Obama
-America dream, no wall will ever contain
-Anazungumzia jinsi demokrasia inavyofanya kazi katika kutafuta suluhu ya matatizo katika jamii
-Anaongelea values za Amerika na hasa Patriotism
Ametokea HC na wapo pamoja
Obama amezungumza kwa hisia na kuwa tough sana kwa Trump
Tathmini inafuata
General wa Navy
Huyu aliongea ili kuhakikishia watu jeshi la Marekani ni imara
Alikusudiwa kumjibu Gen aliyekuwepo Republican convetion aliyeponda sana Obama kuhusu Jeshi la Marekani
Jenerali wa Dem aliongea ili ku set tone kwa mashambulizi dhidi ya Trump
Joe Biden
Uncle Joe anajulikana kwa kusema bila kumung'anya maneno
Yeye alimwendea Trump moja kwa moja akitumia hoja za Jenerali
Kwamba, Trump ni hatari kwa kueleza kuhusu kauli ya kumkaribisha Putin kutafuta emails za Clinton.
Alichokusudia Joe ni kuonyesha jinsi Trump alivyo hatari katika usalama na alivyo vulnerable kwa ''dikteta' Putin.
Joe alifanikiwa kumchonganisha Trump na Putin, na kuonyesha hatari yake kwa umma wa Marekani. Alikuwa na hotuba kali iklenga GOP
Lakini pia Joe akiwa mshiriki wa mambo ya seneti, alionyesha namna GOP walivyopinga miswada iliyopelekwa, alichonganisha congressmen/Women , masenata na wapiga kura
Leon Panetta
Huyu alikuwa WH secretary wakati wa Bill Clinton, na akawa CIA Dir
Uwepo wake ulikuwa kuonyesha hali ya usalama ilivyo ili kutofautisha na kauli za Trump na GOP zinazoonyesha nchi ipo katika wakati wa hatari
Pia alionyesha jinsi Trump alivyo novice katika mambo ya usalama wa Taifa
Ni kwa bahati mbaya hotuba yake ilikatishwa na wafuasi wa Sanders
Lengo la Panetta lilikuwa kuwahikishia Wamerekani kuwa nchi ipo salama tofauti na hofu wanayoieleza Republican
Panetta alikuwepo situtaion room wakati wa shambulizi la Osama.
Picha hiyo alikuwepo Hillary pia.
Hapa ilikusudiwa kuonyesha Hillary ana uelewa vyombo vya ulinzi vinavyofanya kazi
===============================SIKU YA TATU
Ilikuwa ya kujibu hoja zinazogusa Taifa.
Eric Holder
Mwanasheria mkuu wa serikali ya Obama. Uwepo wake ulikuwa kueleza justice system ilivyo na matatizo kwa mtazamo wa kisheria. Ililenga Black lives matter.
Akina mama wa waliotathirika
Hawa walizungumzia mauaji ya watoto wao. Hii ilikuwa kuunganisha kati ya kauli za Eric Holder na tatizo lililopo
Mkuu wa Polisi
Aliongea mkuu mmoja wa Polisi kueleza tatizo hilo hilo, ingawa pia kueleza matatizo yanayokabilia kazi za Polisi.
Walichkusudia Dem ni kuonyesha uwepo wa matatizo kwa pande mbili
Na kwamba, suluhu ni kuongea , kurekebisha sheria na kulinda watunza amani. Walikuwa wana strike balance katika tension iliyopo
Katika hili, Dem walifanya kosa la kifundi. Walitakiwa waalike ndugu za Polisi walioathirika na mauaji ya karibuni kama Dallas na Lousiana.
Mkuu, wanaokuja si kwa Dem, hata Republican wamefanya hivyo===============================
Asante sana kwa uchambuzi.
Mimi najaribu kuangalia uteuzi wa wagombea hasa wa Dem (chama tawala) kupitia utaratibu wa uendeshaji wa siasa zetu hapa nchini.
Hivi ni sahihi Navy, mkuu wa Polisi, mwandamizi wa CIA kuja jukwaani tena la chama cha Siasa (Dem) kumpigia Kampeni Hillary? Hii wapi 'neutrality' ya vyombo vya usalama vya Marekani kwenye siasa?
Hivi tuna haja tena ya kulalamikia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kutuhumiwa kukibeba chama tawala? Wakati wale wanaoutuongoza kwa ubora wa demokrasia na ambao tunaiga kwao masuala ya demokrasia na utawala bora wanatenda tofauti na wanaovyotuelekeza?