maguzu masese
JF-Expert Member
- Jan 22, 2013
- 283
- 139
Bila ya Azimio la Arusha madini ungeyakuta. Kuna mambo mengi yaliofanya madini uyakute. Moja ya ni technologia. Nikiwa shule ramani ya Tanzania ilionyesha sehemu nyingi zenye madini. Lakini sababu kubwa iliyosababisha kuto-extract rasilimali hiyo ilikuwa ni initial investment costs. Hata serikali ilijaribu wakati wa Nyerere lakini costs were prohibitive.
Miaka ya karibuni maendeleo ya kitechnologia na kuibuka kwa China kumefanya mambo mengi kuwezekana. Hivyo kusifu Azimio la Arusha wakati kulikuwa na pingamizi la kimitaji na kitechnologia itakuwa tunapoteza hoja.
Kuhusiana na Azimio la Arusha, ukweli wa mambo sio lazima litumike hili mambo mazuri yafanyike. Nimelisoma na sioni kitu chochote kipya au cha ajabu. Unaweza kulitumia kujipatia umaarufu wa kisiasa kwa umma masikini. Lakini huwezi kulitumia kama msingi wa kuwasaidia masikini wenyewe.
Azimio la Arusha ilikuwa ni kazi ya mtu mmoja. Lilikuja kama amri za Mungu zilizoletwa na Nabii Musa pale alivyotelemka kutoka kwenye mlima Sinai. Watanzania hawakuwa na mchango wowote. Hivyo kuwapa watanzania ownership ya kitu ambacho sio chao si kuwatendea haki. Azimio la Arusha ni mali ya chama cha mapinduzi, libakie huko huko lilipo.
Kama unaliona linafaa unaweza kulifuata. Unaweza kufuata miiko yake. Unaweza kujenga vijiji vya ujamaa na kuishi huko. Kama utafanikiwa tutakufuata.
Kuhusiana na ujenzi wa taifa. Umefika wakati mnaolipenda Azimio la Arusha, kukubali kuwa kuna watu hatuliamini Azimio hilo kama msingi wa maendeleo na tuna haki zetu za kikatiba. Pili nchi inaongozwa kwa kutumia katiba na sheria za nchi. Azimio la Arusha sio sehemu ya katiba au sheria ya nchi. Ulikuwa ni mwongozo wa TANU na CCM. Tusio wanachama wa CCM mwongozo huo hautuhusu.
Kuna kitu unaki miss ktk Uchangiaji wangu, Kama ukinielewa nadhani tunaweza kwenda sawa. Sipo kutetea azimio la Arusha kwa maana ya kwamba tunapaswa kurudi na kulitumia, Bali nipo kulitetea azimio la Arusha kwa maana ya kwamba, mabadiliko ya mifumo mingi ktk Taifa letu yalipashwa kujengwa ktk misingi ya azimio la Arusha kisha tukaenda nadhani tungekuwa pazuri sana na huenda utendaji kazi mbovu wa serikali ya sasa usingekuwepo.
Tofauti na Kukuta madini, Suala la kutokuwepo kwa ukabila mbona hujagusia kuwa ni zao la azimio la Arusha? Kumbuka pia kuwa Ardhi ambayo Leo hii hata masikini kabisa nchi hii anaweza kuimiliki ni zao la azimio la Arusha, bila hivyo Leo hii Ardhi yote nchi hii ingekuwa inamilikiwa na vigogo, mfano mzuri ni Kenya, angalia Ardhi inamilikiwa na kina nani?, Zimbabwe Leo hii Mugabe anachukuwa na Magharibi kisa ni Ardhi. Acha hiyo, Kiswahili je? I wish ungejua thamani Yake ambayo sisi tunaichukulia poa tu.
Ukisema azimio la Arusha ni kazi ya mtu mmoja ni kweli, lakini tambua kwamba kuwa kazi ya mtu mmoja sio sababu hasa ya kufanya jambo kuwa baya, nikukumbushe tu kuwa hata hii siasa na mifumo yote ni kazi ya mtu mmoja mmoja na muendelezo wake ulianzia kwa huyo mtu mmoja kwa kuchambua Udhaifu na uimara na kisha kuja na kizuri zaidi kulingana na mabadiliko ya mazingira na nyakati
Mfano, Katiba ya Marekani, Katiba yeye Democrasia kuliko zote( kwa sasa na kwa tafsiri ya Democrasia ) ni kazi ya mtu mmoja ' Thomas Jefferson '.Pia alitumia kazi ya mtu mmoja John Locke ( hivyo suala la mtu mmoja sio Tatizo)
Ukisema umelisoma na huoni kitu Kipya , ni kweli inawezekana, lakini haijalishi ulichosoma, Bali ulichosoma na kutafakari .
Point yangu kubwa ni kwamba, Kuna vitu vingi sana tulikurupuka katika Taifa hili, na ninapojaribu kuhusisha azimio la Arusha ni kwa maana ya kwamba, Mabaya ktk Taifa letu hivi sasa, ( huenda) hata tusingekuwa nayo endapo misingi ya ujenzi wa Taifa letu ingeanzia ktk azimio la Arusha,( this is what I think, na sitaki kulazimisha Maoni yangu yawe kweli, Bali napokea Maoni tofauti na kuyafanyia kazi pia). Na Kama Leo hii Taifa letu lingekuwa pazuri zaidi kuliko Enzi ya azimio la Arusha, hakuna Mtanzania angewaza kuhusu azimio la Arusha tena ( tunalazimika ku kumbuka kutokana na kuwa kwa sasa tulipo ni pabaya kuliko kule nyuma Enzi za azimio la Arusha ), Kabla ya kuyumba kwa serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa ccm kwa miaka mingi, hakuna aliyekuwa anawaza kuhusu azimio la Arusha.
Nadhani kidogo utakuwa umenielewa sasa.