisiliba katika Fikra zetu, na ni sumu ya ustawi wetu. Kuna watu leo wa wanaamini CDM ikishika nchi, ataishi kwenye gorofa na kama CDM ikifa, naye ni mfu tayari. Nani wa kumuokoa kama si aina ya uchambuzi wetu? Kwanini tusianze kuvunja fikra hizi mfu kwa watu kwanza? Tukiweza, ni wao wenyewe watakaounda Strong Civil Societies.

Hiki unachosema hapa Mkuu wangu sijakikataa. Labda hujanielewa vizuri. Nilichohoji ni hiki, Ni kwanini tumeruhusu Taasisi hizi Uchwara kushikilia mustakbali wa Uhai na Ustawi wa Taifa letu? Natambua wazi kabisa kwamba vyama vya siasa leo hii vinaweza kuyumbisha taifa, sasa kwanini tumeruhusu hili? Mkuu wangu gfsonwin anasema kwamba hawa wanasiasa ni waratibu tu si watendaji.
Ni hakika kabisa kazi ya siasa ilipaswa kuwa ni kuratibu Uchumi na Tamaduni za watu, namna gani UCHUMI na UTAMADUNI vihusiane kuleta ustawi wa Taifa, wanasiasa si watendeji hawakupaswa kuwa watendaji.
Lakini ukweli ni kwamba hili kwetu lipo kinyume, Wanasiasa wetu ndio watendaji wakuu. Ndio maana nahoji ni kwanini Tumeruhusu hili kutokea? Ni wazi Mkuu Nguruvi3 maranyingi umekemea hili. Wapo wanasiasa wanao-act directly kama watendaji na vile vile wapo wanao-act indirectly kama watendaji. Kwa maana kwamba wapo watendaji wanaofanya kazi kwa kushinikizwa, mahaba, ulimbukeni na ujuha wao juu ya vyama fulani au mwanasiasa fulani. Hili ni janga.

Asante! Alternative ya kuondoa mustakbali wa taifa letu toka mikononi mwa vitasisi uchwara ni kuwa na Strong Civil Societies. Kama hazipo ni lazima tutaangukia huku kwenye vyama uchwara. Tumeishia wapi katika kuunda Strong Civil Societies? Nani anawajibika kuziunda? Muhimu hapa ni nini tunawaambia wananchi. Mahubiri yetu humu majukwaani yanaonesha vyama ndio wakombozi wetu, huku ni kuwadanganya wananchi. Ni lazima kuwahubiria ukweli wananchi sio kuwalaghai na vyama vya siasa.
Kama tunaamini katika Civil Societies, kushindwa kwetu kuziunda hakuhalalishi upuuzi wa vyama uchwara.

Hujanipata nadhani Mkuu wangu. Nilichosema ni kuwa katika kufuata misingi na kanuni za demokrasia, Zitto ni Mkosaji na misingi hiyo inawajibu wa kumuadhibu vile inavyostahili. Nimesema tena hivi, Pili, Kwa mazingira yanayosemwa yapo ndani ya chama CDM (ambayo hakuna hoja ya wazi iliyotolewa na watuhumiwa kuyakanusha -turejee baadhi ya madai ya waraka), basi Zitto na wenzake walioandaa waraka huu wapo sahihi kabisa. Kwani mazingira hayo hayakutokana na utekelezaji wa kanuni bali ukiukwaji wa kanuni. Sasa kwanini hawa waliokiuka kanuni tuwaunge mkono kutoa adhabu? Je, wewe hutotokea dirishani kama mateka?

Hapana Mkuu wangu, sikusema hivyo. Nilichosema kama mazingira yanayodaiwa yapo CHDM, tumeyasikia muda mrefu sana nami sijawahi ona utetezi wa maana, Mazingira haya kama yapo ndiyo yahalalishayo waraka.

Kutokea dirishani ni kosa lakini si kizuizini. Wanachodai Zitto na Kitila ni kuwekwa kizuizini kisiasa, huko ndiko kurikofanya kuvunja dirisha. Kwangu si kosa kwa maana wangepita mlangoni wangekutana na rungu la kichwa. Na kwa mujibu wao, walishajaribu kukatisha mlangoni, walichotoka nacho ni majeraha. Kwa mazingira hayo hata mimi ningefanya sawa au zaidi kabisa.

Kinachoshangaza humu ni kwanini hatutaki kuchunguza mazingira hayo, badala yake tunatoa hukumu tu ya andiko. Kwanini sasa tusitafute ushahidi huu na kuwawajibisha mateka kama wapo kweli? Ukisema ni kufuata kanuni utakuwa ni uongo kwani hakuna anayezifuata CDM, sasa nani anastahili kuvunja kanuni pasi na kuwajibika?
Suala la kutoa malalamiko au kutotoa hakuhalalishi watu kuvunja kanuni. Halafu ni kwanini utake Zitto aseme mwenyewe wakati kwenye kumuhukumu tunatumia madai ya tuwaitao Team Zitto? Je, hao hawakuwahi kusema madai hayo?
Huku ni kuegemea upande mmoja.

Mwishoni zote hizo mimi ninaziita contradictions za Demokrasia kujaribu kuishi mahali pasipostahili. HATUTOKI.
JingalaFalsafa , Kitila na Zitto wangeachia nafasi zao ili wapite mlangoni salama.
Ukishakuwa insider unawajibika kwa insiders na kwenda kinyume na maazimio ambayo wao ni sehemu yao ni espionage.

Kuna vitu viwili watu wanavichanga ima kwa kutoelewa au makusudi.
Ninachokiona ni watu kutaka kuetetea waraka kwa njia zisizohusiana na waraka.

Tumesema kuwa yapo yanayohitaji kujibiwa na uongozi na tumeyaorodhesha.
Moja walililojibu japo kwa kuchelewa ni suala la ratiba ya uchaguzi.
Mengine kama conflict of interest ya tenda yanahitaji majibu kama mengine.

Inaonekana tumechukua upande, watu wasichokielewa ni kuwa waraka uliopo na uetetezi ni vya Kitila na Zitto ambavyo tunavijadili. Swali kubwa lilikuwa 'wapi makosa ya waraka huo?' nasi tukasema tuungalie waraka kama ulivyo kwanza.

Tumepitia mstari mmoja hadi mwingine na kuanisha makosa.
Hakuna anayekuja kutueleza tumeainisha wapi kwa makosa na hatukutenda haki wapi.

Waraka wa kitila na Zitto unasema Mbowe hana akili na ana elimu ya magumashi.
Hatukuandika maneno hayo, yapo katika waraka.

Tulichofanya ni kuhoji tu kuwa wao kwa elimu yao wameona kuandika mtu ana akili ndogo na elimu ya magumashi ndiyo tatizo la CDM?

Ndio mabadiliko wanayotaka kuyaleta ya majungu kama yale yanayoandikwa katika khanga za dada na mama zetu?
Ndio usomi wenyewe huo?

Waraka ukasema Zitto akifanya mapenzi iwe kwa siri na hata akifanya Nepotism iwe kwa siri.
Upande wa pili wanasema kiongozi aliyepo ni mhuni kama inavyoelezwa na akina mama hata kupora wake za watu.
Tumehoji rationale ya kauli hizi mbili katika waraka mmoja ni sahihi? Ndio usomi wenyewe huo?

Hata ukiangalia waraka mambo mengi sana yamepotoshwa.
Mathalan kusema akina mama wanampenda Zitto ni upotoshaji.

Zitto hawafahamu akina mama kwasababu hajawahi kuishi nao.
Hana mke na kama ni tafsiri zaidi basi yeye anaweza kuwa na tatizo zaidi la kudhalilisha wanawake.
Hajawahi kuoa, hawajui akina mama na matatizo yao na wala hajui matatizo ya familia kwasababu hajawahi kuingia katika taasisi kongwe duniani ya ndoa.

Matatizo unayosema yamesemwa siku nyingi, FYI ni watu hao hao waliokuwa wanatumia ID tofauti. Hebu rejea bandiko #92 .

Ni watu walioshindwa kusimama mbele ya vipaza sauti na kueleza matatizo, wakajificha vichakani wakitumia vijana na mabinti kutimiza kiu zao na wala si kiu za demokrasia. Huo kama si uhuni sijui ni kitu gani.

Mandela alipohukumiwa katika kesi ya Rivonia, alisimama na kusema yupo tayari kwa lolote kwasababu aliamini alichokisimamia. Hakujificha kusema hakubaliani na udhalimu.

Kama yapo matatizo wajitokeze waseme na si kujificha na kuandika waraka wa kitoto, dhalili na kihuni usiokidhi haja ya demokrasia, usomi au uongozi. Hili limewashushia heshima sana mbele ya uso wa duni.

Itachukua miongo mingi kwa baadhi yetu kumuamini Zitto. Historia yake imezidi kuchafuka licha ya ukweli kuwa ilishachafuka siku nyingi.
 
Last edited by a moderator:
ZIARA YA DR SLAA IMEKUSUDIA KUFIKIA MALENGO YAPI?

Bandiko#125 nilisema ziara ya Dr Slaa Kigoma ilikuwa ni kukurupuka. Ni ziara isiyohitajika katika wakati CDM ilio nao.
Washauri wake hawakukaa kitako na kutathmini kwa undani ni repercussions zake kisiasa.
Jana amezua sokomoko huko Kasulu kwa mkutano kuvunjika kutokana na vurugu.

Vurugu zinaweza kuwa katika yafuatayo
a) CCM kuchochea mgogoro zaidi kwa kujifanya ni wanaCDM wanaomuunga Zitto Mkono. Kitu kisichoeleweka ni kuhusu CCM kumuunga mkono Zitto wakati huo huo wakiwa hawapo tayari kumpokea.

b)Makundi ya 'waraka' yamekirihika baada ya mkakati kutibuka na njia rahisi ya kuonyesha hasira zao ni kuzuia mikutano kama hiyo.

c)Kigoma ni nyumbani kwao Zitto kuna ile hali ya kawaida kukubalika.

d)Mbegu alizopanda Zitto: Siku zote hakemei hoja za ukanda akiwa kiongozi na ndiye mwasisi wa suala hilo kwa kutumia makundi yaliyopita ya akina Kafulila, Shonza na Masalia. Ukisoma mabango suala lililotawala ni ukanda na uchaga.
Wapo wanaoamini hivyo kwasababu ya kuaminishwa na wapo wanaoamini kwasababu ya Zitto.

Kitendo cha Dr Slaa kwenda sikielewi kililenga nini. Tatizo lipo makao makuu na tatizo si wanchama bali vongozi na uongozi wa CDM uliogawanyika. Hakuna shaka katika timbwili hili wapo watakaoondoka CDM kwasababu nyingi
1)Ima kupinga namna chama kinavyoshughulikia matatizo
2) Kwasababu tu Zitto kaondolewa nyadhifa n.k.

Ziara hiyo imekuwa na matukio yaliyoshirikisha Polisi. Kifupi ni ziara ya vurugu ambayo sijui kwanini CDM wameamua kuifanya. CDM wanawapa CCM nguvu ya hoja kuwa wao ni chama cha vurugu. Wakati viongozi w.a CCM wakiendelea kueneza chama ni rahisi kuona vurugu zinazoendelea na kuzihusisha na CDM.

Vurugu za Kasulu zinaweza kutumiwa kama yard stick na maeneo mengine. Hata kama watakaopinga watakuwa 10 , wakiweza kuvunja mkutano hilo litasambaa kama moto wa nyikani na kusababisha ugumu zaidi makao makuu

Hatudhani kupima nguvu ya upinzani ndani ya chama kwasasa ni kipimo kinachoweza kutumika katika hatua yoyote tarajiwa. CDM iwe taasisi inayosimama katika taratibu, sheria na kanuni na wala si personality. Kwanini Slaa ahangaike na wafuasi wa Zitto ambao wameamua kwa hiari yao kuwa wafuasi bila kuvunja kanuni yoyote ya CDM?

Ni vema Dr Slaa na wenzake wakasitisha ziara hizo, warudi kushughulikia mambo makao makuu ikiwa ni pamoja na kujibu tuhuma zinazotolewa ambazo hazina majibu muafaka na kuchukua hatua za kurejesha nidhamu makao makuu
 
KAULI YA MZEE MTEI

Kuna nyuzi inaendelea kuhusu kauli aliyoitoa mzee Edwin Mtei ambaye ni member wa JF.
Naweka nukuu kwa marejeo

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...chadema-lakini-ameamua-kuondoka-mwenyewe.html

Mzee Mtei amekuwa na kauli tata katika baadhi ya nyakati.
Hakuna sababu ya kumsihi asiongee kama Mtanzania mwingine na kama mwasisi wa CDM lakini kauli zake ziwe zimenyooka bila utata. Na endapo ananukuliwa vibaya ni vema akajitokeza na kuweka rekodi sawa badala ya kukaa kimya

Katika nyuzi inayoendelea hapo juu wachangiaji wameonekana kuchukua ushabiki zaidi badala ya mantiki.
Wapo wanao chochea mgogoro kwa kauli hiyo na wapo wanaotaka kuwasafisha wazee wa waraka kwa kutumia kauli hiyo

Kwa mtazamo wangu ambao si lazima uwe sahihi kwa kila mmoja, mzee Mtei amekataa suala la Mbowe kumuandaa mrithi wake kwa kuuliza ni kwa namna gani.

Katika nukuu hiyo kilichofuata ambacho sioni kama sentensi iliyounganika ni Mtei kusema 'tumemuandaa Arif ameondoka, Zitto anavuruga na Dr Kitila Mkumbo very good lakini anashiriki mambo tusiyoyaelewa'

Nadhani alimaanisha kuandaa kutokana na nafasi walizo nazo kwa kuwa watakuwa na uzoefu wa kutosha wa ukaribu na uhusika wa mambo ndani ya chama.

Ndivyo hata katika mshirika ilivyo ya kuwa kiongozi anapokuwa anakaimu nafasi, anapokuwa naibu au msaidiz ni sehemu ya kumuandaa kushika nafasi pindi inapotokea.

Sioni tatizo la kuandaa watu ndani ya chama na nimesema mara nyingi upinzani wa sera ndani ya chama chochote hukifanya kiwe imara. Sioni tatizo la kina Kitila kumuandaa Zitto kuwa kiongozi.

Tatizo ni njia walizotumia katika kufikia lengo hilo. Njia hizo ni pamoja na kuzusha mitafaruku kwa nayakati fulani kama ule wa Shonzo, Kafulila, masalia na ule wakati wa uchaguzi ambao Zitto aliuzusha makusudi pengine kumharibia mgombe wao kwa kuzua tafrani.

Tatizo ni maudhui ya waraka ambayo hayakulenga kuandaa mtu bali kashfa, kejeli matusi na kadhia nyingine.
Ni waraka wenye elements za kulaani mambo na kutafuta njia za kubomoa chama chao wenyewe kama alivyofanya Zitto.

Tatizo ni pale njia za ujasusi,usaliti na utoto zinapotumika ili mgombe wao awe na nafasi hata kwa gharama ya chama

Tataizo ni kuingiza mambo ambayo tayari yana tuhuma katika CDM kama kete yao ya ushindi.
Waraka umeeleza kuhusu udini ambao viongozi hao hao huhubiri majukwaani wamejifungia kuandika kwa namna nyingine kile wasichokitaka kitokee katika taifa.

Kuna tofauti za kuandaa kiongozi kwa njia za uongozi na kuandaa kiongozi wa mapinduzi kwa njia haramu na za kihaini kama zilzivyo katika waraka.

Hata hivyo kauli ya Mzee Mtei inaweza kuwa na tafsiri nyingi na hivyo ni vema angejitokeza na kuweka rekodi sawa.
Yaweza kuwa alinukuliwa vibaya na mwanadishi kwa malengo mengine
Yawezekana aliyeleta kipande kile cha mahojiano aliondoa baadhi ya kauli
Yawezekana kuna namna CDM wavyoandaa viongozi wao kama alivyodai
n.k.

Kwa vile mzee Edwin Mtei ni mmoja wetu tungemuomba atumie fursa hii kutusaidia kuelewa alilenga nini na kwasababu zipi, na je ndivyo alivyonukuliwa?

Hili litakisaidia chama chake kinachopita katika wakati mgumu ambacho hakihitaji msaada zaidi wa matatizo bali suluhu

Mzee Edwin Mtei karibu sana duru za siasa
 
Wadau mtanisamehe sana kwa haya nitakayosema kuhusu vyama vya siasa nchini.

Kwanza kaisa napenda kuwapongeza kwa hoja mutilibu zilizonipoza roho japo bado kabisa sikubaliani na maamuzi yanayofanywa na kundi la watu wanaojiita viongozi kuhusiana na kumvua kiongozi mwenzao kutokana na hila zilizopewa jina la Usaliti ama Uhaini. Na binafsi yangu sioni kosa la wanachama wa CCM kumtetea Zitto ikiwa hushangai kuona kuna baadhi yetu wana Chadema wanapingana na maamuzi hayo. Kwa nini tusisherehekee ama nasi ni wahaini vile vile.

Jambo nalotaka kuzungumzia n uundwaji wa vyama vyote vya Upinzani. Kusema kweli swala hili lilitokea tu kwamsukumo wa nchi za magharibi. vyama vikaundwa na wenyewe kina Mrema< Mtei na Sharrif Hamad na mtindo huo umeendelea hadi vyama vipya vinaundwa na mtu mmoja akikusanya wafuasi (wanachama) kama anavyotakiwa na sheria ya usajili. Havitokana na kupinga mrengo wala sera za CCM bali kujaza hoja ya kuwepo demokrasia ya vyama nchini.

Na maadam vyama hivi vimeundwa na wenyewe, yaani kila chama kina mwanzilishi wake, basi itabakia kuwa vyama vyetu vitaendelea kuwa na wenyewe. Ebu tuitazame CCM utagundua kwamba siku waloamua kuunda chama hiki, watu walifanya kikao na maamuzi yakapita. Mzee marehemu Ally Sykes atakumbukwa kwa kutoa jina la chama na pia uchaguzi ulipita ambapo Nyerere alishinda na kuwa kiongozi. Hivyo Nyerere sii mwanzilishi wa chama hiki bali kiongozi wa kwanza aliyechaguliwa kwa kura za wajumbe walokuwa na nafasi sawa za kugombea. Hii ndio tofauti kubwa baina ya CCM na vyama vingine vyote na ndio maana huko CCM kuna mvutano mkubwa wa uongozi iwe kwa siri ama uwazi, chama hicho hakina mwenyewe.

Ni hayo tu, haya ya kina Zitto na wengineo waliopita nyuma yao, bila shaka mfumo wa vyama ndio tatizo kubwa na demokrasia haiwezi kusimama ikiwa vyama vitaendelea kuundwa na mtu mmoja anayejisikia kufanya upinzani..
 
Wadau mtanisamehe sana kwa haya nitakayosema kuhusu vyama vya siasa nchini.
Kwanza kaisa napenda kuwapongeza kwa hoja mutilibu zilizonipoza roho japo bado kabisa sikubaliani na maamuzi yanayofanywa na kundi la watu wanaojiita viongozi kuhusiana na kumvua kiongozi mwenzao kutokana na hila zilizopewa jina la Usaliti ama Uhaini. Na binafsi yangu sioni kosa la wanachama wa CCM kumtetea Zitto ikiwa hushangai kuona kuna baadhi yetu wana Chadema wanapingana na maamuzi hayo. Kwa nini tusisherehekee ama nasi ni wahaini vile vile.

Jambo nalotaka kuzungumzia n uundwaji wa vyama vyote vya Upinzani. Kusema kweli swala hili lilitokea tu kwamsukumo wa nchi za magharibi. vyama vikaundwa na wenyewe kina Mrema< Mtei na Sharrif Hamad na mtindo huo umeendelea hadi vyama vipya vinaundwa na mtu mmoja akikusanya wafuasi (wanachama) kama anavyotakiwa na sheria ya usajili. Havitokana na kupinga mrengo wala sera za CCM bali kujaza hoja ya kuwepo demokrasia ya vyama nchini.

Na maadam vyama hivi vimeundwa na wenyewe, yaani kila chama kina mwanzilishi wake, basi itabakia kuwa vyama vyetu vitaendelea kuwa na wenyewe. Ebu tuitazame CCM utagundua kwamba siku waloamua kuunda chama hiki, watu walifanya kikao na maamuzi yakapita. Mzee marehemu Ally Sykes atakumbukwa kwa kutoa jina la chama na pia uchaguzi ulipita ambapo Nyerere alishinda na kuwa kiongozi.

Hivyo Nyerere sii mwanzilishi wa chama hiki bali kiongozi wa kwanza aliyechaguliwa kwa kura za wajumbe walokuwa na nafasi sawa za kugombea. Hii ndio tofauti kubwa baina ya CCM na vyama vingine vyote na ndio maana huko CCM kuna mvutano mkubwa wa uongozi iwe kwa siri ama uwazi, chama hicho hakina mwenyewe.

Ni hayo tu, haya ya kina Zitto na wengineo waliopita nyuma yao, bila shaka mfumo wa vyama ndio tatizo kubwa na demokrasia haiwezi kusimama ikiwa vyama vitaendelea kuundwa na mtu mmoja anayejisikia kufanya upinzani..
Mkuu Mkandara , ahsante kwa uungwana, mawazo yako kuhusu vyama vya upinzani hayana tatizo ,ndio njia inayotuwezesha kuyaangalia mambo kwa mitazamo tofauti na yenye kufikirisha.

Kuna kundi la viongozi ambalo limewavua uongozi wanaojiita viongozi
Wanaojiita viongozi ni hao waliokuwa katika uongozi kwa minajili ya espionage na wala si sehemu ya uongozi.
Hao ndio wanajiita maana hawakuwa katika uongozi kama waraka unavyosomeka hapo juu.

Hao wanaojiita viongozi wanaitwa wasaliti na wahaini kwasababu zilizowazi kabisa.
Wasaliti kwa kuwa walikuwa sehemu ya uongozi. Walipopanga uundwaji wa kanda walikuwemo, ukisoma waraka wao wanaponda uundwaji wa kanda hizo hizo walizoshauri, usaliti wa kiwango kizuri tu.

Ni wahaini kwasababu mipango ya espionage wakishirikiana katika ngazi ya taifa na mikoa ililenga kuleta mapinduzi.
Mbinu hiyo haina jina jingine isipokuwa uhaini.

Kuhusu CCM sina tatizo wakimtetea Zitto kwasababu ni sehemu ya watanzania.
Kinachosumbua akili ni pale utetezi hauna majibu dhidi ya uhalifu wa Zitto.
Tena wanAchotaka kukiona ni Zitto anabaki CDM kama kiongozi. Hoja yao anaonewa bila kusema kwa lipi.
Kwa fikra za kawaida CCM waliotoa kusudio la kuua upinzani kabla ya 2015 wasingeweza kushabiki CDM ibaki.

CCM wangehakikisha mtu anayewasumbua kwa hoja kama Zitto anaondoka katika mkondo huo kama walivyomvua Kaborou na wengine. La hasha! wao wanasisitiza kiongozi wa CDM awe Zitto.

Watu wanahoji huu wema wa CCM kwa wapinzani umeanza lini?
Na kwanini wema huo uwe kwa Zitto? Kwanini usiwe kwa waliotangulia?

Na endapo Zitto ni mtu muhimu sana kwa uongozi kwanini wasingemkaribisha CCM kwenye neema kama walivyowakaribisha vijana wa Zitto binti Shonzo na Mtela? Kwanini hawataki wanataka abaki huko huko,why?

Kuhusu uundwaji wa vyama ni lazima liwepo wazo halafu utekelezaji. Hakuna chama kinachoota kwa wingi siku moja.
Ni lazima kuwe na chanzo ambacho ni wazo. Tatizo linalokabili vyama vya siasa ni kuwa mtoa wazo anaweza kuhodhi shea fulani ndani ya chama hicho.

Tatizo la wanchama ni kuogopa personality na hivyo kushindwa kuvunja nguvu za waanzilishi.
Ndivyo Hamad Rashi alivyoshindwa na ndivyo Mrema alivyoshindwa ndani ya NCCR.
Njia moja muhimu ni kuvunja nguvu za waanzilishi kwa kufuata sheria, kanuni, na taratibu.

Mkuu, ndio maana unatakiwa uunge mkono hatua zozote za kuleta nidhamu.
Kinachoitesa CDM na CCM ni ukosefu wa nidhamu.

Nadhani uwapongeze CDM kwa hatua nusu na ya reja reja ya kudhibiti waanzilishi.
Tena kama unakumbuka Zitto alishasema CDM ameteseaka sana, ipo damu yake akimaanisha yeye ni mmoja wa mihimili ya CDM na hivyo yupo juu ya sheria.

Kwavile ni mhimili muhimu ndio maana ameachwa tu kila anapopanga uasi ambao umeitesa sana CDM kwa miaka mingi.
Hakuna jaribio la vurugu lisilo na mkono wa Zitto.

Ili kuleta nidhamu na kuondoa vyama vya siasa mikononi mwa waanzilishi au personality lazima ziwepo hatua madhubuti kabisa za kurejesha nidhamu hata kama zina gharama.
 
Mkuu labda hujanisoma vizuri na kutazama kwa undani mantiki ya hoja yangu.

Ni hivi Tanzania maadam vyama vina wenyewe kila mtu hapa ni mshabiki tu kama tunavyoshabikia Arsenal na MaU au Simba na Yanga. Hao unaowaita wana Chadema au CCM kusema kweli hawajui hata mrengo gani chama chao kinasimamia na hata ikitokea makosa ya msingi kukiuka nguzo za mrengo wao hawaoni maajabu.

Tumeyaona sana CCm ambao hadi nleo wanadai kuwa wanafuata siasa za UJAMAA na KUJITEGEMEA. wanasema wazi kuwa nchi yetu ni ya WAKULIMA na WAFANYAKAZI lakini0hawa ndio wamepuuzwa na ndio hesabu kubwa ya maskini nchini..watu bado wanaishabikia tena kwa nguvu zote kama Arsenal wanavyopiga magoli wakati hawana hata hisa moja.

Binafsi yangu nimeshasema wazi kabisa sipendi na wala sina Ushabiki. Sii mwaa Simba wala yanga ila hutazama mpira na kusifia timu inayofanya vizuri. Hu bet ktk mechi tofauti pasipo fikra za ushabiki ila mtazamo wangu ktk pambano hilo. Na ndivyo nilivyojiunga Chadema sii kwa ushabiki bali kwa kufahamu kuwa Chadema ina nafasi kubwa na nzuri ya kuishinda CCM. hayo ya katiba na sijui Uhaini ama usaliti wakati tunapoteza tumaini la Ushindi kusema kweli binafsi yangu sintoafiki.

Nimejifunza tokana na makosa ya NCCR mageuzi na CUF, wote hawa walidai haya haya ya Usaliti na Uhaini wakapoteza nuru yao,leo hii ni vyama visivyokuwa na tumaini. Huko ndio KUFA kwa chama unaozungumziwa na sii kufutika kabisa..Ni kiswahili tu cha mjini haina maana hapatakuwa na Chadema tena. Hivyo tulishuhudia kifo cha NCCR na CUF japo wapo bado na ofisi zao. Kurudia makosa ama kutojifunza kutokanana makosa ya wengine ni Ujinga mwingine ambao sintokubaliana nao.

Pili, hao CCM wanaopinga maamuzi ya viongozi wetu ni ktk mpango wa kuendeleza kutuvuruga. wanajua wazi kuondoka kwa Zitto kutaleta utata zaidi kila wanapozungumzia hasa ktk maswala ya Udini, Ukanda na Ukabila. Hivyo ni ktk mikakati yao ya kutumaliza na sisi tumeingia kichwa kichwa. Usitegemee watanyamaza leo wala usishangae maana hii ni vita yao dhidi ya Chadema na wapo wengi wataamini kuwa Zitto hakufanyiwa haki kwa sababu ya....Hivyo, we did take the bull by it's horns tusilalamike!

Mimi nasema tu ya kwamba, kupoteza tumaini la ushindi ndio pekee kinachanikera kwa sababu tumecheza karata ambayo CCM walikuwa wanaisubiri kwa hamu miaka yote. na sipo Chadema kufurahia uanachama ama kufuata katiba ya chama bali imani yangu ya mrengo na sera zake. Hakuna mtu anayeweza kunifuta ama kuninyang'anya uanachama kwa sababu hii ni imani yangu kuwa upande wa kati kulia na Chadema ndiye mwakilishi wa mrengo huu.

Kwa maana hiyo,pengine mimi natofautiana sana na wanachama wengine wa Chadema ambao wamejiunga kwa sababu ya Mbowe, Zitto au ushabiki wa chama tukifungwa haina taabu kuna uchaguzi mwingine kama mpira vile. Hivyo maamuzi yoyote nanayotuondolea tumaini la ushindi mwaka 2015 nitapingana nayo kwa sababu hatupo mpirani wala mchezo wa sports.

Na labda nikukumbushe tu ktk historia ya CCM ya kwamba kabla TAA haijawa chama cha kisiasa, Abdul Wahid na Mwapachu walifanya mapinduzi ya kuuondoa uongozi wa Mzee Kreist Sykes ili kukifanya chama hicho kiwe cha kisiasa badala ya chama cha wazee wa mujini. Ni mapinduzi ambayo ndiyo yalokuja tuletea Uhuru wetu, pengine kama sii mapinduzi hayo tusingekuwa tunazungumzia CCM leo hii. tena basi Mzee Kreist alikuwa baba yake mzazi na Abdul Wahid Je, kuna usaliti ama uhaini zaidi ya huo? Sidhani lakini toka hapo TANU ilijengeka na kuwa chama chenye wasomi na watu wa makabila na dini tofauti..

Mkuu tusiogope mabadiliko, usaliti hauwezi kuwa kwa mtu ama kiongozi usaliti na uhaini ni wa kuvunja chama sio mkakati wa kubadilisha uongozi ifikapo uchaguzi wa mwaka 2015. tena basi huo waraka unajieleza wazi kwa kichwa cha habari ukilenga mabadiliko ktk uchaguzi wa mwaka 2013. Mapinduzi yasingelenga siku ya uchaguzi bali yangetokea kwa uvamizi wa ofisi ya makao makuu na kubadilisha ama kudai mapinfuzi.

Mwisho mkuu wangu hapa nilipo sina matumaini ya ushindi mwaka 2015, sina na nitasema wazi kuwa tutakuja jutia utengano ambao hauna maana kabisa kwa sababu huyo Kitila na Zitto wasingeweza kabisa kubadilisha kura za wajumbe wote dhidi ya mgombea ambaye anapendwa na wananchama. Sidhani kaa wana uwezo wa kushawishi kwa fedha ama lugha ambayo kweli ingemkosha Zitto na kuchukua Uenyekiti - Sidhani maana tayari jina la Zitto ktk uenyekiti limekwisha haribiwa.
 
Mrema aliweka historia kuwa kiongozi wa kwanza wa upinzani kubebwa na kusukumwa kwenye gari.

Slaa ameweka historia kuwa kiongozi wa kwanza wa upinzani kurushiwa mawe na kufukuzwa jukwaani kwa mabango.

Lipumba aliweka historia kuwa kiongozi wa kwanza wa upinzani kupewa kibano na polisi.

Slaa ameweka historia kuwa kiongozi wa kwanza wa upinzani kuwaamrisha polisi wawadhibiti wananchi na kuokolewa na kuhifadhiwa na polisi ili asidhuriwe.

Haya yote ni maendeleo...
 
ZeMarcopolo,

Nadhani kuna vitu unaruka katika historia ya nchi yetu, kwa mfano yaliyomkuta mwalimu nyerere wa TANU dhidi ya chama tawala cha mkoloni cha United Tanganyika Party (UTP). Kwa mfano, kesi yake tarehe 9 December 1958 ambapo ilikuwa afungwe jela au kulipa faini ya shilingi 3,000 (sawa na £150 za wakati huo), na isingekuwa wahindi - kina Jhaveri from the Asian association, Nyerere angekuwa kiongozi wa kwanza kufungwa jela na serikali kwa maneno ya uchochezi na matusi dhidi ya wakuu wa wilaya waliokuwa wananyanyasa TANU katika harakati zake za kuwakomboa wananchi. Pia kuna kina Zuberi Mtemvu wa Chama cha upinzani cha ANC kabla ya ukoloni na ndani ya Tanganyika huru ambao walipata misukusuko mikubwa mpaka pale mfumo wa vyama vingi ulipopigwa marufuku rasmi mwaka 1965, na wengine kadhaa - bila ya kumsahau shujaa wetu "christopher mtikila. Matukio yote haya ilikuwa ni harakati za kuwakomboa wananchi kupitia political movement (TANU) na DP ya Mtikila ambayo ilikuwa ni more of a pressure group kudai mengi including kurudi kwa Tanganyika, chama cha upinzani (ANC chini ya zuberi mtemvu) ambapo Mtemvu ilisemekana alikuwa anatumiwa na wakoloni/imperialists kuhujumu TANU, accussations zile zile za leo dhidi ya zitto kwamba anatumika na ccm kuhujumu chadema. Hakika historia hujirudia.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Interesting indeed.

Post yangu ilitarget "contemporary" multipartism in modern Tanzania.

Nitarudi baadae kuchambua uungwana na ziara ta Dr. Slaa Kigoma.
 
Last edited by a moderator:
Mrema aliweka historia kuwa kiongozi wa kwanza wa upinzani kubebwa na kusukumwa kwenye gari.

Slaa ameweka historia kuwa kiongozi wa kwanza wa upinzani kurushiwa mawe na kufukuzwa jukwaani kwa mabango.

Lipumba aliweka historia kuwa kiongozi wa kwanza wa upinzani kupewa kibano na polisi.

Slaa ameweka historia kuwa kiongozi wa kwanza wa upinzani kuwaamrisha polisi wawadhibiti wananchi na kuokolewa na kuhifadhiwa na polisi ili asidhuriwe.

Haya yote ni maendeleo...
Mkuu, mbona unatutoa kwenye hoja? Mkandara kasema hapo juu ni hatari sana kushabikia siasa kama tufanyavyo kwa Man U au Asenali. Nadhani hatupo katika kulinganisha au kueleza madhila ya viongozi nje ya mada. Kama tutafanya hivyo ni kwasababu ya kujenga hoja. Kuna uwezekano unataka kujenga hoja, labda ututanabaishe ni ipi hiyo kulingana na mifano na mada iliyopo?
 
Last edited by a moderator:
Interesting indeed.

Post yangu ilitarget "contemporary" multipartism in modern Tanzania.

Nitarudi baadae kuchambua uungwana na ziara ta Dr. Slaa Kigoma.

Wakati unajiandaa na uchambuzi wa ziara ya Dr. Slaa Kigoma, kwa utafiti wangu mdogo, nimebaini kwamba ratiba ya ziara hiyo ilishawekwa siku nyingi na kwa bahati mbaya au nzuri kutegemeana utaegemea upande upi wa hoja, tarehe za Kigoma zikaingiliana na sakata la zitto kuvuliwa madaraka ndani ya chama. Maswali yanayofuatia kiuchambuzi ni -given kwamba ratiba ya ziara ya Dr. Slaa Kigoma ilikuwepo siku nyingi, je:

*iIlikuwa ni busara kuikatisha ziara husika kwa sababu ya maamuzi yaliyojitokeza ndani ya CC ya Chadema?
*uamuzi wa kukatisha ziara ungekuwa na madhara on consistency and integrity ya chama na taratibu zake, kanuni zake, itifaki zake na katiba yake?
*Je, kuna utofauti gani baina ya ziara hii na ile ya Nape nchi nzima baada ya CC ya CCM kutangaza wajumbe watatu wa CC kama magamba ambayo yanatakiwa kuvuliwa, na Je, ukimya wa Nape katika hili ulitokana na aliyokutana nayo katika ziara hizo au ni kwa sababu ya kitu kingine?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu Mkandara

Kama nitakuwa nimekuelewa vizuri una hoja zifuatazo
1. Kwamba CCM wanashangilia mgogoro uliopo
Sina shaka na hilo na tumewahi kulisema. Lakini pia hakuna shoka linalokata bila mpini.

Ni wajibu wa viongozi kuelewa hilo kabla ya washabiki wa 'Man U na Arseanal' ambao hawana hisa.
Laiti Mkumbo na Zitto wangesimama kidete na hadharani waksema yanayowafunda CCM wasingepata pa kuingilia.

Hiyo ingekuwa karata ya ukomavu wa kisiasa.
Ni karata hiyo ndiyo CCM wanaitumia kuwananga mawaziri katika serikali yako.

Mkumbo na Zitto walikuwa na nafasi ya kuongoza ili CCM wafuate.
Hawakufanya hivyo, nao kama CCM wakajiunga na mfumo wa mtandao bila kujua zama zinabadilika na huko wanakoelekea siko, ni kule kulikopelekea taifa kumkosa Salim Ahmed.

2. Kama yangekuwepo mapinduzi milango ingevunjwa!
Labda kama tuna tafsiri tofauti ya mapinduzi. Mapinduzi si lazima yaambatane na ngeu.

Nimechungulia katika Merriam-webster nikaokoteza vi- def miongoni mwa nyingi sijui kama zita kidhi haja
-''a fundamental change in political organization; especially: the overthrow or renunciation of one government or ruler and the substitution of another by the governed'
-'Revolution-a fundamental change in the way of thinking about or visualizing something'

Walichokusudia hao mabwana hakipo mbali sana na tafsiri nyingi za mapinduzi ndio maana waraka umesema wazi kabisa'iwe siri kubwa na watafutwe watu waaminifu' ili kuwaondoa viongozi haraka iwezekanavyo kwa mujibu wa waraka

Hoja yangu ni kuwa nafasi ya wao kutumia uhuru na demokrasia hawakuitumia, walichokifanya kinafanana sana na njama tena zinazomitiliana na maudhui ya mapinduzi.

3. Kuondoa viongozi ni kupinga mabadiliko
Sina tatizo na kuondoa viongozi. Mandela aliuzwa na CNN je ikitokea ukafanyiwa kama alivyofanyiwa J.F.Kennedy analionaje suala hilo. Mandela akajibu, viongozi ni watu wa kuja na kupita lakini taasisi ni kitu kilichopo.
Kwa muktadha huo huo nasema viongozi wanakuja na kuondoka hivyo sipo kusema nani kiongozi mzuri n.k.

Ninachosisitiza ni kuwa taasisi zipo hata kama viongozi wanakuja na kuondoka.
Kilichokusudiwa na Zitto/Mkumbo ni kuharibu maana ya taasisi kwa kukiuka misingi ya uongozi, maadili, kufuata utawala wa sheria na kusimamia demokrasia.Njia waliyotaka kuitumia ili kupata viongozi wanaokuja na kuondoka siyo njia iliyokusudiwa kwa maana ya demokrasia. Ni njia iliyokusidia kuangamiza taasisi hata kama wao wanakuja na wataondoka

4. Kwamba Zitto na Kitila wasingeweza kubadili mwelekeo wa kura
Hakuna tatizo kuandaa mikakati ya kisiasa tena ikiwa katika sera. Hakuna tatizo wao kuwa viongozi.

Lipo tatizo wao kuwa sehemu ya viongozi halafu kurudi nyuma na kughilibu umma na hasa vijana.
Wamewaghilibu vijana wengi kwa kuwaaminisha kuwa Mbowe hana akili na elimu yake ni magumashi.
Kwa watu wenye weledi kiwango chao hiyo si njia njema kuelekea katika demokrasia na mbadiliko ndani ya chama chao kwanza.

5. Watu wasiogope mabadiliko kwani kufanya hivyo ni kuondoa matumaini
Ni kweli lakini matumaini hayaji kwa kejeli, kashfa, majungu, ukanda na udini.

Hiyo ni njia nyepesi ya kuligawa taifa.Inachukua sentensi moja kuligawa taifa na miaka zaidi ya 10 kuliunganisha taifa kwa kauli hiyo tena kwa gharama kubwa.Kinachotokea Nigeria ni kauli za miaka 100 iliyopita za vongozi. Ni kauli hizo ndizo zilipelekea mauaji Kenya.Mabadiliko wanayohitaji watu ni socioeconomic.
Siyo mabadiliko kwasababu fulani hana degree au fulani anazo nyingi.

6. Abdul Sykes na wenzake walifanya mapinduzi
Kwa zama hizo kulikuwa hakuna muda wa kuongea na dhalimu. Ilikuwa kuchukua hatua za dharura na makusudi.
Miaka 50 baada yao hatupaswi kurudi kule walikoanzia.

Kila kitabu na zama zake, hizi ni za kitabu kingine.
Kama tutachukua model za kina Abdul basi zile degree, diploma na honorary zilizotajwa katika waraka hazina maana.
Na kwanini basi Mbowe ahukumiwe kwa elimu ndogo kama ya Abdul wakati huo huo Abdul aonekane shujaa?

Mkuu, nadhani kuna umuhimu wa kujenga nidhamu. Hapa tulipo ni matokeo ya viongozi kukosa nidhamu.
Hatuwezi kuwa na template ya namna hiyo tena tuakatumaini mabadiliko yatakuja.

Mabadiliko hayateremki kama mvua, yanaundwa.
Mabadiliko hayaanzi kutoka juu yanaanza kutoka chini. Huwezi kupata kiongozi mzuri ngazi ya taifa kama hukuanza na viongozi wazuri ndani ya vyama na serikali za vijiji. Nidhamu ifuatwe bila kuangalia makunyanzi.

Tusipojenga nidhamu tutarudi kule kule kwa siku 30,60, 60 na sasa 720 za kuvuana magamba.
Nchi hii haina upungufu wa viongozi, ina upungufu wa kupata viongozi.
Tuanze kurekbisha wapi kama si kuweka msingi wa nidhamu?
 
Last edited by a moderator:
Wakati unajiandaa na uchambuzi wa ziara ya Dr. Slaa Kigoma, kwa utafiti wangu mdogo, nimebaini kwamba ratiba ya ziara hiyo ilishawekwa siku nyingi na kwa bahati mbaya au nzuri kutegemeana utaegemea upande upi wa hoja, tarehe za Kigoma zikaingiliana na sakata la zitto kuvuliwa madaraka ndani ya chama. Maswali yanayofuatia kiuchambuzi ni -given kwamba ratiba ya ziara ya Dr. Slaa Kigoma ilikuwepo siku nyingi, je:

*iIlikuwa ni busara kuikatisha ziara husika kwa sababu ya maamuzi yaliyojitokeza ndani ya CC ya Chadema?
*uamuzi wa kukatisha ziara ungekuwa na madhara on consistency and integrity ya chama na taratibu zake, kanuni zake, itifaki zake na katiba yake?
*Je, kuna utofauti gani baina ya ziara hii na ile ya Nape nchi nzima baada ya CC ya CCM kutangaza wajumbe watatu wa CC kama magamba ambayo yanatakiwa kuvuliwa, na Je, ukimya wa Nape katika hili ulitokana na aliyokutana nayo katika ziara hizo au ni kwa sababu ya kitu kingine?
Hewalaa! Hili neno. Ahsante
 
It is quite unfortunate that an old man as Dr.Slaa seems to lack fundamental wisdom that comes with old age.There is no denying that Zitto is ambitious, there is no denying that he is squarely against medicrity in Tanzanian politics,there is no denying that he tries to stand out from his fellow "sheep" MPs from CDM even this sometimes brings him to odds with his peers. It is quite obvious that, in CDM leader's eyes ZITTO ni mkosaji, but..., as jesus once famously said, he who is without sin should be the first to throw a stone...,

what we are seeing here is hypocrisy at it's highest stage, same CDM who claimed CCM are opposing freedom of speech wont even let their leader have his.same CDM who are actively trying to remove CCM from power would not tolerate power struggle within itself.

who is naive enough among CDM to believe that not a few of them are aspiring to become party leaders?who is naive enough to even claim that the entire party has a single view on everything?
If CDM can't stand opposition from within will it even tolerate outside opposition once in power? I would have respected Slaa, Mbowe and Team if they called Zitto, told him that we understand what you are trying to do, and we don't like it,but we will co-exist with you.
Kikwete off all his shortcomings gets called funny names by every dick and harry in this country, but no one has been labeled msaliti,mhaini etc.

Then there is another group of CDM supporters who becuase of their medicrity thinks people like LISSU,Mnyika et.al wont do no wrong. they worship and clap at whatever comes out of their mouths.this is something else that is wrong with CDM. there are a bunch of leaders who can't take a NO,and who thinks they are always right.

Here is a piece of advice, no matter how right you are regarding ZITTO and his supporters, i think CHADEMA has missed a big point in this whole fiasco, to me,and many who thinks alike, they have ceased to be a serious party, they are now more or less a popular party. And this won't be enough to take power. This is something that has come as a test to CDM.as we mourn Mandela, CDM has even been given a marking scheme,it's all in the wall for them to see, agenda of the room is reconciliation, not punishment and alienation.

I so long for a day Tanzania has a proper political party. CCM is too rotten to be saved and CHADEMA is just so much a mess to be cherished.

I guess they were right when they said, people choose leaders they deserve.

its painful truth that must be swallowed that we deserve CCM and soon we might deserve a mess that CDM is. Unless of-course if we decide to take action
 
Post yangu nimeirekebisha ili ijumlishe maswala yaliyoibuliwa na Mchambuzi hapo juu.

Uungwana ni vitendo.

Muungwana anapomtembelea mtu humuuliza mtu huyo "una hali gani?" wakati huo muungwana huwa tayari kusikiliza na kumfariji mwenzake kwa lile jibu atakalotoa.

Zitto ni kielelezo cha mkoa wa Kigoma katika siasa za Tanzania. Kigoma inajivunia vitu vingi, kimoja wapo ni kuwa na mwanasiasa hodari - Zitto Kabwe.

Zitto anapopatwa na misukosuko inayomuondolea sifa nzuri katika utendaji wake, wananchi wa Kigoma wanakuwa na dukuduku la kujua ni nini hasa kimetokea na hatma yake ni nini.

Ni uungwana kwa yeyote atakayeenda kwa watu wa Kigoma kwa kipindi kuwa tayari kusikiliza dukuduku hilo la watu wa Kigoma na kuwa tayari kuwafariji katika hali hiyo. Huu ni uungwana wa kitanzania au wa kiafrika kwa upana zaidi.

Siku chache kabla Dr. Slaa hajafunga safari ya Kigoma alitangaza kuwa ni MARUFUKU kwa wanachama wote wa Chadema kujadili swala la Zitto kuvuliwa nyadhifa alizokuwa nazo ndani ya Chadema. Hii ni kumaanisha kuwa kila mwanachama anayemheshimu Dr. Slaa kama Katibu Mkuu anapaswa kukaa kimya kuhusu swala hili mpaka pale Zitto atakapojibu na hukumu ya mwisho kutolewa.

Kiungwana, kauli hii ya Slaa moja kwa moja ilipaswa kumaanisha kuwa ataahirisha safari yake ya Kigoma ambayo imeelezewa bila ushahidi wa kutosha kuwa ilipangwa muda mrefu.

Si uungwana kwa Dr. Slaa kwenda Kigoma leo hii na kuwaambia watu wa Kigoma wasiongelee swala linalowatatiza zaidi kisiasa.

Kwa lugha nyingine ni kwamba safari ya Slaa Kigoma imechochea mijadala ambayo alitangaza kuifunga. Huu si uungwana.

Ninaweza kufananisha kitendo hiki cha Slaa na mtu anayemtembelea jirani yake ambaye amevunjiak mguu yuko kitandani akiwa na maumivu. Mtu huyo kabla ya kumtembelea jirani yake anatuma ujumbe kwamba hataki swala la maumivu ya mguu wa huyo jirani yake liongelewe!

Swali watakalouliza waungwana ni je, kwanini huyu bwana asisubiri mpaka mwenzie maumivu ya mguu yapungue ndio aje kumtembelea. Jibu likitolewa kwamba ni kwa sababu safari hiyo ilipangwa tangu awali litakuwa halitoshelezi, LIMEPWAYA MNO.
Kupwaya kwa jibu hilo kunatokana na ukweli kwamba utu uzima na busara ni pamoja na uwezo wa kubadilisha mipango kulingana na hali halisi inavyobadilika. Hata baba mwenye nyumba inapofika siku ya kukusanya kodi yake akiona mpangaji wake amefiwa na mwanae si uungwana kusema kuwa alishapanga kukusanya kodi tarehe hiyo kwa hiyo ataulizia tu kodi yake.

Hali ingekuwa tofauti kidogo iwapo Dr. Slaa asingepiga marufuku wanachama wa Chadema kujadili sakata hili. Hata hivyo bado kuna kingine cha kuangaliwa.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Kigoma alitoa rai kuwa huu si muda muafaka kwa Slaa kutembelea Kigoma. Alishauri Slaa asubiri mpaka hatma ya sakata la Zitto ifahamike.

Mwenyekiti wa Mkoa anaufahamu mkoa huo kisiasa zaidi ya Kiongozi yeyote wa makao makuu. Kupuuzia ushauri wake si uungwana.

Taarifa nilizopata juzi ni kwamba ofisi ya mwenyekiti huyo wa Chadema mkoa wa Kigoma ilikuwa haijajibiwa barua aliyoandika makao makuu kushauri ziara hiyo ya Slaa iahirishwe. Barua hii aliyoandika mwenyekiti iliwakilisha maamuzi ya vikao halali vya chama. Kutokuijibu na kutokuheshimu ushauri walioutoa sio uungwana.

Hii inafanana sana na jinsi Mh. Arfi alipotangaza kujiuzuru nafasi yake ya makamu mwenyekiti na ofisi ya chadema makao makuu haijasema chochote juu ya hilo!

Uungwana ni vitendo. Safari ya Slaa kigoma katikati ya sakata hili sio ya kiungwana na inatoa picha kwamba swala hili zima linafanyika katika mazingira yasiyo ya kiungwana ikiwa ni pamoja na kupuuzia michango ya viongozi mbalimbali ndani ya chama.

Swala la Nape sijalizungumzia kwa sababu sidhani kama Slaa anachopaswa kufanya ni kufuatisha matendo ya Nape.

NB: Wakati tunatafakari hili, naomba pia mtafakari kauli ya "founder cum owner" wa Chadema Mzee Edwin Mtei kuhusu kumuandaa Mh. Arfi kuwa Mwenyekiti wa chadema.

Kigoma protests.jpg

Cc Mkandara
 
Back
Top Bottom