Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Mkuu magode, Democratic Party (Liberal, left leaning) ilikuwa ya kwanza kuasisiwa mwaka 1828 ikifuatiwa na Republican Party (Conservative, right leaning) iliyoasisiwa mwaka 1854.Mkuu mag3 wakati tunasubiri analysis ya HC kutoka kwa nguruvi3. Hebu kwa faida ya wanajukwaa wengi tukumbushe mara ya mwisho hawa wamarekani kukipa uongozi chama tawala awamu mbili mfululizo. Hapa namaanisha kwa mfano,Democrat wamepata fursa ya kuongoza miaka yote 8 ya obama. Mara nyingi hapa wamarekani wakikipa chama uongozi wa miaka 8 mfululizo,uchaguzi unaofuata(km huu) mara nyingi huwa wanafanya mabadiliko. Nataka unikumbushe mara ya mwisho chama kupata uongozi kwa miaka 12 au 16 mfululizo ilikuwa mwaka gani!!?? Najua chama kikivurunda huwa kinaishia miaka 4 km ilivyokuwa kwa George bush senior miaka ya 90.
Chama cha Republicans kiliweza kufanikiwa kubaki madarakani kwa kipindi cha miaka 12 kuanzia na Ronald Reagan 1981-1989 akifuatiwa na George H. W. Bush pia wa Republicans 1989-1993.
Kabla ya hapo Democrats nao waliweza kuwa madarakani kwa kipindi kirefu zaidi cha miaka 19 na miezi 9 kuanzia Franklin D. Roosevelt 1933-1945 na kupokewa na Harry Truman pia wa Democrats 1945-1953.
Baada ya kifo cha Franklin D. Roosevelt akiwa bado yuko ofisini na akiwa ameanza kipindi chake cha nne, katiba ilibadilishwa kutoruhusu Rais kubaki madarakani kwa vipindi zaidi ya viwili.
Wakisubiri kumpata Rais wa 45 November mwaka huu, USA imekuwa na marais 19 kutoka Republican Party, 16 kutoka Democratic Party na tisa tu kutoka nje nje ya vyama hivi viwili vikubwa.
Marais wanne wameweza kuuawa wakiwa ofisini nao ni Abraham Lincoln (Republican), James A. Garfield (Republican), William Mckinley (Republican) na John F. Kennedy (Democrat)