===============================
Asante sana kwa uchambuzi.
Mimi najaribu kuangalia uteuzi wa wagombea hasa wa Dem (chama tawala) kupitia utaratibu wa uendeshaji wa siasa zetu hapa nchini.
Hivi ni sahihi Navy, mkuu wa Polisi, mwandamizi wa CIA kuja jukwaani tena la chama cha Siasa (Dem) kumpigia Kampeni Hillary? Hii wapi 'neutrality' ya vyombo vya usalama vya Marekani kwenye siasa?
Hivi tuna haja tena ya kulalamikia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kutuhumiwa kukibeba chama tawala? Wakati wale wanaoutuongoza kwa ubora wa demokrasia na ambao tunaiga kwao masuala ya demokrasia na utawala bora wanatenda tofauti na wanaovyotuelekeza?
Mkuu, wanaokuja si kwa Dem, hata Republican wamefanya hivyo
Mwanasheria (AG) mstaafu alikuja GOP kama alivyo Holder.
Rejea uzi wa Republican convention utaona majina
Polisi na Sheriff walikuja Dem kama walivyokuja Republican.
Rejea uzi huo huo
Hapa utaona jinsi siasa za wenzetu zilivyokomaa.
Kwamba Raia wana haki ya kutoa maoni yao bila kuzuiwa.
Wengi wa hao kama wanasheria ni wastaafu.
Hakuna active AG aliyekuja, wote ni retired AG. Hata Jenerali wanaokuja ni wastaafu
Hivyo, naomba urejee uzi wa uchaguzi Marekani ili uone Trump ilikuwaje na Hillary ikoje.
Mkuu Condoliza Rice alikuwa secretary of state sasa hivi anapiga darasa
Kule kwa wenzetu watu wenye uzoefu wanatumiwa
Lakini pia ufahamu wenzetu unafiki wamepita huko.
Sisi tunadhani si haki AG mstaafu kuhutubia convention, hatushangai Jaji mkuu kuchukua fomu ya CCM
Sisi tunaona tabu wenzetu wakitumia wazoefu wao wastaafu, kwetu sisi unafiki
Nikuulize, unaelewe kipi kati ya marufuku ya mikutano leo hii?
Hapa kwetu mbona imetokea pia. Majaji wastaafu kwa umoja wao wamesema!!!!