Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #21
Mkubwa, hawa vijana wanatumia neno hilo kwasababu kuu mbiliMimi ninatatizwa na jambo moja na namuomba yeyote yule anayejua anipe timeline; uzee unaanzia wapi na ujana unamalizikia wapi? Je kama Muungano wetu huu wa serikali mbili ungechukua umbo la kibinadamu, kwa umri huu wa miaka 50, ungekuwa bado Muungano kijana au mzee? Kwa nini nauliza hivi? Ni kwa sababu hawa tunaowaita vijana, wengi wao hawajafikisha miaka hiyo kiumri na hawakuwahi kuishi nje ya huu Muungano. Hii ina maana gani? Ina maana kwamba vijana hawa wamezaliwa baada ya 1964 au kwa maneno mengine wamezaliwa ndani ya Muungano wa serikali mbili na kwa msingi huo hawajawahi kuonja maisha nje ya huu Muungano feki!
Hawa vijana wakati wanazaliwa kero za Muungano wa serikali mbili walizikuta, wakati wanakua kero zilikuwapo, wakati wanasoma matatizo yalikuwapo na sasa wakati wanakaribia kutoka ujanani matatizo yameendelea kuwapo. Mwanzoni, pamoja na kuwa na serikali mbili ndani ya nchi moja, matatizo yalikuwapo lakini siku zilivyosogea matatizo yalizidi kuongezeka na hadi sasa tunazo serikali mbili ndani ya nchi mbili. Hali hii inaashiria nini? Inashiria kwamba ufa wa utengano kama taifa moja unazidi kupanuka. Zamani ulihitaji tu kupiga hatua moja kuvuka kamtaro kutoka bara hadi visiwani, siku hizi unahitaji kuota mbawa uweze kuruka bahari kufika ng'ambo ya pili.
Hawa vijana wakati wanazaliwa, waliwakuta wazee wao wakitoa ahadi za kuzimaliza kero za Muungano na sasa wakiwa wanakaribia kuupa kisogo ujana, na wao sasa wanatoa ahadi hizo hizo. Wengine wao wameshavuka hata umri wa wazazi wao wakati Muungano wa serikali mbili unazaliwa...Mwalimu Nyerere alikuwa na miaka 42! Halafu, bila hata aibu, eti wanadai serikali tatu itavunja muungano! Hii dhana potofu wanaitoa wapi? Cha ajabu ni kwamba hapa wako pamoja na wale wale wazee wao walioshindwa kwa miaka 50 kutatua kero za Muungano na wameamua kuwaunga mkono! Hapa tusidanganyane hawa vijana kawalitakii mema taifa hili!
Nakumbuka mwanzoni mwa 1990, wakati upepo wa magaeuzi ulipotua Tanzania, wimbo na msimamo wa chama tawala ullikuwa huo huo; mfumo wa vyama vingi utaleta vita na kulisambaratisha taifa! Vipindi vya redio na TV vilikuwa na ajenda moja tu, kuwaogopesha wananchi kuwa vyama vingi vitatuingiza kwenye hatari ya vita! Picha na habari zilizooneshwa zilikuwa za nchi zilizo vitani! Bila Mwalimu kuwakemea CCM, sijui hali ingekuwaje. Leo miaka ishirini baadaye...mchezo uleule, mbinu zile zile, njama zile zile, ujinga ule ule... my God! Hata aibu hawana hawa jamaa. Muungano kama ulivyo umegota kwenye lindi la tope...njia ya kujikwamua ni kugeuza njia, nothing less!
Swali kwa vijana, je hapa tulipofikia, mfumo wa serikali mbili utaudumishaje Muungano? Kwa kumdhalilisha Mh. Jaji Warioba? Kwa kupuuzia maoni ya wananchi kupitia Tume? Mbona huko ni kujidanganya! Kwa risasi na mabomu? Nasikia kuna mpango wa kanuni kubadilishwa kwa kuondoa kipengele cha maamuzi kupitia theluthi mbili na kuwa tu wengi wape hata kama ni asilimia 50.1%! Juzi tu tumevua nguo kwa kuweka rekodi mpya ya kutumia kura ya aina mbili, ya wazi na siri, na sasa tunataka kuweka rekodi nyingine duniani kwa kupitisha katiba ya nchi kwa kura chini ya theluthi mbili! Huo ndio msimamo CCM kama chama unaoungwa mkono na eti Vijana wake!
Vijana wa CCM, je mnataka na nyie siku zenu zikifika muwaachie watoto wenu hizo kero za Muungano kama mlivyoachiwa na babu zao?
1. Kuwavutia vijana wenzao wasio na bahati ya kuona kule wanakokuona
2. Hawana fikra za namna nyingine za kujenga hoja bila kutumia ujana.
Vijana hao ambao umri wao hatuufahamu ni kuanzia wapi na kuishia wapi, ndio wanakalishwa kitako na akina Pinda wakiambiwa Tanganyika ipi inayotakiwa, ya mkoloni, wakati wa kupigania uhuru au baada ya uhuru. Eti wanaambiwa kulikuwa na evolution ya Tanganyika.
Na kwa kujua kuwa hawana uwezo wa kujenga hoja, Pinda kawaita na kuwaambia wafunge vinywa vyao. Nao kwavile ni watu wasiojua wanataka nini , wote across the board wakafungia degree zao za ubachela, master and baster, PhD na kumsikiliza yule mtu ambaye hajui Tanganyika ipi ingawa cheti chake cha kuzaliwa ni cha Tanganyika
Kama ulivyosema, hao vijana wapo sambamba na wazee waliosemwa wamechoka tena wazee hao wakiwapeleka mputa.Wamefungwa bendeji za kusema na pale wanaporuhusiwa wameshauriwa wazungumzie matusi kama akina Nchemba.
Vijana hao wametuingiza katika aibu ya dunia. Leo John Mnyika anakubali kuwe na kura ya wazi na siri.
Anaambiwa kura hiyo ilitumika mwaka 1962 wakati huo nchi ikiitwa Tanganyika. Halafu wazee hao inaosemekana wamechoka wanarudi upande wa pili na kuwaambia Tanganyika haikuwepo wakati wanazaliwa.Kama haikuwepo na kura ya wazi haikuwepo inakuwaje ukubali kitu kimoja kingine ikikane?
Vijana hao wameshindwa kujua tofauti ya mkataba na hati ya mkataba. Wameletewa karatasi za kughushi na Mzee Samwel Sitta, wakajua ni za kughushi na bado wakamuacha tu aendelee kuwadanganya.
Eti wanatumia kisingizo cha taifa na nchi kwanza. Hiyo ndiyo hoja ja James Mbatia siku zote.
Ni james huyo ndiye aliyeongoza kampeni ya OMO alipokuwa UDSM.
Leo amesahau utaifa ule kwasababu kamegewa keki ya kuteuliwa.
Ni utaifa gani unaotekelezwa na upande mmoja?
Msekwa kasema saini si yake. Vijana hawashtuki kuwa hilo ni kosa la kisheria na kimaadili. Wamekaa kimya mambo yakiharibika. Wamekumbatia UCCM na Uchadema, UCUF na uTLP bila kujua vyama ni majina nchi ipo hata bila ya vyama.
Vijana wanaaminishwa kwa dhati kuwa mfumo wa serikali mbili ulioshindwa miaka 50 sasa umeapatiwa dawa kutoka Milpark hospital.
Kwamba, kufumba na kufumbua tatizo la muungano litakuwa limekwaisha.
Wameshindwa kutambua kuwa serikali inayotaka kumaliza kero kwa serikali 2 iliyoshindwa miaka 50 ndio hiyo iliytoshindwa kutatua tatizo la umeme kwa miaka 8.
Woga umewajaa, wamepoteza intellect, fikra zao zimejikita kumsubiri Kikwete aje kumsumanga Warioba huku wakilipuka kwa nderemo na vifijo.
Kesho,wanarudi mitaani wakiwa na logo yao ya ujana. Ahadi za kuleta maendeleo, kununua boda boda na udhaifu mwingine kama huo. Tunaambiwa ni wakati wao.
Hapo Dodoma wapo wakibadilishana CD za bongoflavor na Bongo Movie. Hwajui wapi wapate taarifa na tafiti. Tunawasikia wazee akina Lipumba wakilipuka kwa takwimu.
Vijana wetu wanaambiwa hakuna sample ya watu elfu 20, wanalipuka kwa makofi.
Hii dhana ya ujana sasa imefika mwisho. Tunasema, wakija kutomba kura waje kama wachawi au wanga. Wakija na neno ujana tutahamasisha wavurushwe kwa mayai viza.
Vijana wana maono, nia na dhamira. Vijana wanaongoza siyo hawa chui na fisi tunaowaona Dodoma.