East Coast of Africa Music HQ- The Empire of Tanzania

East Coast of Africa Music HQ- The Empire of Tanzania

Mimi sio mpenzi sana wa music but nikisikia mziki wa Congo najua huu ni Congo, Nigeria unajua, South afrika ukipigwa unajua hii ni mziki wa bondeni. Lakini mziki wa Kenya hakuna identity kuna wenyewe kuimba Kikuyu, wengine kuigiza wazungu, wengine wanaimba ki pwani, wengine kikamba hao ndio nikisikia hata na redio nazima yanii kuna.miziki hata ikipigwa mbwa anakimbikia nimeisikia Kenya looh.
kuna wenye wanajaribu...lakini wengi wao wana imba takataka...
 
nimesoma mbili tatu...tamu sana...good stuff
Nitakuletea nyingi tu hapa. Hapa TZ tupo na zaidi ya 100 ya wasanii wa Bongo Flava tena wapo Active.
Tanzania ni nchi ya furaha na ukichunguza muziki wa Tanzania unaongea zaidi kuhusu furaha na amani ya watanzania. Siyo muziki wa nchi fulani hapa mwambao wa mashariki mwa Africa, yaani kama ugomvi kila wakati mzingi wa kugombana tu.
 
kuna wenye wanajaribu...lakini wengi wao wana imba takataka...nakubaliana nawe hapo...
Wapo wanaojaribu mi kwa Kenya afadhali nisikilize muziki ya wajaluo na waluhya kama wanaimba kilugha ila hao wengine kwa kweli hmmm
 
Wapo wanaojaribu mi kwa Kenya afadhali nisikilize muziki ya wajaluo na waluhya kama wanaimba kilugha ila hao wengine kwa kweli hmmm
hahaha...shida yao kwanza hawajui lugha...ndio ubaya wa kuchanganya lugha nyingi Kikuyu, Sheng', Kiswahili, Kiingereza nk...pili huwa wanajaribu kuwa kama wamarekani...ona tu Khaligraph...on the other hand, Nigerians, Tanzanians and SA try to be themselves..thats why they do great...Kenya tuko bad sana..
 
Muziki wa kenya ulizaliwa Mombasa ukafia Nairobi.
 
nimesoma mbili tatu...tamu sana...good stuff...ila mchanueni huyu bro wenu Kilam..sijui ni teenager au?😀😀 ana akili ndogo sana...

Nimefanya nini kwani? Tulia sindano ikuingie.
 
Yap Tz vs Kenya ts like US vs UK, unajua namaanisha nn
wakati mngine huwa tukija hapa tunauliza maswali bila ya nia mbaya wala sio ushabik...kuna jamaa mwingine anaitwa Kilam...akishamwona mkenya dah, kinywa chake kinabadilika na kuwa washing machine.....anamwaga povu kumwaga😀😀😀😀
 
NYOTA Peter Msechu ft Amini


[Verse 1 – Amini]
Sikiliza rafiki, navumilia vingi vitimbwi
Moyoni bado anaishi, ila amejaa usaliti
Aliondoka akaniacha peke yangu
Huku nyuma nikalia na Mungu wangu
Haikufika hata mwezi, alipokosa furaha akarudi
Ameshachora na tattoo, jina la mpenzi wake mdanganyi
Lakini bado nilimpa moyo wangu
Nikiamini kuwa ye ni fungu langu, nilopangiwa

[Chorus – Peter Msechu] x2
Nyota na ing’ae kwako wee (nakuombea)
Nyota na ing’ae kwako wee (nakuombea)
Kesha usiku na mchana ukiomba
Uzidi kusema na Mola ataitika

[Bridge – Amini]
Mapenzi ni wawili, wasioachana solemba
Iwe kwa dhiki, wingi wa mali
Muhimu kupendana
Mapenzi ni wawili, wasioachana solemba
Iwe kwa dhiki, wingi wa mali
Muhimu kupendana

[Verse 2 – Peter Msechu]
Mbona yako ni madogo
Yanayonikuta huwezi niamini
Mpaka leo naishi nae
Anakuja na mpenzi hadharani
Ninachofanya mi nacheza part yangu
Ingawa kidoleni ana pete yangu
Nakusihi vumilia, siku moja ndoto yako itatimia
Malumbano na zogo, ya mapenzi huwezi kimbia
Daima subira ndio ngao yangu
Nawe jaribu kufata nyendo zangu
Utajivunia

[Chorus – Amini] x2
Nyota na ing’ae kwako wee (nakuombea)
Nyota na ing’ae kwako wee (nakuombea)
Kesha usiku na mchana ukiomba
Uzidi kusema na Mola ataitika

[Bridge – Peter Msechu]
Mapenzi ni wawili, wasioachana solemba
Iwe kwa dhiki, wingi wa mali
Muhimu kupendana
Mapenzi ni wawili, wasioachana solemba
Iwe kwa dhiki, wingi wa mali
Muhimu kupendana

[Chorus – Amini & Peter Msechu] x2
Nyota na ing’ae kwako wee (nakuombea)
Nyota na ing’ae kwako wee (nakuombea)
Kesha usiku na mchana ukiomba
Uzidi kusema na Mola ataitika​
 
wakati mngine huwa tukija hapa tunauliza maswali bila ya nia mbaya wala sio ushabik...kuna jamaa mwingine anaitwa Kilam...akishamwona mkenya dah, kinywa chake kinabadilika na kuwa washing machine.....anamwaga povu kumwaga😀😀😀😀

Tokea lini mshabiki wa Gor Mahia akaishangilia AFC Leopards?
 
Linex ft Diamond Platnumz - Salima


Verse 1 – Linex

Salima, Salima woh
Najua maisha yako yaliyumba pale ulipowapoteza wazazi wako
Yule Salima wa jana, sio Salima wa leo
Umekuwa wa kujiinamia, na kujikatia tamaa
Iko wapi furaha yake aliokuwa nayo mwanzo?
Iko wapi furaha yake aliokuwa nayo mwanzo?
Salima ndagusanzi ngasuri kagonga
Waiguye tenga hadi nyanya
Salima, je ni Sande guya yende?
Nda somi nawe Mwenge
Salima, mi ni Sande yule yule
Niliesoma nawe Mwenge
Zimeyeyuka ndoto zako, ulizokuwa nazo Salima

Chorus – Diamond Platnumz & Linex
(Oh Salima)
Mi mwenzako nakupenda (Oh Salima)
Tena nataka niwe wako (Oh Salima)
Tuzae na wana tujejenga (Oh Salima)
Niwe baba wa watoto wako (x2)

Verse 2 – Linex
Naiomba hiyo bahati ya kuishi nawe
Idondokee kwangu isiende kwa mwingine
Yasijekuwa kama yale ya mwanawe hafi nawe
Yasijekuwa kama yale ya mwanawe hafi nawe
Usijikatie tamaa
Kuna wengi wana shida kuliko zako Salma
Wanaamini kupitia ule msemo wa "Riziki agwepa miguuni kwake."
Wanaamini kupitia ule msemo wa "Riziki mafungu saba!", Salima woh

Chorus – Diamond Platnumz & Linex
(Oh Salima)
Mi mwenzako nakupenda (Oh Salima)
Tena nataka niwe wako (Oh Salima)
Tuzae na wana tujejenga (Oh Salima)
Niwe baba wa watoto wako (x2)

Verse 3 – Diamond Platnumz
Moyo unatamani ungelikuwa kitabu ufungue (uufungue)
Usome jinsi gani unavyonifanya niugue, eh
Zainda uli nawe, uwabeshe ewawi ndashishe
Mpaka korera baba, utu na besa, japo niuridhishe
Utamu, utamu moyo wangu mi kupendwa na wewe
Utamu, sa nini tatizo mamii? Basi sema nielewe
Ah Salima oh (oh yaaya)
Salima yee (oh yaaya)
Salima oh (oh yaaya)
Salima eh ee

Chorus – Diamond Platnumz & Linex
(Oh Salima)
Mi mwenzako nakupenda (Oh Salima)
Tena nataka niwe wako (Oh Salima)
Tuzae na wana tujejenga (Oh Salima)
Niwe baba wa watoto wako (x2)

Bridge – Linex
I can pretend I'm inlove with you
I can pretend in my life is you
I can pretend you the only one I need
The only one I trust
Baby, I'm not a perfect man
But I'm going my hard way
I just want to be with u
Me and you forever, and ever!

Chorus – Diamond Platnumz & Linex
(Oh Salima)
Mi mwenzako nakupenda (Oh Salima)
Tena nataka niwe wako (Oh Salima)
Tuzae na wana tujejenga (Oh Salima)
Niwe baba wa watoto wako (x2)

Outro – Linex
Na watoto kede kede
Na watoto kede kede
Sande na shemeji mchange wantenteleta nisaidia
(Salima, Salima, Salima)
 
Rich Mavoko - Pacha wangu


When I wake up in the morning
(In the morning, in the morning)
Assume nikiss mdomoni
(Mdomoni, mdomoni)
Nalala na picha kitandani
(Kitandani, kitandani)
Mapenzi yananiumiza moyoni
(Moyoni, moyoni)
We ndo pacha wangu mrithi wa bibi
Utu na visa vyangu vyote nakukabidhi
Hivi ni mama unaniumiza, usiku ukipiga simu uku unajiuliza
Naskia umeolewa nitaleta zawadi, tunza heshima isiwe mradi

(CHORUS)
Eeehhh
I love you baby baby
I love you baby baby
Japo shida inabidi nizoee
Sina budi nizoee ×4

Ufinyu wa shilingi kwangu, shimo unaliona
Ukatili wa mapenzi yangu, kwa shibe ya dona
Kila siku nasali, namwomba mola mja nilinde na hali najua unaniona
Nishaulizwa sana weehh, hayaa hawaoni tukiongozana wee hayaa
Pacha tusiofanana mimi na we, hayaaaaaah
Kumbe we ndo pacha wangu mrithi wa bibi
Utu na visa vyangu, vyote nakukabidhi
Hivi mama unaniumiza usiku

(CHORUS)

Oooh eeehh mavoko
Oooh baby yoooh
Oooh baby yoooh
Bila wewe I'm ready
Oooh baby yooh
 
Dogo Janja - Kidebe


[verse 1]
Kuna vitu tulifanya, nikaviona havina maana, nikavitupa kwa choo
Kesho haiwez kuwa jana haki nakupenda sana,achana Na mabishoo
We ndo mwali wa mitindo, eeeh
Acha na isidingo eeeeh
Ona naimba wimbo,ibuka ghetto tuchapane fimboo
Nafurahi mama leo nimekuona (Tena)
Vaa beli vaa jeans twende (Sinema)
We mzuri we mkali kama (Wema)
Sio kiburi sio mchafu kama (siwema)
Now nipo safi, sio tena lofa
Mapenzi ya cinema ni ya harmonize na wolper
Kiki naogopa,itakuaje ukiondoka
Tashindwa kutinga beli kali za doka
[Chorus]
Tulipotoka mbali beibe usiskize maneno,
Toka mafuta ya kidebe, leo namiliko doo,
Ona nanananana onananananaa onanananana ona nanana
[Verse 2]
Mambo yangu nayajua,enzi Nlizokutumbua,toka Vile Mudogoo sana
Ukajifanya wakishua,unalazwa kwa mafua,Nilikua Nacheka sanaa
[henda nikutwale kai, ukalange vazazi vyane]x2
Japo ngela alikugonga mi nliona fair,karibu ngarenaro,ona bendera inapepea
Naipendacolour,soft haunywi maji,upo kama Kajala,rafiki yake Hamad
Now nipo safi sio tena lofa
Mapenzi ya sinema ni ya Harmonize na Wolper
Kiki naogopa,itakuajeukiondoka,tashindwa kutinga beli kali za doka
[Chorous]
[Bridge]
Baby umependeza,wengine watageza
Vile ulivyosuka kama mikia ya pweza
Nacheka kingereza,kukukacha never
[Am happy if you happy cheza]
Mi naweza,mateja nimewameza,nipo tayarikufa kuliko kukupoteza,
Waambie wanaobeza am ur clever,​
[Am happy if you happy cheza]
[Chorous]​
 
BUSHOKE FT K-LYNN - NALIA KWA FURAHA


[Chorus] x2
[Bushoke]
Mbona wanitazama, kisha waanza kulia?
Kama nimekukosea, naomba nisamehe
[K-Lynn]
Hapana hujanikosea, mi nalia kwa furaha
Mapenzi unayonipa, sijawahi kupata
[Verse 1 – K-Lynn]
Unaposogea karibu, unaponishika mkono
Unaponitazama machoni, nashindwa vumilia
Mapenzi unayonipa, sijawahi kupata
Najiuliza ni kwanini, hatukujuana mapema
Nimeishi na wasojua mapenzi
Wasojua hata kunyenyekea
Nimeishi na wanaojua ku-force
Wasojua hata kubembeleza
Ninapokuwa na wewe, najiona ndio mwenyewe
Hata kama sina pesa, najiona tajiri
Hata kama sijala, najiona nimeshiba
[Chorus] x2
[Bushoke]
Mbona wanitazama, kisha waanza kulia?
Kama nimekukosea, naomba nisamehe
[K-Lynn]
Hapana hujanikosea, mi nalia kwa furaha
Mapenzi unayonipa, sijawahi kupata
[Verse 2]
[K-Lynn]
Naomba Mungu atujalie, tufunge ndoa mi na wewe
Na watoto pia tuzae, wakuite baba na mi mama
Maisha yangu bila wewe, sawa na basi bila konda
Maisha yangu bila wewe, mbele sitosonga
[Bushoke]
Na bado, na bado, sijafika mwisho
Na bado, na bado, sijamaliza kitabu
Vumilia maisha yangu, utakula vya kwangu
Mimi si wale wanaojisifu kwa ngono
Mapenzi si maneno, mapenzi ni vitendo
Na bado, na bado, nimesema bado
[Chorus] x2
[Bushoke]
Mbona wanitazama, kisha waanza kulia?
Kama nimekukosea, naomba nisamehe
[K-Lynn]
Hapana hujanikosea, mi nalia kwa furaha
Mapenzi unayonipa, sijawahi kupata​
 
Barnaba Classic - Lover Boy



Intro

Akiomba Pesa hataki
na penzi langu amelidhihaki
Amekubali na kubaki
Haki ya Mungu jama Simuachi.
Verse ya Kwanza
Kwenye Life watu wengi wanafeki
Yule wa nyuma ali separate
Maisha siyo lazima Kudate na Videnti (Come On)
Kama ni gari kwako nimefunga brake
Na pendo langu kwako halielezeki
Kwako si act wala sifeki
Siku true ** na warembo Feki
Najua ushaumizwa mengi sana, Ushakutana na ma heart Braker
Ila siyo mimi iii , i am a good boy
Kibwagizo
Walishazichezea hisia zako mpenzi wangu,
Mwisho wa siku wakakuacha ukilia aa , mapenzi ukayachukia aaa
Ila siyo mimi (I am a good boy, I am a Good Boy,Good boy, Good boy, baby)
Kiitikio
Don't call me Lover Boy,Dont call me Lover Lover boy baby
Dont call me lover boy (I am an Innocent baby)
dont call me Lover boy, dont call me call me lover boy
Dont call me Lover boy
I am an Innocent baby
Verse ya pili
No ooo baby na nalia kwa nia siyo kama napendaaa ee

How come mpenzi wako eti unamhudumia
Wengine wanakuja kumtumia (Eboo)
Hamna love siku hizi wananunua ee
Washenzi,Bora wamalize na kutulia
Wakimaliza hawaishi kukutangazia
Eti yule binti si tumemtumia eeh​

Kibwagizo
Walishazichezea hisia zako mpenzi wangu,
Mwisho wa siku wakakuacha ukilia aa , mapenzi ukayachukia aaa
Ila siyo mimi (I am a good boy, Good Boy,Good boy Good boy)

Akiomba Pesa hataki
na penzi langu amelidhihaki
Amekubali na kubaki
Haki ya Mungu jama Simuachi.
Outro

You are my Everything youre my only one. (Dont call me Lover Boy, baby, Dont call lover boy ma Darling )
baby You are my Everything you;re my only one. (Dont call me Lover Boy,Dont call me Lover boy ma Darling)​


 
Karibuni Sana.
Katika thread hii nitaongelea uwezo na nguvu ya muziki wa kitanzania katika pwani hii ya mashariki ya Africa. Nguvu na mabadiliko ya kijamii mara nyingi yanahamasishwa na muziki.

Uzuri wa muziki ni mpangilio wa sauti, vyombo vya muziki na fasihi iliyojificha ndani ya muziki. Kwa upande wa pwani hii ya mashariki, Tanzania ndio makao makuu ya mziki mtamu na wa kuvutia. Mziki wa mwambao huu wa pwani ya mashariki umebatizwa kwa jina la Bongo Flava.

Bongo Flava limetokana na neno Ubongo au kwa maana nyingine akili, kwamba jiji la Dar es salaam linaitwa Bongo. Kwamba Dar es salaam inawakilisha Tanzania. Kwahiyo muziki wa Bongo Flava ni muziki wa akili.

Mashairi ya Muziki wa Bongo Flava mara nyingi yanakuwa katika mpangilio wa vina huku yakijaa maneno ya tafsida na tamathali za semi mbalimbali. Nahau, misemo, misamiati na methali huwa zinaunganishwa katika mashairi ya muziki wa bongo flava ili kunogesha na kufanya wimbo upendeze.

Sauti nyororo na za kubamba za vijana wa bongo zinafanya muziki huu uibuke kidedea na kutetea pwani ya mashariki mwa africa kwa hapa africa na dunia nzima. Mashairi mengi ya Bongo flava yanaandikwa kwa lugha ya kiswahili; kitendo hicho kinawafanya wale ambao hawajui kiswahili wapate hamasa ya kujifunza kiswahili kwa kunguvu ikizingatiwa kwamba kiswahili ni lugha adhimu duniani. Inasadikika kwamba lugha hii ndiyo Adam na Eva walikuwa wakiongea wakiwa bustani ya Aden. Baadhi ya maneno ya kiswahili yanasadiifu ukweli huu kwamba kiswahili ndiyo lugha ya kwanza ya binadamu.

Katika thread hii nitajikita kuonesha ubora wa sauti nzuri za watu wa tanzania katika muziki. Nitaonesha mashairi mbali mbali na kuweka video tofauti tofauti kisha kuzielezea.

Zaidi ya kuwa muziki ni burudani, kuelimisha na kuliwaza, mziki umekuwa biashara na vijana wengi wamekuwa wakijiingizia kipato.

Mungu ibariki Bogo Flava, Mungu Ibariki Tanzania.
Karibuni wenzangu kutoka Kenya muweze kujifunza hapa badala ya kuanza kutoa matusi.
"Usivione Vyaelea Vimeundwa"
[emoji14] [emoji13] [emoji14] [emoji12] [emoji14] [emoji14] [emoji13] [emoji14] [emoji13]
 
MwanaFA Featuring Vanessa Mdee - Dume Suruali


We dume suruali kaa mbali nami
Kama dume suruali kaa mbali nami
Huendani na mimi

Mwana FA
Hudat hudat hii ni salam na ufahamu
Kama unauza mapenzi siyo kwa binamu
Huna haja ya kusubiri hii ni hukumu
Hakuna kitu utapata utangoja kama askari wa zamu
Dume suruali dume kaptula
Shauri zako ilimradi sipati hasara
Usione utani me sihongi hata kwa ishara
Utaniambia nini mpaka unigeuze fala
Kwanza nasikia hongo zinaleta mkosi...

Sentano yangu hugusi hata ukiongea kidosi
Yabaki mapenzi tusileteane ujambazi
Hata upige sarakasi utachonga viazi.
BAHILI KAMA NINI!!!!!!!!! Ndiyo mnavyosema
Na ukiniomba kesho hunisikii tena
Kwani unauza nini dada!
Hunitakii mema.

Kiitikio

We dume suruali kaa mbali nami
Kama dume suruali kaa mbali nami
Huendani na mimi
I want Gucci, Fendi, spend it on the girl like me
My name is Vee Money, money spend on the girl like me

MWANA FA
Nihonge nanunua nini kwa nini yaani!
Kuna kipi nisichokijua ina TV ndani?
Usiulize n’takupa nini dada piga moyo konde
Viuno vingi kama mwali wa kimakonde
Usipende hela kama mfuko
Au fanya unavyofanya upate zako
Vishawishi vingi binti sema na moyo wako
Na ujifunze pesa zinauza utu wako
Tajiri mtata kama Salah
Zipo ila sitoi me ni balaa
Unapenda hela zangu nami nazipenda pia
Kila mtu abaki na zake bye baby tutaongea
MWANAUME WA HIVYO WA NINI SASA!!!!! Ndiyo mnavyosema
Na ukiniomba kesho hunisikii tena
Kwani unauza nini dada
Hunitakii mema

Vanessa
Aje aje ajeeee me mtoto fulani ghali
Nihonge gari Ma sweet sweet baby
Wanna see you today unipeleke party
Aje aje ajeee njoo nikupe TBT

MWANA FA
Siyo kwa enzi ya Magufuli
Zali ilikuwa long siku hizi hakuna la mentali
Nikikuhonga na ukiniacha nitakujia usingizini
Naepusha shari matatizo yote ya nini
Hakuna kipya chini ya jua
Hata nisiyoyafanya nishayasikia
Ningekuwa mhongaji ningeshafulia wangu
Mademu wangu wa zamani wote wangekuwa maadui zangu
MWANAUME HOVYO WEWE!!!!! Ndiyo mnavyosema
Na ukiniomba kesho hunisikii tena
Kwani unauza nini dada
Hunitakii mema

Vanessa
Baki na hamu zako

Kiitikio
We dume suruali kaa mbali nami
Kama dume suruali kaa mbali nami
Huendani na mimi
I want Gucci, Fendi, spend it on the girl like me
My name is Vee Money, money spend on the girl like me

VANESSA
Baba bure huyuu!!!

Mwana FA
Hata pantoni lina staff
Vanessa
Unamwambia nani sasa! Unamwaaambia nani sasa!
 
Back
Top Bottom