Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

Labda hujanielewa tangu mwanzo ktk michango yangu,nilisharudia mara nyingi sana ukisoma michango yangu hapa. Namuunga mkono na mguu Donald trump mpaka kesho,kwa sababu sijawahi kuwaamini wanawake ktk mambo makubwa..! Na sina sababu ya kuwaamini. Kuna kitu usichokielewa hapa,kuhusu sifa za kugombea Donald trump anazo ndo maana aliruhusiwa kugombea.

Nnachosema hapa,wagombea wote,wameonekana kuwa na makando makando mengi sana kiasi kwamba km kungekuwa na umakini mkubwa ktk uteuzi wangeweza kuwaacha.

Naona unataka kutetea hata dhambi ambazo clinton mwenyewe amekiri na kuomba radhi...lkn kwako ni uongo uliopikwa na republican!!! Sisi kazi yetu ni kuangalia wanavyotifuana,lkn mwisho wa siku wamarekani wenyewe ndo wataamua.
Naona wewe hukufuatilia uchambuzi uliofanyika wakati wa primaries tuliposema wazi kabisa kwamba mbinu alizotumia Trump hazingefanikiwa huko mbele ya safari.

Trump alijengwa na media ambazo sasa anazilalamikia kwamba zinampendelea Clinton. Kwa bahati nzuri mimi nafuatilia Sana matangazo ya Fox News na naelewa Sana unachosema.

Walioanza kusema Trump Hana sifa Ni Republicans na hapo mwanzo waliungwa mkono na hao hao wanaomsifu hivi sasa. Wenye msimamo bado wanaamini hivyo lakini wanafiki wamebadilika.

magode, hakuna binadamu mkamilifu lakini Ni uenda wazimu kumweka Clinton na Trump katika mizani inayofanana. Hata wachambuzi wanampa Clinton nafasi kubwa ya kushinda, 93%.

Clinton kafanya makosa ya kiubinadamu lakini kwa Trump uhalifu Ni tabia. Unaposema huwaamini wanawake moja kwa moja unaharibu hoja zako na mjadala wowote nawe unakuwa mgumu.

Naomba samahani kwa makosa mengi kiuandishi, kwa umri wangu simu inanipa shida Sana.
 
"Mag3, post: 18159031, member: 10873"]Naona wewe hukufuatilia uchambuzi uliofanyika wakati wa primaries tuliposema wazi kabisa kwamba mbinu alizotumia Trump hazingefanikiwa huko mbele ya safari.
Tulisema sana. Mbinu za 'character assassination' na kujibu kwa mkato bila sera tulijua zitakwama.

Alianza na Jef, kisha Fiorina, akaja kwa little Rubio,halafu Kasich na mwisho akahamia kwa Ted Cruz

Uchaguzi mkuu si rahisi. Watu wanachuguza kila kitu, wana nafasi kubwa kuliko lundo la watu 16. Wanataka kujua Rais ajaye atakuwaje na wanaangalia sera kwa undani wake. Hapo ndipo penye tatizo kwa Trump
Trump alijengwa na media ambazo sasa anazilalamikia kwamba zinampendelea Clinton.
Akasema hatumii pesa kwa advertisement ingawa leo analalamika
Walioanza kusema Trump Hana sifa Ni Republicans na hapo mwanzo waliungwa mkono na hao hao wanaomsifu hivi sasa. Wenye msimamo bado wanaamini hivyo lakini wanafiki wamebadilika.
Republican wa kweli wamegoma. Gavana mmoja amejitokeza na kuhoji Trump anaposema rigged election ana maana gani ikiwa magavana 37 wa Republican ndio wasimamizi?
Clinton kafanya makosa ya kiubinadamu lakini kwa Trump uhalifu Ni tabia.
Juzi katika mdahalo kasema hakuwafanyia lolote wanawake wanaomtuhumu. Siku mbili kabla ya mdahalo mkewe akiwa na Anderson copper katika mahojiano alisema Trump alimuomba radhi!!!
Unaposema huwaamini wanawake moja kwa moja unaharibu hoja zako na mjadala wowote nawe unakuwa mgumu.
Ndio maana nimemwambia Europe inaongozwa na Merkel. UK pia n.k.
 
Misingi ya demokrasia ya Wamerkani ni mizuri .
....
Misingi gani wakati hawataki watu wajue ukweli wa kinachoendelea? Hivi hoja gani ya kidemokrasia ambayo imeipa nguvu marekani kuzuia Russia kuwa muangalizi wa uchanguzi huu??. Na wao siwanataka, Russia iwe na demokrasia , mbona sasa wanawazuia kuja kuwa waangalizi wa uchaguzi ili wajifunze ?? Hivi Tanzania ingefanya hivyo, nini kingetokea?

Kuzuiwa kwa Russia kumeelezwa kwenye link hii hapa.
United States bars Russian monitors from presidential polls – elections commission
 
Mkuu Tanzania iliwaondoa waangalizi baada ya uchaguzi na sakata la Zanzibar haraka, hakuna kilichotokea !!!

Siasa za US na USSR zipo katika level nyingine. Mawakala 15 wa ulinzi na usalama wamethibitisha Russia kuingilia uchaguzi.
Katika mazingira hayo usidhani USSR itapeleka waangalizi, ni KGB

Hata waangalizi wanaokuja Tanzania ukichunguza sana utaona kazi wanaofanya si moja. Ndiyo maana unaweza kukuta US wana details za Tanzania kuliko wewe na mimi.

Katika level ya wababe hao, si suala tu la kusema karibuni!
 
UnderlineItalic: Waliruhusiwa kushuhudia kampeini na hatua za upigaji kura. Hatukubagua waangalizi kwa kuwazuia.

Blackbold: Mkuu unawaamini hao jamaa...kweli? Jamaa ambao wanamkingia kifua 'mama' ashinde kwa udi na uvumba!! Russia inatumika kukwepesha tuhuma za DNC na ku'rig' kura za maoni za chama hicho za upendeleo. Pia inajaribu kufifisha tuhuma nzito dhidi ya HRC zinazosambazwa na wikileaks. Kudhibitisha kuwa maji sasa yamewafika shingo kwa damage ya emails za wikileaks, leo wame'block' mitandao maarufu zilizokuwa zinasambaza email hizo kwa kasi ikiwemo 'Tweeter'.

RED: KGB ilikuwa ina 'fanya' kazi kipindi cha SOVIET. Kwa sasa wana FBS.
 
Russia inatumika kukwepesha tuhuma za DNC na ku'rig' kura za maoni za chama hicho za upendeleo.
Kama unaamini uchaguzi wa Marekani unaweza kuwa "rigged" kumpendelea HRC basi ni wazi hujui uchaguzi wa Marekani unavyofanyika! Kama hali hiyo ingewezekana, wenye nafasi ya ku'rig' kama unavyodai ni Republicans kwa sababu wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo mengi ni Republicans na kila jimbo lina sheria zake za uchaguzi.
 
Taarifa ya REUTERS ya leo,inaonyesha 70% ya republican wanaunga mkono kauli ya Donald trump kwamba watakubali matokeo km trump atashinda. Hivi ni kweli hakuna tatizo hapo?? Kumbuka pia Al-gore alilalamika kuchezewa rafu aliposhindwa na G.bushi..!! Sisi tulio nje nadhani kuna kitu ambacho huwa tunaaminishwa kipo clear lkn kiuhalisia hakipo vile. Kwakweli mkuu mag3 na nguruvi3 hakuna namna ya kunifanya niwaamini hawa viumbe. Nguruvi3 umejitahidi kuonyesha wanawake waliofanya vizuri,lkn ukiweka orodha ya walio-fail ni aibu kuliamini hilo kundi..
 
Taarifa ya REUTERS ya leo, inaonyesha 70% ya republican wanaunga mkono kauli ya Donald trump kwamba watakubali matokeo km trump atashinda. Hivi ni kweli hakuna tatizo hapo??
Hii umeipata wapi mwenzangu! Je Trump akishindwa? Nadhani unaongelea asilimia 70% ya mashabiki wa Trump na si Republicans!
Kumbuka pia Al-gore alilalamika kuchezewa rafu aliposhindwa na G.bush..!!
Si kweli. Al Gore hakuwa na haja ya kulalamika kabla ya uchaguzi ila katika jimbo la Florida, kura ni lazima zirudiwe kuhesabiwa kama tofauti kati ya wagombea haifikii asilimia fulani. Aliyeagiza hilo kufanyika alikuwa ni gavana wa jimbo hilo ambaye alikuwa ni Republican. Hilo moja, lakini la pili ni kwamba Al Gore alipata kura nyingi kuliko Bush ingawa kwa namna majimbo ya uchaguzi yalivyogawiwa na uongozi chini ya GOP, Bush alipata wajumbe zaidi.

Hilo jambo ni tatizo sana na litaendelea kuleta matatizo hadi hapo magavana waliopo watakapoangushwa na ugawaji mpya wa majimbo ya kura kufanyika kulingana na idadi ya wakaazi bila kujali itikadi.
Sisi tulio nje nadhani kuna kitu ambacho huwa tunaaminishwa kipo clear lkn kiuhalisia hakipo vile.
Inawezekana wewe unajihesabu kama aliye nje, lakini kwa mambo ya Marekani huhitaji kuwa Mmarekani kufuatilia yanayoendelea. Nina hakika miongoni mwetu wako ambao wamekuwepo Marekani kwa zaidi ya miaka 30 na si hivyo tu wako wengi tu wanaojua kuliko hata Wamarekani wenyewe. Usidhani Wamarekani wote ni vipanga..ingekuwa hivyo mtu kama Trump hangefika hapo alipofika.
Kwakweli mkuu mag3 na nguruvi3 hakuna namna ya kunifanya niwaamini hawa viumbe. Nguruvi3 umejitahidi kuonyesha wanawake waliofanya vizuri,lkn ukiweka orodha ya walio-fail ni aibu kuliamini hilo kundi..
Marekani haijawahi kuwa na Rais mwanamke na hivyo hoja hii nafikiri ni mufilisi.

Magobe, kumbuka kitu kimoja...majimbo mengi Marekani yanashikiliwa na magavana kutoka Republican Party na katika nyakati tofauti magavana hawa walikula njama za kugawanya majimbo ya uchaguzi ili kuwawezesha kupata wawakilishi wengi ndani ya House na Senate. Katika sehemu ambazo wanachama na wapenzi wao walionekana kuwa wengi majimbo yaligawanywa na katika yale ambayo yalishikiliwa na Democrats yaliunganishwa.

Matokeo ya zoezi hili ni kwamba ingawa Congress nzima inao Republicans wengi kuliko Democrats, wapiga kura wa Democrats walikuwa wengi kuliko wapiga kura wa Republicans. Ndio maana, pamoja na Obama kupata ushindi mkubwa mwaka 2012, Democrats walipoteza House na Senate. Hii ni sawa na hapa kwetu CCM kushinda Urais kwa kura nyingi lakini kupoteza ubunge! Nadhani ikitokea hivyo hapa, hakutakalika wala kulalika.

Na mwisho naomba nikupe kidogo juu ya mgombea, Donald Trump. Mwaka 1982 (miaka 34 iliyopita) Trump alikuwa tayari anayo mkononi USD 200,000,000! Kama angeziweka tu kwenye stock ama benki ya akiba, hivi leo angekuwa na USD 15,000,000,000 (trilioni 15!) Lakini akaamua kufanya biashara...na kweli kajenga majumba lakini kaishia kupoteza USD 12,000,000,000 (dola trilioni 12!) sawa na Tshs. 30,000,000,000,000!

Trump kama hangekuwa na hela za kurithi toka mwanzo, hivi leo labda angekuwa anasota jela lakini penye udhia penyeza rupia...badala yake na kwa ajabu kabisa eti ndiye mgombea wa Urais Marekani. Hujafa hujaumbika.
 
Marekani iliwahi kutawaliwa na GWBush, kwa hiyo kutawaliwa na DJTrump halitakuwa jambo la ajabu sana, isipokuwa huyu jamaa ana akili ndogo sana kuliko nilivyokuwa naamini. Inaonekana kabisa kuwa ujanja wa kupata hela siyo reflection ya akili katika maisha. Jamaa ni mjanja sana kwenye hela, lakini anapoongea huwa anamwaga pumba tupu. Mtu huwezi kuondoka na chochote kutoka kwenye hotuba zake.
 
Mkuu magode

Hii hoja ya wanawake kama alivyokujibu Mag3 inakutia wasi wasi bila sababu kwa kile kinachojulikana kama 'Male chauvinism'

Ukiangalia katiba ya Marekani ina checks and balances nyingi. Nchi inatawaliwa na haitawaliwi na mtu. Si suala la mtu kuamka na kusema atakalo

Kuna Rais -utawala, Bunge la juu(senate), Bunge la chini (Congress) na mahakama

Kwasababu ya mpangilio huo Obama ameshindwa kutekeleza mambo mengi aliyotarajia

Hoja ya akina Trump ya kujenga infrastructure, architect wake ni Obama.

Seneti na Congress zilikuwa chini ya GOP, alipokea antipathy na kushindwa kutekeleza

Ilifika mahali kulikuwa na government shut down.

Ukirudi katika mamlaka, kwanza ni Rais, Makamu wa Rais ambaye pia ni kiongozi wa Seneti na kisha ni Spika wa bunge (congress), mlolongo unaendelea kufuata seniority ya Cabinet ambapo next baada ya Spika ni secretary of state, sec. Treasurer n.k

Kama utakumbuka Spika wa kwanza wa Congress mwanamke alikuwa Nancy Pelosi, na katika state of union George alisema yeye ndiye Rais wa kwanza kutamka neno 'madame Speaker'

Sasa kama unadhani Rais wa US hawezi kuwa mwanamke, ilikuwaje 3rd inline akawa mwanamke?
Hivi hapa huoni kulikuwa na 'Rais' anayesubiri muda, Nancy Pelosi?

Ukiacha Nancy, yupo Madeleine Albright sec of state ambaye kwa mlolongo niliyokupa alikuwa wa 4 ikiwa kungalitokea matatizo ya Rais, Makamu na Spika kutoweza kushika nafasi ya 'Urais'

Yupo Baroness lady Ttahtcher aliyetawala UK kwa miaka 10 mfululizo.
Huyu naye aliwezaje mara zote hizo

Nilikuonyesha akina Indira Gandhi waliotawala India yenye watu Zaidi ya milioni 900.

Kuna mahali umejenga hoja kuwa wapo waliofeli.

Ndipo tunakuomba utupe elimu ya wanawake waliofeli kwa majina na nafasi zao ili nasi tufunguke macho
 
Marekani iliwahi kutawaliwa na GWBush, kwa hiyo kutawaliwa na DJTrump halitakuwa jambo la ajabu sana, isipokuwa huyu jamaa ana akili ndogo sana kuliko nilivyokuwa naamini. Inaonekana kabisa kuwa ujanja wa kupata hela siyo reflection ya akili katika maisha. Jamaa ni mjanja sana kwenye hela, lakini anapoongea huwa anamwaga pumba tupu. Mtu huwezi kuondoka na chochote kutoka kwenye hotuba zake.
Mkuu Kichuguu hilo la Marekani nalo linawezekana kabisa.

Kuna watu wakiulizwa kwanini wanaamini katika 'Make America great again' hawawezi kutetea kwa sera.Hasira zao dhidi ya serikali iliyopo au Dem zinawasukuma waamini tu

Yupo aliyeulizwa kwanini atamchagua Trump, akasema Trump ni mfanyabiashara anajua uchumi

Huyu kaaminishwa na Trump anayesema yeye anaweza kwasababu aliweza kujenga makampuni makubwa

Hivyo wapo wanaoamini uwezo wa Trump kibiashara ni dalili nzuri ya kukua uchumi.

Hakuna anayejishughulisha kutafuta mengi kuhusu Trump

Kumbu kumbu zinaonyesha amefilisika mara ya 3. Hiyo inaweza kuwa sifa nzuri kiuchumi

Trump ana madeni na yeye amekiri ni king of debts, hilo ni jema?

Tax return hataki kuonyesha, inasemekana utajiri wake ni Bilioni 4.5 na si 10 anazosema

Kuongoza nchi na kuongoza kampuni ni vitu viwili tofauti.
Katika mdahalo aliulizwa maswali mazuri ya uchumi.

Nadhani Hillary alikuwa na majibu, Trump hakuwahi kutetea sera zake.

Hii maana yake uchumi binafsi hau reflect uchumi wa jamii kutokana na hali mbali mbali

Ni kwa mantiki hiyo, kwa mara ya kwanza Republican wanapoteza kuungwa mkono na watu wenye college education and above.

Hili ni kwasababu ya hoja uliyoitoa kuwa 'ukimsikiliza ni ngumu sana kupata substance'

Tumeliongelea hili jambo hadi baadhi wakatuhumu kwa dhati tunamshambulia tu.

Ukweli ni kuwa hata leo alipotoa mada ya nini atafanya katika siku 100, alichoweza ni kusoma teleprompter , hakufafanua sidhani kama anajua kilichoandikwa kiuhalisia

Republican wengi wanajisikia aibu hasa wakiwakumbuka akina John Kasich, mtu anayejenga hoja kweli

Lakini kwa US kuna nyakati za surprise kama ilivyokuwa Bush Jr.

Tofauti na Trump Bush alikuwa Gavana, alishaurika na alielewa hata kama sera hazikukubali au alikwenda kombo. Huwezi kuwaweka katika mizani
 
Hizi siyo habari njema kwa team HRC. Ni zile za Trump kusema nini atafanya siku 100 akipata urais.
======
Trump told the rally that on his first day in office, his administration would announce six measures to "clean up the corruption and special interest collusion" in Washington:

Constitutional amendment to impose term limits on all members of Congress.

Hiring freeze on all federal employees to reduce that workforce through attrition, exempting jobs in the military, public safety and public health.

Requirement that for every new federal regulation, two existing regulations must be eliminated.

Five-year ban on White House and congressional officials becoming lobbyists after they leave government service.

Lifetime ban on White House officials lobbying on behalf of a foreign government.

Complete ban on foreign lobbyists raising money for American elections.
======
Ameyasema haya, kwenye kampeni zake huko Gettysburg, Pa.
 
Mkuu

Nguruvi3
Km nchi ya marekani ina cheks & balances haitawaliwi na mtu kutokana na mfumo wao. Tatizo liko wapi sasa kwa DT kuwa Rais wakati unajua karibu kila kitu anaweza kudhibitiwa!!?

Hoja kwamba Trump hawezi kujenga hoja wala kutolea ufafanuzi yale anayoahidi mbona lipo wazi,trump si mwanasiasa na hajawahi kufanya siasa. Wenye maneno mazuri ni wanasiasa,ndo maana HC anawavutia wengi kutokana na uwezo wake wa kujenga hoja na lingekuwa jambo la kutisha km angezidiwa na trump kujieleza wakati yupo ktk siasa more 30yrs.

Hoja ya utajiri wa trump na kujenga uchumi,hakuna ubishi kwamba mfanyabiashara km trump aliyeimarisha urithi wa baba yake hadi hapo alipo anaweza kusaidia sana kujenga uchumi imara kwa kushirikiana na taasisi za ikulu.
Kule kuanguka kwake km mfanyabiashara, ndo kumemjenga zaidi na utajiri wake kwa mujibu Forbes ni 4.6bl. Lkn kwa mujibu wake mwenyewe,anadai utajiri wake unafikia 10bl. Mkuu kwenye biashara ukianguka unajengeka zaidi,. Me ni mmoja wa watu walioanguka sana mwaka 2007. Huwezi amini mwaka 2009 nilikuwa nakosa hata nauli ya daladala,lkn leo miaka 6 baadae,namalizia nyumba hapa mjini ambayo kiwanja peke yake nimenunua tsh.17ml. Kwa mfano wangu na wa trump mwenyewe hoja ya kufilisika ni hoja mfu.

Kuhusu wanawake walio-fail ni pamoja na markel mwenyewe,na hata chama chake amekishushia umaarufu.

Mwingine ni Rais aliyeondolewa kwa aibu huko brazil. Hapa nchini sijawahi kuona hata kiongozi mmoja mwanamke akifanya vizuri..hata wabunge wanawake wa upinzani wanaoonekana kufanya vizuri ni kutokana tu upande walipo. Lkn hata huko bado wapo wanaoonyesha udhaifu wa kushangaza km huyu mbunge anayehangaika kumtetea Lipumba.

Watu waliompigania mpaka kupata jimbo leo anawaona punguani halafu aliyemkimbia kawa lulu. Clinton sifa pekee aliyonayo ni hiyo ya kujieleza na inatokana na kufanya siasa kwa muda mrefu lkn huyo ni More satan...!! Kuna watu wanamuona trump km mtu hatari,lkn ukweli ni kwamba,mfanyabiashara km yeye,hawezi kuanzisha vita kwa sababu vita ni pesa. Huyu akiingia white house,marekani haitakuwa na vita kwa kipindi chote cha utawala wake.
 
Mkuu nimesikiliza live katika hiyo hotuba

Hayo uliyoweka ni machache sana pengine kulingana na source zako ambazo nakuhakikishia ni tofauti kwa maudhui na kile kilichosemwa.

Trump aliongelea kuwafungulia mashtaka wanawake wanaomtuhumu baada ya uchaguzi
Akasema ata repeal Obamacare
Atavipa vyombo vya ulinzi zana nzuri kukabiliana na wimbi la uvunjaji wa sharia na hapa akilenga Police
Orodha ni ndefu sana, kwa ufupi ni mambo 8 yenye vipengele

Katika hoja zilizomletea tatizo ni ile ya kuwafungulia wanawake mashtaka ambayo kwa kutokuwa na uzoefu wa siasa hakupaswa kuichanganyana na mambo mengine.

Kwasasa ndiyo inayozungumzwa kuliko mengi

Pamoja na hayo wachunguzi wa mambo wanauliza kama hoja alizotoa zinatekelezeka.
Na kama ulikuwa ni wakati muafaka.

Midahalo 3 ameshindwa kujenga hizo hoja , jambo lililomnyima fursa ya kuwasiliana na watu Zaidi ya milioni 100 ambao kati yao wapo wapiga kura.

Kwa wakati huu watu wanaendelea na kura za awali na inakadiriwa 30-40% wameshapiga kura

Je, hotuba ya jana ambayo haikuwa katika prime time imewafikia wapiga kura?

Hoja zinazojichanganya ni za deregulation.

Wakati wa Bush hakukuwa na regulations , matokeo yake ni recession kwasababu watu wali abuse system.

Fuatilia collapse of house market na gang of 9 utaelewa
Kama deregulation ingefanya kazi kwanini haikuwahi kufanya kazi kipindi cha Bush?

Regulation zina maana moja, kuhakikisha mwananchi wa kawaida hawi victim wa tycoon kama Trump.

Huwezi kuamini katika recession watu walitengeneza pesa, na Trump akisema mwenyewe ulikuwa wakati mzuri wa kununua estates na Nyumba.
Hivyo hilo liangalie kama litasaidia au la

Katika mambo anayolalamikia Trump ni pamoja na executive order za Rais.

Hata hivyo yeye anataka kufuta hizo executive order kwa executive order.
Bila hivyo hawezi kufanikiwa kwasababu kuna sharia zinazopita bungeni

Constitution amendment lazima ipite katika mkondo husika.
Hao wanaoguswa ndio watakaopitisha sharia

Trump akasema polls zinaoaminika zinaonyesha akiwa anaongoza.
Well, akiongoza poll zinaaminika, kinyume chake zinakuwa rigged

Katika suala la 'rig' hapa pia ameogelea, kwamba kuna fraud zinaendelea.

Wapo wataalam wanaomuonyesha kuwa uchaguzi wa Marekani ni decentralized kiasi kwamba kama kuna fraud ni kituo kimoja haiwezi kuwa national wide

Kwa uchache, alichosema ilipaswa akiseme miezi mingi, kwa kuhofia challenges akasubiri muda huu ili pamoja na kukwepa hoja afiche udhaifu wa matatizo ya akina mama yanayomkabili

Nadhani tafuta hotuba yake ili upate details, ulichonukuu ni 1/10 ya kilichosemwa
 
Hizi siyo habari njema kwa team HRC. Ni zile za Trump kusema nini atafanya siku 100 akipata urais.
======
Trump told the rally that on his first day in office, his administration would announce six measures to "clean up the corruption and special interest collusion" in Washington:

Constitutional amendment to impose term limits on all members of Congress.

Hiring freeze on all federal employees to reduce that workforce through attrition, exempting jobs in the military, public safety and public health.

Requirement that for every new federal regulation, two existing regulations must be eliminated.

Five-year ban on White House and congressional officials becoming lobbyists after they leave government service.

Lifetime ban on White House officials lobbying on behalf of a foreign government.

Complete ban on foreign lobbyists raising money for American elections.
======
Ameyasema haya, kwenye kampeni zake huko Gettysburg, Pa.
Naona mko wengi mnaodhani Urais wa Marekani ni sawa na Urais wa Tanzania, poleni...!
 
Mkuu

Nguruvi3
Km nchi ya marekani ina cheks & balances haitawaliwi na mtu kutokana na mfumo wao. Tatizo liko wapi sasa kwa DT kuwa Rais wakati unajua karibu kila kitu anaweza kudhibitiwa!!?

Hoja kwamba Trump hawezi kujenga hoja wala kutolea ufafanuzi yale anayoahidi mbona lipo wazi,trump si mwanasiasa na hajawahi kufanya siasa. Wenye maneno mazuri ni wanasiasa,ndo maana HC anawavutia wengi kutokana na uwezo wake wa kujenga hoja na lingekuwa jambo la kutisha km angezidiwa na trump kujieleza wakati yupo ktk siasa more 30yrs.

Hoja ya utajiri wa trump na kujenga uchumi,hakuna ubishi kwamba mfanyabiashara km trump aliyeimarisha urithi wa baba yake hadi hapo alipo anaweza kusaidia sana kujenga uchumi imara kwa kushirikiana na taasisi za ikulu.
Kule kuanguka kwake km mfanyabiashara, ndo kumemjenga zaidi na utajiri wake kwa mujibu Forbes ni 4.6bl. Lkn kwa mujibu wake mwenyewe,anadai utajiri wake unafikia 10bl. Mkuu kwenye biashara ukianguka unajengeka zaidi,. Me ni mmoja wa watu walioanguka sana mwaka 2007. Huwezi amini mwaka 2009 nilikuwa nakosa hata nauli ya daladala,lkn leo miaka 6 baadae,namalizia nyumba hapa mjini ambayo kiwanja peke yake nimenunua tsh.17ml. Kwa mfano wangu na wa trump mwenyewe hoja ya kufilisika ni hoja mfu.

Kuhusu wanawake walio-fail ni pamoja na markel mwenyewe,na hata chama chake amekishushia umaarufu.

Mwingine ni Rais aliyeondolewa kwa aibu huko brazil. Hapa nchini sijawahi kuona hata kiongozi mmoja mwanamke akifanya vizuri..hata wabunge wanawake wa upinzani wanaoonekana kufanya vizuri ni kutokana tu upande walipo. Lkn hata huko bado wapo wanaoonyesha udhaifu wa kushangaza km huyu mbunge anayehangaika kumtetea Lipumba.

Watu waliompigania mpaka kupata jimbo leo anawaona punguani halafu aliyemkimbia kawa lulu. Clinton sifa pekee aliyonayo ni hiyo ya kujieleza na inatokana na kufanya siasa kwa muda mrefu lkn huyo ni More satan...!! Kuna watu wanamuona trump km mtu hatari,lkn ukweli ni kwamba,mfanyabiashara km yeye,hawezi kuanzisha vita kwa sababu vita ni pesa. Huyu akiingia white house,marekani haitakuwa na vita kwa kipindi chote cha utawala wake.

..hoja yako kwamba Raisi mwenye background ktk biashara anaweza kubadilisha muelekeo wa uchumi na siasa za Marekani ina mashiko.

..ninachopingana na wewe ni kama Donald Trump ni aina ya mfanyabiashara ambaye Marekani inamhitaji kama kiongozi wake.

..umezungumzia kwamba kupanda na kushuka ni hali ya kawaida ktk biashara. Umejenga hoja kwamba hata wewe uliwahi kuanguka kibiashara na baadaye ukaibuka tena.

..Tatizo la Trump ni jinsi biashara zake zinavyoanguka na baadaye kupanda.

..mwananchi wa kawaida kama wewe anapopata matatizo ktk biashara ni nadra kuwatupia mzigo wa hasara wateja na washirika wake ktk biashara.

..lakini Donald Trump biashara inapomuendea vibaya hutangaza kufilisika/bankruptcy halafu mzigo wa hasara huutua kwa wateja, wawekezaji wenzake, wafanyakazi aliwaajiri, na mabenki yaliyomkopesha, huku yeye Trump akiendelea kuishi kifahari.

..Trump amewahi kutangaza kufilisika/bankruptcy mara tatu.

..kwa msingi huo utaona kuwa Trump siyo mfanyabiashara wa kupigiwa mfano hata kidogo. Kwa rekodi (3 bankruptcies )kama mfanyabiashara hastahili kuwa Raisi wa taifa lenye nguvu duniani, na leader of the free world.

..vilevile hata ukiangalia jinsi Trump anavyoendesha makampuni yake ambapo yeye ndiye alfa na omega, muamuzi wa kila jambo, na haiba yake ya kuzozana na kutukana kila asiyekubaliana naye, lazima utakubaliana na mimi kwamba atasababisha mtafaruku mkubwa ikiwa atachaguliwa kuwa Raisi wa Marekani.

..Nafasi ya Uraisi wa Marekani, kutokana na mfumo wa demkrasia yao na utawala, inahitaji mtu anayeweza kuwaunganisha watu, au mtu anayeweza kuwavumilia na kuwasikiliza wale wanaotofautiana naye kisiasa. Trump hana haiba hiyo.
 
Mkuu JokaKuu ahsante kwa hoja hapo juu

Uchumi wa Marekani unategemea ufungamano wa vitu vingi, ikiwemo uchumi, siasa na ulinzi na usalama

Hivi vitu vitatu kwasasa haviwezi kutengenishwa kwani vinategemeana kwa Taifa lenye nguvu duniani

Nikimsikiliza Trump naweza kusema siasa hakuna, ulinzi na usalama ni 'sensational' na uchumi unatia shaka
Katika mdahalo wa pili, alijinasibu kwa kusema anataka kuongoza nchi kama alivyoongoza makampuni yake

Hapa niliona Wamarekani wapo katika mtego mkubwa. Kama ulivyosema, Trump amefilisika mara 3 na zote akibwaga mzigo kwa watu wengine. Trump ana madeni hadi kujiita king of debt.

Kibaya Zaidi hajaweka wazi rekodi ya kodi 'tax file' kubaini ukubwa na njia za biashara zake

Trump akisema ni king of debt ndiye anamlaumu Obama kwa deni kuwa double ingawa wapo wasemao deni limepungua kwa 1/3. Hoja hapa si deni, bali, Trump mwenye madeni ndiye analaumu madeni?

Utajiri wa Trump haupo wazi kama wa Warren Buffet the least to say.

Anasema atatafuta watu smart wa ku negotiate trade.
Trump aelewe si suala la kupata wachumi, ni lazima negotiation hizo zitazame siasa na ulinzi na usalama.

Kwa mfano, Marekani ilipokuwa na mpango wa AGOA, millennial goal inaonekana ni masuala ya kiuchumi.

Nyuma ya pazia hizi ni mbinu za Marekani kuwa karibu na nchi za Afrika kupambana na China influence, ku compete katika resources. Haya yote yapo chini ya mwamvuli wa ulinzi na usalama wa Marekani

Trump anaposema ata negotiate trade kama separate entity, je ameangalia impact katika maeneo mengine?

Nimemsikia akisema ataruhusu keystone pipe, na kuruhusu makampuni yachimbe mafuta.

Kuanguka kwa bei ya mafuta kunatokana na US kujitisholeza,nchi inayotumia 10% ya mafuta duniani

Hata hivyo,Marekani ina push OPEC wakae pamoja kupunguza production nchi kama Saudia zithiarike Zaidi.

Athari zake zimeonekana baada ya Saudi kuzalisha mafuta kwa wingi na kupelekea tatizo la bei hata Marekani

Sasa Trump anaposema atachimba tu, bado hajaangalia ufungamano au utatu wa uchumi, siasa na ulinzi

Lakini pia anazungumza bila kufikiri mambo kama global warming ambayo yeye haamini kama yapo
 
....Nafasi ya Uraisi wa Marekani, kutokana na mfumo wa demkrasia yao na utawala, inahitaji mtu anayeweza kuwaunganisha watu, au mtu anayeweza kuwavumilia na kuwasikiliza wale wanaotofautiana naye kisiasa. Trump hana haiba hiyo.
Na hili ni tatizo kubwa sana kwa wakati huu. Tukitizama senate mgawanyo upo katika 47 na 49 in favor of Republican

Kati yao wapo the establishment wasioingia katika ballot box wakati huu. Wapo wanagombea kurudi
Tayari wame ji dissociate na Trump kutokana na hali ilivyo wakihofia wanaweza kwenda naye pasipotarajiwa

For the sake of discussions hata Trump akiwa Rais bado atapambana na upinzani wa ndani kutoka kwa the establishment na manusura watakaofaulu mwezi November. Hapo hatujazungumzia Democrat

Ndiyo maana kwasasa Dem wameelekeza nguvu katika states za Utah na Arizona. Hizi ni Red state na zina miongo mingi hazijawahi kupigia democrats.Kwanini Dem wanaenda kule kunakoenekana impossible?

Kwanza, wameona uwezekano wa kushinda majimbo hayo upo

Pili, wanataka ikiwezekana wanyakue viti kama si congress basi ni seneti

Tatu, wanataka Trump aondoe nguvu Penn, Ohio , Virginia Florida ambako kuna maseneta walio katika wakati mgumu arudi Utah na Arizona ili Dem wachukue nafasi hizo ikiwezekana

Hili linaeleza kuwa Trump anaweza kuwa Rais asiwe na ima seneti au congress kwa uchache

Katika mtifuano wa aina hii, the establishment , wanaorudi, dem, senate na congress, inatengeneza kitu kinachoitwa market uncertainty. Market zipo sensitive sana na siasa, sera n.k.

Market uncertainty haiwezi ku spur economy. Matokeo ni slowdown katika investment

Interest rate ni flat wakiangalia hali inavyoendelea. Market zimeongezeka na investment pia
Hili lina maana, investors wana confidence na policy na calmness ya Obama wakati wa crisis

Na hilo lina reflect approval rate yake katika 50% kiwango kikubwa

Najaribu kufikiria, kwa flip flop, unclear policy, unpredictable and erratic Trump , market zita react vipi ikifika November kuelekea Jan kama atakuwa Rais
 
Kuna vitu vingi vinanishangaza...kwa walimu wetu wa demokrasia(US). Mojawapo ya vitu hivyo ni namna wanavyomshambulia Trump kwa kitendo chake cha kutokuwa tayari kukubali matokeo ya uchaguzi kabla ya kura kupigwa. Tena na jana mpizani wake, HRC, kamuita Trump 'a sore loser', kisa msimamo wa Trump juu matokeo ya uchaguzi mwaka huu. Tena huyo 'mama' akaongeza kuwa tabia za Trump ni za watawala wa nchi za kidikiteta zenye uchovu wa demokrasia. Lakini ni watu hawa hawa (US na West ) ambao vyama vya upinzani katika nchi zijengazo demokrasia vikianza kulalamika kuwa kuna dalili za kuibiwa kura huwa wana wapa ushirikiano wa kutosha; kiasi wakati mwingine uwatia kibri cha kuangusha serikali zilizochaguliwa kihalala na wananchi wa nchi hizo kwa njia ya mtutu baada ya uchaguzi. Mifano ipo mingi.

Sasa, kwa dalili ambazo amekwisha ziona Trump kuwa kuna kila dalili za kubebwa mpinzani wake na federal security units, wall Street, na wengineo wenye nguvu huko US; kwa nini asikatae kukubali matokeo kabla ya kushuhudia mchakato mzima wa uchaguzi utakavyokuwa? Kwa wababe hao wa US wanashindwa nini kuyumbisha tume za chaguzi kwenye majimbo na federal? Kumbuka issue ya Al Gore (2000) hajasahaulika; demokrat walilalamika sana kuibiwa kura Florida.Mimi na sema Trump ana haki juu ya msimamo wake.

Kwa songombingo hii ya Uchaguzi, inaonyesha kumbe utofauti wa demokrasia ya nchi zetu changa na nchi zao ni kwa asilimia ndogo sana tofauti na tulivyokuwa tunaaminishwa. Sema wenzetu wametuzidi sana kwa asilimia uwezo wa kuficha unafiki wao.

Wabillah Tawfiq!
 
Mkuu JokaKuu ahsante kwa hoja hapo juu
.Hapa niliona Wamarekani wapo katika mtego mkubwa. Kama ulivyosema, Trump amefilisika mara 3 na zote akibwaga mzigo kwa watu wengine. Trump...
Nimemsikia akisema ataruhusu keystone pipe, na kuruhusu makampuni yachimbe mafuta.
Kuanguka kwa bei ya mafuta kunatokana na US kujitisholeza,nchi inayotumia 10% ya mafuta duniani
.Hata hivyo,Marekani ina push OPEC wakae pamoja kupunguza production nchi kama Saudia zithiarike Zaidi.
Athari zake zimeonekana baada ya Saudi kuzalisha mafuta kwa wingi na kupelekea tatizo la bei hata Marekani
Asante kwa maelezo juu hili. Lakini Mwalimu wangu, una hakika kuwa US anania njema na Saud Arabia na hao OPEC? (Venezuela ni mnufaika wa 'ushiriki' huu).

Hivi kama US anania njema na Saud Arabia, angemlazimisha kununua silaha zake kwa ela tasilimu (rejea link hapo chini) wakati uchumi wake unategemea mafuta kwa kiasi kikubwa? Hivi pia angemshawishi akapigane vita visivyo na kichwa wala miguu huko Yemen, wakati rais anayetetewa yuko uhamishoni (hana serikali)? Hivi US angekuwa na nia njema na OPEC angeendeleza usumbufu huko Venezuela, mpaka akafikia hatau ya "kumuondoa" Hugo Chavez kwa kansa, rais aliyekuwa anatetea wavenezuela kunufuakia na utajiri wao wa mafuta? Sasa hivi Maduro (rais wa sasa) anahangaika kuwadhibiti 'wahuni wa US' ,ambao wanajivika vilemba vya Opposition parties. Hii ni mifano michache inayoonyesha US hana nia njema na OPEC.
Zichunguze kwa umakini nchi zote za OPEC uangalie nini kina sumbua nchi hizi na nini chanzo cha usumbufu huko nakuhakikishia asilimia 80 ya chanzo kuwa ni US.

US anataka kuzizamisha nchi za OPEC!!

Why does Saudi Arabia spend so much money purchasing arms? - Quora
 
Back
Top Bottom