Bora utengeneze mifumo ya kuunga unga kupitia watu wako ambao watakua kidogo kidogo,kuliko kutumia mifumo ya nje, kwani hujui usalama wa data zako.Makampuni mengi makubwa serikali zao zina backdoor kwenye hizo taasisi,so wakitaka kutindua wana tindua. Dunia hii ya sada information/data ni power,so huwezi kumpa mtu data zako akuhifazie ambaye,humjui,haujamfanyia vetting, wala ambaye hajala kiapo.
Wewe unafikiri hayo makampuni makubwa yalianza na kukimbia ghafla?Si walianza kwa kukaa,then wakasimama,wakatembea then wakakimbia. Wewe jiulize kwa nini Kompyuta ya kwanza ilikuwa kama kabati,je walishwa kutengeneza kama hizi tulizo nazo sasa?
Hivi unazania huko Kenya kwenye hayo makampuni makubwa ya IT,ambao wamefungua ofisi, unazani serikali imehost au kuiweka hiyo mifumo yao kwenye platforms zao? Ukiiona serikali imehost service kwenye hizo platforms, jua huo mfumo sio critical. Huwezi kuweka mfumo ambao ni critical kwenye clouds na hamna serikalini yoyote duniani inayofanya hivyo. Kenya wana taasisi yao kama eGa kwa ajili ya mifumo yao critical na watu wanayo itengeneza wamewafanyia vetting, wamewaapisha na still wanawafuatilia.
Msifanye masihala na taarifa nyeti za serikali.