EATV na EA Radio wasitisha kucheza nyimbo za Wasanii wa WCB

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Tangu kutolewa kwa tuzo za EATV awards vituo vya eatv na ea radio vimekuwa havipigi nyimbo za msanii wowote wa WCB wala kutoa habari zao

Tetesi zinasema kitendo cha WCB kutoshiriki tuzo hizo hakijawafurahisha Eatv na kuamua kusitisha huduma hiyo
Ikumbukwe Eatv awards ilikuwa ili kushiriki msanii lazima ajaze form za kujipendekeza kwenye vipengele kitendo kilichofanya wasanii wengi wasishiriki.

Ikumbukwe mwaka 2015 Eatv na radio walikuwa hawapigi nyimbo za Diamond platnumz mpaka mapema mwaka huu mwezi wa 4 waliposuluhisha pande zote mbili.
1481895963837.jpg
 
Zile tuzo mi nilijua tu kuna mtu ana tafutwa, na walio kuwa wakimtafuta walijua kwa njia ile wata mpata tuu.
Japo ni shabiki mkubwa wa EA TV na Radio, kwa hilo naona wamefanya blunder kama ni kweli, kwani wao yaan hawawezi kumrudisha diamond nyuma hata kidogo kwa figisu zao, waendelee kumtisha huyo huyo Ali Kiba.
 
Kama kweli hawapigi nyimbo zao kwa kigezo cha kutoshiriki hizo tuzo basi management ya EATV ni mambayumbayu.

Wao wenyewe walitoa option ya Msanii kujipendekeza,basi wakubali kuwa hawakua tayari kujioendekeza.

Kuna tuzo pia za Movie,pia akina Wolper,Wema Sepetu na Wasanii wengine wa tasnia ya Filamu,je hii itawagusa nao kiasi kwamba filamu zao hazitachezwa kwa sababu ya Kutojipendekeza?
 
Waendelee kupiga za Weusi na hao wengine wanao piga ,

Kwenda kuchukua fomu kujaza unapotaka ushindanishwe alafu uambatanishe na kazi ulizo fanya karibuni? wakati huo huo n msaanii bora wa Africa... hahaha, [HASHTAG]#Udhalilishaji[/HASHTAG]

Watazipiga tu watakapoona inafaa kufanya hivyo
 
Binafsi niliona ni utoto kwa kituo kikubwa kama hicho kuwa na think tank kama wakina sallama zaidi ya kujua kutangaza hawajujui chochote kuhusu management ya mziki. Huwezi ukawambia wasanii wajipendekeze kwa ajili ya tuzo..that's was insanity.. Siyo haki kabsa.. !! Ni upuuzi sana style yao hiyo. Kwann msiwambie watu wapige kura wawapendeke wasanii.

Tatzo nchi hii media kuwa na nguvu zaidi ya wasanii..naombea E TV ya majizo isiyo na mambo ya kipuuzi hivi.
Natangaza na mm tokea Leo siangalii tena TV yenu kwanza Hamna kipind cha maana. Hii ngozi yetu imelaaniwa.
 
Tangu kutolewa kwa tuzo za EATV awards vituo vya eatv na ea radio vimekuwa havipigi nyimbo za msanii wowote wa WCB wala kutoa habari zao
Tetesi zinasema kitendo cha WCB kutoshiriki tuzo hizo hakijawafurahisha Eatv na kuamua kusitisha huduma hiyo
Ikumbukwe Eatv awards ilikuwa ili kushiriki msanii lazima ajaze form za kujipendekeza kwenye vipengele kitendo kilichofanya wasanii wengi wasishiriki.
Ikumbukwe mwaka 2015 Eatv na radio walikuwa hawapigi nyimbo za Diamond platnumz mpaka mapema mwaka huu mwezi wa 4 waliposuluhisha pande zote mbili.
View attachment 446963
Bongo hakuna zuri hata cku moja. Cdhani kama hizi habari ni za ukweli
 
Nilijua tu kuna wasanii wao wanapenda kujikomba sana kwa radio
Ndiomana tuzo zote zilikua na wasanii wasiozidi wa 8 na haohao ndio walikua wanajirudi katika kategori
Upuuzi wa media zetu ndio hizo
 
Tangu kutolewa kwa tuzo za EATV awards vituo vya eatv na ea radio vimekuwa havipigi nyimbo za msanii wowote wa WCB wala kutoa habari zao
Tetesi zinasema kitendo cha WCB kutoshiriki tuzo hizo hakijawafurahisha Eatv na kuamua kusitisha huduma hiyo
Ikumbukwe Eatv awards ilikuwa ili kushiriki msanii lazima ajaze form za kujipendekeza kwenye vipengele kitendo kilichofanya wasanii wengi wasishiriki.
Ikumbukwe mwaka 2015 Eatv na radio walikuwa hawapigi nyimbo za Diamond platnumz mpaka mapema mwaka huu mwezi wa 4 waliposuluhisha pande zote mbili.
View attachment 446963
Mmm sidhani kama ni kweli....juzi tuu nimeona nyimbo ya diamond salome kwenye zote kuntu ...na kama ni kweli hiyo haiwezi kuwa sababu ....
 
Binafsi niliona ni utoto kwa kituo kikubwa kama hicho kuwa na think tank kama wakina sallama zaidi ya kujua kutangaza hawajujui chochote kuhusu management ya mziki. Huwezi ukawambia wasanii wajipendekeze kwa ajili ya tuzo..that's was insanity.. Siyo haki kabsa.. !! Ni upuuzi sana style yao hiyo. Kwann msiwambie watu wapige kura wawapendeke wasanii.

Tatzo nchi hii media kuwa na nguvu zaidi ya wasanii..naombea E TV ya majizo isiyo na mambo ya kipuuzi hivi.
Natangaza na mm tokea Leo siangalii tena TV yenu kwanza Hamna kipind cha maana. Hii ngozi yetu imelaaniwa.

Ni kweli hiyo eatv haina kipindi cha maana?
Hivi E-FM wanacheza nyimbo za Man-fongo?
 
Back
Top Bottom