Bado unahamisha goli, endapo hoja ya umalaya inahusishwa na uongozi wa chama, kwanini hoja ya mapenzi kwa 'tunayemtaka' ipewe uhalali tukijua itahusishwa na chama pia.
The bottom line ni kuwa mapenzi na uongozi havijengi taswira nzuri kwa mujibu wa waraka regardless nani anafanya hivyo. Double standards zina matatizo na ndicho chanzo cha kusema waraka ni too low, haukuandikwa kama muongozo wa kisiasa bali chuki za kujenga uhalali fulani.
Mkuu Nguruvi3, sihamishi goli, naomba kusisitiza kuwa "malaya" ni yule tuu mwenye ndoa, anayetoka nje ya ndoa!. Kijana ambaye bado hajaoa, akibadili mpenzi, its presumed, he is still searching for the right one!. Lazima tukubali the times za enzi za mababu zetu za single choice tena head hunting, ambapo bibi na mama zetu were head hunted and pointed only once and for all tena wakiwa sealed!, they've long gone!.
Mimi nilioa ay 25 years straight from TSJ na wife akiwa ni class mate wangu, darasa letu likiwa na wanafunzi 24 tuu, 12 boys na 12 girls na out of darasa letu six couples walioana!. Hivyo my boys and girls are my friends kama wadogo zangu!. Sasa hao wasichana 12 tuu hapo darasani, kabla couples hazistabilize na kuja kuishia altareni, search, trios and erros za compactibility zilifanyika, jee hizi seach utaziita umalaya?!.
Kwa vile Jemedari is commited, he is expected to practice zero graizing, lakini MM, is not yet commited, so he has the right to graze without being called names!. Nikiwa UDSM, nilimfahamu binti fulani from Christian family, well mannered aliyeamua kufuata mafundisho ya dini, to keep the seal till defloration day!. (Wengine wetu tumejaaliwa a third eye to see the seal!, tulipoanza first year, seals chache ziliweza kuhesabika!, by mwaka wa nne, there was no seal na hakuna ndoa!). Waoaji wa kisasa sio kama wale wa zamani, laliza wavifitishe kwanza viatu kama vina wafit ndipo wanunue na kuvivaa!. Binti wa watu baada ya kuona miaka inapita na umri wa kuolewa unazidi kusogea, akajikuta hana jinsi, bali kukubali kuishi maisha ya ukweli ya dunia hii na sio tuu kufuata maisha ya kufikirika kwenye mafundisho ya duni, mila na desturi!, tulipofika 4th year, akajikuta amekubali kufitisha kiatu kwa hope anayefitisha kitamtosha!, hakikumtosha!, internship akamfitisha mwingine!, hakikumtosha!. Sasa ana kazi nzuri tuu, na amemfitisha mwingine!, sijui kama kitamtosha!, kiukweli huyu binti unaweza kumuita malaya?!.
Kwenye hoja ya umalaya kwenye waraka, nasisitiza hakuna double standards zozote!.
Ila pia Mkuu Nguruvi3, kitendo cha kuubeza waraka kama hivi
The bottom line waraka ni too low, haukuandikwa kama muongozo wa kisiasa bali chuki za kujenga uhalali fulani
sio kuutendea haki!. Kiukweli kila member humu anazo standards zake kwa ma GT mbalimbali humu jf, kwenye list yangu, Mkuu Nguruvi3, umo kwenye top 3!, nilikuambia tatizo lako ni dogo tuu, ume take side!, kitendo ambacho kimepelekea wewe kupata a little blurred vision ya waraka, hivyo kwa kiasi kikubwa umepoteza objectivity na impartiality yako katika kuuhukumu waraka, ndio maana saa zote unauponda!. Nakushauri vua hiyo miwani ya upande unaoigemea, usome tena waraka, nimekueleza waraka ule ni "The Creation of a Winning Coalition", hii ni very valid political theory!, its a great piece of political litarature!, tena namsisitiza Dr. Kitila aifanyie taratibu za kisomi, utumiwe kama "a working document" katika somo la political science kwa vyuo vikuu vya hapa nchini!.
Please don't let me down na wale wenye mawazo kama mimi, nikakusogeza out of the top 3!. Baadhi ya GT wa calibre na level yako humu, waliomua ku take side, wameeleza wazi humu upande wao kisha wamejinyamazia!. Wewe ume take side halafu unaendelea kuubeza waraka, sio kujitendea haki!, please utendee haki waraka!.
Pasco.