East Coast vs TMK Family nani alikuwa mkali?

East Coast vs TMK Family nani alikuwa mkali?

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
TMK Wanaume Family ni kundi la muziki wa kizazi kipya kutoka Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam Tanzania. Kundi lilianzishwa rasmi mnamo Septemba 16 2002 mjini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa albamu ya Juma Nature iitwayo Ugali na hadi sasa limejijengea umaarufu katika albamu zake mbili ilizotoa ambazo ni Kutokea Kiumeni na Ndio Zetu.

Wasanii wa kundi baadhi kabla ya wengine kujiengua ni Juma Nature, KR, Doro, D Chief, Mh Temba, Mzimu, Luteni Karama, Chegge, Yp, Y Dash, na wengineo, halafu baada ya kutengana kukawa na "Tmk Wanaume Halisi" na Tmk Wanaume. Tmk Wanaume kiongozi wa kundi ni Mh Temba na Chegge wakati Tmk Wanaume Halisi kiongozi wa kundi ni Juma Nature na Inspector Haroun.​

Unalikumbuka kundi la muziki la East Coast Team!?​

Baadhi ya wasanii ambao walikuwa
wanaunda kundi hilo ni Ambwene Yesaya‘AY’, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’, mwanadada Judith Wambura ‘Jide’ na GK.

 
Haya makindi yalikua yanawakilisha matabaka Fulani katika jamii zetu. Kwa mfano TMK ilikua inawakilisha tabaka la vijana wa uswahilini na hii iliwapa nguvu kubwa sana ya kupatia mashabiki wengi kwenye show zao ndani ya Dar na nje ya Dar.

Pia East Coast ni kundi lililokua linawakilisha Vijana wa Ushuani yaani vijana flani hivi Maisha mzuri mabishoo flani hivi, hii ilipelekea kupata wafuasi flani wa Maisha kama hayo.
 
P Funk mwenyewe atakuambia Bongo records nyimbo nyingi zilizotamba ni kutoka ukanda huo TMK
 
Ata kwaakili yakwaida tu bado utagundua east coast ilikua nawatu smart sana tofaut na TMk ila kwasababu maisha yakitz yaliegemea kwenye uswahili sana ndio maana Tmk walibamba
 
2005 kama huna tshirt ya ECT (East Coast Team) au Kiraka...basi wewe sio mjanja...East coast kulikua kuna jamaa anaitwa Stanboy now yupo UK,unamkumbuka??Snare, Buffy G,
 
Binafsi yangu mimi niliwakubali wote sawa sawa maana nyimbo zao zilikua nzuri, uandishi kwa ujumla ulikuwa muziki mzuri na ulichangamsha sana Game ya Bongo.
 
Back
Top Bottom