Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,887
Karibuni Sana.
Katika thread hii nitaongelea uwezo na nguvu ya muziki wa kitanzania katika pwani hii ya mashariki ya Africa. Nguvu na mabadiliko ya kijamii mara nyingi yanahamasishwa na muziki.
Uzuri wa muziki ni mpangilio wa sauti, vyombo vya muziki na fasihi iliyojificha ndani ya muziki. Kwa upande wa pwani hii ya mashariki, Tanzania ndio makao makuu ya mziki mtamu na wa kuvutia. Mziki wa mwambao huu wa pwani ya mashariki umebatizwa kwa jina la Bongo Flava.
Bongo Flava limetokana na neno Ubongo au kwa maana nyingine akili, kwamba jiji la Dar es salaam linaitwa Bongo. Kwamba Dar es salaam inawakilisha Tanzania. Kwahiyo muziki wa Bongo Flava ni muziki wa akili.
Mashairi ya Muziki wa Bongo Flava mara nyingi yanakuwa katika mpangilio wa vina huku yakijaa maneno ya tafsida na tamathali za semi mbalimbali. Nahau, misemo, misamiati na methali huwa zinaunganishwa katika mashairi ya muziki wa bongo flava ili kunogesha na kufanya wimbo upendeze.
Sauti nyororo na za kubamba za vijana wa bongo zinafanya muziki huu uibuke kidedea na kutetea pwani ya mashariki mwa africa kwa hapa africa na dunia nzima. Mashairi mengi ya Bongo flava yanaandikwa kwa lugha ya kiswahili; kitendo hicho kinawafanya wale ambao hawajui kiswahili wapate hamasa ya kujifunza kiswahili kwa kunguvu ikizingatiwa kwamba kiswahili ni lugha adhimu duniani. Inasadikika kwamba lugha hii ndiyo Adam na Eva walikuwa wakiongea wakiwa bustani ya Aden. Baadhi ya maneno ya kiswahili yanasadiifu ukweli huu kwamba kiswahili ndiyo lugha ya kwanza ya binadamu.
Katika thread hii nitajikita kuonesha ubora wa sauti nzuri za watu wa tanzania katika muziki. Nitaonesha mashairi mbali mbali na kuweka video tofauti tofauti kisha kuzielezea.
Zaidi ya kuwa muziki ni burudani, kuelimisha na kuliwaza, mziki umekuwa biashara na vijana wengi wamekuwa wakijiingizia kipato.
Mungu ibariki Bogo Flava, Mungu Ibariki Tanzania.
Karibuni wenzangu kutoka Kenya muweze kujifunza hapa badala ya kuanza kutoa matusi.
"Usivione Vyaelea Vimeundwa"