Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

Kuna vitu vingi vinanishangaza...kwa walimu wetu wa demokrasia(US). Mojawapo ya vitu hivyo ni namna wanavyomshambulia Trump kwa kitendo chake cha kutokuwa tayari kukubali matokeo ya uchaguzi kabla ya kura kupigwa. Tena na jana mpizani wake, HRC, kamuita Trump 'a sore loser', kisa msimamo wa Trump juu matokeo ya uchaguzi mwaka huu. Tena huyo 'mama' akaongeza kuwa tabia za Trump ni za watawala wa nchi za kidikiteta zenye uchovu wa demokrasia. Lakini ni watu hawa hawa (US na West ) ambao vyama vya upinzani katika nchi zijengazo demokrasia vikianza kulalamika kuwa kuna dalili za kuibiwa kura huwa wana wapa ushirikiano wa kutosha; kiasi wakati mwingine uwatia kibri cha kuangusha serikali zilizochaguliwa kihalala na wananchi wa nchi hizo kwa njia ya mtutu baada ya uchaguzi. Mifano ipo mingi.

Sasa, kwa dalili ambazo amekwisha ziona Trump kuwa kuna kila dalili za kubebwa mpinzani wake na federal security units, wall Street, na wengineo wenye nguvu huko US; kwa nini asikatae kukubali matokeo kabla ya kushuhudia mchakato mzima wa uchaguzi utakavyokuwa? Kwa wababe hao wa US wanashindwa nini kuyumbisha tume za chaguzi kwenye majimbo na federal? Kumbuka issue ya Al Gore (2000) hajasahaulika; demokrat walilalamika sana kuibiwa kura Florida.Mimi na sema Trump ana haki juu ya msimamo wake.

Kwa songombingo hii ya Uchaguzi, inaonyesha kumbe utofauti wa demokrasia ya nchi zetu changa na nchi zao ni kwa asilimia ndogo sana tofauti na tulivyokuwa tunaaminishwa. Sema wenzetu wametuzidi sana kwa asilimia uwezo wa kuficha unafiki wao.

Wabillah Tawfiq!

..sidhani kama demokrasia ya Marekani unaweza kuilinganisha na ya nchi zetu za dunia ya 3, Tz in particular.

..hapa Tz mikutano ya kampeni ya vyama vya siasa imewahi kupigwa mabomu na vyombo vya dola. Je umewahi kuona hilo likifanyika Marekani?

..umewahi kuona au kusikia kiongozi wa upinzani Marekani akapigwa na kubebwa kama mzoga kama ilivyotokea kwa Prof.Lipumba?

..lini umesikia vyombo vya dola vya wamarekani vikikamata na kuwahoji wale wanaokosoa sera za Raisi Obama?

..Au umewahi kuona polisi wa Marekani akiua mwandishi wa habari kama ilivyotokea kwa daudi mwangosi?

..hapa Tz kuna madai ya polisi kuua raia zaidi ya 200, lakini husikii vyombo vya habari vikifuatilia suala hilo kwa uzito unaostahili.

..kwa wamarekani polisi akiua raia uwezekano mkubwa ni familia iliyopoteza mtu wao kulipwa fidia mamilioni ya fedha.

..kwenye masuala ya haki na demokrasia Marekani wamezitangulia nchi nyingi sana.
 
Kuna vitu vingi vinanishangaza...kwa walimu wetu wa demokrasia(US). Mojawapo ya vitu hivyo ni namna wanavyomshambulia Trump kwa kitendo chake cha kutokuwa tayari kukubali matokeo ya uchaguzi kabla ya kura kupigwa. Tena na jana mpizani wake, HRC, kamuita Trump 'a sore loser', kisa msimamo wa Trump juu matokeo ya uchaguzi mwaka huu. Tena huyo 'mama' akaongeza kuwa tabia za Trump ni za watawala wa nchi za kidikiteta zenye uchovu wa demokrasia. Lakini ni watu hawa hawa (US na West ) ambao vyama vya upinzani katika nchi zijengazo demokrasia vikianza kulalamika kuwa kuna dalili za kuibiwa kura huwa wana wapa ushirikiano wa kutosha; kiasi wakati mwingine uwatia kibri cha kuangusha serikali zilizochaguliwa kihalala na wananchi wa nchi hizo kwa njia ya mtutu baada ya uchaguzi. Mifano ipo mingi.

Sasa, kwa dalili ambazo amekwisha ziona Trump kuwa kuna kila dalili za kubebwa mpinzani wake na federal security units, wall Street, na wengineo wenye nguvu huko US; kwa nini asikatae kukubali matokeo kabla ya kushuhudia mchakato mzima wa uchaguzi utakavyokuwa?

Kwa wababe hao wa US wanashindwa nini kuyumbisha tume za chaguzi kwenye majimbo na federal? Kumbuka issue ya Al Gore (2000) hajasahaulika; demokrat walilalamika sana kuibiwa kura Florida.

Mimi na sema Trump ana haki juu ya msimamo wake.

Kwa songombingo hii ya Uchaguzi, inaonyesha kumbe utofauti wa demokrasia ya nchi zetu changa na nchi zao ni kwa asilimia ndogo sana tofauti na tulivyokuwa tunaaminishwa. Sema wenzetu wametuzidi sana kwa asilimia uwezo wa kuficha unafiki wao
Hili suala la uchaguzi wa US tumelieleza kuwa ni decentralized.

Kama unafuatilia, TV zinaweza ku(project) matokeo kutokana na takwimu wanazokusanya.

Kura zainazopigwa huhesabiwa katika kituo husika na matokeo hubandikwa kwa kusainiwa na wahusika.

Wakuu wa state wanashughulikia process nzima kwasababu kila state ina utaratibu wake wa uchaguzi. Na bahati nzuri Magavana wengi ni Republican

Kama kuna fraud, inaweza kutokea kwa kitongoji na si nchi nzima.


Hili linaelezwa na waliokuwa katika tume za uchaguzi, Republican na Dem

Wazo kuwa security organ au Wall street wataingilia limnishtua.
Wall street wanaingilia kwa mlango gani?

Hakuna chama kinacholalamika kuhusu kutangazwa matokeo.

Anayelalamika ni Trump ambaye si mara ya kwanza kufanya hivyo.
Akiwa katika primaries alilalmika kuwa Republican wana 'rig' asishinde.

Mwezi uliopita takwimu ilionyesha kiwango cha kikubwa cha ajira zilizotengenezwa. Trump akasema kuna 'rig' za takwimu.

Mwezi huu takwimu zimeonyesha kuiwango kidogo, Trump anazitumia kwa usahihi, kwa maana kuwa siyo rigged tena

Elewa Republican hawajalalamika na wanafedhehesheshwa, ni Trump

Hili linawadhalilisha sana Wamarekani.
Ni kitu kinachoingilia 'the essence core of the US Democracy''

Trump anafanikiwa sana kupumbaza watu.
Akiulizwa electoral process inavyoweza kuwa rigged, jibu ni tofauti na lako.

Trump anasema media zipo skewed wewe unasema electoral process

Hata siku moja Demokrasia ya vinchi masikini haifiki hata 1/20 ya US
 
Asante kwa maelezo juu hili. Lakini Mwalimu wangu, una hakika kuwa US anania njema na Saud Arabia na hao OPEC? (Venezuela ni mnufaika wa 'ushiriki' huu).

Hivi kama US anania njema na Saud Arabia, angemlazimisha kununua silaha zake kwa ela tasilimu (rejea link hapo chini) wakati uchumi wake unategemea mafuta kwa kiasi kikubwa? Hivi pia angemshawishi akapigane vita visivyo na kichwa wala miguu huko Yemen, wakati rais anayetetewa yuko uhamishoni (hana serikali)? Hivi US angekuwa na nia njema na OPEC angeendeleza usumbufu huko Venezuela, mpaka akafikia hatau ya "kumuondoa" Hugo Chavez kwa kansa, rais aliyekuwa anatetea wavenezuela kunufuakia na utajiri wao wa mafuta? Sasa hivi Maduro (rais wa sasa) anahangaika kuwadhibiti 'wahuni wa US' ,ambao wanajivika vilemba vya Opposition parties.

Hii ni mifano michache inayoonyesha US hana nia njema na OPEC.
Zichunguze kwa umakini nchi zote za OPEC uangalie nini kina sumbua nchi hizi na nini chanzo cha usumbufu huko nakuhakikishia asilimia 80 ya chanzo kuwa ni US. US anataka kuzizamisha nchi za OPEC!!

Why does Saudi Arabia spend so much money purchasing arms? - Quora
Nadhani hujanisoma vizuri na kama umenielewa itakuwa tofauti.

Nilichosema ni kuwa Marekani inajitosheleza katika mafuta kwasasa na kupelekea kuanguka kwa bei ya mafuta.

Marekani inatumia takribani 10% ya mafuta ya dunia.

Hilo limesababisha mashindano ya bei middle east, Saudi ikizalisha kwa wingi na kuzidisha tatizo la bei.

Marekani inaingilia kati kwa kusukuma OPEC na Saudia kufikia maafikiano.

Hili nimelizungumzia kuwa ni kwasababu za kisiasa, kiuchumi, kiulinzi na usalama. Nilifafanunua utata huo (siasa, ulinzi/usalam na uchumi)

Sijasema Marekani ina nia njema au mbaya mahali popote!

Nimejaribu kuweka picha nzima kwa ujumla wake nikizingatia hilo la siasa za Marekani zinazoangalia mambo matatu kwa ujumla wake
 
..hizi kampeni zina maneno mengi sana. Kwa hiyo inabidi kuwa makini kutenganisha pumba na mchele.

..Elizabeth Warren na Bernie Sander wameshawahi kuielezea Marekani kwa mtizamo kama wa Donald Trump. Tena wakitumia kauli " the system/economy is rigged."

..kuna segment ya Wamarekani ambao hali yao ya kiuchumi ni mbaya. Kundi hilo ama limepoteza ajira kutokana na makampuni kuhamisha viwanda kwenda Mexico China etc, au limekosa elimu na ujuzi kuweza kuajiriwa ktk nafasi zinazojitokeza ndani ya Marekani.

..sasa katika wagombea wote Donald Trump ndiye aliyeweza ku-connect na kundi hilo.

..tatizo ninaloliona mimi ni upungufu wa Trump ktk kuwasilisha hoja zake. Kwanza ana appeal kwa kundi dogo. Pili anajenga hasira na hofu. Tatu havutii idadi kubwa zaidi ya Wamarekani kumuunga mkono.

..Trump hawaelezi ukweli mashabiki wake kwamba kazi zilizohamia China na kwingineko ni vigumu kurudi Marekani. Mfanyakazi wa Marekani ni aghali mno kuliko mfanyakazi wa China au Mexico.

..Pia Donald Trump anatumia slogan "make america great again." Ni kana kwamba kuna kipindi Marekani ilikuwa nzuri kuliko wakati huu. Hapa inategemea unazungumza na kundi gani la wamarekani.
 
..hizi kampeni zina maneno mengi sana. Kwa hiyo inabidi kuwa makini kutenganisha pumba na mchele.

..Elizabeth Warren na Bernie Sander wameshawahi kuielezea Marekani kwa mtizamo kama wa Donald Trump. Tena wakitumia kauli " the system/economy is rigged."

..kuna segment ya Wamarekani ambao hali yao ya kiuchumi ni mbaya. Kundi hilo ama limepoteza ajira kutokana na makampuni kuhamisha viwanda kwenda Mexico China etc, au limekosa elimu na ujuzi kuweza kuajiriwa ktk nafasi zinazojitokeza ndani ya Marekani.

..sasa katika wagombea wote Donald Trump ndiye aliyeweza ku-connect na kundi hilo.

..tatizo ninaloliona mimi ni upungufu wa Trump ktk kuwasilisha hoja zake. Kwanza ana appeal kwa kundi dogo. Pili anajenga hasira na hofu. Tatu havutii idadi kubwa zaidi ya Wamarekani kumuunga mkono.

..Trump hawaelezi ukweli mashabiki wake kwamba kazi zilizohamia China na kwingineko ni vigumu kurudi Marekani. Mfanyakazi wa Marekani ni aghali mno kuliko mfanyakazi wa China au Mexico.

..Pia Donald Trump anatumia slogan "make america great again." Ni kana kwamba kuna kipindi Marekani ilikuwa nzuri kuliko wakati huu. Hapa inategemea unazungumza na kundi gani la wamarekani.
Naweza kuwaelewa Elizabeth Warren na Bernie Sander wanaposema economy is rigged.

Hili linaelezeka kwa kutumia recession ambayo ukiitazama ilikuwa ni rigged na kuleta matatizo makubwa.

Trump anasema uchaguzi upo rigged. Akiulizwa ni namna gani electoral process ipo rigged, anazungumzia media kuwa biased.

Media zile zile zilizomjenga zinapokuwa against yeye zinakuwa rigged
Haelezi media zina influency rigging katika process nzima kwa naman gani

Lakini pia watu wanauliza kuhusu maana ya rigged kwa Trump
-Alisema uchaguzi wa Republican upo rigged. Akashinda na kusifu process
- Anasema takwimu za ajira zipo rigged. Zikiwa katika favor yake ni sahihi
- Akasema Judge wa kesi yake mahakama ipo rigged. Akishinda ni sahihi
-Akasema Emmy award ipo rigged kwasababu hajashinda

Kwa ufupi, hawezi kueleza maana ya rigged, isipokuwa inapokuwa against

Pili, Trump ana appeal kwa kundi lenye grievances kwa kutumia hofu

Kwa mfano, anasema atatengeneza ajira milioni 25 kwa miaka 10.
Hajaeleza miaka 8 iliyopita ngapi zimetengenezwa. Hadi sasa ni takribani 15milioni

Tatu, anazungumzia ISIS. Anapoulizwa atafanya nini tofauti, jibu lake ni lawama kwa Hillary kule Benghaz na Syria. Haelezi atafanya nini

Nne, anaulizwa, wachumi wa Republican wanaona sera zake zitaleta deficit kubwa na kuongeza deni.

Hatetei sera, anamlaumu Obama kwa kazi kwenda Mexico.

Tano, inapofika katika foreign policy, haijulikani anasimama wapi.

Mara zote anatofautiana na VP wake akibadilisha position kila mara.

Sita, anazungumzia law and order, haelezi ni kwa namna gani hilo litaondoa racism ambayo ndiyo core issue.

Ametangaza siku 100 za kwanza atatoa vifaa kwa police, sasa hilo lina address vipi issue inayolalamikiwa na kuleta 'disobedience' mitaani?

Saba, anaulizwa, kama kuzuia wageni wasije itasaidia kukabiliana na ugaidi, je walioko ndani atafanya nini?
Hana jibu anasema atafanya vetting kali kwa wajao

Kampeni yake imejikita kueleza madhaifu na makosa, haina solution.
Ndiyo maana katika educated people ana tatizo kubwa sana

Lakini pia kama ulivyosema, hana broad appeal na hilo nalo ni tatizo

Alichofanikiwa ni kujenga hofu kuwa Marekani ya leo ni mbaya sana kuliko ile ya Bush na siku za nyuma. Katika hili ana strong support ya kundi lake
 
Kwa songombingo hii ya Uchaguzi, inaonyesha kumbe utofauti wa demokrasia ya nchi zetu changa na nchi zao ni kwa asilimia ndogo sana tofauti na tulivyokuwa tunaaminishwa. Sema wenzetu wametuzidi sana kwa asilimia uwezo wa kuficha unafiki wao!
TUJITEGEMEE, hapa ni kama unajaribu kulinganisha giza na mwanga na kweli kama unaamini unalolisema basi ni wazi hiyo Marekani unayoiongelea ni ya kufikirika, haipo!
  • Ni nchi ipi katika dunia ya tatu Rais anaweza kuitwa "muongo" bungeni na moja wa wabunge wakati analihutubia taifa na asipotezwe?
  • Ni nchi ipi katika dunia ya tatu mgombea kutoka upinzani anapewa ulinzi kama anaopewa Donald Trump hivi sasa na vyombo vya usalama?
  • Ni nchi ipi katika dunia ya tatu Rais aliyeko madarakani anatukanwa kwa kuitwa "stupid" hadharani na moja wa wagombea akapona?
  • Ni nchi ipi katika dunia ya tatu mbunge anatamka bila kificho kwamba hatamuunga mkono mkono mgombea wa chama chake?
  • Ni nchi ipi katika dunia ya tatu Spika wa Bunge, bila unafiki, anakataa kumkampeinia mgombea Urais kutoka chama chake?
  • Ni nchi ipi katika dunia ya tatu, wagombea wahasimu, wanakutanishwa pamoja na kupewa nafasi ya kutoleana madongo kiutani?
  • Ni wapi katika dunia ya tatu wananchi wa kawaida wana uhuru wa kufanya maamuzi yao bila kujali tofauti zao kiitikadi?
  • Ni nchi gani katika dunia ya tatu, kila jimbo linaruhusiwa kujitungia sheria zake za uchaguzi bila kubanwa na serikali kuu?
  • and the list goes on and on...
Please stop whining...that's a disease and it catches!
 
..naomba nijikite katika slogan ya "make america great again."

..sasa kuna watu wanauliza iwe great " again " kama wakati gani?

..kama wakati wa kennedy, lyndon johnson, nixon, ford, carter, reagan, bush 1, clinton, au bush 2?

..wakati wa kennedy ndiyo kulikuwa na maandamano ya civil rights. Lyndon johnson ilikuwa ni era ya vita ya vietnam.Nixon alikuwa na watergate scandal. Unaweza kuendelea hivyo kwa kila Raisi.

..Je, America ya awamu hizo zilizopita ilikuwa better kuliko hii ya awamu ya Obama?

..swali hilo lina majibu tofauti kwa jamii mbalimbali za Marekani.

..Suala lingine ni kama ni kweli USA imeporomoka, au ile gap kati yake na washindani wake imepungua. Au washindani wa Marekani wamekuwa kwa haraka kuliko ambavyo Marekani inakua.

..huu ni mjadala mpana na endelevu.

..yupo aliyehoji kuwa ikiwa mfumo wa uchaguzi wa marekani ni mzuri na wa kupigiwa mfano imekuwaje mgombea wa hovyo-hovyo kama Donald Trump akapitishwa kuwa flag bearer wa moja ya chama kikuu Marekani?

..wachangiaje lazima tukumbuke hakuna mfumo ambao ni perfect. Kwa hata huu mfumo wa uchaguzi wa Marekani unahitaji maboresho.

..Yes, mgombea wa hovyo-hovyo anaweza kupenya ktk uchaguzi wa Marekani lakini mpaka awe Raisi kuna vizingiti vya kampeni ya muda mrefu, midahalo ( uchaguzi huu ilikuwa kama utitiri), mahojiano na vyombo vya habari, na mikutano ya kampeni ambayo iko well covered. Mgombea anatakiwa avuke vizingiti vyote hivyo.

..kwa hiyo kwa kiwango kikubwa wananchi wanapopiga kura wanakuwa na uhakika wanachagua mgombea wa aina gani.

..binafsi nimejifunza mengi ktk kufuatilia kampeni za Uraisi za Marekani.

..Yapo mengi mazuri ambayo waTz tunapaswa kuyaiga.

Cc zumbemkuu, TUJITEGEMEE, Nguruvi3, Mag3, magode
 
Mkuu JokaKuu

Kwanza, kama ulivyosema hakuna perfect democracy achilia mbali mfumo wa uchaguzi.

Bado kuna malalamiko ya mgawanyo wa delegates katika uchaguzi n.k.

Tunapoongelea democracy hatuwezi kusema ni kitu uniform.

Ukamilifu wa demokrasi ni kutekeleza kile jamii ilichokubaliana

Tumeamua Rais akitoka bara makamu atoke visiwani.

India wana utaratibu wao, UK wa Queen, Marekani wana delegates na si popular vote n.k.

Tofauti inakuja namna gani tunaheshimu maamuzi na makubaliano yetu

Kwa mfano, wenzetu wanahoji uhalali wa kufuta uchaguzi znz, hawahoji uhalali wa namna ya kupata viongozi wetu kwa mfumo wetu

Kuhusu kauli ya Trump, hili nalo ni tatizo kwasababu ameshindwa kuitetea

Ameuliza 'great again kama wakati gani'?
akasema jeshi la Marekani limekuwa dogo si kama wakati wa FDR.

Jibu alilopewa ni kuwa mwaka 1946 ilihitaji Batallion 1 kufanya kazi fulani
Mwaka 2016 wanahitaji watu 20 kufanya kazi hiyo kutokana na technology

Mwaka 1946 walitumia ndege za vita, mwaka 2016 watu wanatumia guided missile yanayopiga umbali nusu ya dunia with high precision na less casualties

Hivyo hoja ya make America great again bado ina mjadala, ni kiuchumi au kijamii au kisiasa na kulinganisha na wakati gani

Kwa mfano, post recession US ime recover zaidi ya block 2 combined
Job creation ni kubwa kuliko ya EU na Japan combine

Bado US ni taifa lenye nguvu duniani.

Hivyo unabaki mjadala great again kwa kulinganisha na wakati gani
 
Nguruvi3,
Asante kwa mjadala huu mnono wa uchaguzi wa USA,
Kuna kitu kinanisumbua kdg, hivi mtandao wa weakleak, unatoa habari za kweli au upo kupambana na H. Clinton kimkakati?? Maana naona kila siku wa azusha vitu against HC and nothing concerning Trump, nikawa najiuliza inamaana hawa mtandao wa kuchunguzi mbona wapo kumshambulia mtu mmoja tu wakati walipaswa kuwa balanced?? Au ndio kuchagua upande as usual..
 
Nguruvi3,
Asante kwa mjadala huu mnono wa uchaguzi wa USA,
Kuna kitu kinanisumbua kdg, hivi mtandao wa weakleak, unatoa habari za kweli au upo kupambana na H. Clinton kimkakati?? Maana naona kila siku wa azusha vitu against HC and nothing concerning Trump, nikawa najiuliza inamaana hawa mtandao wa kuchunguzi mbona wapo kumshambulia mtu mmoja tu wakati walipaswa kuwa balanced?? Au ndio kuchagua upande as usual..
Mkuu mtandao wa WikiLeaks upo muda mrefu
Habari unazotoa ni za kweli. Ugomvi wa WikiLeaks na Hillary Clinton ulianza wakati akiwa secretary of state

Mtandao wa WikiLeaks ulivujisha habari za state department kuhusu mission ya kumuua Osama
Hilo lilikarisha serikali ya Obama na kwavile lilitokea state dept, Hillary akalishikia bango, Assange akamatwe na kupelekwa US kwa mashtaka. Ni kuanzia wakati huo akawa amejificha ubalozi wa Ecuador UK

Kuna Snowden aliyejificha Russia. Huyu ni Raia wa US na Assange ni wa Australia

Hawa wote inasemwa wanashirikiana kwa kuunganishwa na Russia.

Mwanzo mwa mwaka huu wali hack emails za DNC wakapata emails. Wali hack kwa Republican pia

Katika retaliation wao wana target Hillary Clinton ili kumvurugia mbio zake za white house

Agency 15 za US zinazohusika na mambo ya ulinzi na usalama zimesema upo uhusiano wa Assange, Snowden na Russia. Na kwamba, hizo ni mbinu za Russia ku interfere uchaguzi wa Marekani

Wiki iliyopita internet ya Assange katika ubalozi ilikatwa.
Kuna collaboration kati ya US na UK ambayo inaoneokana kuitisha Ecuador in a way.

Hata hivyo WikiLeaks walimwaga habari nyingi na kuamsha hisia kuwa amekufa.
Habari hizo zilikanushwa na TV ya Russia jambo linaloonyesha uhusiano kati yao

Assange bado yupo hai

WikiLeaks hawawezi kutoa habari za Republican kwasababu nia yao ni kumharibia mbaya wao Clinton

Siyo kwamba hawana habari za GOP, bali ni katika kuhakikisha wanafanikiwa katika mpango wao

Ni kwasababu hizo, mgombea wa GOP Marco Rubio anayegombea useneta Florida, amewaonya Republican kutoshangilia emails za Clinton kutolewa hadharani kwasababu ' Ipo siku itawarudi Republican'

Kwa Assange, maisha yake yana matatizo. Jambo hilo ingawa linaonekana kama la kisiasa kwa sasa, kwa ujumla wake linachukuliwa kama cyber attack na Marekani. Utawala wa Obama umesema wataijibu Russia wakati ukifika

Kitu kimoja kuhusu mataifa makubwa kama US, wana long memory na hufanya mambo yao kitaalamu.

CIA kwa hali yoyote wapo kazini na ni suala la muda tu ima atapatikana au atatoweka

Ni mwendo wa KGB na Litinenko hakufahamu watampaje, in the end walimpata perfect and square

Kwa minajili ya mjadala, utakumbuka Alwaki Raia wa Marekani aliyeasi na jinsi alivyopatikana
Kuna akina Zakhawi na usifanye kosa kudhani Ayaman Alzawahiri wa Alqaeda yupo salama!
 
HOJA
Kwanini mfumo wa Marekani unaosemwa kuwa mzuri unaweza kutoa mgombea kama Trump?

Hoja hii ilitolewa na mwenzetu magode na imerudiwa kwa ufafanuzi bandiko 427 na JokaKuu

Mfumo wa uchaguzi wa US kama alivyosema Jokakuu unachuja kiasi cha watu kujua Rais ajaye atakuwaje

Kilichotokea safari hii si mfumo wa US ni mfumo ndani ya Republican kutokana na uongozi hafifu

Mwaka 2004 Dem walikuwa na wagombea wengi kama akina Howard Dean maarufu kwa 'aaaargh!
Baada ya primaries za Iowa/New Hampshire uelekeo ulijitokeza,uongozi ukaweka mashinikizo kwa dhaifu kujitoa

Mwaka 2008 walikuwepo akina Obama, Hillary, Richardson, Joe Biden,Edward n.k., kundi kubwa
Baada ya primaries chache, dhaifu akina Richardson, Edward, na Joe wakashinikizwa kujitoa. Mtifuano ukabaki kati ya Hillary na Obama

Mwaka 2012 walikuwepo akina Romney, Newt Ginrich, na Huckabee n.k. Baada ya primairies chache shinikizo likawekwa wajitoe . Dhaifu wakaondoka akabaki Gingritch na Michae Huckabee , mwisho Romney

Mwaka 2016 wakajitokeza 16. Hii ikatengeneza chaos kwasababu hakukuwa vetingt mapema
Kundi hilo likaachwa liendelee kwa wingi wake kwa matumaini watajichuja

Trump alikuwa na tea party na message yake iliyoridhisha kundi lake la asilimia 30 ya Republican.

Katika uzi uliopita tulieleza , angalia ushindi wa Trump, kila mara alikuwa kati ya 25-30%

Wale 15 waliobaki wakgawana 70% , matokeo yake wakawa na wajumbe 9 wengine 4 wengine 10

Uongozi wa Republican haukuweka shinikizo kwa adhaifu kujitoa. Mchujo ukaengua hata wazuri

Hili likawaumiza akina Gavana Kasich, Senta Rubio, Ted Cruz,Scott Walker, Lindsey kwani wakati wanabaki na Trump alikuwa na 30% intact wengine wakigawana. Ndio maana mwishoni waliunganisha nguvu ikiwa too late.

Hivyo uongozi wa Republican ulitakiwa kushinikiza wale dhaifu wajitoe, haukufanya hivyo na hao dhaifu wakawa sehemu ya uchaguzi na kuleta udhaifu kwa kufunika wale waliotarajiwa kama akina Linsey, Kasich, Rubio n.k.

Kwa mantiki hiyo, Trump hakupenya system ya uchaguzi ya Marekani, alipenya system dhaifu ya Republican

System ya Marekani inajikuta imempata Trump kwa makosa ya system nyingine. Hata hivyo bado inaonyesha system inavyochuja kwani short cut ya Trump ku knock out wenzake kwa character assassination inaonekana kuwa ngumu

Hata akishinda, system imefanya kazi ya kuonyesha wapiga kura Rais wao ajaye
 
Mkuu

Joka kuu & nguruvi3

Nimependa sana jinsi mlivyorudi kwenye mjadala na kujadili yale mambo ya msingi kuhusu mifumo ya uchaguzi ya Taifa kubwa kabisa Duniani.

Me nna mtizamo tofauti kidogo kuhusu mifumo yote miwili kwa GOP na uchaguzi wenyewe hasa kumhusu D.trump!

Jokakuu umetilia shaka mfumo mzima,tatizo lako lipo kwa Trump..kwa nn apatikane mgombea wa hovyo hovyo ktk Taifa ambalo ni baba wa Demokrasia!!?? Me nakuondoa shaka,mfumo hauna tatizo lolote kwa pande zote 2. Trump anazo sifa za jumla za kuwa mgombea wa urais wa U.S kile kinachoonekana km ni tatizo kubwa sana kwa DT ni maisha yake binafsi.

Maisha ya DT kwa kutumia utajiri wake,anaishi maisha ya anasa sana na kwa vile hakuwahi ktk nafasi yoyote ktk jamii,hata km watu walikerwa na matendo yake,lkn jamii ilishindwa kuanika mambo yake kwa sababu hakuwa mtu muhimu sana ktk jamii km ilivyo hivi sasa.

Kelele zote zinazopigwa kipindi hiki kumhusu Trump,ni kujaribu kumuonyesha kuwa nafasi anayoiomba anakwenda kuwa jicho ktk jamii ya wamarekani. Hivyo anapewa ujumbe wa kujiandaa kuishi maisha mapya pindi akifanikiwa kuingia ikulu ya white house.

Sina shaka kabisa na mfumo wa US wa uchaguzi,trump hata akishinda mfumo uliopo automaticaly utamuongoza yeye mambo mengi ya kufanya kuliko anayotaka yeye kufanya. Mfano mzuri ni Obama na ahadi yake ya kufunga gereza la guantanamo,kwa nje analaumiwa kwa kushindwa kutimiza ahadi yake hiyo muhimu. Lkn nyuma ya pazia ni system imezuia kutii mawazo yake...!!

Nguruvi3 ameonyesha makosa ya GOP wakati wa uteuzi. Mtazamo wangu ni ule ule,trump anazo sifa za jumla za kugombea isingekuwa Rahisi kumzuia asigombee. Na wamarekani hasa republican walionyesha wanahitaji mtu tofauti na wanasiasa,ndo maana Trump alikuwa na wafuasi wa kutosha. Trump maisha yake ya anasa na mdomo wake kukosa brake ndo vimemuangusha sana,lkn ukweli wanarekani walitaka mtu wa aina yake na si wanasiasa.
 
..Habari hizo zilikanushwa na TV ya Russia jambo linaloonyesha uhusiano kati yao
Fact:

Television za Russia na mtandao mingine ya huko ilipata habari za Assange kuwa yu hai kwenye mtandao huo wa WikiLeaks. Inaoneokana TV za Russia zilianza kutangaza habari hizo kwa sababu Mainstream Media karibu zote za West zinasusa kutoa habari za mtandao huo kwani habari nyingi kipindi hiki zina mgusa kipenzi Chao cha urais US yaani 'mama' na haziwafurahishi.

Wikileaks: 'Julian Assange announcement' TOMORROW after conspiracy claims he is DEAD
 
Nguruvi3 ameonyesha makosa ya GOP wakati wa uteuzi. Mtazamo wangu ni ule ule,trump anazo sifa za jumla za kugombea isingekuwa Rahisi kumzuia asigombee. Na wamarekani hasa republican walionyesha wanahitaji mtu tofauti na wanasiasa,ndo maana Trump alikuwa na wafuasi wa kutosha. Trump maisha yake ya anasa na mdomo wake kukosa brake ndo vimemuangusha sana,lkn ukweli wanarekani walitaka mtu wa aina yake na si wanasiasa.
Kuna uzi wa uchaguzi wa Marekani ambao tulieleza mengi kuhusu hoja hii

Kwanza, hakuna mahali tumeseme Trump alipaswa kuzuiwa.

Tunachoeleza ni mtiririko uliowafikisha Republican walipo
Kuna mgawanyiko, uungwaji mkono wa mgombea ni kiwango cha chini

Spika 'top ranking' hapigi kampeni, kama maseneta wanasuasa na DNC wanaelekeza nguvu zao kwa maseneta na wabunge ni dhahiri lipo tatizo

Hivyo tunaangalia ilikuwaje ikifika hapo kwa mtazamo mpana na wala si suala la DT anafaa ua hafai pekee.

TUJITEGEMEE suala la Wikileaks ni zito kuliko unavyodhani.

Hili si la siasa za uchaguzi ni la usalama wa mataifa.

Inapotokea Russia wakaliunga mkono inaongeza ukubwa wa tatizo

Hoja ya ''wanamtaka Hillary'' ni mtazamo wako si vema kusema ni sahihi au la

Ninachoweza kukuambia, hacking inatia hofu mataifa kuliko unavyodhani.

Mfano, walipo hack state dept na kutoa siri za OBL, nchi zilizohusika zilitajwa

Kumbuka, CIA haifanyi kazi pekee yake, kuna M15, Scotland Yard, MOSSAD na mashirika mengine mengi tu duniani katika zama hizi

Wikileaks ni tishio kwa maana ya cyber attack ikitumiwa na mataifa mengine.

Madhara ya cyber attack yanakwenda mbali hadi katika biashara, uchumi n.k.

Kumkatia internet ni jitihada za pamoja na haitachukua muda yatamkuta

Ndiyo maana US wanasema watwajibu Russia na si Wikileaks, ikiwa na maana wikileaks inatumiwa na mataifa katika ''cyber war''

Unapoliangalia kwa mtazamo wa uchaguzi, kuna mengi unayokosa
 
.....

TUJITEGEMEE suala la Wikileaks ni zito kuliko unavyodhani... Hili si la siasa za uchaguzi ni la usalama wa mataifa....Mfano, walipo hack state dept na kutoa siri za OBL, nchi zilizohusika zilitajwa...Wikileaks ni tishio kwa maana ya cyber attack ikitumiwa na mataifa mengine....

Ni kweli ni suala zito. Lakini, hivi ni ipi dhambi kubwa kati ya kudukua (hacking) na kutega sikio kwa siri za mwenzako (eavesdropping). EU ilikasirishwa sana na kitendo cha NSA kuwasikiliza mipango yao wakati wanajiandaa kufanya lobbying na US. Mambo haya US kayasabisha mwenyewe.

Wikileaks...wanafanya investigative journalism, wanatafuta ukweli...sioni ubaya wao kutuonyesha kuwa US walitumia cluster bombs kuiangusha Iraq ya Saddam (R.I.P) kwa sababu za uongo kuwa ana silaha za maagamizi. Tena walikuwa wanaua raia hovyo. Kumbuka US ametia saini kuzuia matumizi ya silaha za namna hiyo. Kuna ubaya gani...wikileaks kutueleza kuwa Sander alihujumiwa na viongozi wa DNC ili 'mama' apite? Wakati DNC wanajitapa ni wajuvi wa demokrasia? mifano ipo mingi...Wikileaks wanafanya jambo jema kwa ustawi wa amani na haki kwa Dunia.

Mkuu na tena Mwalimu wangu, hivi malalamiko haya ya kuhatarisha usalama wa mataifa..mbona hayakupata 'mwendokasi' ....zilipotoka 'Panama Papers'? Gazeti la Ujerumani lilopata taarifa hizi likiwa la kwanza na kuzitoa, mbona halikushambuliwa hivi? Au kwa kuwa lilificha...wakwepa kodi maarufu wa US (Makampuni makubwa ya US na elites wengine)...!??

Mimi nasema Wikileaks wanawezesha demokrasia duniani tena demokrasia ya kujieleza tena kueleza ukweli. Wikileaks...hawataki unafiki...ambao umekuwa ndiyo 'expertise' ya US na washirika wake...katika mambo mbalimbali. Kuwafugamanisha Wikileaks na Russia ni kuendeleza kile cha kuficha madhambi wanayofanya hao 'experts in hypocrisy'.
Wikileaks waachwe wafanye kazi yao.
 
Ni kweli ni suala zito. Lakini, hivi ni ipi dhambi kubwa kati ya kudukua (hacking) na kutega sikio kwa siri za mwenzako (eavesdropping).

EU ilikasirishwa sana na kitendo cha NSA kuwasikiliza mipango yao wakati wanajiandaa kufanya lobbying na US. Mambo haya US kayasabisha mwenyewe.

Wikileaks...wanafanya investigative journalism, wanatafuta ukweli...sioni ubaya wao kutuonyesha kuwa US walitumia cluster bombs kuiangusha Iraq ya Saddam (R.I.P) kwa sababu za uongo kuwa ana silaha za maagamizi. Tena walikuwa wanaua raia hovyo. Kumbuka US ametia saini kuzuia matumizi ya silaha za namna hiyo. Kuna ubaya gani...wikileaks kutueleza kuwa Sander alihujumiwa na viongozi wa DNC ili 'mama' apite? Wakati DNC wanajitapa ni wajuvi wa demokrasia? mifano ipo mingi...Wikileaks wanafanya jambo jema kwa ustawi wa amani na haki kwa Dunia.

Mkuu na tena Mwalimu wangu, hivi malalamiko haya ya kuhatarisha usalama wa mataifa..mbona hayakupata 'mwendokasi' ....zilipotoka 'Panama Papers'? Gazeti la Ujerumani lilopata taarifa hizi likiwa la kwanza na kuzitoa, mbona halikushambuliwa hivi? Au kwa kuwa lilificha...wakwepa kodi maarufu wa US (Makampuni makubwa ya US na elites wengine)...!??

Mimi nasema Wikileaks wanawezesha demokrasia duniani tena demokrasia ya kujieleza tena kueleza ukweli. Wikileaks...hawataki unafiki...ambao umekuwa ndiyo 'expertise' ya US na washirika wake...katika mambo mbalimbali. Kuwafugamanisha Wikileaks na Russia ni kuendeleza kile cha kuficha madhambi wanayofanya hao 'experts in hypocrisy'.
Wikileaks waachwe wafanye kazi yao.
TUJITEGEMEE nadhani haya ni maoni yako, sidhani kama ni vema kusema ni sahihi au ni makosa

Ninachokiona ni ''prejudice'' dhidi ya western kwa kuangalia maneno katikati ya mistari.

US wanaona wikileaks ni tishio la usalama, ni kwa mujibu wao ambao si lazima iwe sahihi kwa mwingine. Tunajadili kwa mujibu wasemavyo

Kuna hacking na espionage. Hacking unaposema ni jambo zuri, pengine ni wakati huu. Ukimuuliza JK hawezi kukubaliana nawe hata kidogo

Na siku wikileaks watakapomwaga siri za ulinzi wa nchi yetu sijui kama utasimama na kutetea hilo ni jambo jema na ni uendelevu wa demokrasia

Ukifuatilia uchaguzi wa Marekani, suala la wikileaks hata kwa Republican hawajalishikia bango isipokuwa Trump for short term political gain

Na mwisho, investigative journalism na hacking ni vitu tofauti kabisa

Ahsante
 
KUELEKEA NOVEMBER 8

Kuelekea November 6 polls zimekuwa zinatoka kila wakati kutoka vyanzo tofauti.

Katika hali ya uchaguzi wa Urais wa Marekani hali imekuwa hivyo wakisema ni 'fluid' dakika za mwisho

Kuna Polls zimetoka za Fox zikionyesha Hillary akiongoza kwa ujumla kwa tofauti ya point nne(national wide)
Zipo za Bloomberg zinazoonyesha Nevada na Arizona sasa ni battle state na Nevada ni dead heat 43%

Arizona ni Red state na Nevada ni blue state. Arizona ina 11 electoral vote, Nevada ina 4 electoral vote

Utah 6 electoral vote na ni traditionally red state ingawa sasa inakuwa tight kutoka Dem

New Hampshire ina 4 electoral vote na inaelekea kuwa Dem, Iowa ikielekea kuwa Trump

Hapa ndipo tunarudi kwenye ramani ya mabandiko ya awali kuhusu viti (electoral vote)

Kwa wakati huu wagombea wamejikita battleground state na hapa ni Florida
Polls zinaonyesha Trump mbele point 2 within margin of error.

Kwanini wagombea wamezama Florida?

1. Florida ni big prize of the day. Ina viti 29.

Hii ina maana moja, ukichukua viti vya Nevada, Arizona, New Hampshire, Iowa kwa pamoja hiyo ni sawa na viti vya Florida peke yake

Katika viti 270 vya ushinda, atakayepata Florida atakuwa atatafuta viti 241 kufikia magic number

2. Ramani inaonyesha Florida ni must win kwa Trump kutokana na mgawanyo wa asili wa states ambao ni kama utamaduni.

Kwamba California ni Dem, Texax ni Republican n.k. huku kukiwa na swing states

Trump anaelekeza nguvu huko kwasababu ili kugonga 270 hapaswi kupoteza Florida

Hillary anazama Florida kuimarisha wigo wa ushindi kwani ana alternative way to 270

Lakini pia Clinton anambana Trump kule Florida ili asiweze kuelekea maeneo kama Ohio, eneo jingine lenye viti vingi sana.

Hivyo hapa kuna namba na psychology. Na kwa hilo utaona Trump kazama sana Florida

3. Upigaji kura wa awali unaendelea maeneo mbalimbali ikiwemo Arizona na Florida, wagombea wanafanya final push kwa early voters ili likitokea lisilotarajiwa watakuwa tayari wameshapata wapiga kura hao

Ni makosa kampeni zote kudhani kuwa polls zinaeleza kila kitu, na ni makosa kuzidharau

Mwaka 2012 kura za maoni zote zilionyesha Romney na Obama katika dead Heat na nyingine zikionyesha Trump yupo mbele.

Matokeo yalikuwa kama yalivyoonyeshwa katika polls, overall yalikuwa tofauti

Obama alitarajiwa kushinda kwa viti 272 na matokeo ya mwisho alishinda kwa viti 330

Hili nalo linaeleza kitu tutakachojadili mbele ambacho wengi hukisahau kuhusu upigaji kura

Inaendelea.....
 
KUELEKEA NOVEMBER 8

Kuelekea November 6 polls zimekuwa zinatoka kila wakati kutoka vyanzo tofauti.

Katika hali ya uchaguzi wa Urais wa Marekani hali imekuwa hivyo wakisema ni 'fluid' dakika za mwisho

Kuna Polls zimetoka za Fox zikionyesha Hillary akiongoza kwa ujumla kwa tofauti ya point nne(national wide)
Zipo za Bloomberg zinazoonyesha Nevada na Arizona sasa ni battle state na Nevada ni dead heat 43%

Arizona ni Red state na Nevada ni blue state. Arizona ina 11 electoral vote, Nevada ina 4 electoral vote
Utah 6 electoral vote na ni traditionally red state ingawa sasa inakuwa tight kutoka Dem

New Hampshire ina 4 electoral vote na inaelekea kuwa Dem, huku Iowa ikielekea kuwa Trump

Hapa ndipo tunarudi kwenye ramani ya mabandiko ya awali kuhusu viti (electoral vote)

Kwa wakati huu waombea wamejikita katika battleground state na hapa ni Florida ambako polls zinaonyesha Trump akiwa na point 2 within margin of error. Kwanini wagombea wamezama Florida?

1. Florida bni big prize of the daya. Ina viti 29. Hii ina maana moja, ukichukua viti vya Nevada, Arizona, New Hampshire, Iowa kwa pamoja hiyo ni sawa na viti vya Florida peke yake

Katika viti 270 vya ushinda, atakayepata viti 29 vya Florida atakuwa anatafuta viti 241 tu kufikia magic number

2. Ramani inaonyesha kuwa Florida ni must win kwa Trump kutokana na mgawanyo wa asili wa states ambao ni kama utamaduni. Kwamba California ni Dem, Texax ni Republican n.k. huku kukiwa na swing states

Trump anaelekeza nguvu zake huko kwasababu ili aweze kugonga 270 hapaswi kupoteza Florida
Hillary anazama Florida ili kuimarisha wigo wa ushindi kwani ana alternative way kufikia 270.

Lakini pia Clinton anambana Trump kule Florida ili asiweze kuelekea maeneo kama Ohio, eneo jingine lenye viti vingi sana. Hivyo hapa kuna namba na psychology. Na kwa hilo utaona Trump kazama sana Florida

3. Upigaji kura wa awali unaendelea katika maeneo mbalimbali ikiwemo Arizona na Florida, hivyo wagombea wanafanya final push kwa early voters ili likitokea lisilotarajiwa watakuwa tayari wameshapata wapiga kura hao

Ni makosa kwa kampeni zote kudhani kuwa polls zinaeleza kila kitu, na ni makosa kuzidharau

Mwaka 2012 kura za maoni zote zilionyesha Romney na Obama katika dead Heat na nyingine zikionyesha Trump yupo mbele. Matokeo yalikuwa kama yalivyoonyeshwa katika polls, overall yalikuwa tofauti

Obama alitarajiwa kushinda kwa viti kati ya 272 na matokeo ya mwisho alishinda kwa viti 330

Hili nalo linaeleza kitu tutakachojadili mbele ya safari ambacho wengi hukisahau kuhusu upigaji kura

Inaendelea.....
Kwa mara ya kwanza tangu kampeni zianze, polls za Rasmussen zinamuonesha Clinton akiongoza kwa point moja...! Kama kawaida LA Times bado inamuonesha Trump mbele kwa pointi moja.


Reuters/Ipsos: Clinton 43, Trump 37...Clinton +6

USA Today/Suffolk: Clinton 49, Trump 39...Clinton +10

LA Times/USC Tracking: Clinton 44, Trump 45...Trump +1

IBD/TIPP Tracking: Clinton 43, Trump 41...Clinton +2

ABC News Tracking: Clinton 51, Trump 43...Clinton +8

Rasmussen Reports: Clinton 44, Trump 43...Clinton +1

Associated Press-GfK: Clinton 54, Trump 41...Clinton +13
 
1.TUJITEGEMEE nadhani haya ni maoni yako, sidhani kama ni vema kusema ni sahihi au ni makosa

2.Ninachokiona ni ''prejudice'' dhidi ya western kwa kuangalia maneno katikati ya mistari.

3.US wanaona wikileaks ni tishio la usalama, ni kwa mujibu wao ambao si lazima iwe sahihi kwa mwingine. Tunajadili kwa mujibu wasemavyo
.

4.Kuna hacking na espionage. Hacking unaposema ni jambo zuri, pengine ni wakati huu. Ukimuuliza JK hawezi kukubaliana nawe hata kidogo

5.Na siku wikileaks watakapomwaga siri za ulinzi wa nchi yetu sijui kama utasimama na kutetea hilo ni jambo jema na ni uendelevu wa demokrasia
...
Ahsante
1. Upo sahihi kabisa

2.Hapa Mwalimu wangu umenishambulia kiaina! Lakini twende nadhani ni matatizo ya mwanafunzi mtukutu.

3.Wakisema ukweli tena kwa manufaa ya demokrasia na amani ya dunia,tujadili kwa kuwapongeza. Lakini wakisema uongo na kutufanyia unafiki tuwaseme tena bila kupepesa macho ili waache tabia hizo. Na tuwaonyeshe tunakerwa nazo hizo tabia.

4. Espionage ni treason offence(Idd Amin, aliwahi kusema mtenda kosa la namna hiyo, huyo ni wakupeleka moja kwa moja kwenye uwanja wa firing squad). Hacking ni high order crime, ila kama uchunguzi wa kuwatia mbaroni wadhalimu utahusisha hacking kwa wahusika tu, nadhani hakuna shida.

5. Nadhani hapa unai' demonise ' wikileaks, Mwalimu wangu, ni lini ulisikia Wikileaks wamevujisha siri za security code za silaha za nyuklia za nchi, siri zenye nia njema za majeshi , nakadhalika ? WikiLeaks wanafichua frauds katika maeneo yote bila kujali nani anakwazika.
=============
Tuachane na hayo, turudi kwenye uchaguzi wa US.
Jana Trump kasema, 'mama' ataanzisha vita ya tatu ya Dunia. 'Mama' hajakanusha mpaka sasa. Je. hamuoni kuwa huyu 'mama' ana nia ovu juu ya ulimwengu?
 
======Tuachane na hayo, turudi kwenye uchaguzi wa US.Jana Trump kasema, 'mama' ataanzisha vita ya tatu ya Dunia. 'Mama' hajakanusha mpaka sasa. Je. hamuoni kuwa huyu 'mama' ana nia ovu juu ya ulimwengu?
Kampeni za Marekani ni za kiwango cha juu

Zinaongozwa na watu waliobobea katika masuala ya siasa, uchumi, jamii n.k.
Kila eneo lina watu waliobobea wanaomshauri mgombea nini cha kusema nini asiseme au kujibu

Marekani imeingia katika civil war, imekuwapo wakati wa WW1 and WW2, inajua matatizo ya vita hasa ikizingatiwa ni Taifa lenye nguvu duniani na ikitokea dunia itaiangalia.

Marekani imekuwa katika vita na mataifa mbali mbali kama Vietman, na hivi karibuni Iraq, Syria, Libya n.k.
Inafahamu what is at stake!

Lakini pia Mkuu, habari kama hizi si suala la nani kasema. Ni suala la kuwa na evidence
Ungetueleza comment hizo zime base katika ushahidi upi

Nitashangaa ikiwa Hillary atajibu tuhuma zitazotolewa kwa mfano ' anataka kuoelewa na Timberlake'

Atakapokaa kimya, Mkuu Tujitegemee atauliza kwanini hajakanusha
 
Back
Top Bottom