Unregistered said:
Udikteta maradufu
Hutaki wazanzibari watoe maoni yao? Kutoa maoni sio kukana uraia. Hilo ni dhana laki zuzu kabisa.
Zanzibar, COMESA, SADAC na EAF
Kwa zaidi ya miongo mitatu, Zanzibar imekuwa chini ya minyororo ya watanganyika. Kwakweli hili si swala laku puuzwa bila kulitazama kwa maakini. Kuna maswali kadha ya kujibiwa:
1. Zanzibar imenyanyaswa vipi?
2. Zanzibar inahaki yaku jiunga na makundi kama SADAC/COMESA n.k.
3. Zanzibar inapaswa kuwa pamoja na Tanganyika katika shirikisho la Afrika Mashariki
4. Uaamuzi ni wa wazanzibari
Zanzibar Imenyanyaswa Vipi
Baada ya kunyonya mali ghafi ya Zanzibar, walafi na mabaradhuli toka bara sasa wana tuchukulia hivi hivi! Karafuu ya Zanzibar, kwa zaidi ya miaka 30 imeisaidia kuinua uchumi wa Tanganyika uliokuwa matatani kwa shauri ya serere holela za chama tawala (Ujamaa). Leo wazanzibari walo amua kukimbilia nchi kama Oman, UAE (kwajumla Umangani) na hata Ulaya na marekani wameweza kuji mudu na kwakweli wana uwezo waki fedha. Hizo hela wanazituma mara baada ya mara ilikuwasaidia ndugu jamaa na marafiki. Wanaipa TRA nafasi yaku toza ushuru za uwongo na kweli!
Kweli tulidanganywa kabisa kujumuika na mahayawani walio nyonya mali ghafi ya Zanzibar! Laiti Zanzibar ingelikuwa peke yake leo tusingalikuwa namatatizo ya kiuchumi. Tume beba mzigo wa Tangayika na sasa wana taka kutupele SADAC! Jamaani tuna ukoo upi nahao wana SADAC wanao pigiwa debe kila kukicha? Lazima tuamke. Wazanzibari wote wajitokeze kwenye kikao hichi na waseme waziwazi hatutaki hiyo SADAC ukoo wetu ukaribu na wenzentu walo COMESA k.m. Misiri, Libya ambao wako COMESA. Pili wenzetu wako Kismayu (Somalia), Lamu, Siyu, Pate n.k. Hatutaki hiyo SADAC. Tumeikataa katukatu! Unyanysaji ni lazma ukome.
Zanzibar inahaki yaku jiunga na makundi kama SADAC/COMESA n.k.
Zanzibar ni mwana chama kamili wa Islamic Conference Organization (ICO), FIFA n.k. Zanzibar inahaki ya kujiunga na COMESA. Nimuhimu sana kwa waakilishi wetu wa upinzani na serekali waungane pamoja ilitulitatue swala hili la muhimu sana kwa wafanyi biashara Zanzibar. Miaka nenda miaka rudi tumekuwa tukizungumzia free port je hii free port ni yakuwanufaisha wa lafi toka Tanganyika? Unyanyasaji utakoma.
Zanzibar inapaswa kuwa pamoja na Tanganyika katika shirikisho la Afrika Mashariki
Tangayika itajiamulia yenyewe, Zanzibar siyo koloni ya Tanganyika. Matokeo ya kura yata onyeshwa waziwazi kwamba Wazanzibari wote wana tazama mashariki na watanganyika Kusini (Je kwa wale walo wahi kuishi umangani mwakumbuka ile riwaya ya mkusni?) Kwa hivyo si lazma tuwe pamoja. Hapo ndipo unyonyaji wa mali ghafi ya Zanzibar uta koma kabisa!
Uaamuzi ni wa wazanzibari
Haya yote, kama ilivyo desturi ya wazanzibari yata aamuliwa kupitia kura. Pasipo kuingiliwa kati na mahayawani big brother ukweli utajitokeza. Baada ya kura, Zanzibar itakuwa huru na unyanyasaji na unyonyaji wa mali ghafi utakoma!
Zanzibar itakuwa huru! Free at last
..