Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #321
Suala zima limefanyika katika mtazamo wa uchaguzi.Wakuu mag3 na nguruvi3,mna maoni gani kuhusiana na kura ya turufu ya rais obama kwenye mswada wa JASTA,kukataliwa na bunge la congress,hakuna athari ya moja kwa moja kwenye uchaguzi wa november kwa wagombea hawa wanaochuana vikali!!?? Km mswada utabaki hivi na kuwa sheria,nani atanufaika kati ya Replican na Democrat na km wabunge watabatilisha uamzi wao nani atanufaika!!? Nimesoma mahali baadhi ya wabunge wa replican wameanza kujutia maamuzi yao. Hebu nipeni maoni yenu..
Mswada umepingwa katika hali ya kuchonganisha wananchi na Obama/Democrats
Akiongea na Veterans Obama amelieza vema kwanini ali veto.
Ukiangalia kura ndani ya seneti na congress mswada umepita kirahisi na kwa kura nyingi bila kujali vyama
Hili maana yake ilikuwa kutengeneza mazingira kuwa Democrats wanakataa familia zisiweze kushtaki Saudia.
Kwa maneno mengine ni kuwaweka Democrats wanaogombea seneti na congress katika mazingira ya kushindwa
Nao kwa kuhofia 'backlash' ya wananchi wakapinga veto
Katika mdahalo ujao hili litaulizwa wagombea walitolee ufafanuzi
Clinton ana wakati mgumu kumpinga Obama au kukubaliana na wabunge.
Trump anaweza kusimama nalo limjenge, lakini lazima awe na ufahamu wa kutosha kuhusu mambo ya ulinzi, kinyume chake lita mu'expose' katika mazingira mengine magumu kama ilivyokuwa NATO mdahalo uliopita
Hata hivyo karata zinaweza kuchezwa na Dem ili kuhakikisha haliathiri matokeo ya uchaguzi na haliwi agenda katika siku za mwisho
Obama haku veto kwasababu tu alitaka.
Alifanya hivyo kwa kuzingatia usalama na masilahi ya nchi.
Alikuwa na taarifa kutoka vyombo vya ulinzi na usalama.
Sasa kwamba lina athari katika uchaguzi, hilo ni wazi kwasababu nia nzima ililenga uchaguzi na itaendelea kuwa hivyo.