Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

Kampeni za Marekani ni za kiwango cha juu

Zinaongozwa na watu waliobobea katika masuala ya siasa, uchumi, jamii n.k.
Kila eneo lina watu waliobobea wanaomshauri mgombea nini cha kusema nini asiseme au kujibu

Marekani imeingia katika civil war, imekuwapo wakati wa WW1 and WW2, inajua matatizo ya vita hasa ikizingatiwa ni Taifa lenye nguvu duniani na ikitokea dunia itaiangalia.

Marekani imekuwa katika vita na mataifa mbali mbali kama Vietman, na hivi karibuni Iraq, Syria, Libya n.k.
Inafahamu what is at stake!

Lakini pia Mkuu, habari kama hizi si suala la nani kasema. Ni suala la kuwa na evidence
Ungetueleza comment hizo zime base katika ushahidi upi

Nitashangaa ikiwa Hillary atajibu tuhuma zitazotolewa kwa mfano ' anataka kuoelewa na Timberlake'

Atakapokaa kimya, Mkuu Tujitegemee atauliza kwanini hajakanusha
Kwa temperament kama kuna mtu anaweza kusababisha WW3 ni Donald Trump na si Hillary Clinton. Clinton hana haja ya kutoa maelezo yoyote kwa dai kama hilo kwa sababu halina msingi wowote...!

Hii ndiyo hali kwa sasa...hakuna poll inayoonesha Trump akiongoza.​

polls-jpg.425389

Labda maajabu yatokee lakini hakuna namna Donald Trump ataiona Ikulu ya Marekani!​
 
Tar.09/11/2016. Tutakuwa tumeshajua nani atakuwa Rais ajaye wa US. Mkuu mag3 tafadhali sana usikimbie siku hiyo. Me nakuhakikishia hakuna namna huyo bibi asiyeaminika kukabidhiwa white house..!! Kuna taarifa nimeona hata CNN wameshaanza kuwa na wasiwasi wa kupata namba 270. Nguruvi3 anaakili sana huyu jamaa,huyu hata km kuna mgombea anampenda lkn amejitahidi kutokuwa na upande anajua huu ni uchaguzi na lolote linaweza kutokea. Hii wiki ya mwisho hata poll zote utaziona zinabadilika..!!
 
Si swala la kupenda au kutopenda, ni swala la kuangalia tu hali halisi...mimi si Mmarekani na kupiga kura sipigi, sasa kumpenda au kutompenda mgombea kunanisaidia nini?
2016-simulation
 
Si swala la kupenda au kutopenda, ni swala la kuangalia tu hali halisi...mimi si Mmarekani na kupiga kura sipigi, sasa kumpenda au kutompenda mgombea kunanisaidia nini?
2016-simulation
Hakuna hali halisi kwa sasa,hali halisi ni Tar.08
/11/2016. Kilichopo kwa sasa ni kampeni kwa kila upande. Lkn sisi km binadamu bila kujali km kuna faida au hasara kwa maamuzi watakayofanya wamarekani,lkn hata sisi wenyewe kila mmoja kwa namna anavyouangalia uchaguzi wa us,tuna upande ambao tungepende ushinde.

Kwa mfano mimi nimeonyesha tangu mwanzo,nisingependa ashinde huyo bibi. Maana yake akishinda HC me lazima niumie hata km maumivu hayo hayana athari ya moja kwa moja ktk maisha yangu. Vivyo hivyo kwa upande wako,akishinda DT lazima utaumia bila kujali hayo maumivu ni ya aina gani..!

Hii ni sawa tu na maumivu anayopata mtu kwa kushabikia manchester utd inapofungwa..!! Yule mama hizi poll za sasa zitamsababishia kifo cha mapema,atakuwa anaziwaza sana kwa kuongoza kisha kwenye hali halisi anatupwa nje. Fox news wanaonyesha Trump amepiga hatua,sasa national poll wanaonyesha mama yupo mbele 44%(+3) dhidi ya 41% awali mama alikuwa mbele kwa 49% (+5) dhidi ya 44% za DT.
 
Naona mjadala unaendelea vizuri wakuu... Kuna mambo kadhaa nimekuwa nikijiuliza.

Kwa nini katika uchaguzi huu wagombea wanaopewa coverage ni Clinton na Trump ili hali kuna wagombea wengine binafsi Johnson na Stein lakini hawapati coverage kabisa? Hata kwenye midahalo yote mitatu walishiriki ni Clinton na Trump pekee huku hawa wengine wakiachwa pembeni. Na hii imekuwa ni utaratibu wa miaka yote kwamba wagombea kutoka vyama vingine au wagombea binafsi wanaonekana kuwa ni wasindikizaji tu wasio na impact yoyote. Inawezekana sina uelewa mkubwa sana wa siasa za marekani lakini naona kuwa ni mfumo ulio 2-dimension zaidi... yaani lazima either uwe democrat au republican, lazima uwe na msimamo wa ki-liberali au kihafidhina (conservative) na sio nje ya hapo! Nafikiri kwa taifa kubwa la kidemokrasia kama marekani hali hii ni udhaifu wa aina fulani.

Wakuu Nguruvi3 joka kuu Mag3 na wengineo mnaweza kunisaidia kufafanua hili?
 
Why Trump-Loving Christians Owe Bill Clinton an Apology

Nimekutana na hii article hapo juu ikanifikirisha kidogo kuhusiana na nafasi ya evangelical christians katika uchaguzi wa marekani. Hawa miaka nenda rudi wamekuwa ni wafuasi watiifu kwa chama cha republicans kutokana na msimamo wa chama hicho kuhusiana na masuala ya ndoa za jinsia moja na utoaji mimba. Wakati Bill Clinton anaandamwa na kashfa ya ufuska na Monica Lewinsky hawa evangelicals walikuwa mstari wa mbele kumshambulia kwa kukosa maadili n.k.

Sasa upepo umebadilika ambapo wanapata wakati mgumu kumtetea Donald Trump anayeandamwa na kashfa zile zile za ufuska na unyanyasaji kingono wanawake. Pamoja na kashfa zote bado hawa wako tayari kumuunga mkono Trump na kusahau kashfa zote zinazomuandama ambazo kimsingi ni kinyume na maadili ya republicans.

Uchaguzi huu unazidi kuibua mengi kwa kweli.
 
Naona mjadala unaendelea vizuri wakuu... Kuna mambo kadhaa nimekuwa nikijiuliza.

Kwa nini katika uchaguzi huu wagombea wanaopewa coverage ni Clinton na Trump ili hali kuna wagombea wengine binafsi Johnson na Stein lakini hawapati coverage kabisa? Hata kwenye midahalo yote mitatu walishiriki ni Clinton na Trump pekee huku hawa wengine wakiachwa pembeni. Na hii imekuwa ni utaratibu wa miaka yote kwamba wagombea kutoka vyama vingine au wagombea binafsi wanaonekana kuwa ni wasindikizaji tu wasio na impact yoyote. Inawezekana sina uelewa mkubwa sana wa siasa za marekani lakini naona kuwa ni mfumo ulio 2-dimension zaidi... yaani lazima either uwe democrat au republican, lazima uwe na msimamo wa ki-liberali au kihafidhina (conservative) na sio nje ya hapo! Nafikiri kwa taifa kubwa la kidemokrasia kama marekani hali hii ni udhaifu wa aina fulani.

Wakuu Nguruvi3 joka kuu Mag3 na wengineo mnaweza kunisaidia kufafanua hili?
Mkuu midahalo huandaliwa na (CPD) commission on presidential debate. Kuna vigezo vinavyotumika mgombea kukaribishwa katika mdahalo
1.Uwezekano wa kupata viti 270 katika uchaguzi mkuu
2. Na wastani wa asilimia 15 katika sample 5 za kura za maoni
3. Uhakika wa mgombea kukidhi matakwa ya kikatiba kuwa Rais wa Marekani

Utaona Johnsona and Stein hawakufikia kiwango hicho na hivyo kutokuwa katika debate

Kuhusu coverage, nalo linategemea. Kwa mfano, sasa hivi kuna mgombea anaitwa Evan Mculum kutoka Utah
Utah ni jimbo la waamuni wa Momom ile dini ya mgombea Mitt Romney

Kura za maoni zainzonyesha Utah inaelekea kuwa battleground state. Kiasili hii ni pure Red state
Hillary na Dem hawajaweka jitihada huko, Trump akiwa na uhakika ni Red State kwasababu haijawahi kupigia kura Dem kwa Zaidi ya miaka 30.

Mtu anyeleta matatizo kwa Trump na GOP ni Evan wa Momom ambaye anachukua kura za Republican, na hivyo Democrats wanapanda. Kwa lugha rahisi kura za Republican zinagwanywa kwa Trump na Evan, wakati kura za Democrat zinabaki vile vile. Hilo ndilo linabadilisha hali ya Utah

Utaona media zimeanza kuwka attention Utah kutokana na hilo, lakini haziwezi kuweka attention kwa Evan au Johnston ambao hawapo New York, California, Mississippi au Boston. Hapa ni suala la nani ana impact

Johnson na Stein utawasikia pale ambapo impact yao itaathiri matokeo ya wawili waliobaki

Ni kama hapa kwetu, nani alikuwa na msisimko na Kuga Mziray wa TPP, au Jahazi asilia au chama cha Mrema?

Lakini pia ukumbuke , hata katika party level kuna kiwango wagombea wanaruhusiwa kushiriki debate

Ukiwa na uungwaji mkono wa 1 au 3% unaweza kutoshirikishwa.

Ndivyo ilivyokuwa kwa midahalo ya GOP ambapo wagombea 16 kuna baadhi ima walipewa debate kutimiza wajibu au hawakushirikishwa
 
Why Trump-Loving Christians Owe Bill Clinton an Apology

Nimekutana na hii article hapo juu ikanifikirisha kidogo kuhusiana na nafasi ya evangelical christians katika uchaguzi wa marekani. Hawa miaka nenda rudi wamekuwa ni wafuasi watiifu kwa chama cha republicans kutokana na msimamo wa chama hicho kuhusiana na masuala ya ndoa za jinsia moja na utoaji mimba.

Wakati Bill Clinton anaandamwa na kashfa ya ufuska na Monica Lewinsky hawa evangelicals walikuwa mstari wa mbele kumshambulia kwa kukosa maadili n.k.

Sasa upepo umebadilika ambapo wanapata wakati mgumu kumtetea Donald Trump anayeandamwa na kashfa zile zile za ufuska na unyanyasaji kingono wanawake. Pamoja na kashfa zote bado hawa wako tayari kumuunga mkono Trump na kusahau kashfa zote zinazomuandama ambazo kimsingi ni kinyume na maadili ya republicans.

Uchaguzi huu unazidi kuibua mengi kwa kweli.
Mkuu ahsante kwa hoja nzuri sana zinazolingana na maana halisi ya mjadala na kuangalia mambo kutoka angle tofauti na kwa mantiki

Mkuu, Evangelical ni Christian wanaoamini katika suala na haki ya kuzaa na wasiopenda suala la abortion
Kama ujuavyo, Republican ni prolife wakati waliberali wao wapo 'open' kwa kila jambo

Kwa mantiki hiyo, suala la abortion na same sex marriage lina impact sana kwa evangelical na hivyo kujikuta wakisimama na Republican always

Pili, evangelical ni watu wanaisi kwa wingi vijijini huko marekani wakiita country.

Tatu,huko vijijini wengi wanaamini katika umiliki wa silaha (second amendment)

Trump
Kwanza, msimamo wake kuhusu abortion na same au gays unabailika kila mara
Trump siyo prolife kwa baadhi ya nyakati na kuna wakati aliwahi ku support ushoga

Hillary, kama Dem anaunga mkono abortion na ushoga kama ilivyo sera za Waliberali

Evangelical
Ukichanganya hoja hapo juu evangelical mwaka huu wana wakati mgumu sana.

Kwanza, hawakubaliani na misimamo ya Trump kuhusu masuala ya ubaguzi wa dini kama ilivyo kule Utah kwa Momon.

Pili, hawana uhakika kama Trump ni pro life wa kweli au ni wa uchaguzi

Kwa upande mwingine, hawakubaliani na Hillary kwasababu tulizoeleza hapo juu

Kwasasa, evangelical wanaonekana kutishika na suala la second amendment.

Trump anawaambia Hillary atachagua Jaji ambaye atazuia umiliki wa silaha.
Kama utakumbuka hawa wanaishi vijijini na ndio wanamiliki silaha kwa wingi.

Lakini pia wana wasi wasi jaji atakayeteuliwa na Hillary anaweza kuruhusu abortion

Kwa mantiki hiyo wapo katika uchaguzi wa 'lesser evil' na hapa kwao Trump ana afadhali licha ya mazonge zonge yake na wanawake.

Evangelical wanaona interest zao zitalindwa Zaidi wakiwa na Trump kuliko Hillary, hilo la wanawake wa Trump ni funika kombe

Tusemezane
 
USIMAMIZI WA UCHAGUZI NA YANAYOJIRI

Mabandiko haya yanakusudia sisi sote tujifunze wenzetu wanafanya nini wana mapungufu gani, mazuri gani n.k.

Hii ni pamoja na uchujaji wa Wagombea kuanzia hatua za vyama na kufikia kupiga kura.

Katika mwendelezo wa hayo yote habari ni ile inayojitokeza kwa maswali, hoja, maoni n.k.

Halijawa suala la nani anashinda nani anashindwa. Kufanya hivyo hakutusaidii tukijua chaguzi za wenzetu zina hatua mbali mbali za wazi na nyingine zinazohitaji ufafanuzi.

Hilo ndilo linapelekea kuzungumzia mambo kama popular vote vs electoral votes, demography, upigaji kura n.k. ambavyo si rahisi kueleweka kwa wengi

Upigaji kura unatayarishwa na majimbo husika. Marekani kuna tume ya uchaguzi ya watu 6 katika federal level

Hiyo inashughulikia masuala mazito kama vile electoral college zitakaposhindwa kuthibitisha Rais na VP

Lakini pia tume inatafsiri kwa upana federal law ambazo haziingiliani na state law panapotokea mtafaruku

Uchaguzi huandaliwa na state na kila state ina sheria zake. Mfano, kuna state inaruhusu registered voters wapige kura kwa kutumia mail. Kuna state zina early voting kama ilivyo sasa kwa Florida, Ohio,Texas n.k.

Jana kumetokea taarifa wapiga kura wa Texas wameshangazwa na kupiga kura kwa DT, jina linalotokea Hillary. Habari hizi hazijulikani chanzo chake na zimesambaa katika vyombo vya habari

Donald Trump anayezungumzia 'rigging' amedakia na kusema tayari kuna fraud.

Alipoulizwa ushahidi wa hilo, Trump kasema amesikia linatokea!!!

Gavana wa Texas ni Rick Perry ambaye ni Republican. Uchaguzi upo chini ya Republican katika state.

Wasimamizi wote ambao ni Republican wamejitokeza na kukanusha habari hizo.

Mlolongo mzima wa uchaguzi umeelezwa kwa kina kiasi cha kuondoa shaka inayosambaa mitaani

Trump amesema mara nyingi kuna rigging. Kila alipoulizwa kama mchakato wa uchaguzi una tatizo, alisema tatizo lipo katika media zinazomwandika kuliko mwenzake na hiyo ndiyo rigging.

Leo anazungumzia mchakato mzima wa uchaguzi Texas kwamba unathibitisha madai yake

Makamu wake Mike Pnece, ameulizwa na kusema ana Imani na mchakato mzima wa uchaguzi na kwamba fraud haiwezi kutokea kwa upana unaofikiriwa.

Mike alimaanisha kunaweza kutokea tatizo sehemu, lakini hilo tatizo halifanyi mchakato mzima kuwa batili.
Mike Pence anapingana na top ticket Donald Trump!!

November 8 siku ya uchaguzi kutakuwa na uzi maalumu kwa jina la ' Election centre, election night in US'
Uzi huo utaleta matokeo in real time kuwajulisha wahusika nini kinatokea na matokeo mazima

Tusemezane
 
Naona mjadala unaendelea vizuri wakuu... Kuna mambo kadhaa nimekuwa nikijiuliza.

Kwa nini katika uchaguzi huu wagombea wanaopewa coverage ni Clinton na Trump ili hali kuna wagombea wengine binafsi Johnson na Stein lakini hawapati coverage kabisa? Hata kwenye midahalo yote mitatu walishiriki ni Clinton na Trump pekee huku hawa wengine wakiachwa pembeni. Na hii imekuwa ni utaratibu wa miaka yote kwamba wagombea kutoka vyama vingine au wagombea binafsi wanaonekana kuwa ni wasindikizaji tu wasio na impact yoyote. Inawezekana sina uelewa mkubwa sana wa siasa za marekani lakini naona kuwa ni mfumo ulio 2-dimension zaidi... yaani lazima either uwe democrat au republican, lazima uwe na msimamo wa ki-liberali au kihafidhina (conservative) na sio nje ya hapo! Nafikiri kwa taifa kubwa la kidemokrasia kama marekani hali hii ni udhaifu wa aina fulani.

Wakuu Nguruvi3 joka kuu Mag3 na wengineo mnaweza kunisaidia kufafanua hili?
Mkuu Mwalimu kama ulifuatilia hatua za mwanzo za michauno ndani ya vyama (primaries) viko viwango vimewekwa na ili uruhusiwe kushiriki katika midadalo ni lazima ufikie kiwango fulani cha kukubalika. Hatua hii iliwekwa makusudi kuhakikisha mtu haamuki tu na kutangaza kugombea Urais hata kama haungwi mkono na wananchi wa kutosha.

Ndani ya vyama kiwango kiko chini kwa sababu idadi ya wanaojitokeza na kutangaza kugombea huwa ni wengi na namna pekee ya kuwachuja ni kuweka kiwango maalum cha uungwaji mkono. Ndio maana kwenye primaries mathalani za GOP idadi ya waliotangaza nia ya kugombea ilikuwa ni zaidi ya 40 lakini walioshiriki mdahalo walibaki 17 tu.
 
NEW TWIST

SIKU 10 KUELEKEA SANDUKU LA KURA

DEM WAJIKUTA KATIKA WAKATI MGUMU

Kwa wiki kadhaa WikiLeaks wametoa emails walizo hack kutoka kampeni ya Hillary
Nyingi hazikuonekana kuwa na mashiko ya kisheria. Katika siku chache wametoa Zaidi

FBI wameiandikia kamati ya bunge kuhusu emails wanazosema ni 'pertinent' katika uchunguzi

Habari hizi zimekuja wakati kukiwa na habari za uchumi kukua katika kiwango cha asilimia 2.9

Donald Trump kashikia bango suala hili kama ilivyokuwa kwake wiki chache zilizopita

Turudi nyuma kidogo kuhuu suala hili
Hoja kubwa ya Republican ilikuwa kuhusu matatizo yaliyotokea Libya, Benghaz

Kamati ya Bunge inayoongozwa na GOP iliona hakuna tatizo.

Mtakumbuka katika uzi wa uchaguzi wa Marekani tulisema silaha za Republican wanazipata kwa Bernie Sanders. Udhaifu wote wa emails unatokana na hoja za Sanders ambazo Republican wanazitumia

Ingawa hili linakuja kwa mlango mwingine, bado ni mwendelezo wa email za Sanders

WikiLeaks
Hawa walidhamiria kuharibu kampeni ya Clinton kwa kutoa emails.
Kosa walilofanya ni kutozitoa mapema ili ziwe mjadala katika midahalo

Kuelekea siku za mwisho, wameachia emails nyingi ambazo FBI

Hili la leo ni tofauti, kwani limetoka nje ya WikiLeaks na linahusiana na Uma na Winer

Muda
FBI wanasema hawajui uchunguzi utakamilika baada ya muda gani.
Hii ni dhahiri kuwa kukiwa na siku 10 ni unlikely uchunguzi huo utamalizika kabla ya uchaguzi.

FBI wanasema haionekani kama emails zimetoka kwenye private server
Na kwa kuzingatia uchaguzi wa awali umeshaanza, linabaki swali nini kitatokea

Impact katika uchaguzi
Kwa wafuasi wa Trump watampigia kura, na wa Hillary nao watafanya hivyo no matter what

Tatizo linakuja kwa undecided voters ambao huenda kwa namna Fulani walikuwa wanasubiri siku za mwisho
Hili litakuwa na impact kubwa sana kwa kampeni ya Clinton

Kwa Hillary, hili litaendelea ku overshadow kampeni yake, jambo ambalo ni baya katika wakati huu.

Kwa upande wa Trump, hii ni zawadi kwani sasa anapata cha kuongelea baada ya wiki tatu mbaya
Hivyo, Republican watatumia ku motivate wafuasi wao.

Tutaendelea kuleta kinachojiri
 
Hili suala la email naona lina mu attack vibaya sana H . Clinton, mpaka sasa naona vyombo vingi vya habari vimeishambulia hii isu na kuwa ajenda kubwa sana, naona ka a hili suala litamletea sana twist kubwa, na mbaya zaidi muda umeisha sana kutecover any damage within time
 
New development

Source ya uchunguzi wa FBI inatokana na uchunguzi uliokuwa unaendelea ukimhusu Anthony Weiner ijulikanayo kama sextings. Hapo ndipo info 'pertinent'zilipopatikana

Tutaendelea kufuatilia
 
CLINTON ATOA STATEMENT

Muda huu Hillary Clinton ametoa kauli kuhusu sakata la email

Katika statement, anasema, ni siku 11 kabla ya uchaguzi na wananchi wanataka kupata ukweli
Ana uhakika hii hatitabadili matokeo ya hitimisho lililofikiwa July 2016
Kwasasa anajikita katika kukabiliana na cgangamoto

Maswali
Clinton anasema habari hizi amezipata kuiptia vyombo vya habari kama wana habari walivyopata
Kuhusu kama watu watamfikiriaje, anasema watu wameshafikia na wajitokeze kupiga kura
Kama FBI wamewasiliana na kamati ya bunge ya GOP basi watoe maelezo kuhusu hilo
Anasema hana wasi wasi kuhusu email hizo

Amemaliza
 
  • Thanks
Reactions: BAK
CHIMBUKO LA emails

Sakata hili linamhusu Uma Abiden aliyekuwa mke wa Anthony Weiner. FBI walichukua kifaa(computer?) kuhusu mawasiliano yake na hasa sakata linalomhusu Anthony Weiner kuhusu ufataki kwa binti wa miaka 16

Katika email hizo kati ya Uma na Anthony Weiner vijana wa FBI waliona uwepo wa 'pertinent' information zinazohusiana na sakata la email

Kwahivyo hadi sasa haijulikani kama kuna classified information ambazo Uma na mumewe

Ndiyo maana Clinton anasema angependa kupata full information kuhusiana na hili sakata na kuwataka FBI watoe matokeo haraka.

Director wa FBI anasema hata yeye hajui kwa uhakika kama kuna classified infromation

Hapa kuna mtego, je, FBI wataweza kutoa information hizo katika siku 11?

Tutafutailia
 
HC haaminiki hawezi kuwa Rais wa US. Wamejaribu kumbeba tangu kwa bernie senders wakati wa uteuzi lkn hili ni sikio la kufa....Bernie senders mpaka leo ana kinyongo ingawa hajatoka hadharani. Lkn mkuu nguruvi3 km FBI wakiona kuna makosa ambayo HC anastahili kushitakiwa,na taarifa hizo zikawa tayari ndani ya wiki ijayo kabla ya november 08.

Km ikitokea hivyo,na HC akaamua ku-jiuzuru,nini kitatokea! Uchaguzi utasimama au itakuaje!!??
 
.....

Sasa upepo umebadilika ambapo wanapata wakati mgumu kumtetea Donald Trump anayeandamwa na kashfa zile zile za ufuska na unyanyasaji kingono wanawake. ....

Trump kasema hao wanawake wanamsingizia, na ameahidi kuwa shughuli za uchaguzi zikiisha lazima awafungulie mashtaka. Mpaka hapo, hilo suala kasha limaliza...hata wakitokea wengine...hawatakuwa na impact. Ni kwa sababu hii ya Trump hao evangelical christians...wamerejesha imani kwa Trump; nao wanaona kasingiziwa, vinginevyo hasingetishia kwenda mahakamani.
....

Kwa wiki kadhaa WikiLeaks wametoa emails walizo hack kutoka kampeni ya Trump......
Ni kweli Wikileak wamehack kampeni ya Trum, kumtia hatiani HRC?
 
Hili suala la email naona lina mu attack vibaya sana H . Clinton, mpaka sasa naona vyombo vingi vya habari vimeishambulia hii isu na kuwa ajenda kubwa sana, naona ka a hili suala litamletea sana twist kubwa, na mbaya zaidi muda umeisha sana kutecover any damage within time

Nadhani wengi wetu tunaongea kishabiki tu bila kuangalia significance, impact na repercussion ya barua ya FBI kwa kamati ya bunge kuhusu uchunguzi wa Emails za Clinton na timing yake. Kama FBI wanao ushahidi wa kutosha wa kuweza kumtia hatiani Clinton, basi uchaguzi umekwisha na hapo Clinton hatakuwa na namna bali kusalimu amri.

Lakini kama itatokea kwamba hakuna ushahidi unaotosha kumchukulia hatua Clinton, kitendo hicho cha Comey kinaweza kusababisha hali tofauti kabisa na wengi mnavyofikiria. Hiyo barua yake itatafsiriwa fotauti kabisa kimtazamo na pande mbili na kama maelezo sahihi na ya uhakika hayatatolewa na FBI, wanaodhani wamepata inaweza kula kwao.

Hapa kuna mambo mawili...la kwanza ni kwamba Comey kaandika hiyo barua akiwa na vielelezo vinavyotosheleza tayari mkononi. La pili ni ni kwamba Comey hakuwa na namna bali kufanya hivyo hata kama vielelezo haavitoshelezi. Tusisahau kwamba kama angesubiri hadi uchaguzi umalizike, angeweza kujikuta katika matatizo makubwa zaidi.

FBI miaka yote imejijengea sifa ya kufanya kazi yake bila kujali tofauti za kisiasa na imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutoyumbishwa na wana siasa. Lakini kitendo cha Comey, siku 11 kabla ya Uchaguzi Mkuu, hata ikitazamwa vipi, imeonesha kuyumbishwa na matamshi ya wana siasa na hapa lazima watoe maelezo yanayotosheleza, why now!

Ndani ya siku tatu zijazo, tutegemee kuona mambo mawili...msisimko mkubwa kwa upande wa wapiga kura kutegemea majibu yatakayotolewa na FBI. La pili ni Democrats kuitaka FBI kuanika kwa wananchi kila wanachojua kabla ya uchaguzi wakiungwa mkono na Republicans ambao mapenzi yao kwa taifa wanayapa kipaumbele kuliko itikadi.

Wakurupukaji wao tayari wamepata wimbo lakini kwa wachambuzi, hili jambo ni zito na si la kuchukulia kimzahamzaha. Wapo wanaojiuliza kwa nini FBI imekaa kimya kuhusu tuhuma zilizothibitishwa hadi na FBI yenyewe za hacked emails na nchi isiyo rafiki huku wakivalia njuga tuhuma wasizo na uhakika nazo siku 11 kabla ya Uchaguzi Mkuu!
 
Km ikitokea hivyo,na HC akaamua ku-jiuzuru,nini kitatokea! Uchaguzi utasimama au itakuaje!!??
Kama inatokea kwamba mgombea mojawapo anajiondoa kwenye uchaguzi kwa sababu zozote zile, katiba ya Marekani imewaachia wanachama kumchagua mgombea mwingine kulingana na katiba ya chama chao. Kwa Democrats, mwenyekiti wa chama ataitisha kikao ambacho kitawapigia kura wenye sifa na ambaye anashinda ndiye atakuwa mgombea. Hivyo ndivyo naelewa lakini inawezekana kuna mwenye uelewa zaidi.
 
Nadhani wengi wetu tunaongea kishabiki tu bila kuangalia significance, impact na repercussion ya barua ya FBI kwa kamati ya bunge kuhusu uchunguzi wa Emails za Clinton na timing yake. Kama FBI wanao ushahidi wa kutosha wa kuweza kumtia hatiani Clinton, basi uchaguzi umekwisha na hapo Clinton hatakuwa na namna bali kusalimu amri.

Lakini kama itatokea kwamba hakuna ushahidi unaotosha kumchukulia hatua Clinton, kitendo hicho cha Comey kinaweza kusababisha hali tofauti kabisa na wengi mnavyofikiria. Hiyo barua yake itatafsiriwa fotauti kabisa kimtazamo na pande mbili na kama maelezo sahihi na ya uhakika hayatatolewa na FBI, wanaodhani wamepata inaweza kula kwao.

Hapa kuna mambo mawili...la kwanza ni kwamba Comey kaandika hiyo barua akiwa na vielelezo vinavyotosheleza tayari mkononi. La pili ni ni kwamba Comey hakuwa na namna bali kufanya hivyo hata kama vielelezo haavitoshelezi. Tusisahau kwamba kama angesubiri hadi uchaguzi umalizike, angeweza kujikuta katika matatizo makubwa zaidi.

FBI miaka yote imejijengea sifa ya kufanya kazi yake bila kujali tofauti za kisiasa na imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutoyumbishwa na wana siasa. Lakini kitendo cha Comey, siku 11 kabla ya Uchaguzi Mkuu, hata ikitazamwa vipi, imeonesha kuyumbishwa na matamshi ya wana siasa na hapa lazima watoe maelezo yanayotosheleza, why now!

Ndani ya siku tatu zijazo, tutegemee kuona mambo mawili...msisimko mkubwa kwa upande wa wapiga kura kutegemea majibu yatakayotolewa na FBI. La pili ni Democrats kuitaka FBI kuanika kwa wananchi kila wanachojua kabla ya uchaguzi wakiungwa mkono na Republicans ambao mapenzi yao kwa taifa wanayapa kipaumbele kuliko itikadi.

Wakurupukaji wao tayari wamepata wimbo lakini kwa wachambuzi, hili jambo ni zito na si la kuchukulia kimzahamzaha. Wapo wanaojiuliza kwa nini FBI imekaa kimya kuhusu tuhuma zilizothibitishwa hadi na FBI yenyewe za hacked emails na nchi isiyo rafiki huku wakivalia njuga tuhuma wasizo na uhakika nazo siku 11 kabla ya Uchaguzi Mkuu!
Mkuu mwnasheria mkuu na DOJ wanasema walimshauri Comey asiandike barua bila kuwa na ushahidi wa kutosha katika muda huu.

Comey anasema kwavile aliitwa na kamati ya bunge siku za nyuma, hakuwa na namna bali kuandika tena kuhusu hilo

Hillary anasema barua waliyoandikiwa bunge hakupewa taarifa.
Akasema, Comey alimweleza hata yeye hajui nini hasa kilichomo.

FBI wamekuwa katika uchunguzi wa sexting ya Anthony Weiner kwa mwaka mzima.

Hili nalo linaleta habari nyingine , kwamba kwa muda hawakuweza kupata habari hizo

Lakini pia kuna namna nyingine, kwamba, kama mawasiliano ni ya Uma na Anthony Weiner nje ya server ya Clinton hilo linawezaje kumu implicate Hillary?

Kitendo cha Hillary kutaka kila kitu kiwekwe wazi kinaeleza anachojua kuhusu email hizo na impact yake

Hatudhani angeweza kutoka mbele na kusema zwekwe wazi aki jeorpadize nafasi yake

Pressure ipo kwa FBI ima kuweka wazi katika siku 10 zilizobaki au wakae kimya na kusababisha malalamiko kwa upande mwingine wa Republican.

Kwa hili Comey yupo katika wakati mgumu

Watu wakumbuke kuna mambo matatu au manne katika hili sakata
1. Kuna matumizi ya private email kwa classified doc ambayo FBI walisha rule out
2. Kuna email za Benghaz ambazo ndizo Republican wanazotumia kama hoja
3. Kuna emails za Wikilelaks
4. Kuna emails za Huma Abiden na Anthony Weiner

Haya ni mambo tofauti na kwasasa FBI inatakiwa iweke wazi uhusiano wa Huma na Anthony na Clinton katika hayo hapo juu.

Ikibainika kuna classified information, kinachoangaliwa Clinton alihusika.

Kinyume chake litakuwa suala la Huma na Anthony Weiner

Tunaedelea kufuatilia
 
Back
Top Bottom