Sasa haya ndiyo mmbo ya maana kuchangia, siyo mambo ya udini, ukabila ... mtu anayechangia mambo kama hayo ananyesha alivyofilisika ...
______________________
Hivi tujiulize sana kuna sababu gani kwetu sisi watanzania kuingia kwenye muungano huu?
Labda:
- Wananchi wetu watapata kazi huko kenya na uganda?
- Viwanda vyetu vitapata soko la bidhaa zake huko kwa wenzetu?
- Tutakuwa na uwezo wa kupata ardhi ya kulima huko kwa wenzetu?
- Je, tutakosa nini kwa kutokujiunga?
- Je, tutapata nini kwa kujiunga?
- Kwani sasa hivi tunakosa nini?
Katika kujibu maswali hayo, ni wajibu wa kila mtanzania kutafakari kwa undani (not superficially), akiangalia historia ya nchi hizi tatu.
Nitachangia kidogo, wengine mtanisaidia:
EAC iliyovunjika iliweka malengo kadhaa ya ushirikiano, moja kuu likiwa ni kuwepo kwa usawa kwa nchi zote katika faida itokanayo na umoja huo, kwa mfano mgawwanyo wa viwanda. Kwa mfano iliamuliwa kwamba viwanda vya matairi ya magari viwe Tanzania tu. Tukajenga kiwanda cha General Tyre. Kabla wino wa mkataba huo haujakauka, Kenya iliamua kujenga kiwanda cha matairi cha Firestone.
Kumbe wenzetu walitaka sisi tuwe soko lao.
Je dhamira hiyo ya wenzetu sasa imekwisha? Au nia yao bado ni hiyo, sisi tuwe soko lao?
Kumbe wanataka kututawala hawa. Watawale uchumi wetu toka Nairobi!! Watanzania gundueni hilo haraka ...
Wakati sisi tunapigania ukombozi wa Afrika, ikiwa ni pamoja na Afrika Mashariki (Uganda) wakenya walikuwa wanafanya biashara na kutengeneza utajiri. Baada ya kupatikana kwa amani, limekuwa ni soko zuri kwa mitaji ya wakenya.
Ni muhimu kwa wakenya kuchangia kwa njia moja au nyingine kwenye gharama za kuwepo kwa amani katika eneo hili. Gharama ambayo ilikuwa ni ya watannzania pekee.
Tuanzie hapo kwanza ...
Nasema Shirikisho Hapana, Hapana, Hapana kwa sasa.
Wakaenya wanasema tanzania inahitaji miaka 20 kuwafikia kiuchumi. Namimi nasema tunahitaji miaka 25 kabla hatujafikiria kuwa na federation!#
tutaendelea ...