Mtandao huu unaleta maana kwa sababu kila mzalendo anaweza kutoa maoni yake bila hofu. Licha ya hayo, tuna wajibu wa kutoa maoni ya kujenga wala sio kukashifu upande wowote. Uzalendo halisi ni ule unaoleta maendeleo na sio kudumaza. Tuchukulie kwa mfano nchi ya Merikani. Walio uendeleza na kujenga sio wazawa bali ni jamii ya watu wlioishi pamoja kwa kufanya kazi kwa bidii na mashindano (capitalism).
Watanzania hawana sababu yeyote ya kuhofu kuja kwa Mkenay, Mganda Mhindi au mtu yeyote mgeni kufanya biashara au kazi. Tukitazama kwa upande wa kazi, Mtanzania ana nafasi nzuri sana kufaulu kupata kazi kutokana na sababu kadha:
1. Ni mzawa kwa hivyo haitaji kibali (dola 600)
2. Yupo nyumbani na kampuni haina majukumu makubwa kwake
3. Anaweza kufanya kazi mda mrefu bila kwenda likizo ya mara kwa mara kwa vile familia nzima wako karibu.
4. Ni mzoefu wa mji kwa hivyo gharana ya maisha iko chini kwake
5. Ni mzawa kwahivyo anaweza kuongoza wenzake kwa ufasaha
6. Ni mzawa kwahivyo anauwezo wa kutafuta biashara kwa urahisi.
na sababu nyinginezo.
Kitakacho mkwamisha mtanzania ni :
1. Ujuji
2. Utiifu
3. Bidii kazini
4. Kujitole kufundisha wenzetu
5. Kujiendeleza kimasomo kazini.( tusiridhike na nafasi tulio nao)
Licha ya hayo, sio kila mtanzania anauwezo wa kwenda kenya na kujifunza kuto kwao. Mbona wasije na tujifunze kwa mda mfupi ili wapate ushindani wa kutosha na wao wenyewe watatoroka.
"Every cloud has a silver linning", mtanzania anaye jiamini hawezi kuhofia wageni na ndio maana kila siku tunaangaika kwenda merikani, afrika kusini ili tushindane nao huko kwao.je ukipata nafasi kufanya kazi nje ya nchi utaiacha?
Naomba mjadili hili swala kwa upeo ya msomi.Vijana wengi wanafuzu chuoni na hao wakenya watakipata ushindani. 'Arrogance' yafaa ingangaliwe kwa undani sana. Umsome mtu hata mwili wake (body language) kabla ya kutoa uamuzi. Merikani ukiambiwa 'go to hell' si kuwa uende jehanamu bali ni kuwa hakubaliani na mawazo yako. is that arrogance. Naomba tusaidiane kwa hili jambo na kila mtu afaidike. Wachache walio na hofu huenda waka waharibia wengi walio na nia nzuri. (personal ambitions are dangerous to development)
Mzalendo jasiri wa Afrika mashariji .
Unregistered said:
Nadhani mumemsikia au kumsoma wenyewe namna mkenya alivyo "arrogant". Anasema Kenya ni super power ya Afrika Mshariki. Anasema kuwa watanzania kazi yetu ni kukaa chini ya minazi kusubiri ruzuku ya serikali kama ilivyokuwa wakati wa vijiji vya ujamaa. Anasema kuwa katika eneo hili la Afrika mashariki inayofahamika ni Kenya tu iwe michezoni na kadhalika. Huyo ni Mkenya halisi na lugha yao siku zote.
Lakini Mkenya huyo hakusema upande wa pili kwamba wao pia ni wezi; kwamba katika jiji la Nairobi pamoja na kuwepo mjumba mazuri ya ghorofa pia kuna nyumba za maboksi; ambapo watu huweka vinyesi kwenye mifuko ya plastiki kwani hawana vyoo; kwamba wizi wa Kenya pia upo katika fikra zao ambapo ukipanda Kenya Airways unapoingia Tanzania huwa hawasemi kuwa sasa unaingia Tanzania isipokuwa utasikia tu upande ule wa kushoto au kulia kuna mlima Kilimanjaro ili abiria wafahamu kuwa Mlima Kilimanjaro upo Kenya.
Mkenya huyo licha ya kuikashifu Tanzania hajazungumzia umaskini mkubwa uliopo Kenya. Hao ndio Wakenya wanaotaka Shirikisho la Afrika Mashariki kwa manufaa yao ya kiuchumi na kibiashara.
Je, mnawataka Wakenya hao? Hiyo ndiyo sura yao halisi. Lugha ya jeuri na majivuno kwamba wao wamesoma sana na kwamba watanzania hupeleka watoto huko Kenya. Ni kweli watanzania hupeleka watoto wao huko Kenya na pia Uganda, kwa hiyo kwa Wakenya hiyo ni sifa tosha kweli kweli. Wao ni Super Power.
Nawathibitishieni wao ni super power katika wizi na "arrogance". Vipi Kijeshi? Sina hakika na hilo, pengine pia ni Super power. Labda siku moja wakati wa Shirikisho tutakuja ona ni nani super power kati ya tanzania na Kenya, kwani kwa maoni yangu kama ndio tabia hii ya wakenya ya kuwadharau watanzania itaendelezwa ndani ya shirikisho ni lazima litajitokeza jambo na hapo ndipo super power wa kweli atakapofahamika. Wakenya hao waje, Tanzania na watamke lugha hiyo vijijini ndani ya Tanzania waseme nyie watanzania hamjasoma, hapo ndipo watatambua maana ya kuzuia ulimi wao.
mzalendo halisi