East Coast of Africa Music HQ- The Empire of Tanzania

East Coast of Africa Music HQ- The Empire of Tanzania

Rayvanny - Natafuta kiki


Verse 1
Nataka nitoke kwenye gazeti
Niuze sura!
Niseme ninatoka na Jokate
Kitandani kwisha na Feza Kessy
Ama Snura
Nilete matata mpaka kwa Grace
Kwenye redio zote, mpaka runinga
Nitangaze kwa kuvimba
Kwamba Lulu anayangu mimba
Au niwatukane wote wanaoimba
Kwa dharau na kuvimba
Mpaka yule anajiita Simba!
Niseme madam Ritha katetema
Akiniona anashindwa hata kuhema
Au Vanessa kanena ananitaka na Jux atatemwa
Nataka nifanye sinema
Kwa alozaa na Ney, Siwema
Kiki ipi iko njema, au niende kwa Sepetu Wema?
Chorus
Ati ntokeje?
Mwenzenu ntokeje?
Ati ntokeje?
Mwenzenu ntokeje?
Verse 2
Nasikia Uwoya mkali, wanasemaga Shishi asali
Wolper atakubali akimwage ki Harmo chali
Ninatafakari, kichwani maswali
Nimtongoze Zari, akijua Mondi si hatari?
Ee-hee, Rose Ndauka, Kajala pia hadi na Salama
Mose Iyaba asijeninua kwa Aunty lawama
Mkubwa Fella, Tale Salami leaders nizushe pesa wamenipiga
Chege na Madee wasije nikwida
Iyowee!
Nataka nibadili ratiba, kwangu isije leta msiba
Nitoke Wasafi niende kwa Kiba
Chorus
Ati ntokeje?
Mwenzenu ntokeje?
Ati ntokeje?
Mwenzenu ntokeje?
Outro
Nataka nifanye masekere
(Sekere oh sekere)
Sekere
(Sekere oh sekere)
Sekere
(Sekere oh sekere)
Yaani Bongo nzima makelele
(Sekere oh sekere)
Sekere
(Sekere oh sekere)
Sekere
(Sekere oh sekere)
Iih! Nikinukishe kinoma noma
(Sekere oh sekere)
Sekere
(Sekere oh sekere)
Sekere
(Sekere oh sekere)
Iih! Macho kuvimba wataisoma
(Sekere oh sekere)
(Sekere oh sekere)
(Sekere oh sekere)
Ta ntira rara

 
Young Killer | Ft. Mr Blue | Kumekucha

Verse 1 – Young Killer
Waswahili washasema shughuli kumchezesha Young Killer ngoma ya watoto
Ona wanavyohangaika kama wamemeza ugali wa moto
Bongo nyoso, walisema wakubwa
Mswahili hata akose company vipi sehemu yoyote hawezi kwenda na muda
Verse 2 – Mr Blue
Akili haifanyi kazi bila kuwa na maarifa
Mwanaume kwenye kazi huwaga silewi sifa
I'm the best sijasubiri nikifa
Nazichana top 10 niite Doggy wa Latifah
Popote kambi ukiniweka natusua
Na ukweli sio dhambi, dhambi ya uwongo kuyazua
Aah unafuga kitambi, hilo si jipu ungetumbua!
Mama angu na chambi chambi za kuuza vitumbua
Anatulea tunakua unajifanya unatujua
Aah, unatujua!
Aah, unazingua
Mic kama mtaji, bila hii sifanyi
Mungu kanipa kipaji kweli sidanganyi
Mapenzi na kazi, mmh, kweli sichanganyi
Na mi na dogo dogo kweli hatufanani
Harufu kama choo nasaka dough kila mahali
Flow inakaba koo, ni soo bila kabari
Bizzy Babylon, niite upepo unapovuma
Nachana kwa microphone na mtoto wa kisukuma, Killer!
Hook
- Mr Blue -
Wacha si tufanye mambo kama yalivyo
Wacha si tupige dili kama zilivyo

- Young Killer -
Ni Msodoki na Baisa, sa shituka
Waliolala wambie kumeshakucha

- Mr Blue -
Wacha si tufanye mambo kama yalivyo
Wacha si tupige dili kama zilivyo

- Young Killer -
Ni Msodoki na Baisa, sa shituka
Waliolala wambie kimeshanuka
Verse 3 – Young Killer
Moyo hauridhiki, sio mboyoyo za wanafiki
Nashangaa emcee mchoyo anavyogawa mashabiki
Ukiwa loyal unani-fit
Maana kwenye moyo ukizama umezama huogeli hata boya ulivae vipi
Ni Msodoki na Baisa, aah, stuka
Leo namtusi mamba kwenye mto na navuka
Sina wivu wala pupa
Maana ridhiki anaegawa Mungu: ndiye anayetunyima na anaetupa
Naposikia beat kali ni raha tu
Hapo hisia zangu zina-enjoy iwepo ndani sayari ya tatu
Nakaza kamba za viatu, wote wanatambua
Baada ya giza ni Young Killer anaongoza kuficha watu
Halafu hamuwezi niona mimi tu
Zingine mechi ngumu na dakika ni tisini tu
Siwezi uchukia umasikini, duh! Japo siupendi
Ila shida ingekuwa sumu basi tungekufa wengi
Siku zinakwenda kama mbio za defender
Ila naomba Mungu nidumu kama nguo nisioipenda
Na demu mmoja nampenda
Sina skendo ya kugonganisha magari, sijawahi kuwa daraja la Surrender
Kila kukikucha nakua, uwezo unaongezeka najua
Mateso yakizidi ndo kutusua
Young Killer usicheze ngoma ya watoto
Ona wanavyohangaika kama wamemeza ugali wa moto
Nyoko!
Hook
- Mr Blue -
Wacha si tufanye mambo kama yalivyo
Wacha si tupige dili kama zilivyo

- Young Killer -
Ni Msodoki na Baisa, sa shituka
Waliolala wambie kumeshakucha

- Mr Blue -
Wacha si tufanye mambo kama yalivyo
Wacha si tupige dili kama zilivyo

- Young Killer -
Ni Msodoki na Baisa, sa shituka
Waliolala wambie kimeshanuka

 
Roma Feat Story - 2030



Tanzania eeehhh (Tongwe Records Baby)
nchi yangu ooohhhh…
Verse 1
Huwezi kuijenga roma haikujengwa kwa siku moja
Iwe kwa raha leo au simba mtoto tanga watakuja
Hata pacho pia ni mwamba ila bado anakata viuno
Kaskazini bila tanga ni msondo bila gurumo
Alisema juu ya mwamba atalijenga kanisa
Na halitatikisika waumini tuianze misa
Kwenye njaa kula kuku aliyechinjwa na padre hewallah
Adhana ikilia amka ukamuombe allah!
Bwaa sheikh mrudie Mungu masanja kawa mchungaji
Sujudu Mecca Madina tajiri hataki kuhiji
Maulid Ubungo Kibangu ndo mishahara ya madrasa
Ona rafiki wa padre kawa muhasibu wa kanisa
Tenda wanapeana kindugu mwanangu kua uyaone
Familia ilikata ringi na mama alibaki mjane
Sikuwa na damu ya kiarabu kwamba nitayarithi mabasi
Dingi hakutupa msingi ona gari twaifanya taxi
Tazama gongo la mboto mtoto kamzaa mtoto
Na atalelewa na nani baba ake mmemfunga keko
Wape buku waue winga wale watoto wa morocco
Mungu atazidi kukulinda kesho utaiona sabato
Mzee wa bandari kastaafu kajenga banda la uani
Ana wake wa3 je watoto watarithi nini?
Ndo chanzo cha kurogana na ku2piana majini
Huyu akimpandisha makata yule maimuna subian
Maana pesa ndo ilifanya tusiwe na tanga ndugu
Pesa ilileta ubaguzi kati ya loyola na pugu
Pesa ndo ilichochea beef ya nice na dudu
Na pesa ndo ilimaliza vita ya ruge na sugu
Chorus
(Tanzania eeehhh)
Mwanangu kua uyaonee boss acha kisirani gonga muhuri tuwahiii
(Nchi yangu ooohhh)
Mwanangu kua uyaone Traffic hasira za mkeo barabarani hazifai
(Tanzania eeehhh)
Mwanangu kua uyaone wanahonga mashabiki ngoma zao wazi-request
(Nchi yangu ooohhh)
Mwanangu kua uyaone Udini wa ma-presenter wapagani unatucost
Verse 2
Aminini nawaambieni ujana ni maji ya moto mtoto
Humzika mama leo mama anamzika mtoto
Ndo maana mama alisema nisimchumbie mmachame
Muraa shusha mapanga naileta posa tarime
Leo bahari imechafuka mpemba haishemu karafuu
Hatari kama nungwi nahodha sio kirikuu
yakhee nirushie mtumbwi mie mwamba sio kichuguu
Hii ni vita ya msambaa mbondei usitie maguu
Ona kipindi cha bunge dodoma inanuka ngono
Spika akiahirisha bunge wengi watau-support mgomo
Wabunge mnadai posho muhonge dada zetu
Kuna wanafunzi wa mama salma vyuoni usicheze peku
Wazanzibari hawaioni thamani ya huu muungano
Ila kulichoma kanisa sio njia ya kuvunja agano
Sioni sababu ya ubaguzi na kuua wasio na hatia
Wakati aliochanganya mchanga mchanga umeshamfukia
Muislamu gani unahonga bongo movie mamilioni
Mama anakufa mwaisela kakosa dripu ya quinine
Ni heri ujenge msikiti tuitukuze mitume
Anasa za bakulutu unatunza wacheza sebene
Unamuheshimu ramadhani unazini mbele ya shaban
Kama ilishushwa quran twendeni misikitini
Anaedhihaki msahafu pengine kanisa halijui
So kulichoma kanisa ni kuuza bible dubai
Usihofu kumpoteza mmoja ili kumi waishi vema
Watanzania tuna uoga sio amani mnadanganywa
Sacrifice for your son and daughter amka kifikra
Damu yako iwe chachu ya ukombozi dokta ulimboka
Mkinga usimuue mama ili uongeze kipato
Utajiri upo kaburini watu wamekufa na ndoto
Leo ridhiwani haufanani na makongoro dah!!
Sina hela ya kiroba rashidi nigongee ugoro
Suka kaiangusha lori ya mafuta yote magendo
Waziri anaziuza pembe za ndovu na meno ya tembo
Nchi imejaa misitu tuna uhaba wa madawati
Tunakula vitu feki TBS mko wapiii
RPC usitume kikosi ili uishushe chadema
Italipwa damu ya mwangosi iringa semeni amina
Okoa wagonjwa wa saratani mpakani zuia wakimbizi
Kuliko kumwaga pesa kwenye tume za uchunguzi
Muhimbili naumwa goti eti dokta kapasua kichwa
Mbeya wanapigwa nyundo ili raia wauze mabucha
Amana wanatelekeza watoto wanalia mwananyamala
Wanatuua na hawaendi jela Jela anakwenda Kajala
Chorus
(Tanzania eeehhh)
Mwanangu kua uyaonee boss acha kisirani gonga muhuri tuwahiii
(Nchi yangu ooohhh)
Mwanangu kua uyaone Traffic hasira za mkeo barabarani hazifai
(Tanzania eeehhh)
Mwanangu kua uyaone wanahonga mashabiki ngoma zao wazi-request
(Nchi yangu ooohhh)
Mwanangu kua uyaone Udini wa ma-presenter wapagani unatucost
Verse 3
Sauti hii itasikika mpaka oldonyo lengai
Nikifa naomba nizikwe tanga na mje kwa shambalai
U can kill me bro but u wont kill what am standing for
Usiutamani urithi wa baba ikimshuka cd4
Eti tuzo sikustahili haa haaa hii ni hatari
Tuzo ina chapa ya nani ya kaisari mpe kaisari
Hii sio masaki ni ngaramtoni mama anaiuza dadii
Muziki umejaa stress kila nyumba ina msanii..(woyoooo!!!)
Yanga wamemfukia mbuzi golini simba ana bundi
Viongozi wanataka umate umate hawaujali ushindi
Utawasikia chuji kachuja kiburi choma mahindi
Kapigwa ligi ya jogoo shahidi kamati ya ufundi
Vijijini 2po wengi mleteni daktari bingwa
Ana ngoma utasikia kalogwa twende kwa mganga
Pesa za kujikimu ndo ulichongesha kitanda
Kulea mimba sio mchezo ba kijacho haujajipanga
Profesa kanyimwa penzi utasikia carol kadisco
Carol analea ndugu kwa pesa ya bodi ya mikopo
Poleni mnaotafuta C mwaka wa 4 mna risiti
Huku headmaster kaenda mjini eti shule imeishiwa chaki
Msiwaue wachimbaji wadogo geita inalia
Kaburu umempa migodi udsm tuna engineers
Unapewa contena la condoms uionge dhahabu
Mv spice ilipozama tv inaonyesha taarabu
Kamanga hawaiweki lami ili 2vukie busisi
Dereva usinitoe kafara ili utimize hesabu ya boss
Sina cha kuweka rehani kwenye asasi za mikopo
Bajeti ya kilimo kwanza mkulima silioni soko
Tanga mmekosa nini amkeni acheni umwinyi
Hawa wachaga hawatuwezi ona manka bara 20
Bandari chanu relwe chali makamba iinue katani
Zito akiroga kasulu si tunamrogea pangani
Uchafu wa mrisho unafanya msafi aonekane benja
Msisadiki magazeti waandishi wengi kanjanja
Vijana ndo nguvu kazi ila wengi wamejaa lutindi
Mitaani wamekata ringi hadi figo wanaziweka bondi
Majibu ya postmotam ameshayanunua wakili
Na hakimu kapewa kiwanja kimara apige kufuli
Cheki dola wanainunua kesi napewa kapuku
Nawa mpole kama ngamia mbele ya hakimu wa kisutu
Chorus
(Tanzania eeehhh)
Mwanangu kua uyaonee boss acha kisirani gonga muhuri tuwahiii
(Nchi yangu ooohhh)
Mwanangu kua uyaone Traffic hasira za mkeo barabarani hazifai
(Tanzania eeehhh)
Mwanangu kua uyaone wanahonga mashabiki ngoma zao wazi-request
(Nchi yangu ooohhh)
Mwanangu kua uyaone Udini wa ma-presenter wapagani unatucost

 
fair enough.....unaeza kuwa unasema ukweli ila mbona wengine wachahe wana relocate either SA or Kenya...wakienda SA ama Nigeria nitaelewa kwani nchi hizi zina music industry zenye nguvu...ila mbona kenya...Kenya's music is not better than Bongo's...sielewi..pengine iwe govt yenu inawanyanyasa sijui...ndio maana nikauliza...sina ubaya wowote..kuuliza tu..thread nzuri hii
Ungetaja wasanii Watz wanaorelocate Kenya ingekuwa vizuri.

By the way hao wachache ni wale walioishiwa kisanii hapa TZ nahwana soko huku kama kina Mr Nice na wasanii walioshindwa kupenya soko gumu hapa Bongo lakini kwa Kenya ni rahisi kuingiza na kuburuza wasanii wa huko.

Kuna siku nilisoma msanii mmoja hajulikani hata jina hapa TZ lakini huko Kenya ni lulu na maarufu!
 
Mbona wanamuziki wa tanzania huwa hawa shoot muziki zao nyingi tz? alafu jana nimeskia Rayvanny akisema anataka ku relocate Kenya kwa interview ya Citizen TV...Rose Muhando ana toroka...Wema sepetu pia nimeskia akiwa na interest ya kuhamia nairobi...Diamond na mkewe wanaishi Afrika Kusini...Hivi, Bongo kunani?

Mada inazungumzia "Muziki" wewe unazungumzia "Makazi" wapi na wapi?
 
Lady JayDee - Yahaya


Chorus
Yahaya unaishi wapi Kwani jina lako halisi nani Yahaya eeehh
Oooh Yahaya, Oooh Yahaya, Oooh Yahaya
Maskani yako Kinondoni, Nyumba namba haijulikani Yahaya eeeehh
Oooh Yahaya, Oooh Yahaya

Verse 1
Huyu kijana mwenzetu, Kila siku tupo nae maskani
Anakula ofa za watu, Anakoishi hata hapajulikani
Tumetafuta, tumeuliza, hakuna ajuae
Anavyozuga, anavyopita Si umdhaniae
Na hafananii kabisa, na fix anazofanya
Akidanganya kwa kina, Unaingia kingi unafuata, kumbe hana helaaaa

Chorus

Verse 2
Kwa story za vilingeni, Utafikiri kweli yeye ndio bosi
Suruali zake na mashati, Anasema anafanya kazi benki
Mara anasema usalama wa Taifa, Hakuna ajuae
Kalubandika wa kizazi kipya, usomdhaniae
Na hafananii kabisa, na fix anazofanya
Akidanganya kwa kina, Unaingia kingi unafuata, kumbe hana helaaaa

Chorus

Verse 3
Mara anasema usalama wa Taifa Hakuna ajuae
Kalubandika wa kizazi kipya Uso mdhaniae
Na hafananii kabisa na fix anazo fanya
Akidanganya kwa kina, unaingia kingi unafuata Kumbe hana helaa​

The only Tanzanian song I like. I am not a huge fan of Bongo music. Pia kuna mwana by Ali Kiba
 
Inasadikika kwamba lugha hii ndiyo Adam na Eva walikuwa wakiongea wakiwa bustani ya Aden. Baadhi ya maneno ya kiswahili yanasadiifu ukweli huu kwamba kiswahili ndiyo lugha ya kwanza ya binadamu.
hahahahahahahahahahahahahaha. Kiswahili ni a Bantu language with a lot of borrowed Arabic words na other words from other languages. Alafu unasema Adam and Eve were speaking Swahili, a language which developed in AD years? Ama you are just using it kwa your text?Hope hauko serious man
 
The only Tanzanian I rate ni Freddy Mercury. Lead singer wa Queen, you know, the super famous rock band. Generally I find Bongo genre very boring. Thats just me
 
The only Tanzanian I rate ni Freddy Mercury. Lead singer wa Queen, you know, the super famous rock band. Generally I find Bongo genre very boring. Thats just me

I used to like Bongo music by the likes of Prof J, Ali Kiba, Marlaw but the current crop the likes of Diamond, nonono! They are trying to change Bongo Music to have Afro Beat, something i don't like at all! They should just have maintained their Bongo flavor, Afro Beat leave it to Nigerians.
 
Kenya namkubali sana Jaguar, nonini na wyre pia yule jamaa alieimba genge nimemsahau.
 
Back
Top Bottom