Why Trump-Loving Christians Owe Bill Clinton an Apology
Nimekutana na hii article hapo juu ikanifikirisha kidogo kuhusiana na nafasi ya evangelical christians katika uchaguzi wa marekani. Hawa miaka nenda rudi wamekuwa ni wafuasi watiifu kwa chama cha republicans kutokana na msimamo wa chama hicho kuhusiana na masuala ya ndoa za jinsia moja na utoaji mimba.
Wakati Bill Clinton anaandamwa na kashfa ya ufuska na Monica Lewinsky hawa evangelicals walikuwa mstari wa mbele kumshambulia kwa kukosa maadili n.k.
Sasa upepo umebadilika ambapo wanapata wakati mgumu kumtetea Donald Trump anayeandamwa na kashfa zile zile za ufuska na unyanyasaji kingono wanawake. Pamoja na kashfa zote bado hawa wako tayari kumuunga mkono Trump na kusahau kashfa zote zinazomuandama ambazo kimsingi ni kinyume na maadili ya republicans.
Uchaguzi huu unazidi kuibua mengi kwa kweli.
Mkuu ahsante kwa hoja nzuri sana zinazolingana na maana halisi ya mjadala na kuangalia mambo kutoka angle tofauti na kwa mantiki
Mkuu, Evangelical ni Christian wanaoamini katika suala na haki ya kuzaa na wasiopenda suala la abortion
Kama ujuavyo, Republican ni prolife wakati waliberali wao wapo 'open' kwa kila jambo
Kwa mantiki hiyo, suala la abortion na same sex marriage lina impact sana kwa evangelical na hivyo kujikuta wakisimama na Republican always
Pili, evangelical ni watu wanaisi kwa wingi vijijini huko marekani wakiita country.
Tatu,huko vijijini wengi wanaamini katika umiliki wa silaha (second amendment)
Trump
Kwanza, msimamo wake kuhusu abortion na same au gays unabailika kila mara
Trump siyo prolife kwa baadhi ya nyakati na kuna wakati aliwahi ku support ushoga
Hillary, kama Dem anaunga mkono abortion na ushoga kama ilivyo sera za Waliberali
Evangelical
Ukichanganya hoja hapo juu evangelical mwaka huu wana wakati mgumu sana.
Kwanza, hawakubaliani na misimamo ya Trump kuhusu masuala ya ubaguzi wa dini kama ilivyo kule Utah kwa Momon.
Pili, hawana uhakika kama Trump ni pro life wa kweli au ni wa uchaguzi
Kwa upande mwingine, hawakubaliani na Hillary kwasababu tulizoeleza hapo juu
Kwasasa, evangelical wanaonekana kutishika na suala la second amendment.
Trump anawaambia Hillary atachagua Jaji ambaye atazuia umiliki wa silaha.
Kama utakumbuka hawa wanaishi vijijini na ndio wanamiliki silaha kwa wingi.
Lakini pia wana wasi wasi jaji atakayeteuliwa na Hillary anaweza kuruhusu abortion
Kwa mantiki hiyo wapo katika uchaguzi wa 'lesser evil' na hapa kwao Trump ana afadhali licha ya mazonge zonge yake na wanawake.
Evangelical wanaona interest zao zitalindwa Zaidi wakiwa na Trump kuliko Hillary, hilo la wanawake wa Trump ni funika kombe
Tusemezane