Hizi siyo habari njema kwa team HRC. Ni zile za Trump kusema nini atafanya siku 100 akipata urais.
======
Trump told the rally that on his first day in office, his administration would announce six measures to "clean up the corruption and special interest collusion" in Washington:
Constitutional amendment to impose term limits on all members of Congress.
Hiring freeze on all federal employees to reduce that workforce through attrition, exempting jobs in the military, public safety and public health.
Requirement that for every new federal regulation, two existing regulations must be eliminated.
Five-year ban on White House and congressional officials becoming lobbyists after they leave government service.
Lifetime ban on White House officials lobbying on behalf of a foreign government.
Complete ban on foreign lobbyists raising money for American elections.
======
Ameyasema haya, kwenye kampeni zake huko Gettysburg, Pa.
Mkuu nimesikiliza live katika hiyo hotuba
Hayo uliyoweka ni machache sana pengine kulingana na source zako ambazo nakuhakikishia ni tofauti kwa maudhui na kile kilichosemwa.
Trump aliongelea kuwafungulia mashtaka wanawake wanaomtuhumu baada ya uchaguzi
Akasema ata repeal Obamacare
Atavipa vyombo vya ulinzi zana nzuri kukabiliana na wimbi la uvunjaji wa sharia na hapa akilenga Police
Orodha ni ndefu sana, kwa ufupi ni mambo 8 yenye vipengele
Katika hoja zilizomletea tatizo ni ile ya kuwafungulia wanawake mashtaka ambayo kwa kutokuwa na uzoefu wa siasa hakupaswa kuichanganyana na mambo mengine.
Kwasasa ndiyo inayozungumzwa kuliko mengi
Pamoja na hayo wachunguzi wa mambo wanauliza kama hoja alizotoa zinatekelezeka.
Na kama ulikuwa ni wakati muafaka.
Midahalo 3 ameshindwa kujenga hizo hoja , jambo lililomnyima fursa ya kuwasiliana na watu Zaidi ya milioni 100 ambao kati yao wapo wapiga kura.
Kwa wakati huu watu wanaendelea na kura za awali na inakadiriwa 30-40% wameshapiga kura
Je, hotuba ya jana ambayo haikuwa katika prime time imewafikia wapiga kura?
Hoja zinazojichanganya ni za deregulation.
Wakati wa Bush hakukuwa na regulations , matokeo yake ni recession kwasababu watu wali abuse system.
Fuatilia collapse of house market na gang of 9 utaelewa
Kama deregulation ingefanya kazi kwanini haikuwahi kufanya kazi kipindi cha Bush?
Regulation zina maana moja, kuhakikisha mwananchi wa kawaida hawi victim wa tycoon kama Trump.
Huwezi kuamini katika recession watu walitengeneza pesa, na Trump akisema mwenyewe ulikuwa wakati mzuri wa kununua estates na Nyumba.
Hivyo hilo liangalie kama litasaidia au la
Katika mambo anayolalamikia Trump ni pamoja na executive order za Rais.
Hata hivyo yeye anataka kufuta hizo executive order kwa executive order.
Bila hivyo hawezi kufanikiwa kwasababu kuna sharia zinazopita bungeni
Constitution amendment lazima ipite katika mkondo husika.
Hao wanaoguswa ndio watakaopitisha sharia
Trump akasema polls zinaoaminika zinaonyesha akiwa anaongoza.
Well, akiongoza poll zinaaminika, kinyume chake zinakuwa rigged
Katika suala la 'rig' hapa pia ameogelea, kwamba kuna fraud zinaendelea.
Wapo wataalam wanaomuonyesha kuwa uchaguzi wa Marekani ni decentralized kiasi kwamba kama kuna fraud ni kituo kimoja haiwezi kuwa national wide
Kwa uchache, alichosema ilipaswa akiseme miezi mingi, kwa kuhofia challenges akasubiri muda huu ili pamoja na kukwepa hoja afiche udhaifu wa matatizo ya akina mama yanayomkabili
Nadhani tafuta hotuba yake ili upate details, ulichonukuu ni 1/10 ya kilichosemwa