Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #241
DEMOKRASIA GANI YA 'WAJUMBE' NA SI WAPIGA KURA?
Kabla ya kuiangalia ramani, ni vema tukazungumzia hoja nyepesi inayokuzwa bila sababu
Wapo wanaohoji mtindo wa Marekani ambapo Rais anachaguliwa kupitia wajumbe, na kwamba anaweza kupatikana hata akiwa na kura chache, kuna demokrasia ya kweli?
Swali hilo liliulizwa Wabunge wa conservative Uingereza walipomchagua mrithi wa Cameron bila wananchi kupiga kura. Wapo wanaohoji iweje Malkia awe mkuu wa nchi bila kuchaguliwa? Je, ni demokrasia ya kweli ? Na je wana haki ya 'kuzogoa' wengine?
Majibu ya maswali haya yapo sehemu moja.
Kwamba, demokrasia haiishii katika uchaguzi bali uchaguzi ni sehemu tu ya demokrasia.
Demokrasia ni makubaliano ya kujiendesha, kwa kupanga, kuchagua na kutenda
Demokrasia zinatofautiana, muhimu ni kuwa ili demokrasia ifanye kazi , makubaliano ya jamii husika yanapaswa kutimizwa
Kwa utaratibu wa Marekani, kuanzia mchujo wa wagombea hadi Urais wananchi wanashiriki. Tofauti ni kuwa, ushiriki wao si wa moja kwa moja kama wa wetu
Kwa asiyejitokeza kupiga kura chaguzi za awali (primaries and caucus) na asiyejitokeza kuchagua wajumbe 'electoral college' hatakuwa amemchagua Rais na hilo ni tatizo lake
Ndivyo Uingereza ilivyokubaliana Malkia ni mkuu wa nchi, waziri mkuu ni kiongozi wa serikali anayepewa ridhaa na wananchi.
Tukihoji demokrasia za US na UK zilikomaa, tusiache kujiuliza, iweje makamu wa Rais atoke Zanzibar kwa sababu tu ya uzanzibar ikiwa sisi ni Taifa moja?
Iweje asitoke eneo jingine kubwa kiuchumi na idadi kubwa ya wananchi?
Well, tulikubaliana kiongozi akitoka upande mmoja, makamu anatoka upande wa pili.
Hiyo ndiyo sehemu ya demokrasia yetu, hakuna anayehoji utaratibu huo na atakayehoji atakuwa ametuingilia kwa kiasi na kasi kubwa.
Inapotokea mambo kinyume na makubaliano yetu wenyewe, ndipo wenzetu wanahoji, mbona tunakwenda kinyume na makubaliano yetu?
Kwa mfano, tumekubaliana taratibu za chaguzi zetu ambazo kwa viwango vyetu ndiyo demokrasia tuliyo afiki. Inakuwaje yanatokea kama yale ya kufuta uchaguzi mzima ambayo hayapo katika makubaliano yetu?
Inakuwaje tumeunda vyombo kama msajili wa vyama ili kuratibu shughuli za kisiasa, kinyume chake jukumu hilo linageuka kuwa la mtu au upande chama kimoja?
Tumekubaliana kwa demokrasia yetu matatizo ya vyama vya siasa yana mlezi msajili wa vyama,mbona haonekani kuchukua jukumu lake hili la mikutano kupigwa marufuku?
Jukumu la msajili si kutoa vibali bali kufafanua sharia alizokabidhiwa kama zinawiana na hali iliyopo. Vipi amekaa kimya kana kwamba kila jambo ni shwari?
Mivutano hii ya kisiasa tunatatuaje ikiwa hatuheshimu makubaliano yetu ya uendeshaji wa siasa zetu nchini?
Ni kwa mtazamo huo, kuhojia demokrasia zilizokomaa kama za Marekani au Uingereza ni suala lisilo na mashiko.
Pengine kabla ya kulalamika kuhusu kuingiliwa na nchi za magharibi, ni vema tukajiuliza, je tunatenda tulichokubaliana kama sehemu ya demokrasia yetu!
Tusemezane