Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Pamoja na kukalia kiti cha uraisi kwa kipindi kifupi, marehemu Ebrahim Raisi wa Iran aliyekufa kwa ajali ya helkopta atakumbukwa kama mmoja wa viongozi mashujaa wa nchi hiyo.
Katika kipindi chake vitu vingi visivyotarajiwa kufanywa na nchi ambayo haijatajwa kama nchi iliyoendelea kama zile za bara la Ulaya na Marekani yaliweza kutokea. Miongoni mwao kwa kumbukumbu zangu ni haya yafuatayo.
Aliweza kuikoa nchi ya Venezuala kutokana na shida kubwa ya mafuta japokuwa ni nchi mzalishaji mkubwa wa bidhaa hiyo duniani.
Shida ya Venezuela ni kutokana na kuwekewa vikwazo na Marekani kiasi kwamba viwanda vyote vya uchakataji wa bidhaa hiyo vilikuwa kama magofu kutokana na ukosefu wa vipuri.
Wakati wa uongozi wa Ebrahim raisi alifanikisha malengo ya mtangulizi wake kwa kuipelelekea mafuta ya msaada nchi hiyo sambamba na vipuri vya kufufua viwanda vyake. Meli zilipoleka misaada hiyo zilipitia ugumu wa hali ya juu katika safari,lakini hata hivyo kwa kutumia mbinu tofauti hatimae ziliweza kufikisha mafuta na vipuri.
Katika kipindi hicho hicho cha Ebrahim ilikuwa ni kisa mkasa.Meli ya Iran ikizuiwa kwa sababu yoyote ile na wao wanazuia meli ya taifa lililongoza kwenye utekaji wa meli zao.
Kipindi hicho kilishuhudia nchi hiyo ikiuza vifaa vya kivita vilivyotengenezwa Iran kwa mataifa mengine na hasa taifa kubwa la Urusi katika kuiadhibu Ukraine. Ukali wa droni za Iran aina ya shaheed zilililala mikiwa mno na Ukraine kuonesha kuwa zilifanya kazi zilizokusudiwa. Hilo halikuwa kufikiriwa kutoka kwa nchi kama Iran.
Kubwa kuliko yote ni ujasiri wa kuipiga Israel kwa makombora ya masafa marefu ambayo yaliweza kutua kwenye uwanja mkubwa wa kijeshi wa Israel na maeneo mengine na kuleta madhara na muadhara kwa nchi hiyo inayoogopewa na mataifa karibu yote ya kiarabu.
Ujasiri wa kuipiga Israel ulikuja baada ya Israel kuyashambulia na kuyaharibu majengo ya ubalozi wa Iran nchini Syria