Zinedine
JF-Expert Member
- Apr 9, 2011
- 1,187
- 694
Mwisho, kuhusiana na nini kifanyike baada ya siku kumi na nne kumalizika, naungana mkono na wewe, lakini niongezee tu kwamba chadema kimvue uanachama zitto LAKINI kimpe nafasi ya kuomba tena uanachama wa chadema na kikae na kushauriana iwapo itafaa kumruhusu tena awe mwanachama au hapana. Asipoomba, hilo litakuwa ni kosa lake, na umma utaliona hivyo kwani kwa waraka ule, hiyo ni adhabu stahili kwa mujibu wa katiba ya chama chake. Sasa chadema isimamie hilo.
Nini itakuwa madhara yake? Umejadili vyema kuhusiana na 2015 kwani kuna dalili kwamba chadema wamejipanga sana kuingia ikulu 2015, na hata Mbowe alishasema na kunukuliwa na vyomba vya habari kwamba, Chadema isipochukua nchi, basi atajiuzulu siasa. Kwa kauli hii, iwapo maamuzi ya CC baada ya siku kumi na nne kupita yatalenga zaidi malengo ya chama 2015, hakika chadema watafunika kombe mwanaharamu wapite.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Nikubaliana nawe katika masuala mengi uliyobainisha kwenye post hii, lakini hapa kwenye conclusion yako, iko vema lakini sidhani kama itazingatiwa na pande mbili zote. Kwamba possibility ya CDM kumtimua (kumvua uanachama) Zitto ni kubwa sana kwani squad yote ya CDM haina mtizamo kuwa na compromise na Zitto katika hili lakini sioni dalili za Zitto kuomba tena uanachama iwapo atavuliwa uanachama. Kwasababu ukijaribu kumsoma Zitto katika maelezo yake, anaamini kwamba yeye ni "Innocent" katika haya yanayoendelea na kwamba kinachofanywa na CDM ni kama kutotothamini mchango wake katika Chama.
Hata hivyo, akitokea kufuata ushauri huu wa kuomba tena uanachama, in the short run atakuwa looser ingawa in a long run anaweza kuwa Hero wa Siasa za baadaye. Kwa upande mwingine, iwapo CDM kumtimua uanachama na kumpa nafasi ya kuomba tena na kaomba, in the short run, baadhi ya wana CDM watakuwa winners ingawa in the long run watakuwa looser. Binafsi naona ikitokea ametimuliwa, ni vema ajiondoe kwenye siasa(kama Lamwai), lakini hii ni option ambayo siioni kwake. Nasema hivyo ni kwasababu naamini kwamba back-up ya Zitto iko kutoka pande zote tatu, baadhi ya wana CDM, wana CCM na wasio na vyama ambao wanaamini Zitto "akikomaa" anaweza kuisaidia sana nchi, hivyo possibility ya kupata uteuzi wa kitendaji kutoka Taasisi za Umma au binafsi ni kubwa.