e-GA inahujumiwa

Ukipewa ajira unaanza kuruka ruka, unaongea kwasababu haupo ndani ya mfumo wa ajira. Mapungufu ya hii serikali yetu ni budget ndogo, 10%. Watendaji au Wafanyakazi wapo vizuri sana tena sana kuliko nyie wapiga zumari wa mitandaoni.
 
Hapa umeeleweka mkuu. Basi,wanaojua kuchakachua wamefanya yao.
 
Yule mama Wakudadavua X-Chadema jamani yupo atakuwa na watoto wangapi Sasa X-Nàibu Waziri
Duu kuwa uyaone Dunia Duara
 
Hujui unachokiongea?
yaani kisa ni NMB msign kuipa billions of money kutengeneza mifumo ambayo tayari ipo serikalini?
ESB ipo up and running pale e-GA ,unataka kutengeneza nyingine ili ugundue nini?
watu wanapiga hela mnaendekeza unazi
Serikali na Bank nani anafanya vetting ya kutisha?

Umewahi fanya kazi Bank?

Unazijua Internal control za mabenki?

Mkuu tumia akili ,Hivi hayo mabilioni ya fedha za serikali si yanakaa NMB na CRDB unadhani wana mifumo dhaifu?
 
Kwani,kama ni open tender, na NMB ina watu wanaoweza kufanya hiyo kazi, tatizo lipo wapi?
Kama unadai issue ya taarifa nyeti, nani hawezi kuzifikia kama ni successful bidder(aliyeshinda tender)! Au unadhani kila developper anaweza kufanya hiyo kazi?
Tatizo NMB si taasisi ya teknolojia iliyo rasmi kwa mkataba waliosaini. Leseni yao ni kuuza fedha.

Huwezi kusema kwa kuwa huyu ni daktari akapasue moyo. Kuna madaktari wengine ni wa vinywa tu. Atatuua.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Aiseee, ndo zinachepushwaje hizo hela za manunuzi ya umeme?
 
Sasa mnataka mtengeneze mifumo ya fedha kwa kutumia open source application ambazo usalama wake ni tia maji,
Mnadhani kwa vile unajua kutengeneza basi, kila kitu kinawezekana kama vile ulivyofanya project yako ya chuo
NMB ni taasisi binafsi je usalama wa serkali mtandao unalindwa kwa namna gani? Issue si ujuzi kama hakuna wataalam serkali si ikasomeshe watu wa ndani?. NMB anapokuja unadhani wataalam ni hawa akina Mwaipopo? Ni watu wa nje ambao ndio watatengeneza hiyo mifumo kupitia tenda ya serkali na taasisi hiyo. Ovyo kabisa
 
Wanahisa wengine wakiwemo watu binafsi na makampuni/mashirik yao.... 🤔
Sioni shida

Core business ya eGA siyo development ya mifumo

Yeye ni regulator

What we need ni strong regulation and protection ha mifumo inayotengenezwa
 
Sioni shida

Core business ya eGA siyo development ya mifumo

Yeye ni regulator

What we need ni strong regulation and protection ha mifumo inayotengenezwa
Nilikuwa namtaarifu Ivan Stepanov #11 aliyehoji 60% inamilikiwa na nani kama Serikali ina 40%.
Otherwise, wataalamu wa IT serikalini ni shida. Ndio maana mifumo yote ya Serikali iliyowahi kubuniwa na iliyopo haifanyi kazi kwa viwango....
Angalau mabenki kwenye IT yanajitahidi Lakini haiwezi kuhalalisha NMB kufanya kazi zisizowahusu. Single source hii haiwezi kuwa tofauti na ile ya ujenzi wa reli ya SGR.
 
Sasa huyo GEPS unauona ni mfumo wa maana sana? Unahitaji exposure sana.
Mfumo kama 3 year project ya watoto wa chuo
Unajua unacho kiongea Bro? Sometimes bora kukaa,kimya mfumo unaopitisha matilion ya shillingi ufananishe na mfumo wa final Yr project ya mwanafunzi wa chuo......?

Halafu sio GEPS ni GEPG.
 
Share holders wa NMB ni nani? Je Serikali haipo? na kama ipo huu uzi ni void!! Futa fasta kulinda heshima yako.
 
Tanzania Inachezewa Sana Na Viongozi Wanafanya Makisudi Haya Yote
 
Bora utengeneze mifumo ya kuunga unga kupitia watu wako ambao watakua kidogo kidogo,kuliko kutumia mifumo ya nje, kwani hujui usalama wa data zako.Makampuni mengi makubwa serikali zao zina backdoor kwenye hizo taasisi,so wakitaka kutindua wana tindua. Dunia hii ya sada information/data ni power,so huwezi kumpa mtu data zako akuhifazie ambaye,humjui,haujamfanyia vetting, wala ambaye hajala kiapo.

Wewe unafikiri hayo makampuni makubwa yalianza na kukimbia ghafla?Si walianza kwa kukaa,then wakasimama,wakatembea then wakakimbia. Wewe jiulize kwa nini Kompyuta ya kwanza ilikuwa kama kabati,je walishwa kutengeneza kama hizi tulizo nazo sasa?

Hivi unazania huko Kenya kwenye hayo makampuni makubwa ya IT,ambao wamefungua ofisi, unazani serikali imehost au kuiweka hiyo mifumo yao kwenye platforms zao? Ukiiona serikali imehost service kwenye hizo platforms, jua huo mfumo sio critical. Huwezi kuweka mfumo ambao ni critical kwenye clouds na hamna serikalini yoyote duniani inayofanya hivyo. Kenya wana taasisi yao kama eGa kwa ajili ya mifumo yao critical na watu wanayo itengeneza wamewafanyia vetting, wamewaapisha na still wanawafuatilia.

Msifanye masihala na taarifa nyeti za serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…