game over
JF-Expert Member
- Jan 1, 2016
- 10,727
- 24,840
- Thread starter
- #101
Japo sikipendi chuo cha Udom lakini sina wasiwasi na ukubwa wake. Kile chuo ni kikubwa aisee na wanafunzi wote wanaishi ndani ya chuo. Wanaosema kiko scattered sana basi ni ushamba tu unawasumbua. Huwezi ukaweka ndaki (colleges) za vitu tofauti karibu karibu maana itakua vurugu na kelele.
Ukubwa wa chuo sio idadi ya wanafunzi bali ni eneo. Maana shule ya kata inaweza kuwa na wanafunzi 1500 ndani ya eneo lenye ukubwa wa kiwanja cha mpira lakini shule kongwe mfano Tanga school ikawa na wanafunzi 800 ndani ya ekari 70. Hapo ni ujinga kusema ile shule ya kata ni kubwa kwa sababu tu ina wanafunzi wengi.
Kwenye mashindano ya vyuo vya East Africa yaliyofanyika UDOM, chuo kiliwahifadhi wanamichezo 4000+ bila kumhamisha mwanfunzi yeyote. Baadhi wanafunzi walikua wanapotea kuonyesha ni jinsi gani chuo kilivyo kikubwa. Wale wanafunzi 7000+ wa special diploma ya ualimu waliondolewa na Magufuli lakini wala haikoonekana kama kuna watu wamepungua. UDOM bado haijajaa na ndio maana baadhi ya wizara ziko ndani ya chuo. Eneo langu pendwa pale Udom ni lile lenye ndaki za sheria, humanities, na biashara. Kuna swimming pool pale nilipendelea sana kwenda kupumzika.
Ukubwa Udom haina mpinzani ila kwenye ubora wa elimu inayotolewa pale sitii neno lolote.
Safi mkuu, Uzi huu unazungumzia ukubwa,
Tukija kwenye Ubora wa Elimu hii ni changamoto ya Africa nzima, Pengine Egypt niwaondoe hapa maana walau they’ve got something to show, pengine kidogo na SA,
Wengine wote tumezalisha wezi tupu wanaozungumza Kingereza.