Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

thedealer, hivi mtu mpaka uitwe mwanasiasa, unatakiwa utimize masharti gani? Unawatenganishaje watu wawili mpaka moja umwite mwanasiasa zaidi ya mwenziwe? Mathalani tuchukue mifano ya watu wawili humu, Nguruvi3 na thedealer...je yupo mwanasiasa kati yenu kuliko mwingine?

Ziko uthibitisho kwamba Donald Trump alianza kuutamani Urais wa Marekani toka miaka ya 1990s ingawa kwa sababu anazozijua yeye, alikuwa anasita kugombea. Je ana tofauti gani kwa mfano na Rais wa sasa wa Marekani Barack Obama ambaye aliamua ghafla bin vuu kugombea Urais miaka ya 2000s?

Je Barack Obama aliyeshindana na Hillary Clinton, yupi ungemweka katika kundi la establishment na iliwezekanaje kwa Obama kuwa mgombea mteule wa Democrats? Pamoja na hilo iliwezekanaje akashinda uchaguzi na kuwa Rais wa Marekani dhidi ya mgombea wa establisment kutoka chama cha Republicans?

Swali langu la pili kwako ni hili, je kati ya Donald Trump na Hillary Clinton, yupi aliyepitia mashambulizi makali zaidi toka kwa wapinzani na vyombo vya habari kuliko mwingine kwa muda mrefu? Nadhani tofauti kubwa kati yao ni moja nalo ni namna walivyoweza kukabiliana na hayo mashambulizi yalipotolewa.

Je umefanya angalau utafiti kidogo kujua tofauti zao kimaisha toka wakati wakiwa vijana baada ya kumaliza shule na shughuli walizoshughulika nazo? Marekani kila mgombea hupitia tanuru la moto na haijalishi unatokea chama cha upinzani au chama tawala, watu watataka wajue maisha yako ya awali.

Vyombo vya habari hutumika sana katika kuwapasha wananchi wasiokufahamu vizuri, ulivyoendesha maisha yako kabla na wananchi wategemee nini ukipewa madaraka. Yako mambo mengi yatatendeka k.m. mijadala itatayarishwa, maoni yatatolewa, maswali yataulizwa, midahalo itaandaliwa na uchambuzi utatolewa.

Ukweli ni kwamba Donald Trump anawakilisha kundi la Wamarekani wenye chuki dhidi ya watu wanawaona kama si wenzao. Donald Trump ameamsha hisia hatari za wabaguzi ambao hawana nafasi Marekani katika dunia ya leo na tofauti na wewe, naamini hata ikitokea miujiza akashinda Urais hawezi kumaliza kipindi chake.
 
Mkuu Nguruvi3 sijakuelewa vema unavyomujumuisha Bernie Sanders kwenye kundi la establishment, ninavyomfahamu mimi ni kama 'independent' ambaye amekaribishwa ndani ya chama cha 'Democrat' kama kujaribu bahati yake ya kutafuta u-nominee kwa tiketi ya Democrat. Lakini pamoja na hayo bado kwa sehemu kubwa ameegemea mawazo ya outsiders yaani upande wa Donald Trump.
Bernie Sanders kwa vigezo vya the establishment yeye ni sehemu.

Huyu ni Seneta ambaye ni independent na hivyo kuwa sehemu ya Washington!
Kuwa independents hakumuondoi katika 'filibusters' au Ney za DC

Alipewa fursa ya kugombea kama demokrasia ya wenzetu inavyoonyesha

Hata hivyo, Dem wengi hasa ''leftist'' hawakuridhia kwa roho zao.
Sasa ameamua kurudi seneti kama independent
 
Bernie Sanders kwa vigezo vya the establishment yeye ni sehemu.

Huyu ni Seneta ambaye ni independents na hivyo kuwa sehemu ya Washington! Kuwa independents hakumuondoi katika '
filibusters' au Ney za DC

Alipewa fursa ya kugombea kama demokrasia ya wenzetu inavyoonyesha

Hata hivyo, Dem wengi hasa ''leftist'' hawakuridhia kwa roho zao.
Sasa ameamua kurudi seneti kama independent
Labda TheDealer, anayo tafsiri tofauti ya establishment. Seneta Bernie Sanders alianza kugombea uongozi wa kisiasa toka miaka ya 1970s ingawa hakuweza kushinda. Mara ya kwanza kabisa kushinda ni pale alipogombea Umeya wa mji wa Burlington, Vermont mwaka 1981. Miaka kumi baadaye, 1991 aliweza kugombea Congress na kushinda na kuwa Congressman kwa muda wa miaka 16.

Mwaka 2006 aligombea Usenata na kushinda na kwa miaka 10 amekuwa Senator wa Vermont. Akijua hawezi kugombea na kushinda Urais kupitia chama chake cha Independents mwaka jana akaamua kugombea kupitia tiketi ya Democratic Party. Alikuwa outsider kwa Democrats lakini si outsider wa Washington, establishment.
 
"Mag3, post: 17073081, member: 10873"]thedealer,
Je Barack Obama aliyeshindana na Hillary Clinton, yupi ungemweka katika kundi la establishment na iliwezekanaje kwa Obama kuwa mgombea mteule wa Democrats? Pamoja na hilo iliwezekanaje akashinda uchaguzi na kuwa Rais wa Marekani dhidi ya mgombea wa establisment kutoka chama cha Republicans?
Obama aliingia katika mpambano akiwa Junior senator
Swali langu la pili,je kati ya Donald Trump na Hillary Clinton, yupi aliyepitia mashambulizi makali zaidi toka kwa wapinzani na vyombo vya habari kuliko mwingine kwa muda mrefu? Nadhani tofauti kubwa kati yao ni moja nalo ni namna walivyoweza kukabiliana na hayo mashambulizi yalipotolewa.
Point! Hillary yupo katika media na spotlight kwa muda mrefu sana
Hoja zinazotumiwa dhidi yake ni kwasababu ya hizo.Tofauti kati yao ni jinsi wanavyo handle matatizo. Hapa ndipo suala la damage control linapokuja.

Kwa mfano, gold star families na Khan. Alichotakiwa kusema Trump ni ku appreciate service ya mtoto au angekaa kimya. Badala yake akingiza suala la mkewe Khan.

Alitakiwa kujua alikuwa tete a tete na makundi kadhaa. Moja, immigrants wanaosimama na Khan. Pili, akina mama kwa k 'sensitivity' ya jinsia uchaguzi huu.
Tatu, Veterans. Urefu wote wa mjadala upo katika mambo hayo matatu

Kinyume , badala ya damage control, yeye alita ku divert mjadala
Je umefanya angalau utafiti kidogo kujua tofauti zao kimaisha toka wakati wakiwa vijana baada ya kumaliza shule na shughuli walizoshughulika nazo? Marekani kila mgombea hupitia tanuru la moto na haijalishi unatokea chama cha upinzani au chama tawala, watu watataka wajue maisha yako ya awali.
Obama na Bush walikiri mapema kabisa'kula sigara kubwa yenye mvuto' katika ujana wao.Mapemaa! walijua hawataachwa

Kwa wenzetu lazima kiongozi ajulikane kuanzia maisha yake, ndiyo maana hoja ya birth certificate aliyoishikia bango Trump ilijadiliwa bila huruma au upendeleo.

Katika convention, Hillary alisema' ....anamshukuru Bill, wamekuwa pamoja katika raha na shida na zipo nyakati za majribu'Alikusudia ni kuweka rekodi sawa ili isiwe mjadala

Utashangaa watu hawakujua Trump kiasili ni Mjerumani. Wengi walidhani ni Myahudi.
Watu hawakujua Sanders ni Myahudi, uchaguzi umeweka wazi hilo.
Uchaguzi wa wenzetu si ule wa 'huyu ni mwenzetu' lazima mtu apite katika tanuru
Vyombo vya habari hutumika sana katika kuwapasha wananchi wasiokufahamu vizuri, ulivyoendesha maisha yako kabla na wananchi wategemee nini ukipewa madaraka. Yako mambo mengi yatatendeka k.m. mijadala itatayarishwa, maoni yatatolewa, maswali yataulizwa, midahalo itaandaliwa na uchambuzi utatolewa.
Kazi ya media inapoonekana. Na bado , tutafahamu mengi tu kadiri siku zinavyosonga mbele.
Ukweli ni kwamba Donald Trump anawakilisha kundi la Wamarekani wenye chuki dhidi ya watu wanawaona kama si wenzao. Donald Trump ameamsha hisia hatari za wabaguzi ambao hawana nafasi Marekani katika dunia ya leo na tofauti na wewe, naamini hata ikitokea miujiza akashinda Urais hawezi kumaliza kipindi chake
Siasa kama za kutenga Marekani ni hatari. Obama alipohutubia AU au anapofanya ziara ni katika kulinda masilahi ya Marekani yenye ushindani kuliko wakati mwingine.

Akiwa Addis Ababa alisema ' Hakuna tatizo nchi za kiafrika kushirikiana na China, yeye yupo ku advance mahusiano ya US na nchi hizo'Hapa alionyesha China inavyoanza kukamata maeneo muhimu ya kiuchumi Duniani. Ndivyo anavyoona Russia na ubabe

Uwepo wa majeshi ya Marekani Asia, Europe n.k. si hisia ni kwa interest za Marekani
Je, Trump anaona interest hizo hazina maana kiasi cha kufikiri kuitenga Marekani?
 
Jioni ya jana kaingia katika ugomvi na 'katoto' kalikolia katika mkutano wake

Ana create controversy kama means za kuwa katika media, kuua hoja au kupoteza directions ''

Katika kitu kilichonishangaza jana,nikuona hiyo ya kukifukuza kitoto,sikuamini masikio yangu,sijui ni kwanini lakini na mimi sasa nimeshaona jamaa atakuwa na matatizo flani.Na inavyoonekana atakuwa aliingia kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi kujaribu tu na kuweka Historia kuwa aliwahi kugombea.Nadhani hakutegemea kabisa kufika hapo alipofikia.Ndio maana hizo Controversy anazocreate kila siku zimeleta sintofaham hadi kwenye Team yake ya Kampeni,ni kama hata wao hawajui anapokuwa kasimama kuongea atazua kioja kipi?

Nguruvi3 au Mag3 pana mmoja wenu alichangia kuwa uwezo wa Damage Control kwenye Team yake ni mdogo sana na ndipo hapo Wanasiasa wazoefu kina Hillary wanapomweka ktk Corner anabakia kuwa defensive zaidi.Ni maoni yangu

La kuongezea hapa natizama CNN kipindi cha Wolf pana wachangiaji wanasema "AIDES SCRAMBLE TO GET TRUMP ON TRACK"
 
La kuongezea hapa natizama CNN kipindi cha Wolf pana wachangiaji wanasema "AIDES SCRAMBLE TO GET TRUMP ON TRACK"
Uchaguzi wa Marekani kama alivyosema Mag3 wagombea wanapita katika tanuru zito

Awamu ya chaguzi za vyama, Trump aliwavuruga wenzake kwa 'character assassination'
Kuelekea uchaguzi mkuu hali hubadilika sana kwasababu wanabaki wawili na sera

Mapungufu hayawezi kuzibwa kwa hila. Kinachoangaliwa ni sera na ukweli au uhakiki wake

Hapo ndipo unaweza kuona Trump anafokea 'katoto kanakolia' hell get outta here

Jana Republican wawili, mshauri wa Jef Bush wametangaza kumpigia kura Clinton

Republican wana hofu si ya Hillary, bali Trump ataamka na kitimbwi gani

Jana swahiba wake Gav Christie alifanya damage control kumnusuru Trump

Baada ya hilo, likazuka jingine.

Ndiyo maana tunamwambia ndugu TheDealer anayetengeneza habari ni Trump wala si watu.

Na kwa msingi huo itaonekana mwenzake anapata 'free way'
 
Duuuu....nawashukuruni sana wakuu Mag3 , Nguruvi3 .

Ila namna huyu jamaa yangu anavyochambuliwa nazidi kupata wazimu fulani hv. Nakubali huo uchizi wake maana najua ni chizi fulani hv lakini sasa anavuka mipaka. Sijui atashindaje huko mbeleni. Enewei kama Mungu wake kamwandikia atakuwa rais atakuwa tu, kama hajaandikiwa ndio hvyo tena.

Juzi ameanza kulalamika kuwa haoni kama mfumo wa uchaguzi utakuwa salama na huru. Anahofu itakuwa 'rigged'. Ameanza kuwalalamikia CNN kuwa hawamtendei haki kwa polls. Muda si mrefu pia alianza kuwananga 'The Washington Post' kuwa its going to die hivyo haina madhara kwake! Daaah kichwa kinauma.

Kiukweli Trump unanivuruga sana we jamaa. Mimi nilikuwa na matamanio yangu ukae 'oval office' lakini naona unazidi kunichanganya na kunipotezea mwelekeo wangu! Damn......!
 
Kiukweli Trump unanivuruga sana we jamaa. Mimi nilikuwa na matamanio yangu ukae 'oval office' lakini naona unazidi kunichanganya na kunipotezea mwelekeo wangu! Damn......!

TheDealer sio wewe tu anaekuvuruga,Team yake ya Kampeni imeshapotez mwelekeo,fikiria hadi baadhi ya walio kwenye Team wanaleak Information kwenye Media kuwa wako Frustrated.Jana usiku (kwa tuliopo Bongo) alikuwa busy kuwahakikishia kuwa "PANA UNITY KATIKA KAMPENI TEAM YAKE" ukiona hivyo ujue pana tatizo tena kubwa tu.
 
YALIYOJIRI UCHAGUZI

Baada ya RNC Cleveland, kura za maoni zilionyesha Republicans na Trump wakiwa wame gain point katika majimbo yanayotarajiwa kuamua nani awe Rais (Key states)

Umuhimu wa majimbo hayo ni , kwanza, idadi ya wajumbe 'delegates' ni wengi.
Na pili, mengine yamekuwa yanabadilika badilika, swing states

Kura za maoni wiki za jana na juzi baada ya DNC Philly zinaonyesha Hillary Clinton akiwa ame gain national wide na katika kesy states tulizosema, kwingine akiwa na double digit lead

Ni kawaida baada ya convention chama hupata nguvu mpya na kuungana. Kura hizo za maoni zitabadilika kadri siku zinavyosonga na kampeni zinavyoendelea.

Hata hivyo, yapo mambo yanayo influence hali ya sasa. Wiki iliyopita haikuwa nzuri kwa Trump kutokana na sakata la Mr Khan. Republicans wengine wameonyesha wazi kuchukizwa huku kampeni ikiwa inavurugana 'disarray' kwa kutommudu Trump

Hoja kubwa ya Republican ni kuwa mgombea Trump habebi agenda za chama Zaidi ya awazo yake binafsi yanayokinzana na tahamani za chama.

Katika kura za maoni kuna jambo linawatisha GOP. Kwamba, Hillary anaungwa mkono na sehemu kubwa ya GOP kuliko sehemu ya Dem inayomuunga mkono Trump

Pili, Hillary anaungwa mkono na wasomi katika kiwango cha vyuo na Trump akiungwa mkono Zaidi na wale wasio na elimu ya vyuo

Tatu, Kampeni ya Hillary imefanikiwa kuwavuta watu na si wale wasiompenda Trump

Nne, Idadi ya Dem wanaomuunga mkono Clinton ipo katika 84 na Trump 63 kwa mujibu wa takwimu za kura hizo za maoni

Kundi la wasomi wa vyuo limekuwa sehemu kubwa ya GOP, hivyo kulipoteza kunatia kiwewe GOP. Wakati huo huo Dem wanaendelea kunyemelea kundi la wasio na elimu

Katika wiki hii, kampeni ya Clinton imekaa kimya bila utata . Hii ni makusudi ili hoja za utata zizidi kumuumiza mgombea Trump

Trump ameonekana na hoja iliyowapendeza GOP kana kwamba amerudi katika mstari baada ya wiki ya maudhi

1. Kuhusu kiasi cha milioni 400 zilizolipwa Iran ambazo zinasemwa ni 'Ransom' ya kukomboa wamarekani waliokuwa wameshikiliwa.

Tutaifafanua hoja hii bandiko lijali

2. Trump kudai serikali ya Obama ita 'jecha' uchaguzi ujao

Inaendelea...
 
YALIYOJIRI

Tunaendelea na hoja ya Pesa za Iran
Hii imekuja baada ya Trump kubofoa kuhusu Ukraine , Russia na Crimea.
Ilionekana mgombea wa GOP hakufahamu tatizo hilo kubwa lililopo Ulaya

Kwa mara nyingine aka wa 'embarrass' GOP,kauli na utetezi wake vilitisha kwa kiasi. Surrogates wa GOP waliita 'political gaffe' kusiko eleza umakini wa mtu, ingawa damage ilishatokea

Tukio lilikumbusha 2008, mgombea mwenza Sarah Palin alipobofoa kuhusu siasa za kimataifa katika mahojiano na Kate Curie.

Jarida maarufu la Wall street limeandika Marekani kupeleka milioni 400 siku walipoachiwa waliokuwa wanashikiliwa na Iran.

Republicans na Trump wanaliongelea kama dhalili kwa Taifa na kwamba kwanini kiasi hicho kilipelekwa kwa Cash.

Trump ameenda mbali na kusema video inayozunguka mitandaoni ni ushahidi wa hilo

Kubwa ni kumfunganisha Hillary Clinton, Obama na pesa kuonyesha jinsi ulinzi na usalama ulivyodhoofika. Sehemu kubwa limechukua vichwa vya habari huku Trump akilipigia debe

OBAMA
Leo Rais Obama amekutana na makamanda makao makuu ya Pentagon.
Baadaye ameongea na waandishi kueleza mambo kadhaa ikiwemo ISIS n.k.

Obama aifahamu swali la pesa za Marekani zinazodaiwa ni Ransom litaulizwa

Obama ameeleza kwa kirefu na kina. Ni pesa za Sha wa Iran aliyetaka kuuziwa silaha na hakuuziwa. Iran waliomba zirudishwe lakini vikwazo havikuruhusu.

Kwavile vikwazo vimeondolewa kama sehemu ya nuclear Deal pesa zinarudishwa

Obama akasema wataakam wa sheria wameona, likienda international tribunal Marekani italipa bilioni 10. Kwa sasa ni takribani bilioni 1.4 kwasababu ya Interest, milioni 400 ni sehemu ya pesa hizo

Akaendelea kusema, ilibidi zilipwe kwa njia za kijima za Cash kwasababu hakuna mawasiliano ya kibenki au hazikuweza kupelekwa kwa 'wire'.

Akasema, lilizungumzwa kwa waandishi mwezi wa kwanza, siyo geni kama linavyoelezwa

Wachunguzi wa habari wamebaini video inayoonyesha ndege iliyobeba kiasi hicho si ya kweli.

Ni tukio lililotokea sehemu nyingine. Hapo ndipo Trump anaingia katika mtego wa kushabiki vitu bila kuwa na reliable sources. Huenda ukawa mjadala mpya utakaoleta sintofahamu

Majibu ta Obama yalionyesha utulivu na weledi. Ingawa mjadala utaendelea hasa kwa Republican, hoja zilizolenga kumuunganisha Hillary Zimepoteza nguvu kwani sasa ni suala la Rais wa Marekani.

Kwanini approval rate ya Obama ipo juu, na inaeleza nini kuhusu uchaguzi?

Inaendelea
 
TRUMP NA HOJA YA 'UJECHA'
Katika kuzua jipya na kupata attention, Trump amesema serikali itachakachua matokeo ya uchaguzi mkuu. Kauli hii imezua utata kama zilivyo kauli za Trump na kwa kiasi kikubwa imefunika hoja ya Mr Khan

Kama tulivyoeleza katika bandiko moja, Obama amejibu akiwa Pentagon kuwa uchaguzi wa Marekani hausimamiwi na serikali kuu 'federal' bali state, county hadi vituo. Akasema, kinachofanywa na serikali kuu ni kuona integrity ya zoezi pale penye utata

Hapa alimaanisha ikioneka kuna tatizo, FBI na vyombo vingine ndipo hushiriki, si kuhusu matokeo bali kuhakiki zoezi kwa uhalali. Ndio msingi wa hoja yake kuwa kuiba uchaguzi ni kichekesho kingine cha Trump

Wakati huo huo, approval rate ya Obama imefikia asilimia 55 karibia na Clinton 57 na Reagan katika wakati kama huu. Swali wanaojuliza wengi nini kimefanya imeongezeka kiasi hicho?
Hakuna jibu la mkato, hali ya uchumi bado si nzuri

Je, ni kwa Obama alivyoivusha Marekani katika deep depression iliyotokea?
Je, ni kwasababu ya siasa zake za nje ambazo kwa kiasi Fulani zimelenga kfuata uhasama?

Pengine ni kwasababu ulinganifu wa waombea 2016 na Obama unaonekana

Hakuna jibu la mkato

Huu ni mtaji mzuri wa kisiasa Clinton anaonekana kujifungamanisha na Obama

Lengo ni kutumia hii political capital kubakiza wagombea wanaomuamini Obama.
Clinton ametumia mifano akiwa secretary kuhusu maamuzi kadhaa

Hili lina advantage na disadvantage na Hillary acheze nalo vizuri.

Kujifungamanisha kutamuunganisha na mambo unpopular ya Obama.

Muhimu ni yeye kuwa yeye na kuchukua advantage ikibidi na si kujifungamisha kwa ujumla

Historia ya siku za karibuni inachanganya kuhusu Rais aliyepo madarakani kumsaidia mgombea. Mfano, Reagan alikuwa na approval rate takribani 57%.

Aliweza kumsaidia George Bush Senior kushinda uchaguzi

Bill Clinton alikuwa na approval rate ya 57% lakini haikuweza kumsaidia Al Gor kushinda

Je, Obama factor inaelekea wapi? Kwa Reagan au kwa Bill Clinton?


Tusemezane
 
Ahsanteni kwa michango yenu mizuri wadau wote wa hili Jukwaa!

Imenibidi niingie chimbo nichimbue kuhusu kile kitoto alichokikemea Mr Trump. Ukweli ni kuwa suala hilo halijabeba uzito wowote kwenye siasa zake tofauti nilivyokuwa nafikiria. Maana kamwambia tu kawaida kama baba anavyomwambia mtoto wake anyamaze au asepe kama baba anaongea. Sio ishu kuuubwa sana, japo naelewa siasa za wenzetu ni 'vulnerable' sana. Hili alisome mkuu Nyamizi

Yote ya yote namuona jamaa yangu akishinda, bado sijaona lolote la kumzuia hadi sasa sijui huko tuendako na matimbwili yake. Jamaa yangu anachotakiwa kufanya kwa sasa ni kutoparamia mambo bila ueweledi maana atazua la kuzua. Bora awatafute washauri wanaofahamu haya mambo ya 'system' kwa undani zaidi. Akiwa kwenye convention alikiri kuwa bintiye Ivanka alimshauri kidogo awe presidential na kuacha kushambulia sana, na matokeo yake kura zake za maoni kupanda. Aendelee kukumbatia ushauri wa bintiye!

Ishu ya Khan naona kama ya kitoto sana kufanywa na mtu wa hadhi yake, vile vile ishu ya 400ml USD na ndege iliyobeba ni kutojiongeza tu kwa mtu wa hadhi kama yeye. Anapaswa kuwa na 'timu' imara yenye weledi mkubwa katika masuala ya ki system ili kuepusha yanayoepukika. KUWA RAIS HAINA MAANA KUWA NI KUJUA KILA KITU. Najua akitulia na kuacha bange zake ana uwezo mkubwa sana wa kushawishi na kuelezea jambo kwa ufasaha mkubwa, lakini hatuliagi mara nyingi sana jamaa huyu utadhani shabiki wa nyimbo za ndi ndi ndi.

Pamoja na hayo mimi nina swali moja tu. Hv imewahi kutokea kwenye siasa za USA mgombea kupata kura nyingi za polls lakini kwenye uchaguzi halisi akashindwa? Just curious! Nafahamu kidogo kuhusu Romney na Obama kipindi fulani kulitokea jambo kama hilo.

Kuhusu Obama factor naona haitambeba Mama Clinton. Hii factor ndio iliyowaibua akina Trump na hata Sanders. Kama Hillary akijifunganisha na Obama itakula kwake. Salama yake ni kuwa yeye kama yeye.

Tuendelee kusemezana.
 
Nguruvi3 mkuu umeongelea issue ya approval rate ya Obama...kimsingi naona ni mtu anayesikilizwa sana na ana influence.Katika pitapita yangu YouTube nimeona katika vyama vyote viwili...Michelle amepata viewers wengi zaidi kuliko wote.Nini nguvu ya Michelle katika s iasa za marekani?
 
Nguruvi3 mkuu umeongelea issue ya approval rate ya Obama...kimsingi naona ni mtu anayesikilizwa sana na ana influence.Katika pitapita yangu YouTube nimeona katika vyama vyote viwili...Michelle amepata viewers wengi zaidi kuliko wote.Nini nguvu ya Michelle katika s iasa za marekani?
Mkuu Obama anasikilizwa kwasababu ya uwezo wake wa kujenga hoja au kuzitetea kwa mantiki.

Siyo kuwa anakubalika kwa wote la hasha hata wanaompinga wanakubali uwezo wa ujenzi wa hoja.

Michelle kama first lady wa kwanza Mwafrika aliwaondoa watu shaka juu ya uwezo wake wa kujieleza

Mwaka 2008 akiwa katika convention ya DNC alikwenda mbali na matarajio ya wengi na kuwa kivutio

Michelle ameondoka katika ule utamaduni wa FL kuwa 'too official' anachangamana na makundi ya jamii katika vipindi kama talk show, na hata kueleza anavyopendelea kama show ya Amrica Idol au America got the talents. Ni vitu vidogo lakini vinamweka karibu na jamii

Kikazi za FL ambazo si rasmi, ameshughulikia askari waliorudi kutoka vitani na wajane
Mara nyingi amewaalika na hivyo kuonekana ana jali.

Kitu alicho nacho ni 'charisma' ambayo pamoja na weledi wake inatengeneza mchanganyiko mzuri

Hotuba yake imeangaliwa sana kwasababu ya utata wa hotuba ya Melania
Ilitegemewa angeliongelea hilo, hakuzungumzia, jambo lililompa heshima zaidi

Ukiisikiliza hotuba yake ilikuwa ya ulezi zaidi ya siasa. ndipo anavuta wa pande zote

Kisiasa hana nguvu, bali kimvuto anao, na ndio Clinton kampeni inategemea kuutumia
Kwamba,anakundi linalo mhusudu na ndiko panapo lengwa
 
"TheDealer, post: 17091978, member: 110303"]Imenibidi niingie chimbo nichimbue kuhusu kile kitoto alichokikemea Mr Trump. Ukweli ni kuwa suala hilo halijabeba uzito wowote kwenye siasa zake tofauti nilivyokuwa nafikiria-Nyamizi
Hii issue ya katoto inaangaliwa kwa mitazamo miwili. Kwanza, ni wakati wa sakata la Familia ya Khana na Gold star.

Ilionekana kukosa subra kwa katoto kwasababu tayari ana 'strings' za Khan Family
Hili linaweza kuwa dogo, kukiwa na makando kando linaunganishwa

Pili, kwamba mtoto kulia iliweza ku-distract katika hotuba yake.
Ni busara akaa kimya wakati mzazi anamuondoa ukumbini.
Hakuwa na sababu za kuvuruga mtiririko kwa sauti ya katoto.

Wapo wanaoona hilo kama lack of focus na temperament isiyo sahihi
Bora awatafute washauri wanaofahamu haya mambo ya 'system' kwa undani zaidi.
Anao tayari lakini wapo frustrated na jinsi ya kummudu.
Ishu ya Khan naona kama ya kitoto sana kufanywa na mtu wa hadhi yake, vile vile ishu ya 400ml USD na ndege iliyobeba ni kutojiongeza . Anapaswa kuwa na 'timu' imara yenye weledi mkubwa katika masuala ya ki system ili kuepusha yanayoepukika. KUWA RAIS HAINA MAANA KUWA NI KUJUA KILA KITU.
Ni kweli, haina maana ya kujua kila kitu.

Rais anapaswa kutengeneza timu ya kumsaidia kupata habari za uhakika.
Leo asubuhi ameamka na kukiri kuwa video hajaiona.

Jana katika mikutano miwili alishadidia hiyo. Huenda timu haikmshauri, hakuwasikiliza au NI spinning kama za chaguzi za GOP. All in all,la video limeunganishwa na issue nyingine

Trump alimshambulia VP wa Dem Tim Kaine kuwa hakufanya kazi nzuri New Jersey.

Tunajua Tim Kaine ni kutoka Virginia na hajawahi kufanya kazi New Jersey

Kilichotokaea ni Trump kuchanganya, Tom Kaine aliyekuwa gavana miaka ya 1990 na Tim

Katika kampeni, wapinzani wameunganisha video ya Iran na hili la Tom na Tim Kaine kumuonyesha asivyo makini au not well informed
Najua akitulia na kuacha bange zake ana uwezo mkubwa sana wa kushawishi na kuelezea jambo kwa ufasaha mkubwa, lakini hatuliagi mara nyingi sana jamaa huyu utadhani shabiki wa nyimbo za ndi ndi ndi
Ana uwezo wa kushawishi si kwa ufasaha bali mbinu nyingine.

Labda nikuulize lini Trump ameeleza jinsi atakavyo deal na Mexico kulipia ukuta?

Pili, hebu tuambie, anaposema atawafyeka ISIS ni kwa mbinu gani ikiwa wapo katika miji si kwa 'conventional war' bali Ugaidi.

Trump atawamalizaji walioko Belgium au France?
Katika eneo ambalo ni vulnerable ni katika details, na siku za midahalo utathibitisha hilo
Pamoja na hayo mimi nina swali moja tu. Hv imewahi kutokea kwenye siasa za USA mgombea kupata kura nyingi za polls lakini kwenye uchaguzi halisi akashindwa? Just curious! Nafahamu kidogo kuhusu Romney na Obama kipindi fulani kulitokea jambo kama hilo.
Imeshatokea sana.

Polls haziwakilishi jamii kwa ujumla, zinatoa mwelekeo tu.

Mfano, Hillary alikuwa anaongoza point 9 Michigan, Sanders akashinda.

Sanders alipewa nafasi California, Hillary akashinda 10 points

Polls ni nzuri , tatizo lake ni kutokwenda nazo kila siku.

Mabadiliko kidogo tu yanaharibu polls kwa sehemu kubwa sana.

Kwa mfano, post convention ya DNC Hillary na Trump walikuwa karibu sana within margin of errors, baada ya Khan na Russia/Crimea mabadiliko hadi kufikia tofauti ya 10 points

Hizi Polls zitabadilika, unaweza kushangaa mwezi ujao Trump akawa anaongoza
Kuhusu Obama factor naona haitambeba Mama Clinton. Hii factor ndio iliyowaibua akina Trump na hata Sanders. Kama Hillary akijifunganisha na Obama itakula kwake. Salama yake ni kuwa yeye kama yeye.
Kuhusu Obama factor, nadhani tumejadili kuhusu Reagan na Clinton.

Tulisema zipo faida na hasara za kuambatana naye.
Tofauti na 2008 ambapo GOP walijitenga kabisa na Bush, unaweza kuona Dem wapo karibu na hasa wafuasi wake

Kuna nyakati za msaada kama jana kuhusu Iran, kuna nyakati inakuwa na tatizo.

Kuhusu Trump, hawa wahawakuibuliwa na Obama.
Mag3 ameeleza, ni sehemu ya Ubaguzi tu

Ukisoma historia, Trump hakumpenda Obama kuanzia siku ya kwanza, unawezaje kusema amechukizwa na Obama.

Mag3 kaonyesha azma ya Trump kugombea siku nyingi kuanzia 1990 huko.

Hivyo si kweli kuwa Obama ndiye chanzo cha akina Trump

Kuhusu Sanders, naye tumejadili sana uzi mwingine.
Nakumbuka tuliuliza nani yupo nyuma ya kundi la Sanders?

Huyu ni independents aliyemdharau Obama from day one

Naye kama Trump alikuwa na ambition siku nyingi, lilikuwa suala la muda

Wawili hao katika mizani, Sanders ni mzuri sijui kwanini unadhani aliibuliwa na Obama.

Ni mzuri wa sera anazoamini na kujieleza pamoja na kuunda timu.
 
BRIEFING

Kila siku Rais wa Marekani hutaarifiwa nini kinaendelea katika nchi na dunia hasa mambo ya usalama

Jana Rais Obama kasisitiza sana kuhusu wagombea kuwa makini na briefing hizo

Kwa sheria za Marekani, wagombe katika hatua ya mwisho hupata briefing za WH kila uchao

Ni habari nyeti zinazohusu ujumla wa nchi na dunia

Kwa waliomsikiliza Obama, watakubaliana kuwa anajua nini kinaendelea na anaongelea nini

Haya ndiyo mambo Rais mtarajiwa yoyote anatakiwa ayafikie

Hatua ya Clinton na Trump ni 'karibu' sana na kupewa nuclear code

Ikitokea Rais akapewa briefing za Australia na kuchanganya na Austria, si kuwa lina embarrass bali linaweza kuleta diplomatic row isiyo na ulazima
 
Nguruvi3 , Mag3 , jitegemee , Nyamizi na wakuu wengi wote ambao sikuwataja heshima iwe kwenu wote!

Tumeona namna Trump anavyopita kwenye tanuru gumu wiki sasa. Well, kujifunza kutoka kwake mnadhani nini Trump anapasa kufanya ili

a. hayo yasitokee kama yanavyotokea
b. kufanya damage control

Tusemezane
Mimi nadhani,Trump anapaswa sasa kubadili kabisa style yake ya Kampeni,anapaswa kujua kuwa Kampeni ya sasa si kama ile ya GOP.
Kwa sasa anapaswa kuwavutia Swing Voters zaidi na ikiwezekana hata wale ndani ya Democrat ambao hawampendi kabisa HC.Apende asipende anapaswa kufahamu kuwa GOP ina wenyewe,hawa awaangukie ili waweze kusawazisha mambo na wasonge mbele as Team,akiendelea hivi hivi huku Chama kikiwa kimegawanyika ajue kabisa kura za kwanza kukosa zitaanzia ndani ya Chama chake,nimeangalia CNN kuna baadhi ya waliokuwa wanamkubali sana wakati wa uchaguzi wa ndani,sasa hivi wanakiri kujuta kumchagua, pana mama mmoja alipouulizwa kura yake atampigia nani,alijibu "Hillary Clinton and there is no turning Back".

Hii inatoa picha mbaya sana kwake maana hujui ni wangapi sasa anawadissapoint,achilia mbali hawa Swing Voters ambao ndio kabisa hatawapata.
Papara zake za kuongea bila kuwa na uhakika zinampunguzia sana point kiasi cha kufikia watu kuhoji Utimamu wa akili yake.Awaachie wataalamu wamwamndalie Speech na akubali kabisa kuwa stage hii ya Kampeni si ya mbinu za kitoto tena,vinginevyo "Oval Office"atasikia na kuiona kupitia kwenye TV
 
Nguruvi3 , Mag3 , jitegemee , Nyamizi na wakuu wengi wote ambao sikuwataja heshima iwe kwenu wote!

Tumeona namna Trump anavyopita kwenye tanuru gumu wiki sasa. Well, kujifunza kutoka kwake mnadhani nini Trump anapasa kufanya ili

a. hayo yasitokee kama yanavyotokea
b. kufanya damage control

Tusemezane
Mkuu kuna makosa ya kifundi anayopaswa kuyarekebisha
Kwanza, lazima atambue ushindi unaanzia ndani ya chama chake.

Ana kazi ya kuvuta independent voters na mwisho kuwavuta Dem wasiompenda HC

Hilo litafanikiwa kwa kuondoa mtafaruku kati yake na GOP establishment , Tea party na core conservatives. Hivi tunavyoongea kuna uchaguzi wa ndani kwa seneta na congressmen and women. Hapa naomba kufafanua kuhusu hili

Seneti na Bunge la Marekani hufanya uchaguzi mara mbili katika kipindi cha miaka 4. Yaani wapo watakaochaguliwa uchaguzi huu, na wapo waliochaguliwa 2014 wakiita midterm election. Hii ina maaana term ni ya miaka 4, midterm ni kati kati ya miaka 4

Seneta MCain anagombea katika uchaguzi huu pamoja na Spika wa congress Paul Ryan
Nao hupitia mchujo ndani ya chama ambao ni mwisho wa mwezi huu.

Ndio maana kuna ugomvi na Trump kwasababu Trump amekataa kuwa endorse akiunga mkono wapinzani wao ndani ya chama

Habari zilizopo sasa hivi, baada ya VP kuwa endorse, Trump naye amefanya hivyo.

Kwahiyo kuna mtifuano ndani ya chama, kati ya Republicans tea party, conservatives na the establishment kama Paul Ryan na McCain. Tea party/conservative wanamuunga mkono Trump baadhi yao. The establishment hawana muafaka naye

Trump anapaswa kuleta harmony kwani hata akifanikiwa kuwa Rais, kama atapoteza uongozi wa seneti na Congress itamwia tabu sana.

Tumeona jinsi Obama alivyozuiwa mengi kwa kukosa majority ya seneti/ Congress.

Tuliona Obama alivyotumia majority kipindi cha kwanza kupitisha healthcare reform.

Pili, Trump ana washauri wazuri sana alioajiri.
Ana uwezo wa fedha na kuweza kupata the best. Tatizo ni kutowasikiliza na kufuata ushauri wao

Anachotakiwa ni kusoma hotuba, kuzielewa na kuzifanyia tathmini kwa lugha yenye stara
Huu ni uchaguzi mkuu ambapo sera zinazangaliwa Zaidi kuliko matusi ya primaries au caucus

Kwasasa anaangaliwa kama Rais mtarajiwa na lazima awe katika std hiyo. Si muda wa maigizo bali ukweli wa sera zake siku za baadaye

Kuhusu damage control, kwanza, arudi katika message na policy anazoamini.
Ajiuzie kurudia makosa yasiyo na ulazima.
Awe mwepesi wa kutafuta muafaka na pande atakazokwaruzana nazo na si ubabe

Ubabe kama wa gold star families uliendeleza mtifuano bila sababu za maana kwa muda mrefu na kusababisha uharibifu mkubwa.
 
RAMANI YA UCHAGUZI MKUU

Tunadhani ni muhimu tukaelewa ramani ya uchaguzi wa Marekani.
Ramani hii inaeleza mambo mengi sana, na kuifahamu itarahisisha sana kufuatilia habari

Mathalan, kwanini wagombea hawafanyi kampeni eneo kama Montana
Na kwanini kuna kitu kinaitwa swing, solid or lean states

Kwa ufupi uchaguzi wa Marekani hauhusishi kura za wananchi moja kwa moja.
Kura za wananchi zinatumika kupata wajumbe wa 'wajumbe' wanaomchagua Rais.

Wajumbe hupatikana kwa viti vya kuchaguliwa vya kila jimbo 'electoral college'

Ndiyo maana mgombea anaweza kupata kura nyingi za wananchi 'popular vote' na asiwe Rais

Angalia ramani hii ili tufuatane katika hoja hizo hapo juu za

2016_08_04_pres.png
 
Back
Top Bottom