E fm yazidi kuwafunika Clouds fm


Mkuu kidogo wewe umechangia bila kuonyesha mihemko yako binafsi...napenda sana jinsi ulivyochambua hivyo vipindi pamoja na wahusika wake,niko mkoani sijawahi kuisikiliza hii radio E-FM ila majina ya vipindi tu jinsi yalivyo umenishawishi namimi niwasikilize nione kama yaliyomo yamo kweli au laah....ebu tusaidie na mida ya vipindi vyao bhasi ili niwasikilize kwenye tunein app
 
Tunaipata Efm kupitia kisimbusi cha Azam.....so haipatikani dar pekee
 
Kweli za kuambiwa changanya na zako, hivi kweli Clouds uifananishe na E.fm kweli ??? Labda kama mnaongelea kuja kwa kasi lakini si kuifikia Clouds hata kidogo. Ni kweli Clouds wanamapungufu yao kama zilivyo Redio zote TZ kama si Dunia nzima, hasa linapokuja swala la matangazo ni too much,ni kama walivyo E.fm kuwa na muda mreeeeeeeefu wakiongelea michezo. ( sio watu wengi wanapenda hivyo) Clouds kwa sasa inasikika karibia nchi nzima,wakati hiyo E.fm ni Dar tu.
 
Hao Efm nao wamekariri dar tu huku mikoani hapana wananiboa sana
 
Clouds ni bado redio yenye jina kubwa, ila ukiskilza Efm unajua ni redio iloyo kikazi zaid
Na hasa department ya michezo kina Maulod wana piga kaz
Mi naikubal sana Efm kwa kweli
Choice toka waingie kwenye kiswahili kama siwaelewi hivi
 
Clouds ni bado redio yenye jina kubwa, ila ukiskilza Efm unajua ni redio iliyo kikazi zaid
Na hasa department ya michezo kina Maulid wana piga kaz
Mi naikubal sana Efm kwa kweli
Choice toka waingie kwenye kiswahili kama siwaelewi hivi
 
Ratiba ya monday to friday hii
Joto la asubuhi saa 12 asubuhi hadi saa 3 asubuhi ( gerad hando, p.j na adeliya)

Sports headquaters saa 3 asubuhi hadi 6 mchana(kitenge, oscar, sudy, maestro, musa, omary, tunu)

Uhondo saa 6 mchana hadi saa tisa mchana( dina, swebe, bi hindu)

Ladha 3600 saa tisa hadi saa 10 jioni (jabir saleh)

Ubaoni saa 10 jioni hadi saa moja ucku (emma, mpoki, bikra wa kisukuma)

E Sports saa moja ucku hadi saa mbili ucku (omary katanga, ibrahimu masoud "maestro", maulid kitenge, tunu hassan, musa n soudy)

Genge saa mbili hadi 5 (kicheko) hapa ndo zinapigwa sana visingeli

Weekend uwa sikilizagi sana radio ila kuna vipindi km old skullz jam, muda wetu, afro bet
E.Sports saa moja ucku hadi saa mbili jumamoc n jumapili ipo pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…