E fm yazidi kuwafunika Clouds fm

E fm yazidi kuwafunika Clouds fm

Nakubaliana na hoja me n msikilizaji wa radio zote e.fm wanafanya vizuri hata ukilinganisha vipindi clouds washapigwa gap
Power breafast vs Joto la asubuhi > p.b cku izi ina imeopooza ngoja j'3 tutaona joto la asubuhi itakuaje

Leo tena vs Uhondo > leo tena ya sasa sio km ya zaman yule da huu, mus na jose mara hamna wanchofanya zaidi ya kuongea umbeya, n uteam uhondo hata mpangilio vitu unavyosiki vimepangiga dina n swebe wanafanya vizuri

Jahazi vs Ubaoni > jahazi kimebaki kipindi cha matangazo na kupeana salama mda mrefu n bora hata usikilize ubaoni utojuta n utafurahi

Sports xtra/roundup vs Sports headquaters hapa clouds ndo wameachwa mbali wakina shafii wamebaki kutoa habari za goal.com kwny uchambuzi yule alex na wakina issa maeda hamna kitu, mbwiga anapiga kelele tu na ukija e.fm unasikiliza michezo n uchambuzi hadi unafurahi uku oscar ocar, ibrahim masoud "maestro", tunu hassan, kitenge maulid, suddy mkumbo, musa mwakisu. Yusuphmkule uwezi kuona gap hata mmoja asipokuwepo

Clouds wamebakiwa n xxl na amplifier tu ndo vipindi wanaweza kujivuniA

Mkuu kidogo wewe umechangia bila kuonyesha mihemko yako binafsi...napenda sana jinsi ulivyochambua hivyo vipindi pamoja na wahusika wake,niko mkoani sijawahi kuisikiliza hii radio E-FM ila majina ya vipindi tu jinsi yalivyo umenishawishi namimi niwasikilize nione kama yaliyomo yamo kweli au laah....ebu tusaidie na mida ya vipindi vyao bhasi ili niwasikilize kwenye tunein app
 
Katika hali ya kustaajabisha ni kwamba redio mpya tena ina miaka miwili tu tangu ianzishwe na inakamata mkoa mmoja tu(DSM),inazidi kubamba na kupaa kila kukicha kiasi kwamba imezifunika redio kongwe zote,hadi Clouds fm ambayo ndio redio inayosumbua kwa hapa Tz inafunikwa na redio ndogo tu (E fm),kama unabisha basi wewe una lako ila kwa hapa DSM habari niE fm tu kila kona.na ndio maana clouds wameamua kuibadilisha ile redio yao ya Choice fm(102.5).wameamua kuiharibu hiyo redio na kuifanya iwe kama E fm ila haiwezekani,kwa wanaoijua choice fm ilivokuwa mwanzo na sasa watanielewa ninachomaanisha.soon tutaisikia clouds nao wanaanzisha vipindi vya miziki ya minanda na miduara,tusubiri kuona clouds ikiendelea kuongeza watangazaji kila siku
Tunaipata Efm kupitia kisimbusi cha Azam.....so haipatikani dar pekee
 
Kweli za kuambiwa changanya na zako, hivi kweli Clouds uifananishe na E.fm kweli ??? Labda kama mnaongelea kuja kwa kasi lakini si kuifikia Clouds hata kidogo. Ni kweli Clouds wanamapungufu yao kama zilivyo Redio zote TZ kama si Dunia nzima, hasa linapokuja swala la matangazo ni too much,ni kama walivyo E.fm kuwa na muda mreeeeeeeefu wakiongelea michezo. ( sio watu wengi wanapenda hivyo) Clouds kwa sasa inasikika karibia nchi nzima,wakati hiyo E.fm ni Dar tu.
 
Clouds ni bado redio yenye jina kubwa, ila ukiskilza Efm unajua ni redio iloyo kikazi zaid
Na hasa department ya michezo kina Maulod wana piga kaz
Mi naikubal sana Efm kwa kweli
Choice toka waingie kwenye kiswahili kama siwaelewi hivi
 
Clouds ni bado redio yenye jina kubwa, ila ukiskilza Efm unajua ni redio iliyo kikazi zaid
Na hasa department ya michezo kina Maulid wana piga kaz
Mi naikubal sana Efm kwa kweli
Choice toka waingie kwenye kiswahili kama siwaelewi hivi
 
Mkuu kidogo wewe umechangia bila kuonyesha mihemko yako binafsi...napenda sana jinsi ulivyochambua hivyo vipindi pamoja na wahusika wake,niko mkoani sijawahi kuisikiliza hii radio E-FM ila majina ya vipindi tu jinsi yalivyo umenishawishi namimi niwasikilize nione kama yaliyomo yamo kweli au laah....ebu tusaidie na mida ya vipindi vyao bhasi ili niwasikilize kwenye tunein app
Ratiba ya monday to friday hii
Joto la asubuhi saa 12 asubuhi hadi saa 3 asubuhi ( gerad hando, p.j na adeliya)

Sports headquaters saa 3 asubuhi hadi 6 mchana(kitenge, oscar, sudy, maestro, musa, omary, tunu)

Uhondo saa 6 mchana hadi saa tisa mchana( dina, swebe, bi hindu)

Ladha 3600 saa tisa hadi saa 10 jioni (jabir saleh)

Ubaoni saa 10 jioni hadi saa moja ucku (emma, mpoki, bikra wa kisukuma)

E Sports saa moja ucku hadi saa mbili ucku (omary katanga, ibrahimu masoud "maestro", maulid kitenge, tunu hassan, musa n soudy)

Genge saa mbili hadi 5 (kicheko) hapa ndo zinapigwa sana visingeli

Weekend uwa sikilizagi sana radio ila kuna vipindi km old skullz jam, muda wetu, afro bet
E.Sports saa moja ucku hadi saa mbili jumamoc n jumapili ipo pia
 
Back
Top Bottom