Capital hamna shida bro. Labor ni tatizo kwa kuwa hao jamaa ni vilaza tu. Hakuna ujuzi wanaoleta, waje wafundishe kiingereza watoto wetu kwa bei poa, hiyo labda. lakini hawana lolote jingine. Hatuhitaji mhasibu wa kuja kuhesabu hela hapa TZ, we can do it good. Kwenye sciences they are going to spoil our kids, nilisoma na wakenya na waganda..kichwani watupu. Na ninajua kwa nini! Kutandika vitanda, hata waTZ nadhani wanajua sana au watajua. Hizi nchi zote nimeshazitembelea, hizo huduma wanazosema wanajua, ni mtazamo. Nilshasubiri huduma kwenye vinchi vyao kama ninavyosubiri hapa Bongo, hamna lolote. Bongo hapa inategemea unakwenda wapi na management iko vipi, na kwao ni hivyo hivyo tu. Michosho tu, hakuna cha nini wala nini. Wasituletee njaa zao kwa ku-take advantage ya wala rushwa wa immigration. Lakini kitaeleweka, sisi tumeshika mpini. Na wewe Smatta unasema nini kuhusu kibaki, kile kikongwe kijizi cha urais, unadhani kinaweza dictate terms kuhusu Jamhuri ya Muungano? Au ni kujiliwaza tu. Nasikia Raila amepata mtindio wa ubongo, pole bwana. Nadhani ni stress ya kuibiwa kura na kibaki na kupokwa urais!
Ndugu zanguni, msiogope MCHAKATO WA hii EAC.
Katika mazingira yeyote yale TZ ndio tutawaongoza na ndio maana wanatulilia.
Kwanza nchi yetu ni kubwa kuliko zao.
Pili idadi yetu ni kubwa kuliko wao.
Tatu kisiasa tumejipanga vizuri zaidi kuliko wao.
Nne tunakubaliana sana wenyewe kwa wenyewe licha ya tofauti za makabila kuliko wao.
Tano sauti yetu ndio kubwa kuliko wao, angalia tulivyochelewesha mpango mzima mpaka hapa tulipo fikia kwani wao walitaka mambo yote yatokee kwa mwaka mmoja tu bila kupanga mikakati.
Sita, wanajua kuwa wao wanatuhitaji zaidi kuliko tunavyowahitaji hivyo ikiwa mambo yatakwenda mrama kwetu kuuvunja huo muungano ni jambo la siku moja tu. Tulishawahi kufanya hivyo si wageni wa hilo. Hii inawafanya wao wawe na tahadhari kabisa.
Saba tunaongoza katika hali ya hewa nzuri, ardhi nzuri katika kilimo, madini, misitu, maji (mito, maziwa, bahari) na hata watalii huongezeka kuja TZ mwaka hata mwaka huku Kenya iliyokuwa ikiongoza kwa watalii leo wanapungua. Sasa mnahitaji nini zaidi!
Hivyo napenda kuwatoeni wasi wasi kabisa kuwa mambo yatakuwa shwari. La msingi hapa ni kwa Watanzania kila mmoja wetu kuchukua nafasi kama kiongozi popote pale alipo. Uongozi, ninamaana kuwajibika na kuwa mstari wa mbele katika ubunifu na utendaji wa kazi ambao ndio utamuwezesha mtanzania kuwa na uchumi bora.
Kwa maneno mengine, pengine ningesema kuwa - kila mtanzania lazima aichukulie nafasi hii kama positive katika kukuza uchumi wake binafsi na kuacha kukaa vijiweni na kulalamika kuwa wanakuja kuchukua mali zetu, kwani wewe uko wapi? Huu ndio utandawazi hatuwezi kuuzuia, kilichopo ni kuvua nguo na kuogelea katika bahari hiyo.