East Coast of Africa Music HQ- The Empire of Tanzania

East Coast of Africa Music HQ- The Empire of Tanzania

fair enough.....unaeza kuwa unasema ukweli ila mbona wengine wachahe wana relocate either SA or Kenya...wakienda SA ama Nigeria nitaelewa kwani nchi hizi zina music industry zenye nguvu...ila mbona kenya...Kenya's music is not better than Bongo's...sielewi..pengine iwe govt yenu inawanyanyasa sijui...ndio maana nikauliza...sina ubaya wowote..kuuliza tu..thread nzuri hii
Kuna mwanamuziki mmoja anaitwa Husein Machozi alihamia Kenya, huko akafanya wimbo unaitwa Addicted. Lakini relocation yake haikusaidia kuuboost muziki wake.
Addicted ilikua kali lakini, kama unavyosema kua muziki wenu hauna nguvu, jamaa alifeli vibaya mno.

Mwingine ni Mr. Nice, alihamia Kenya akajaribu kufanya muziki akitokea huko lakini ilikua hola. Nyimbo alizotoa zilikua nzuri lakini ilishindikana kuuboost muziki wake.
Ni basi tu wanashindwa kujua chochote ambacho Kenya wanacho kwenye muziki sisi tunacho bora zaidi ya hiko.

Hao wanaohamia kama waliangalia ya wenzao basi watakua wamejizatiti vya kutosha.
 
Siri - Barnaba Ft Vanessa Mdee


[Intro]
Tosa la secret baby
Jamais
Oh mamaa maa
Oh nanaa naa
Yooo zane valee baby
Yooo zane valee papaaa

[Verse 1 – Barnaba & Vanessa Mdee]
Treni langu la kutongoza
Limefunga breki na kituo ndo wewe (ndo wewe kipenzi)
Sina mengi mimi
Sio mtoto wa mjini
Nimefundwa jandoni kipenzi

Hadithi Hadithi uwongo njoo
Nae anieleze porojo
Mie bado mdogo
Ivi ni juzi ulikuja na mauwa (yes!)
Ulikuwa na barua ila sukuifunguaa na na naa (why?)

Ungesoma ndani (why?!)
Ungejua vingi (no!)
Vile moyo wangu ulivyojawa na vigingii iih
Wewe una mume (nampenda)
Nami nina mke
Twaweza iba bado wasishituke (loh!!)

[Bridge – Vanessa Mdee]
Kumbe muhuni iih iih iihi
Aku siwezi kushare penzi no way
Kasoro yangu nini iih iih iih
Si una mke yule amekosa nini
Ohuu yeah! Uuhu!

[Chorus – Barnaba & Vanessa Mdee]
Kwanza ningekuomba
Kupenzi ukubali iih
Tutafanya siri iih
Ya watu wawili

Utaniponza kwa jambo hili
Hamnaga siri
Ya watu wawili

Kama ukikubali
Nitakupa kagari
Na vi-salary
Utakuwa bonge la sister duu

Aliniifunza mama
Niogope wavulana
Nikae mbali
Nyie wabaya sana

[Verse 2 – Vanessa Mdee & Barnaba]
Kwetu nyumbani iih
Tumekulia kwenye dini mmh
Penda wako nyumbani kwanza
Kisha unipende mimi mmh (awe muwongo baba)

Aaasante
Kwa muda wako
Nimependa majibu yako
Hivi nikuulize swali? (niulize nini?)
Anavyotoka mumeo unajua mangapi anafanya?
Mi muhuni (muongo)
Niseme nini (muongo)
Kila kitu (muongo)
Maneno yangu hayakuvuna pendo

Hunajipya (muongo)
Useme nini (muongo)
Maneno ya (uongo!)
Kibaya zaidi mke wako akijua

[Bridge – Vanessa Mdee & Barnaba]
Kumbe muhuni iih iih iih
Aku siwezi kushare penzi noo way
Kasoro yangu nini iih iih iih
Si una mke yule amekosa nini (oh no no)
Ohuu yeah! uuhuu! (Ebo!)

[Chorus – Barnaba & Vanessa Mdee]
Ukikubali
Nitakupa kagari
Na vi-salary
Utakuwa bonge la sister duu

Aliniifunza mama
Niogope wavulana
Nikae mbali
Nyie wabaya sana

Kwanza ningekuomba
Kupenzi ukubali iih
Tutafanya siri iih
Ya watu wawili

Utaniponza kwa jambo hili
Hamnaga siri
Ya watu wawili

Kama ukikubali
Nitakupa kagari
Na vi-salary
Utakuwa bonge la sister duu

Aliniifunza mama
Niogope wavulana
Nikae mbali
Nyie wabaya sana​
 
BARNABA - MILELE DAIMA



[Chorus]
Nimeshakosa mambo mangapi
Ila bado ukanipa nafasi
Na ukasema kwamba unaachi utanipenda milele
Chozi lako Mola kasikia, na mimi ninakiri upendo nimetulia
Nitakupenda milele daima, daima, daima
Chozi lako Mola kasikia, na mimi ninakiri upendo nimetulia
Nitakupenda milele daima, daima, daima

[Verse 1]
Jamani sijamroga ila ni mapaenzi kwa sana
Akiniona atanikumbatia na kuni-wish zaidi ya jana
Mnatamani muwe mimi mimi, nami niwe nyie nyie
Ila haiwezekani, kashanihifadhi moyoni
Ameshanichunga sana kama mboni nami nimemuweka rohoni
Na kama kunibwaga angeshanibwaga tangu kule nyuma
Na yule mshichana wa zamani, aliponifuma nae
Eh aliponifuma nae

[Chorus]
Nimeshakosa mambo mangapi
Ila bado ukanipa nafasi
Na ukasema kwamba unaachi utanipenda milele
Chozi lako Mola kasikia, na mimi ninakiri upendo nimetulia
Nitakupenda milele daima, daima, daima
Chozi lako Mola kasikia, na mimi ninakiri upendo nimetulia
Nitakupenda milele daima, daima, daima

[Verse 2]
Oh ooh ukinibwaga, ukinibwaga jua watanicheka
Watanicheka wataona nilijikweza, kwa haya nilonena
Haijalishi dini, kabila vyangu na vyake viweze kulingana
Yeye mguu, mimi tanki kiatu nimemfiti wala sijambana aah haa
Na kama kunibwaga angeshanibwaga tangu kule nyuma
Na yule mshichana wa zamani, aliponifuma nae
Eh aliponifuma nae

[Chorus]
Nimeshakosa mambo mangapi
Ila bado ukanipa nafasi
Na ukasema kwamba unaachi utanipenda milele
Chozi lako Mola kasikia, na mimi ninakiri upendo nimetulia
Nitakupenda milele daima, daima, daima
Chozi lako Mola kasikia, na mimi ninakiri upendo nimetulia
Nitakupenda milele daima, daima, daima

[Bridge]
Nasema chozi lako Mola kasikia
Nitakupenda milele nakuapia
Eh! Wuwu wuwu baby
Aah haa baby
Wuwu wuwu kamwali we, kamwali we

[Outro]
Chozi lako Mola kasikia, na mimi ninakiri upendo nimetulia
Nitakupenda milele daima, daima, daima
Chozi lako Mola kasikia, na mimi ninakiri upendo nimetulia
Nitakupenda milele daima, daima, daima
Chozi lako Mola kasikia, na mimi ninakiri upendo nimetulia
Nitakupenda milele daima, daima, daima
Chozi lako Mola kasikia, na mimi ninakiri upendo nimetulia
Nitakupenda milele daima, daima, daima
Daima, daima
Daima, daima​
 
Masogange - Bell9



[Intro]
Upo mbali na masogange
Njoo uutulize mtima wange
Upo mbali na masogange eh

[Verse 1]
Miaka mingi imepita baby, ila mi sijakuona
Miaka mingi imekatika ma, ila mi sijakuona
Lile kidonda changu cha mapenzi, moyoni bado hakijapona
Nitapata afadhali mi, endapo we nikikuona
Kama warembo mi nawaona wengi, tabia zao mi naona noma
Najaribu shinda vishawishi, nisije mi kukupa ngoma

[Bridge]
Bado nakupenda wewe, wapi ulipokwenda
Bado nakupenda wewe, wapi ulikokwenda

[Pre-Chorus]
Ndo maana nakuimbia popote ulipo sikia
Baby, urudi nyumbani
Nakuimbia popote ulipo sikia
Mami, tuishi kama zamani

[Chorus]
Mapenzi yanautesa moyo we
Mapenzi yanaumiza moyo we
Mapenzi yanautesa moyo we
Njoo unipoze roho
Mapenzi yanautesa moyo we
Mapenzi yanaumiza moyo we
Mapenzi yanautesa moyo we
Njoo unipoze roho

Toka long time ago we, nakusaka mrembo we
Nakusaka baby, nijue upo wapi mama

[Verse 2]
Wasiopenda kuona mimi nawe
Tunapeana real love ni wengi
Hawapendi kuona mimi nawe
Kila siku twapeana mapenzi
Wasiopenda kuona mimi nawe
Twapendana my baby ni wengi
Hawapendi kuona mimi nawe
Kila siku twapeana mapenzi

[Bridge]
Chochote watachokuambia, usiwasikilize
Nakusihi mami puuzia, moyo wangu usiumize
Chochote watachokuambia, usiwasikilize
Nakusihi mami puuzia, moyo wangu usiumize

Endapo ukiwasikiliza, moyo wangu utaumiza
Endapo ukiwasikiliza, utaniacha mi kwenye kiza
Endapo ukiwasikiliza, moyo wangu utaumiza
Endapo ukiwasikiliza, utaniacha mi kwenye kiza haya

[Chorus]
Upo mbali na masogange
Njoo uutulize mtima wangu
Upo mbali na masogange
Njoo uutulize mtima wangu

Mapenzi yanautesa moyo we
Mapenzi yanaumiza moyo we
Mapenzi yanautesa moyo we
Njoo unipoze roho
Mapenzi yanautesa moyo we
Mapenzi yanaumiza moyo we
Mapenzi yanautesa moyo we
Njoo unipoze roho

Upo mbali na masogange
Njoo uutulize mtima wangu
Upo mbali na masogange
Upo mbali na masogange
Njoo uutulize mtima wangu

Mapenzi yanautesa moyo we
Mapenzi yanaumiza moyo we
Mapenzi yanatesa moyoni
Mapenzi yanatesa rohoni
Mapenzi yanautesa moyo we
Mapenzi yanaumiza moyo we
Mapenzi yanautesa moyo we
Njoo unipoze roho
Mapenzi yanautesa moyo we
Mapenzi yanaumiza moyo we
Mapenzi yanautesa moyo we
Njoo unipoze roho

[Outro]
Wewe, toka long time ago
Nakusaka mrembo nijue uko wapi mama ah
I love you, i need you!​
 
Nitampata wapi - Diamond Platnumz



sura yake mtaratibu mwenye macho ya aibu
kumsahau najaribu ila namkumbuka sana
umbo lake mahbibu kwenye maradhi aliye nitibu
siri yang kaharibu bado namkumbuka sanaaa

aliye nifanya silali jua kali nitafute tukale
lakini-(ila) hata kujali, darling, akatekwa na wale x2
ntampata wapi kama yule niliye mpendaga sana
ntampata wapi kama yule anipende sana x2

ai nyotaaa nyota ndo tatizo langu, nyotaa mpaka nalia peke yangu
ai nyotaaa nyota ndo shida yangu, nyota wamenizidi wenzangu
alidanganywa na wale wenye pesa nyumba gari mi kapuku akunijali akanikimbia
alidanganywa na wale wa mapesa nyumba gari mie ungaunga akunijali akanikimbia

aliyenifanya silali jua kali nitafute tukale
lakini hata akujali darling akatekwa na wale x2
nitampata wapi kama yule niliyempendaga sana
nitampata wapi kama yule anipende sana x2

bado ananijia ndotoni ila nikiamka simwoni
bado ananijia nikilala haki ya mungu sio masihara
bado ananijia ndotoni nikiamka simwoni
bado ananijia nikilala haki ya mungu sio masihara

Hii ni sauti ya rais
ilomshindaga ibilisi
kwa wanadamu sio rahisi

Kamwambie
lazima ujue kutofautisha
kati ya msalaba na jumlisha
kuna X na kuzidisha

bado ananijia nikilala
haki ya mungu sio masihara​
 
Kenya walikuwa wanakimbiza miaka ile kabla akina mondi na kiba hawajacharuka
 
Harmonize X Rich Mavoko – Show Me



Ai mwenzako I feel so Good, kipindi nikikuona
Au Huo Mwendo Unafanya kusudi na Ulivyoshona
Wakati Unakwenda au unarudi wakata Kona
Nyuma Ka Katuni za Masudi UlivyoNona
Hivi Unapenda wa Vifua ka Roboti ama Sanamu
Au wazee wa Kununua Mwaga Noti akina Salamu



Ooooh Anita macho kama unaniita, aaah saa Sita
Shepu Vera Sidika aaah
Anita Macho kama Unaiita aaah saa Sita Shepu Vera..

Ah Show Me Show Me Show Me ( Unavyodance)
Show Me Show Me Show Me (Waonyeshe Unavyodance) (x2)

Umenifinyanga kama Dona Mmakonde na Ndonya
Kama Mpira Maradona Kichuya Kona
Na wakisema Na mawenge Waambie Werrason
Wakiringisha Peremende Nitakugawia koni
Chunga Kipenzi Majaribu Mabaya sana Oooh
Na wee Ndo Dokta wa Kunitibu Niwe Salama Ooooh

Oooh baby Anita macho kama Unaniita aaah
Saa Sita Kiuno ka Yondo Sister aaaah
Anita macho kama Unaniita aaaah
Saa Sita Kiuno ka Yondo Sister

Ah Show Me Show Me Show Me ( Unavyodance)
Show Me Show Me Show Me (Waonyeshe Unavyodance) (x2)

Asa Mombasa Nairobi (Sakata Dance)
Kampala Kigali (Sakata Dance)
Zimbambwe Kwatobi (Sakata Dance)
Naija Somali ( Toto Sakata Dance)
Wanangu wa Panya Road (Sakata Dance)
Chaukucha kwa Sadali (Sakata Dance)
Na Unyamani Biomi (Sakata Dance)
Kizonga kwa Natali (Toto Sakata Dance)

Aaaah …. aaaah …. aaaa… (Unavyodance) (Waonyeshe Unavyodance)​
 
Ochu Sheggy ft Aneth – Kiingereza


Seductive Records
Iyelele mama, iyelele mama eeh (×2)

Kale kasuti kangu ka zawadi alikonipa kaka wa Dar-Es-Salaam
Ndio katanipa umaridadi ukumbini kote watanifahamu
Naomba uipige pasi mke wangu ila chunga usiunguze
Nina kikao na wazungu mama inatakiwa nipendeze
Ona ulivyokosa haya unanifanya mtoto mdogo
Umekalia umalaya sema unakwenda nyumba ndogo
Utaongea nini na wazungu wakati hujui kiingereza?
Umesahau mke wangu mbona nikilewa naweza
Tena kata fujo piga pasi naomba uniharakizie pombe
Nikilewa mapema itakuwa safi ili nikifika nikikoroge

Kiingereza (mama wee) nikilewa naweza
Kiingereza (eeee) ni rahisi usijali mke wangu
Kiingereza ngoja nilewe nitakuonyesha
Kiingereza usijali ni rahisi utaona ninavyoongea
Kingereza…

Kiingereza chenyewe mpaka ulewe aibu mume wangu
Kwanza siendi na wewe nakwenda mwenyewe wala usijipe tabu (wewee)
Usiposema ukweli kasuti kako nitakaloweka
Unaeleza nzuri naona unataka talaka
Utakua unanionea na unatumia mfumo dume
Sio kama nakuonea nawe tumia mfumo jike
Kwani humu ndani mwanaume nani naomba nikuulize
Kwani humu ndani mwanamke nani naomba unielezee
(ah ah) Sitaki kubishana na wewe weka moto kwenye pasi
Pombe nitafuata mwenyewe naona ushaanza nuksi

Kiingereza (mama wee) nikilewa naweza
Kiingereza (eeee) ni rahisi usijali mke wangu
Kiingereza ngoja nilewe nitakuonyesha
Kiingereza usijali ni rahisi utaona ninavyoongea
Kiingereza…

Kingereza (x5)
Ahma wee, Ahma wee, Ahma weeee(x4) yeleleee…yeyeyeyeyeyeye….
Kiingereza.​
 
Lavalava – Tuachane


Aaaaah aaaah aaaaah aaaah
Kama imeshindikana kunirudia isiwe taabu
Usiuforce moyo kupenda usipostahili
Ya nini kung’ang’ania nishachoka kuwekwa sub
Siwezi ooh na mapenzi nishaghaili
Tena niko tayari vipigwe vinumbi kengele kwa sherehe
Kinaghaubagha mbele ya umati tuachane
Na kama hautojali tuite waumini mapadre na masheikh
Yaishe labda sa kwa nini tutesane
Kweli we ndo nikupendae ila unanipa ghadabu jina
Tusitoane nyongo
Na kama umenichoka eh niache kistarabu jina
Usinipe chongo miee

Mwili umebaki kongoro nyama sina ni mifupa
Naiona domboro kabisa siwezi furukuta
Penzi kiporo limeshachina linanuka
Kuishi kokoro purukushani kutwa kucha iyeeh

Bora tuachane bora tuachane siwezi
Bora tuachane yamenishinda mapenzi
Mi naona bora tuachane eeh tuachane siwezi
Bora tuachane yamenishinda mapenzi

Ni dhahiri kisima kimekauka maji
Ndo maana naona ata sina maana tena
Nilifikiri mi gonjwa langu limepata mponyaji
Umeniongezea homa mwili wote watetema
Mi naona basi labda si ridhiki yangu
Kama hunitaki acha tu niende zangu
Ya nini mishikaki natafuta boda yangu
Nijinafasi niipande peke yangu

Mwili umebaki kongoro nyama sina ni mifupa
Naiona domboro kabisa siwezi furukuta
Penzi kiporo limeshachina linanuka
Kuishi kokoro purukushani kutwa kucha iyeeh

Bora tuachane bora tuachane siwezi
Bora tuachane yamenishinda mapenzi
Mi naona bora tuachane eeh tuachane siwezi
Bora tuachane yamenishinda mapenzi

Ooh liwalo na liwe
Na namba zako ntafuta ama unasemaje
Liwalo na liwe
Nguo zako mashuka wacha nikazimwage
Liwalo na liwe
Sio kama nmesusa ila ntafanyaje
Liwalo na lile
We kaa mi nanyanyuka acha tu niage​
 
RAYVANNY - MBELEKO



Wa Safi
Mmmmh
alisemanga dunia ina mapambo yake eeh
ukiacha majumba pesa magari ni wanawake eeh
nimezunguka aah, nimefika kwake eeh
siwezificha nimeshanasa
kwa pendo lake eeh



halabaani
kakuumba kimwana, mwenye sifa ya upole
ata mama kakusifu sana, kitofauti na wale (wajane)
kule nilizama tafadhali niokoe mamamaa. unipulize nipoe

We ndo my queen baby my only, sitopenda uende mbali one day x2
Naficha mbeleko kwa ajili yako (jiachie tu nikubebebe) x2
We kama mtoto mii nakubembeleza (jiachie tu nikubebe)
Na jicho lako lakungu kama la nikonyeza (jiachie tu nikubebe) eeh ummmh umh

Umenivuta kwa ulembo mpaka matendo umenikamata
kisura shepu sio tembo taweka nembo watoto kupata (x2)

koleza motoo tupike tembele kisamvu cha nazi njegele
sisi kutishe kelele sikwachi iih
Linda nashamba wasije ngedele, kuku niitee kwa muchelee
Mii sipigani na wewe manatii iih
Ndio manaa kwako nimezamaa sitaki mii wanitowee mama maaa
Unipulize nipoee

We ndo my queen baby my only, sitopenda uende mbali one day (x2)
Naficha mbeleko kwa ajili yako (jiachie tu nikubebebe) (x2)
We kama mtoto mii nakubembeleza (jiachie tu nikubebe eeh)
Na jicho lako lakungu kama lanikonyeza (jiachie tu nikubebe eeh)

Naficha mbeleko kwa ajili yako (jiachie tu nikubebe) x2
We kama mtoto mii nakubembeleza (jiachie tu nikubebe eeh)
Na jicho lako la kungu kama la nikonyeza
(jiachie tu nikubebe…jiachie tu nikubebe…jiachie tu nikubebe)
We kama mtoto mii nakubembeleza
Na jicho lako lakungu kama lanikonyeza
Ayo Laizer

 
Diamond Platnumz ft Rayvanny – Salome


Kioo hakidanganyi mama umejipodoa umepodoka
Mwendo na shepu vyote mwanana mimi suruari yanidondoka
Tukimbizane nini salome wangu hiyo michezo ya jogoo
Mbona watizama chini salome wangu ukimuona jongoo
Inama kidogo shika magoti nimesimama kama ngongoti
Mtoto jojo sio roboti chumbani bingili bingili sambasoti

Unanitekenyaga ukinyonga salome unanitekenyaga ukinyonga
Unatikenyaga ukinyonga kweli unanitekenyaga ukinyonga aah
Hoera makulu vane hoera ngambe Hoera na Zari hoera ngambe

Utamu kolea aprokoto ting’ari ting’ari ndani kwa moto
Nitamnyongea msokoto niteme sumu kali kama koboko
Eeeh Mapenzi yananipa shida shida maama ni donda lisilokuwa na tiba
Tiba bwana usije baby kanicharanga kanichambua moyo kama karanga
Mie baby kwenye msambwanda huwa siendagi ngenge ni nganganga.

Unanitekenyaga ukinyonga salome Unanitekenyaga ukinyonga
Unatikenyaga ukinyonga kweli unanitekenyaga ukinyonga Aaaha!
Hoera makulu vane hoera ngambe hoera na Zari hoera ngambe

Mie mwenzako nyang’anyang’a mie binzari we ndo nyanya
Baby kwangwaru isimamie kama kangaroo
Ibane kangwaru babu Juma mpige kwakwaru
Kwakwaru kwakwa chambua kama karanga sasa chambua kama karanga
Ichambue kama karanga salome chambua kama karanga

I say washa washa moto washa songa songa ugali songa songa
Mpaka chini mpaka chini
Wenye wivu wajinyonge leo wanye wivu wajiinyonge
Wenye wivu wajinyonge salome wenye wivu wajinyonge
Wenye wivu wajinyonge kweli

Wanakodoa kodo wanakodoa (macho kodo)
(wale kodo)
Ukinyonga (wanakodoa kodo wanakodoa)
Ukisonga (wanakodoa kodo wanakodoa)​
 
Professor Jay ft Diamond Platnumz – Kipi Sijasikia


Niliacha kazi nifanye muziki wakatabiri nitalost, Wengine wakanishawishi tuloge kuondoa mikosi, Nakomaa na muziki ingawa jua la utosi, Naamini wote tunapita na kamwe maiti haijioshi Jina langu lishatumika sana kutajirisha watu, Nyota ndogo alishasema kuna Watu na viatu, Bunduki haiui watu ila watu ndio wanaua watu, Dunia kama jalala tazama kwa Jicho la Tatu,
Ni saa mbaya watu wanahusda na roho mbaya , Tunawaita watakatifu kumbe ndio mavimpire, Yalisemwa mengi demu wangu alivyotoroka, Ni Fundisho tosha na changamoto kwa Mwanachoka Nimepita Mengi mitihani ya kila Namna,
Ndio maana mi sishangai wakiniita mbeba Lawama,
Washkaji wengine fake kwenye deal hawakujui Wanadhani kila jogoo akiwika ni Asubuhi,
Riziki hamuwezi iziba labda mtaichelewesha tuu,
Mnakesha mnishushe Mwenyezi ananipaisha,
Kote mlikobana kidume ndio Natusua,
Mnanijua,Nakamua, Roho za wanga zinaungua
PLATINUM!!!

CHORUS
Unaehukumu ni wewe Mwenyezi Mungu naomba unilindeee..
Kwenye hii vita milele Basi nishike mkono nishindeee..
Unaehukumu ni wewe Mwenyezi Mungu naomba unilindeee..
Kwenye hii vita milele Mwanachoka daima Nishindeee..

VERSE 2
Walishazusha nimekufa, Eti nimepata ajali,
Washindwe na walegee Mwenyezi niepushie mbali
Wakasema nina Ukimwi kwa kuwa nilikonda ghafla,
Wanataka kunizika mzima Kabla sijafa,
Waliosema nina Ngoma wengine tushawafukia, Wanaoomba nife leo naamini Watatangulia,
MAMA Pumzika Pema..Daima tunakulilia,
Na bado wanachonga sana but MAN the KING is here!!
Daima mtaji wangu ni nguvu zangu mwenyewe, Simwamini mtu kamwe najiamini mi mwenyewe, Hata nikinywa maji wanadai nakunywa pombe, Mi sijali, I KNOCK THEM HARD Mwanalizombe! Bado tu napambana kibarua kisiote nyasi,
Daima sitawadhuru wale wote walioniasi,
Nikikaa kimya msidhani Sijasikia,
Sio Bahati sio Ngekewa ni sauti Iliyobarikiwa HOLLA!!!

CHORUS
Unaehukumu ni wewe Mwenyezi Mungu naomba unilindeee..
Kwenye hii vita milele Basi nishike mkono nishindeee..
Unaehukumu ni wewe Mwenyezi Mungu naomba unilindeee..
Kwenye hii vita milele Mwanachoka daima Nishindeee..

Verse 3
Mungu walaze pema Waliosemwa wakajiua,
Ingawa wote tunapita naamini Maisha ni hatua, Maneno ya watu Sumu, Yanaponya na Yanaua, Please nipe ujasiri mpaka siku Ukinichukua,
Wape nguvu wale wote waliokata tamaa, Maneno yanaleta hila na Mzozo kwenye mitaa, Wanahesabu mabaya tuu na mema hawayaoni, Wanakuchekea Machoni, Wanakuroga Moyoni,
Wanacheka chinichini wakati una Msiba,
Wa kwanza kukutangaza kwa watu ukiwa na Shida!!
Wanatamani wapangue kila mola alichopanga, Wanatangaza Amani huku wameficha MAPANGA​
 
Mbona wanamuziki wa tanzania huwa hawa shoot muziki zao nyingi tz? alafu jana nimeskia Rayvanny akisema anataka ku relocate Kenya kwa interview ya Citizen TV...Rose Muhando ana toroka...Wema sepetu pia nimeskia akiwa na interest ya kuhamia nairobi...Diamond na mkewe wanaishi Afrika Kusini...Hivi, Bongo kunani?


Diamond anaishi Tanzania, nenda ofisini kwake WCB utamkuta. Rayvanny anawateka Kenya kwa kuwaambia hivyo, yupo Bongo milele. Hao wengine ni reject.

Hamna Mtanzania mwenye akili timamu anayetamani kuishi Kenya.
 
MwanaFA Featuring G. Nako Warawara - Mfalme


[Mwana FA]
Look around brother
Choir Master!
Ghetto Gospel (Yes!)
Keeping the good music alive!

[G Nako]
Kanipa maarifa loloo (nampa sifa)
Yakanipa nyadhifa loloo (nampa sifa)
Kaziba nyufa loloo (nampa sifa)
Olooh! (Mfalmee!)
Kanipa maarifa yakanipa nyadhifa
Ikajipa sifa, kaziba nyufa
Namwiita ye Mfalmeee
Mfaaalmeee

[Mwana FA]
Holla at ya boy!
Sinung'uniki sina viatu wenzangu hawana miguu
Hawalalamiki wanamshukuru Aliyejuu
Siwezi nikamletea makuu maombi ya kibraza du
Mbwembwe za kuomba magari nawaachia son I'm cool
Kama kipande cha kwanza cha mbao kwenye safina
Mimi ni kitu cha Mungu nafanya alichonituma
Kanipa ubongo na misuli na roho ya kitajili
Sina kitu ila sina roho mbaya tunaishi vizuri
Fukara nayeshukuru au tajiri nisiyekufuru
Najua bata najua hustle mi ni njiwa na kunguru
Kuna vingi vya kumuomba Mungu kabla hujamuomba utajiri
Naishi kwa mapenzi yake hakuna kitu naona hatari
Unapata ulichoandikiwa Mungu hakupi kama hataki
Hata ukipora itapotea ili mradi yatimie maandishi
Mi ndo vito wa kolioni vitu vinaisha my way
Nife nikiwa muumini na everything gon' be I man

[G Nako]
Kanipa maarifa loloo (nampa sifa)
Yakanipa nyadhifa loloo (nampa sifa)
Kaziba nyufa loloo (nampa sifa)
Olooh! (Mfalmee!)
Kanipa maarifa yakanipa nyadhifa
Ikajipa sifa, kaziba nyufa
Namwiita ye Mfalmeee
Mfalmeee
Kanipa maarifa yakanipa nyadhifa
Ikajipa sifa, kaziba nyufa
Namwiita ye Mfalmeee
Mfalmeee

[Mwana FA]
Najua anamipango, anafungua milango
Ndo anatoa michongo, namwita Mfalme Wa Jungle
Boss wa dunia yangu kanipa nguvu na ubongo
Mwenye maamuzi ya mwisho angetaka angeniumba fungo
Mafala wana midomo ka vicheche usiwe kati yao
Wanaosema wenzao rudi angalia maisha yao
Wengine hawana hata kalaki wanaita wenzao maskini
Haki nawaombea mabaya kama wanavyoniombea mimi
Ni hata mtoa wa roho ni malaika, na nahisi ataenda peponi
Achia kuhukumu sio kazi yako, we ni mwenzangu na mimi
Na una dhambi kama mimi, na hatujui kubwa za nani
Labda zako labda zangu, sio kazi yetu ni ya Maanani
Usiniwaze sana mi nawaza maisha yangu
Sina hata mia ya urithi vyote hivi ni vya kwangu
Nshaenda shule bila viatu, nshatoa funza kama buku
Na ipo siku utaniheshimu ama utaheshimu hela zangu

[G Nako]
Kanipa maarifa loloo (nampa sifa)
Yakanipa nyadhifa loloo (nampa sifa)
Kaziba nyufa loloo (nampa sifa)
Olooh! (Mfalmee!)
Kanipa maarifa yakanipa nyadhifa
Ikajipa sifa, kaziba nyufa
Namwiita ye Mfalmeee
Mfalmeee
Kanipa maarifa yakanipa nyadhifa
Ikajipa sifa, kaziba nyufa
Namwiita ye Mfalmeee
Mfalmeee
Kanipa maarifa loloo (nampa sifa)
Yakanipa nyadhifa loloo (nampa sifa)
Kaziba nyufa loloo (nampa sifa)
Olooh! (Mfalmee!)​
 
Lady JayDee - Yahaya


Chorus
Yahaya unaishi wapi Kwani jina lako halisi nani Yahaya eeehh
Oooh Yahaya, Oooh Yahaya, Oooh Yahaya
Maskani yako Kinondoni, Nyumba namba haijulikani Yahaya eeeehh
Oooh Yahaya, Oooh Yahaya

Verse 1
Huyu kijana mwenzetu, Kila siku tupo nae maskani
Anakula ofa za watu, Anakoishi hata hapajulikani
Tumetafuta, tumeuliza, hakuna ajuae
Anavyozuga, anavyopita Si umdhaniae
Na hafananii kabisa, na fix anazofanya
Akidanganya kwa kina, Unaingia kingi unafuata, kumbe hana helaaaa

Chorus

Verse 2
Kwa story za vilingeni, Utafikiri kweli yeye ndio bosi
Suruali zake na mashati, Anasema anafanya kazi benki
Mara anasema usalama wa Taifa, Hakuna ajuae
Kalubandika wa kizazi kipya, usomdhaniae
Na hafananii kabisa, na fix anazofanya
Akidanganya kwa kina, Unaingia kingi unafuata, kumbe hana helaaaa

Chorus

Verse 3
Mara anasema usalama wa Taifa Hakuna ajuae
Kalubandika wa kizazi kipya Uso mdhaniae
Na hafananii kabisa na fix anazo fanya
Akidanganya kwa kina, unaingia kingi unafuata Kumbe hana helaa​
 
Wasanii ambao hawashoot Tz ni wachache kushinda ambao wanashoot Tz na hata ambao hawashoot Tz ni kwa vile wanawafuata directors huko waliko na hiyo ni namna ya kupunguza gharama. Ni kama Eddy Kenzo na wimbo wa Shauri yako alivyoamua kuja kushootia Tz, akiwa anamfuata Director.

Bongo Bahati Mbaya, Tupa Shuka, One day na Tuachane ni miongoni mwa nyimbo mpya ambazo zimefanyiwa shooting Tz.
jibu nzuri...now that wasn't so hard was it? Annael and others dont be insecure.. we are not jealous of ur music industry...we dont even have the same style of music...Bongo is totally different from Kenyan music...Bongo is doing great...thats good...but we all have different tastes...personally i dont even like Bongo but one thing I know, its 10 times better than what we have here...
 
Diamond anaishi Tanzania, nenda ofisini kwake WCB utamkuta. Rayvanny anawateka Kenya kwa kuwaambia hivyo, yupo Bongo milele. Hao wengine ni reject.

Hamna Mtanzania mwenye akili timamu anayetamani kuishi Kenya.
hehe...there we go again....making everything about Kenya vs Tz...some ppl need to grow up...
 
jibu nzuri...now that wasn't so hard was it? Annael and others dont be insecure.. we are not jealous of ur music industry...we dont even have the same style of music...Bongo is totally different from Kenyan music...Bongo is doing great...thats good...but we all have different tastes...personally i dont even like Bongo but one thing I know, its 10 times better than what we have here...

Mimi sio mpenzi sana wa music but nikisikia mziki wa Congo najua huu ni Congo, Nigeria unajua, South afrika ukipigwa unajua hii ni mziki wa bondeni. Lakini mziki wa Kenya hakuna identity kuna wengine kuimba Kikuyu, wengine kuigiza wazungu, wengine wanaimba ki pwani, wengine kikamba hao ndio nikisikia hata na redio nazima yanii kuna.miziki hata ikipigwa mbwa anakimbikia nimeisikia Kenya looh.
 
Back
Top Bottom