EACOP Tanga: Ghati la Mafuta Lazingatia Mazingira

EACOP Tanga: Ghati la Mafuta Lazingatia Mazingira

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911

Dkt. MABULA: Ujenzi wa ghati kwenye Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) Mkoani Tanga umezingatia uhifadhi wa mazingira ya bahari na viumbe hai

Mradi wa EACOP umejenga ghati (jetty) la urefu wa takribani kilomita 2 Chongoleani, Tanga, Tanzania.

Katika maelezo yake Dkt. Makemie Mabula mtaalamu wa mazingira ya Bahari wa mradi huo amesema kuwa ghati hilo ni muundombinu muhimu wa kuhifadhi na kupakia mafuta ghafi kwenye meli na kwamba, wakati wa kubuni na ujenzi, mradi umezingatia viwango vya kimataifa (kama IFC Performance Standards) ili kupunguza athari kwa bahari, matumbawe, samaki, mikoko, nyasi bahari na viumbe hai vingine vilivyopo baharini.

Pia, ameeleza kuwa wanawatalamu waliobobea ambao wametumia teknolojia ya kisasa kuhakisha hakuna umwagikaji wa mafuta kwenye eneo la bahari.

Pia, ameeleza kuwa mradi unatekelezwa kwa ufanisi mkubwa na hakuna hatari ya kimazingira iliyojitokeza na mmea ya baharini iliyoondolewa wakati wa ujenzi wa ghati inaendelea kurejeshwa ili kulinda mazingira ya bahari.
 
Back
Top Bottom