Napongeza marekebisho yanayofanywa na TRA kwenye ukusanyaji wa mapato kwa kutumia njia za kielektroniki. Mabadiliko hayo ni pamoja na mfumo mpya wa kuwasilisha ritani za VAT ambapo mfumo ulioboreshwa na kuanza kutumika kwa mwezi machi 2022 una changamoto kubwa. Kwamba kawaida risiti inayotambulika kwa ajili ya ritani za VAT inapaswa kuwekwa jina, TIN na VRN za mnunuzi. Ni utaratibu ambao tumeutumia kwa kipindi chote cha nyuma kujaza ritani. Sasa baada ya mfumo mpya kuanza kwa ritani za machi 2022 kama risiti iliwekwa jina,TIN na VRN lkn muuzaji akawekwa nafasi au mkato wakati wa kuandika kwenye EFD, mfumo mpya unazikataa. Yaani kuandika kama wao TRA wanavyoandika kwenye TIN au VRN certificate sasa ni kosa!!! Kwanini wasitoa elimu ya kutosha kuhusu jambo hili? Au ni mkakati wa makusudi ili tulipishwe fine??