Kuna vitu vingi vinanishangaza...kwa walimu wetu wa demokrasia(US). Mojawapo ya vitu hivyo ni namna wanavyomshambulia Trump kwa kitendo chake cha kutokuwa tayari kukubali matokeo ya uchaguzi kabla ya kura kupigwa. Tena na jana mpizani wake, HRC, kamuita Trump 'a sore loser', kisa msimamo wa Trump juu matokeo ya uchaguzi mwaka huu. Tena huyo 'mama' akaongeza kuwa tabia za Trump ni za watawala wa nchi za kidikiteta zenye uchovu wa demokrasia. Lakini ni watu hawa hawa (US na West ) ambao vyama vya upinzani katika nchi zijengazo demokrasia vikianza kulalamika kuwa kuna dalili za kuibiwa kura huwa wana wapa ushirikiano wa kutosha; kiasi wakati mwingine uwatia kibri cha kuangusha serikali zilizochaguliwa kihalala na wananchi wa nchi hizo kwa njia ya mtutu baada ya uchaguzi. Mifano ipo mingi.
Sasa, kwa dalili ambazo amekwisha ziona Trump kuwa kuna kila dalili za kubebwa mpinzani wake na federal security units, wall Street, na wengineo wenye nguvu huko US; kwa nini asikatae kukubali matokeo kabla ya kushuhudia mchakato mzima wa uchaguzi utakavyokuwa? Kwa wababe hao wa US wanashindwa nini kuyumbisha tume za chaguzi kwenye majimbo na federal? Kumbuka issue ya Al Gore (2000) hajasahaulika; demokrat walilalamika sana kuibiwa kura Florida.Mimi na sema Trump ana haki juu ya msimamo wake.
Kwa songombingo hii ya Uchaguzi, inaonyesha kumbe utofauti wa demokrasia ya nchi zetu changa na nchi zao ni kwa asilimia ndogo sana tofauti na tulivyokuwa tunaaminishwa. Sema wenzetu wametuzidi sana kwa asilimia uwezo wa kuficha unafiki wao.
Wabillah Tawfiq!
..sidhani kama demokrasia ya Marekani unaweza kuilinganisha na ya nchi zetu za dunia ya 3, Tz in particular.
..hapa Tz mikutano ya kampeni ya vyama vya siasa imewahi kupigwa mabomu na vyombo vya dola. Je umewahi kuona hilo likifanyika Marekani?
..umewahi kuona au kusikia kiongozi wa upinzani Marekani akapigwa na kubebwa kama mzoga kama ilivyotokea kwa Prof.Lipumba?
..lini umesikia vyombo vya dola vya wamarekani vikikamata na kuwahoji wale wanaokosoa sera za Raisi Obama?
..Au umewahi kuona polisi wa Marekani akiua mwandishi wa habari kama ilivyotokea kwa daudi mwangosi?
..hapa Tz kuna madai ya polisi kuua raia zaidi ya 200, lakini husikii vyombo vya habari vikifuatilia suala hilo kwa uzito unaostahili.
..kwa wamarekani polisi akiua raia uwezekano mkubwa ni familia iliyopoteza mtu wao kulipwa fidia mamilioni ya fedha.
..kwenye masuala ya haki na demokrasia Marekani wamezitangulia nchi nyingi sana.