Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

GOP TURMOIL

BEN CARSON NAYE ALAANI

Democrats na Hillary Clinton wamekaa pembeni makusudi wakiacha GOP wajikaange kwa mafuata yao
Katika hali isiyotarajiwa, mgombea wa zamani Dr Ben Carson ambaye ni mtiifu kwa Trump amelaani tukio

Kinachozua tafrani katika sakata hili ni jinsi linavyohusishwa na Republican.
Tangu video itoke, wapiga debe wakiwemo wa GOP wamezungumzia umuhimu wa GOP kujtakasa na sakata

Ukubwa wake ni pale ulipogusa wanawake kwa ujumla wake. Inaonekana mgombea wa Republican ambaye ametiliwa shaka mara nyingi kuhusu maadili yake sasa anabeba message inayowaumiza Republican

GOP wanachokifanya ni kujitenga na kauli za Trump ili zisiwe za chama kwa ujumla
Athari zake zinaweza kwenda mbali hadi uchaguzi wa maseneta na wabunge

Kama Trump atalihusisha na Clinton hilo litakuwa kosa.

Bill Clinton hagombei Urasi, na Hillary ni victim wa mauza uza ya Bill.
Hivyo atapata sympathy ya wanawake kuliko ku balance, kama Trump anavyodhani

Lakini pia litaibua mjadala mpana wa video ya leo na kuleta uharibifu mkubwa katika mjadala wa kesho kwa upande wa Trump

Tunafuatilia kwa ukaribu hali ilivyo

Mkuu Nguruvi3, asante kwa uchambuzi makini mnaoendelea kutujuza pia shule tunaipata,
Ila nimeshangaa sana Daktari bingwa Ben Carson ni mpiga debe wake mkubwa sana Trump na hata hili swala la video bado kamtetea kwa nguvu pamoja na kulaani, yeye anaamini video imetoka kufunika emails za Clinton. Na kaenda mbali zaidi kwa kusema Trump ana wafuasi waaminifu huku Clinton ana wafuasi waiso waaminifu na kwamba uchaguzi huu Trump atashinda. Nimesoma kwenye ukurasa wake wa Facebook nimeshangaa sana.

1 hr ·

Facebook Mentions

·

The recent disclosure of lewd conversations Donald Trump had over a decade ago has caused some disillusionment among GOP stalwarts and conservative voters. In no way do I condone Trumps behavior - in fact I condemn any form of disrespect towards women. We should always honor and respect the dignity of our mothers, sisters and daughters. Even though the incident happened ten years ago, well before Trump entered the political arena, this behavior is unacceptable, especially by someone who aspires to higher office. Trump did the right thing in immediately and unequivocally apologizing.

I feel fairly certain that the progressives have had knowledge of this conversation for a long time and dropped it at this point in time in an effort too obscure the release of damaging information about Hillary Clinton and her desire for open borders. I believe that they have more material that they will release periodically up until the election to keep a negative focus on Donald Trump. They do not want to discuss the vital issues that are destroying our nation and the future of our children, because they do not have logical solutions and offer more of the same that has gotten us into this precarious situation.

Those of us who do not want to see America fundamentally devolve into something worse must be wise enough to recognize the scheme that is being played out here. We must demand not only that the issues be discussed but also that we make our decisions based on issues and not on personalities or decade old statements and behavior by Hillary Clinton or Donald Trump. The political elites and their loyal media are desperate because they are seeing the large enthusiastic crowds for Donald Trump and the meager crowds for Hillary Clinton, and they know that there will be a huge enthusiasm gap on election day.

The question is; will the political elites of both parties succeed in continuing there reign of fiscal irresponsibility and military weakness or will the people understand what is going on and will they be wise enough to thwart those efforts?
 
Mkuu King Suleiman
Kinachotokea kwa Trump kuungwa na mkono na Ben Carson ni mwendelezo wa wafuasi watiifu kwake
Pamoja na mambo yote, Trump ana 'core base' inayomwamini no matter what.

Kundi hili linahusisha akina Dr Ben Carson,the then Mayor wa NY Rudi Gulian, na gavana Christie Christie 'NJ`

Dr Ben ni 'loyal' kwa Trump baada tu ya kujitoa primaries na ameendelea kuwa hivyo

Maelezo kuwa sakata limeibuliwa kuzuia emails halina ukweli.
Taarifa zilizopo, video hiyo iilihodhiwa na kituo kimoja cha TV hadi mdahalo uishe kesho.

Ndani ya TV yupo aliye vujisha kwa gazeti na kutoka hadharani.
Kama ulimsoma Mag3 hapo nyuma, uchaguzi wa US huambatana na shughuli za' biashara'

HALI ILIVYO
Maseneta wameendelea kuondoa 'endorsement zao' hawa ni Zaidi ya 7 waliotangaza ukiachilia mbali waliosita kufanya hivyo kuanzia siku za mwanzo.

Miongoni wa waliojitoa leo ni Seneta Mcaina na Seneta wa Iowa Ron Portman.

Huyu Seneta wa Iowa ana uzito kwasababu hakuna Rais aliyeshinda kutoka Republican bila kushinda Iowa state

Hali ndani ya Republican ni mbaya sana. Katika hali nyingine, secretary of states wakati wa Bush Condoleezza Rice ametoa kauli ya kulaani video ya Trump na kusema enough is enough, Trump aondoke katika kinyang'nyiro

Crisis iliyopo ni kubwa, GOP wakitafuta namna ya kumaliza timbwili katika wakati mgumu sana.
Ni katika siku 30 kabla ya uchaguzi na kura za awali 'absentee ballot' zinaendelea kupigwa

Rule 9 haiwezi kutoa majibu kwasababu ya hali ilivyokuwa ngumu. Hali za maseneta na wabunge nazo ni tata kwasababu yapo makubaliano ya GOP na Trump, pesa zinazochangwa zigawanywe kwa Trump na Republican

Republican kwasasa wanafanya jitihada za kuvunja mkataba huo ili pesa ziwafikie maseneta na wabunge

Kwasasa ofisi ya RNC imeahirisha shughuli ili kutafakari hali ya baadaye katika kipindi hiki

Kuna shinikizo la Mike Pence (VP) ajitoe katika tiketi ili kuweka shinikizo.

Leo Pence alikuwa amwakilishe Trump Wisconsin, alimpigia simu Trump kumweleza hataweza kwenda.

Hii ni baada ya Spika Ryan kukataa kwenda pia.

Hoja inayowasumbua GOP ni kuwa Pence akiwa mgombea, nini hatma yao katika uchaguzi mwezi Novemba?

Tusemezane
 
Hili halina ubishi tena republican wanapitia kipindi kigumu sana ktk huu uchaguzi. Nadhani kwa Trump mwenyewe hana anachopoteza ukiangalia hata namna alivyoomba radhi ni km alikuwa akijitetea kwa kumtwisha mzigo bill clinton wakati bill hagombei.

Lkn inaonekana pia wapo wafia Trump km huyu mgombea wa urais wa zamani.





Nimeona akimtetea trump na kusema atasimama nae.

Dole, a former senator from Kansas, told the Wall Street Journal he would be hard-pressed to back away from the party’s nominee in the wake of Trump’s lewd talk about women caught on tape.
“I look at it a little differently,” Dole said. “I’ve been a Republican forever. The party has been very good to me. I’ve had many opportunities as a Republican, and I find it very difficult to desert the party after Trump won 40 percent of the vote in the primary.”

Dole is now the only former GOP nominee who backs Trump — Mitt Romney has been a steadfast critic of the billionaire, and John McCain rescinded his support Saturday. Both Bush 41 and Bush 43 have stayed silent on the 2016 race.

“It was 11 years ago,” Dole said of Trump's explicit comments. “He shouldn’t have said it, but there’s nothing he can do about it except to do well in the debate. I think he can overcome a lot of this in the debate tomorrow night.”

Sisi yetu macho na masikio. Kuna wengine wanasema pamoja na makosa ya trump lkn ni afadhali kuliko familia ya kihalifu ya clinton.
 
Mkuu King Suleiman
Kinachotokea kwa Trump kuungwa na mkono na Ben Carson ni mwendelezo wa wafuasi watiifu kwake
Pamoja na mambo yote, Trump ana 'core base' inayomwamini no matter what.

Kundi hili linahusisha akina Dr Ben Carson,the then Mayor wa NY Rudi Gulian, na gavana Christie Christie 'NJ`

Dr Ben ni 'loyal' kwa Trump baada tu ya kujitoa primaries na ameendelea kuwa hivyo

Maelezo kuwa sakata limeibuliwa kuzuia emails halina ukweli.
Taarifa zilizopo, video hiyo iilihodhiwa na kituo kimoja cha TV hadi mdahalo uishe kesho.

Ndani ya TV yupo aliye vujisha kwa gazeti na kutoka hadharani.
Kama ulimsoma Mag3 hapo nyuma, uchaguzi wa US huambatana na shughuli za' biashara'

HALI ILIVYO
Maseneta wameendelea kuondoa 'endorsement zao' hawa ni Zaidi ya 7 waliotangaza ukiachilia mbali waliosita kufanya hivyo kuanzia siku za mwanzo.

Miongoni wa waliojitoa leo ni Seneta Mcaina na Seneta wa Iowa Ron Portman.

Huyu Seneta wa Iowa ana uzito kwasababu hakuna Rais aliyeshinda kutoka Republican bila kushinda Iowa state

Hali ndani ya Republican ni mbaya sana. Katika hali nyingine, secretary of states wakati wa Bush Condoleezza Rice ametoa kauli ya kulaani video ya Trump na kusema enough is enough, Trump aondoke katika kinyang'nyiro

Crisis iliyopo ni kubwa, GOP wakitafuta namna ya kumaliza timbwili katika wakati mgumu sana.
Ni katika siku 30 kabla ya uchaguzi na kura za awali 'absentee ballot' zinaendelea kupigwa

Rule 9 haiwezi kutoa majibu kwasababu ya hali ilivyokuwa ngumu. Hali za maseneta na wabunge nazo ni tata kwasababu yapo makubaliano ya GOP na Trump, pesa zinazochangwa zigawanywe kwa Trump na Republican

Republican kwasasa wanafanya jitihada za kuvunja mkataba huo ili pesa ziwafikie maseneta na wabunge

Kwasasa ofisi ya RNC imeahirisha shughuli ili kutafakari hali ya baadaye katika kipindi hiki

Kuna shinikizo la Mike Pence (VP) ajitoe katika tiketi ili kuweka shinikizo.

Leo Pence alikuwa amwakilishe Trump Wisconsin, alimpigia simu Trump kumweleza hataweza kwenda.

Hii ni baada ya Spika Ryan kukataa kwenda pia.

Hoja inayowasumbua GOP ni kuwa Pence akiwa mgombea, nini hatma yao katika uchaguzi mwezi Novemba?

Tusemezane

Ni kweli mkuu, nimeona jana pia gavana wa zamani na sapota mkubwa sana wa Republican Arnold Swaisznegar akisema hatamuunga mkono Trump kwenye uraisi na kwamba Trump hatoshi kwenhe uraisi, anasema kwakwe yeye anaipenda zaidi Marekani kuliko chama yaani Republican, amesema maisha yake yote tangu amepata rights za ku vote 1980s, hajawahi kumpigia kura na kumuunga mkono mgombea wa chama chochote zaidi ya Republican but this time around anasema Trump hafai kuchaguliwa kuwa raisi wa Marekani maana hafai.

Sasa najiuliza hivi hizi kauli zao hazitamuathiri Trump na Republican kwa ujumla wao hata kwenye chaguzi za senet na congress? Maana watu wazito sana hao na celebrities ana ushawishi wao, sasa sijui siasa za marekani kama zinaweza kuyumbishwa na matamko na misimamo yao. Maana kwa mfumo wao na shule uliyowahi kutupa Nguruvi3, sio kura za wanachi zinafanya mtu awe raisi bali ni za wale electro College, hamuoni kwamba wanaweza kutoa suprise lwa kuchaguliwa Trump na si Clinton kama upepo unavyovuma??

Asante kwa uchambuzi tuzidi kupeana elimu.
 
Nb mdahalo leo ni saa ngapi kwa masaa yetu?? nina hamu nao sana napenda mno jamaa wanavyojibishana kwa hoja na oia personal attacks, i can't miss
 
Dakika 10 kuelekea mdahalo

Breaking news: Billy Bush, mwandishi aliyekuwa na Trump katika video amekuwa 'suspended' kutoka NBC news

Trump amealika wanawake waliokuwa na mahusiano na Bill Clinton siku za nyuma.
Alikutana nao kabla ya mdahalo

Tutaendelea kuwajuza
 
Mdahalo wa leo naona Trump amejitahidi kupambana sana na Clinton naona leo yupo more defensive than Offensive, kaelemewa japo Trump hana hoja za msingi sana. Kwa ufupi mdahalo huu Trump kajipanga zaidi ya ule uliopita
 
TATHMINI YA MDAHALO

Sehemu ya I

Kuelekea mjadala, Trump alikabiliwa na suala la video iliyoharibu sana image yake

Matarajio ya wengi suala hili lingechukua sehemu kubwa ya mjadala wa leo

Trump alijua litamaliza kampeni yake na Hillary alijua litazua mjadala wa Bill Clinton

Majibu ya Trump yalikuwa 'vague' kiasi ambacho hakikujibu suala zima la video.

Alichosema hayo ni maongezi tu ya vyumbani.
Aliomba radhi, lakini jibu lake akilihusisha na ISIS, video itarindima kwa muda mrefu ujao

Trump alitakiwa kuomba radhi kwa wanawake waliwakosea na jumuiya nzima ya wanawake, hakufanya hivyo

Hillary hakutaka kulitumia ikiwa ni mkakati wa kumwacha Trump aendelee kujimaliza

Kwa kiasi limemsadia Hillary kuepuka mjadala wa 'matusi' ili ajikite katika issues

Hllary hakutumia video peke yake, alitumia video kufikia black America, Latino, wanawake na independent

Alionyesha udhaifu wa Trump dhidi ya makundi hayo. Hii kisiasa ni point kubwa sana

Kwa namna yoyote ajibu ya Trump hayakujibu hasira za wanawake na wale wanaodhani haikuwa sahihi

UTULIVU
Kama mjadala wa kwanza, Trump alikuwa anaingilia mjadala 'interrupts'

MAJIBU

Trump aliulizwa maswali, kwa namna alivyojibu kuna sehemu mbili za majibu
1)Kwanza, hakujibu maswali aliyoulizwa kama yalivyoulizwa
2)Alijibu katika katika kupendeza 'political base' yake

Mfano, Aliulizwa suala la Allepo Syria na kwamba nini sera zake.
Trump hakuwa na policy, alizungumzia matukio wakati Hillary akiwa secretary of state

Hillary Clinton
Kama mwanzo, mjadala huu alijiandaa pia. Alijua weakness zake zipo katika emails

Kwa sehemu kubwa amejibu vizuri na 'fact check' zimeonyesha sehemu majibu ni kweli

Clinton alikuwa mwangalifu sana na homework zinamsaidia sana.

MKAKATI

Donald Trump alikuwa na mkakati wa kuokoa kampeni yake. Leo ingekuwa tofauti kabisa

Alichoweza kufanya si kujibu maswali, si kujibu tuhuma, bali kuamsha hisia za 'political base' yake

Kwa alivyofanya leo ukilinganisha na mjadala wa kwanza, wafuasi wake wameridhika alifanya vizuri

Tatizo linalomkabili ni moja, mjadala wa kwanza ulibadilisha ramani ya majimbo na uelekeo wake

Mjadala huu alitakiwa azibe mashimo yaliyotokana na mjadala wa kwanza.

Kupita expectations kuna maana moja, kwamba amefaulu kuziba 'damu' inayovuja katika political base yake.

Tatizo, hakuna jitihida za kufikia makundi ambayo kura zinaonyesha yupo nyuma

Kwa mfano, Trump yupo nyuma kwa college millennial women.

Kwa majibu yake ya video na general knowledge, hainonekani kama amesadia hilo.

Inaendelea mkakati -Clinton
 
MKAKATI

Sehemu ya II

Clinton alitaka kuendelea kuonekana presdicential ndiyo maana mara zote alikuwa mtulivu hata alipoguswa

Mkakati wa Hillary ilikuwa katika sehemu kuu mbili

1. Kumwacha Trump aendelee kujimaliza kwa mjadala wa video, akimsitiri mumewe ili habari katika siku zijazo isiwe kuhusu Bill Clinton bali video.

Hilo amefanikiwa kitendo cha Trump kuleta 'michupuko' ya Bill ingalikuwa habari na kuvuruga habari ya video

2. Kuonyesha anaelewa sera anazozungumzia kwa undani.
Ndiyo maana kila ajibu lake lilikuwa na ufafanunuzi

3. Kushinda makundi: Ukimsikiliza kila 'controversy' ya Trump ali address kwa kutumia makundi, iwe blacks, Latinos, wanawake, watoto au wazee.

Hapa alijaribu kuyafikia makundi hayo ikiwa ni pamoja na independents

HITIMISHO LA KWANZA

Inategemea nani aliangalia na kwa jicho gani.
Kwa kuangalia 'substance', temperament and approach Clinton ameshinda mdahalo

Je, mjadala umebadili lolote?
Yes, kwa baadhi ya watu waliokuwa na shaka na wagombea mjadala huu utakuwa umesadia sana. Hapa Clinton ana advantage kwa vigezo vingi

Kwa jicho la ubabe au defiance na hali ilivyo, Trump amefaulu kubakiza kundi lake.

Hakuonekani kama amepata chochote Zaidi ya mijadala itakayomwandama siku zijazo

Mjadala wa kwanza aliandamwa sana na suala la Alicia Machado.

Kwa bahati mbaya leo tena kazungumza jambo jingine litakalomsumbua.

Trump kasema, akiwa Rais atamwagiza AG aunde tume ya kumchunguza Clinton na ''jail her''

Kwa society ya America wanaamini katika justice na kuna vyombo husika.

Ndiyo maana waliweza kukataa veto ya Obama na kuna nyakati Oabama ali veto, na nyakati mahakama kuu inakataa hoja za Obama n.k.

Hii kauli ya kumfunga Clinton inaonekana kama itazua mjadala.

Wachunguzi wanasema tabia hiyo si ya America, ni ya madikteta na haijawahi kutolewa na mgombea kwa mwenzake

Tathmini itaendelea.....
 
Kwa kiasi fulani ile audio clip iliyotolewa ijumaa ikimuonesha Trump akitoa matamshi yenye ukakasi dhidi ya wanawake imechangia kufanya mdahalo huu kuwa ni wa kurushiana vijembe zaid. Trump akijitahidi kujitetea huku naye akirusha vijembe dhidi ya Bill Clinton. Cha kufurahisha zaidi masaa machache kabla ya mdahalo akaitisha mkutano na waandishi wa habari akiambatana na kina mama ambao wamewahi kumtuhumu Bill kwa kuwanyanyasa kingono! Ingawa amejitahidi sana kupambana dhidi ya kashfa zinazomkabili lakini sidhani kama amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuponya majeraha ambayo amepata katika kipindi hiki cha wiki chache huku ile audio clip ikimharibia zaidi. Kwa upande wa Hillary alitegemewa kutumia fursa ya audio clip ile kutoa pigo la mwisho wa Trump ili kummaliza kabisa lakini inaonekana hajafanikiwa kufanya hivyo. Mwisho wa siku sidhani kama debate hii italeta utofauti wowote kwenye kura za maoni kinyuma na ilivyokuwa hapo mwanzoni. Trump bado ana kazi kubwa kutibu majeraha pamoja na kutafuta kuungwa mkono ndani ya chama chake mwenyewe.
 
SHUKRANI wote kwa uchambuzi makini. Bahati mbaya sikuufatilia mdahalo. Nilianzia BBC kutafuta tathimini, ukizingatia Mainstream media ikiwemo BBC hawataki Trump awe rais. Mimi nadhani lugha za Kuudhi nchini Marekani siyo issue sana na haiwezi kuathiri sana mwenendo wa kura. Hivi maneno machafu ya HC dhidi ya raia wa Marekani wanaomuunga mkono Trump niyakuchukuliwa kiwepesi? Hata ya yule Nulad dhidi ya EU yalikuwa ya kumuacha Ofisini? Trump anaweza kuwashangaza Establishment!!!
Trump v Clinton: Who won the debate? - BBC News
 
Nilianzia BBC kutafuta tathimini, ukizingatia Mainstream media ikiwemo BBC hawataki Trump awe rais.

Mimi nadhani lugha za Kuudhi nchini Marekani siyo issue sana na haiwezi kuathiri sana mwenendo wa kura.

Hivi maneno machafu ya HC dhidi ya raia wa Marekani wanaomuunga mkono Trump niyakuchukuliwa kiwepesi? Hata ya yule Nulad dhidi ya EU yalikuwa ya kumuacha Ofisini? Trump anaweza kuwashangaza Establishment!!!
Trump v Clinton: Who won the debate? - BBC News
Mkuu unaposema main stream media hazitaki Trump awe Rais nadhani si sahihi. Leo Speaker wa Congress ametangaza kutokampeni kwa Trump katika siku zilizobaki

Mcain, kaondoa endorsement yake kwa Trump. Condolleezza kasema Trump aachie ngazi

Mitt Romney kasema Trump hafai na aachie ngazi

Gingrich speaker wa zamani ametoa kauli kali dhidi ya Trump

VP wa Trump , Mike Pence hawapo katika same page na top ticket

Congressman and women wameondoa support yao kwa Trump

Katika wagombea waliopita wa Republican, Mitty Romney, Mcain, Bush Jr, Bush snr hakuna aliye endorse Trump

Hawa wote ni Republican si main stream media. Kwa hili unalaumu main stream media kwa lipi?

Kuhusu Kauli kama zina uzito, ndugu yangu zina uzito sana
Ukifuatilia leo TV zote wapambe wapo bize wakifafanunua kauli, hawadharau kwasababu zina madhara sana

Kibaya Zaidi hizi za kutukana wanawake ni mbaya sana.
Unaona Trump anavyo struggle na Latino kwa kauli zake za 'rapist' n.k.

Unaona anavyo struggle kwa blacks baada ya kuhusishwa na kauli dhidi yao

Uchaguzi wa Marekani una mengi sana. Kauli hizo hizo zinazomwathiri Trump kwa upande mwingine zinamjenga kwa wale wanaoamini katika ubabe wa US.

Kwa mfano, Trump aliposema 'will jail her' kauli hiyo ilipendwa na baadhi ya watu ndani na nje ya mdahalo. Lakini kauli hiyo leo inageuka kuwa shubiri!

Ukiangalia kura za maoni ambazo hubadilika, kuna impact kubwa katika wiki mbili
 
Pence amesema baada ya mdahalo kuwa hana pengine pa kwenda akimaanisha ataendelea kusimama na trump.
Mike Pence responds to a rumor about his departure from Trump

Lkn hata Paul Ryan pamoja na kukemea vikali video ya trump,lkn kuna tweet ametweet kuwa hawezi kumuunga mkono HC hii mana yake nae bado anasimama trump.

Ukiacha hao wote,me pia bado nasimama na trump,siwezi kumuunga mkono shetani HC. Sijawahi kuwaamini wanawake tangu nizaliwe..Halafu mkuu nguruvi ukiondoa hizo mainstream media,zipo polls nyingi tu zimetoa ushindi kwa mshua. Km hizi hapa

Wow! Trump won in nearly all online polls last night

Ngoja tuvute subira mpaka november tutaona na kusikia mengi.
 
Lkn hata Paul Ryan pamoja na kukemea vikali video ya trump,lkn kuna tweet ametweet kuwa hawezi kumuunga mkono HC hii mana yake nae bado anasimama trum
Usahihi wa taarifa za muda huu, Spika Paul Ryan ameongea na maseneta na wabunge kwa nyakati tofauti. Ametangaza kutoshiriki katika kampeni za Trump.
 
Usahihi wa taarifa za muda huu, Spika Paul Ryan ameongea na maseneta na wabunge kwa nyakati tofauti. Ametangaza kutoshiriki katika kampeni za Trump.
Mkuu nguruvi3 kutoshiriki kampeni haina maana hamuungi mkono. Amekataa kuwa sehemu ya wapiga pipa wa trump,ameamua kuwa kimya lkn bado yupo nasi!! Hebu msome hapa..
Just in! Trump fires back at Paul Ryan
 
Bahati mbaya siwezi kuchangia sana kwa kutokuwa na internet... Nina ka simu tu. Hata hivyo magode duh! Unafurahisha haswaaaa!
Mkuu katika uchaguzi wa US kuna mengi yanaendele, inahitaji source nyingi kama unavyojua

Tunazo scientific polls kuhusiana na mambo haya.
Hata hivyo tunasita kuziweka hapa kwasababu kadhaa .

Online poll si za kisayansi huwekwa na yoyote na nyakati hizi ni sehemu ya propaganda

Mdahalo wa kwanza, Trump alikwenda mikutanoni akisema online poll zinaonyesha alishinda
Mwisho wa siku, kampeni yake ikasema wazi alishindwa.

Mkakati walioufanya ni kubadilisha 'coach' na kumhusia Trump achukue muda nje ya kampeni kujiandaa

Katika mdahalo wa jana, kuna mambo mawili yanayozungumzwa kuhusu nani kashinda

1. Overall Hillary kashinda,ni kwa kutumia takwimu za kisayansi na kuangali vigezo vingi
Kwa mfano, temperament, substance, policy , message, intended audience, confidence, knowledge n.k.

2. Ukitazama mdahalo wa kwanza, na huu wa pili Trump ameshinda.
Ameshinda si kwa kuangalia vigezo husika bali kulinganisha alivyofanya mdahalo wa kwanza na huu wa pili.
Lakini pia alivyokwenda akikabiliwa na suala la video

Sasa nikimsoma Magode natatizika kidogo na analysis yake.
 
Mkuu katika uchaguzi wa US kuna mengi yanaendele, inahitaji source nyingi kama unavyojua

Tunazo scientific polls kuhusiana na mambo haya.Hata hivyo tunasita kuziweka hapa kwasababu kadhaa .

Online poll si za kisayansi na huwekwa na mtu yoyote na nyakati hizi hiyo ni sehemu ya propaganda

Mdahalo wa kwanza, Trump alikwenda katika mikutano akisema online poll zinaonyesha alishinda
Mwisho wa siku, kampeni yake ikasema wazi alishindwa.

Mkakati walioufanya ni kubadilisha 'coach' na kumhusia Trump achukue muda nje ya kampeni kujiandaa

Katika mdhalo wa jana, kuna mambo mawili yanayozungumzwa kuhusu nani kashinda

1. Overall Hillary kashinda, hii ni kwa kutumia takwimu za kisayansi, kwa kuangali vigezo vingi
Kwa mfano, temperament, substance, policy , message, intended audience, confidence, knowledge n.k.

2. Ukitazama mdahalo wa kwanza, na huu wa pili Trump ameshinda.
Ameshinda si kwa kuangalia vigezo husika bali kulinganisha alivyofanya mdahalo wa kwanza na huu wa pili.
Lakini pia alivyokwenda akikabiliwa na suala la video

Sasa nikimsoma Magode natatizika kidogo na analysis yake.
Mkuu nguruvi3,me nilikuwa najaribu tu kusahihisa kuhusu Paul Ryan,nadhani nilichokisema mimi ndo ukweli ulivyo. Alichokataa Paul Ryan ni kumpigania trump lkn hajaondoa nia yake ya kumuidhinisha km mgombea wa Republican. Hata pence,pamoja na kukosoa vikali matamshi ya Trump,lkn amesema kupitia CNN ni heshima kubwa kwake kuendelea kumuunga mkono trump.

Mkuu mag3 me nivumilie tu,wakati mwingine nawachokoza makusudi ili kunogesha mjadala. Lkn nilishakuambia tangu mwanzo,kwa mimi binafsi sijawahi kuwaamini wanawake ktk mambo makubwa na nnadhani ntabaki hivi mpaka mwisho wa uhai wangu hapa Duniani. Hakuna namna yoyote hata ya kunifanya nimwamini HC hata km wamarekani wote watampigia kura.
 
Back
Top Bottom