Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
KELELE ZA UJANA NA MBIO ZA UONGOZI
HAWANA MAONO, HAWAJIAMINI, WAMEBAKI KULAMBA MIGUU
WAMEVAA NGOZI ZA CHUI, NI WOGA KAMA FISI, NA WASALITI KAMA YUDA
Sehemu ya I kati ya 2
Wanaduru
Tuliwahi kuambiwa vijana ni taifa la kesho na nguvu ya taifa lijalo.
Ghafla vijana wakacharuka na kusema wao ni taifa la leo na nguvu ya leo.
Usemi huo ukabadilisha mitazamo ya wananchi kwa matumaini makubwa.
Matumaini yaliyojengwa katika ukweli kuwa vijana ni wasomi,wamefunguka, wana maono na nguvu za kulisaidia taifa na kizazi cha leo.
Kauli mbiu ya vijana ikabamba, kila aliyetaka kupambana nao katika anga za siasa aliangaliwa umri na kutupiwa makombora ya uzee.
Wengi wakaogopa hata kutaja umri wao, wengine wakificha mvi zao, uzee ukawa janga.
Ukaingia unyanyapaa kwa wazee, busara zikachukua nafasi ya mwisho baada ya ujana na usomi.
Tuliaminishwa umasikini wa nchi hii unatokana na uzee, kwamba wazee walijifungia wakilewa ulanzi. Tukaaminishwa kuwa sasa ni zama za 'digital' hata vijana ni digital
Nafasi za upendeleo zikaanza kutolewa hata kuwa na mkuu wa Wilaya aliye na umri chini ya miaka 25. Bodi za mashirika na taasisi zikajazwa vijana kwa kile kilichosema wazee hawana jipya, hawana maono, kuteuliwa kwao ni kuweka mvinyo wa zamani katika chupa mpya.
Tambo zikahamia katika majukwaa ya siasa, vijana wakichaguliwa kwasababu ya umri na usomi wao. Bunge likasheheni wasomi wa kila aina na fani, wengi wakiwa ni vijana.
Makala zimeandikwa kuhusu vijana chini ya miaka 40, kama kwamba baada ya hapo uzee umepiga hodi na ndio ukomo wa fikra, maono au busara.
Matumaini yakawa makubwa, wananchi wakiwa na kiu ya kuona mbadiliko ya kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni. Wala hawakusita kuliangalia bunge kwa mtarajio ya kusikia fikra mpya, zilizotitia kwa maono, kujiamini na kuongoza.
Miaka 50 iliyopita hatukuwahi kuwa na bunge au baraza la mawaziri lililosheheni vijana kuliko miaka 8 iliyopita. Hali ni hiyo katika mashirika na taasisi.
Matumaini yakaanza kujengwa kwa muonekano wa vijana wachache waliosimama kutete nchi na taifa. Hao wakapewa heshima na kila walipotokea walipata mapokezi ya matumaini na furaha.
Kila kijana akitia chumvi ya ujana kwa kujinasabisha na hao wachache
Tukaanza kuwaona wazee kama watu wasiohitajika katika taifa hili.
Tuliwaona kama maadui walioturudisha nyuma, wasio na elimu,weledi na waliojaa inda na fitna.
Pengine bila kujua, Watanzania tumependelewa na mwenyezi mungu.
Kuna mambo yanayokuja kwa sababu maalumu kutusaidia.
Hili la ujana na uongozi ni mojawapo.
Hatuwezi kuona tahadhari kwasababu sisi ni wanadamu, mara nyingi hatujitambui na tunaongozwa na fikra zetu zaidi hata pale hekima inapotaka kuchukua nafasi yake.
Sote tumejikita kutafuta majina ya na umri ili kuliongoza taifa hili siku zijazo.
Tumejaza ujinga eti wazee wamechoka nasi twaitika 'ndiyo'
Leo kila kijana anatamani kuchukua fomu ili aelekee katika kasri la magogoni kuliongoza taifa hili. Shughuli za kuhonga boda boda, kugawa vitenge na kofia zinapamba moto.
Tumefumba macho na kusema hiki ni kizazi kipya, kile cha dijitali na bongoflavor.
Kama tulivyosema awali, vijana wa leo wana degree za kutosha, wamefunguka 'exposure' wanaifahamu dunia, ni wazuri wa kutumia teknolojia na ni mahiri kuchangamana na jamii.
Endapo hayo ndiyo tunaona ni vigezo vya uongozi wa nchi hii, hewala na iwe.
Kama tunataka kukimbia ili kuwafikia wenzetu lazima tuziangalie hekima za mwenyezi mungu.
Hekima hizo ni hizi zinazoendelea sasa katika bunge la katiba.
Bunge lililosheheni vijana na ujana, wa kike na kiume, mabinti na wabwanga.
Swali la kujiuliza, je ule ujana, maono,nguvu na uongozi unaonekana?
Wale tunaoambiwa wataliongoza taifa hili kuanzia Urais hadi ukuu wa wilaya wana sifa za ujana tunazoimba kila siku?
Hebu tuangalie kwa uchache, huu ujana,katiba mpya na uongozi kama vinakidhi haja ya ujana.
Tuwaangalie hao waliopo Dodoma ili kujiridhisha kuwa umri wa ujana unalisaidia taifa hili na tunahitaji vijana zaidi.
Vijana walioko Dodoma, je ni fahari au ni aibu ya taifa? Tunawategemea kwa lipi?
Je, ni wakweli wa mioyo na dhamira au ni mavuvuzela.
Je, wanauchungu na taifa hili au uchungu na matumbo yao kupitia mirija ya vyama vya siasa?
Wale walioko nje kama akina Nape wanatofuati gani na akina Mbatia, Kangi,Halima Mdee au Mwigulu? Wanaduru tuwaangalie vijana bila hila au hiana. Tutawaaalika mmoja baada ya mwingine waje hapa tuhangaike nao.
Hutwezi kuambiwa January wakati January wa mitaani si yule wa Dodoma!!
Kwanini tuwanyanyapaa wazee wanao ona zaidi ya lundo la vijana wasio na macho au masikio?
Itaendelea sehemu ya 2 kabla hatujasemezana.