Mainstream media bado zina nguvu sana duniani kote,ndio maana utakuta msanii anatangaza kwenye mitandao kwamba wimbo wake umeshika chati namba mojakwa wiki kadhaa katika radio au tv maarufu au za nchi fulani duniani ,hii yote ni kuonyesha appreciation ya namna gani mainstream media ilivyo na nguvu,mitandao ni kweli ina saidia wasanii lakini bado haijakuwa na nguvu kubwa ya kuupeleka muziki au brudani kwa wateja (wasikilizaji na watazamaji) kama zilivyo radio na Tv,mara nyingi nitandao inatumika kama nyenzo saidizi kwa mainstream media hasa katika suala la mauzo.
Japo sijasikia hiyo intavyuu ya Diamond lakini sidhani kama anaweza kuwa mpumbavu kiasi hicho cha kudharau mainstream media ambazo ndizo kwa kiasi kikubwa ndizo zilizomfikisha hapo alipo kisanaa,mimi nadhani hakueleweka na kama alikuwa anamaanisha kama wanavyosema hao jamaa watangazaji basi atakuwa hana shukrani na anavimba kichwa kitu ambacho si kizuri kwa msanii yeyote yule,kwanza wanaosikiliza na kutazama radio na tv ni wengi kuliko wanaoingia mitandaoni.