Ebrahim Raisi, mchinjaji wa Tehran(The Butcher of Tehran) atakayekumbukwa kwa madhila mengi na makubwa

Haha sasa mkeo huko peponi atakuwa moja ya wale bikra alioahidi allah tabarka
 
Netanyahu anatakiwa amsmoke Grand Ayatolah mwenyewe huyo ndio Mzizi wa fitina.
 
Si bora huyo ni watu 8000 tu tena wairani wenzake ,vipi akina Baden, Bush,na akina Netanyau ambao wameshababisha madhira kwa mamilioni ya watu kote duniani mbona hujawahi huwaanzishia uzi?
Ewaaaa leo umeongea point
 
X majuzi tu katoka Kenya jaman Ruth embu elekea huko maramoja kama alitoa ahadi ndio imeisha hiòo
 
Kwa sababu waliofia mikononi mwake hawakufia vitani, ni raia wanaokamatwa mitaani tu kwa mambo ya kisiasa na yanayoitwa ya kimaadili kisha wananyongwa au kupigwa risasi.
Kwahiyo ukipigwa Bomu ndani ya nyumba yako kama kule Gaza ukiwa na mke na watoto wako utakuwa vitani?

Waandishi wa habari wapo vitani? Madktari wanaopigwa mabomu wakiwa hospitali wapo vitani?

Raia 500,000 wa Iraq na Pakitsani wakiwemo Watoto wapo vitani?

Wanaopotea kutokana na watu wasiojulikana wapo vitani?
 
Kwa hiyo haya yote yanahalalisha nini hasa kwa Mchinjaji wa Tehran??
 
Kwa hiyo haya yote yanahalalisha nini hasa kwa Mchinjaji wa Tehran??
my point is simple, kuna 'stereo type' inayosababishwa na western media katika ku manipulate akili za watu hasa third world ambako watu hawana access na information za kutosha wala hawana muda wa kujisomea magazeti au vitabu. Wananua bundle na kuangalia headlines za BBC na CNN tayari wanavamia keyboard

Ku-ua ni ku ua tu hakuna kua kuzuri au kubaya, midhali unaua wewe ni mhalifu tu uwe Mwarabu, Mzungu, Mchina au Mwafrika etc. Watu wetu wetu wafike mahali watumie akili na si kuendeshwa na vyombo vya habari vya magharibi.

Jana pekee jengo limepigwa na kuua Wapalestina 106! nani anaongelea hilo.
Wiki nzima tangu Israel ianze mashambulizi Rafah watu 800 wamekufa! nani anaongelea hilo! Hakuna

Ni kwasababu media za west hazionyeshi , kinachoonyeshwa ni kuhusu Rahisi Ebrahimu alivyokufa na ubaya wake

Huwezi kusema Rahisi Ebrahim kaua watu wengi kuliko 35,000 waliouawa katika miezi 6 ya vita Gaza na Israel.

Sihalalishi mauaji ninachokusudia kukuonyesha ni jinsi gani unavyoshindwa kutetea hoja kwasababu ya kumeza tu bila kufikiri.

Marekani ilitumia mwaka mzima kuzungumzia Mahsa Amini wa Iran aliyeuawa na Polisi.
Kwamba kuna ukiukwaji wa haki za Binadamu.

Wamareakani wenye uchungu sana na mtu mmoja wa Iran hawana uchungu na Watu waliopigwa risasa na Polisi wa Marekani wengi kuliko mtu mmoja. Chicago mtaa mmoja unazika watu 7 kila, haya hamuyaoni , mnaona ya Rahisi wa Iran

Israel inazuia chakula kisiingie Gaza watu wafe kwa njaa , hamuoni mnaona ya Ebrahim Rahis kwasababu ndivyo media zime tune akili zenu na hamuwezi kuangalia left or right.

Kwanini Vijana wa Tanzania hawana uwezo wa kufkikiri kama Wakenya au Zimbabwe. Huko kuna mijadala isiyoangalia upuuzi wa dini au rangi! watu wanachambua, sasa hapa kwetu maswali mawili mtu flat!

Hapa nimesoma watu wanazungumzia magaidi. Ukiwauliza Gaidi ni nani, nani anatoa hadhi ya ugaidi, nani anaondoa hadhi hiyo hawana jibu. Ni kwasababu wameaminishwa hivyo na media na hawana muda wa kutafuta info zingine

JokaKuu
 
Yoda kwa makadirio au taarifa ni watu kiasi gani waliuawa na E.Raisi pale Tehran?

Nguruvi: Nadhani hujui chochote kuhusu historia ya Iran.....Rudia tena uone yule zimwi (Ayatolah Khomeni) Aliporudi 1979 alivyowafanyia Wairan ambao aliwaona ni tishio. Nashangaa hata Waislamu wa Tanzania ambao wengi ni Sunni, hawajui alichowanyia Sunni.....Mkuu Nguruvi3....Wewe ni mweledi......hata kama una mapenzi na hawa jamaa, huyu Marehemu kazi zake za mwanzo ilikuwa ni kutoka hukumu za Kiimla.......!

Kwa kifupi afadhali hata Hamas unajua anataka nini....na adui ni Wayahudi......Huyu Marehemu kahusika kuua Wairan wengi mno.....Wenye Misimamo ya Kijamaa, Wenye mitazamo ya Kiislamu tofauti na wao, nadhani dini ya Bahai waliifutilia mbali.....!

Hiyo Theocracy ina damu nyingi mno!
 
Najua historia ya Iran kuanzia enzi kabla ya Shah. Wakati wote wa Shah hadi akina Shakur Bahtia, Musavi n.k. nawafahamu. Ayatollah Khomeni kabla hajarudi kutoka Ufaransa nilimjua

Sina mapenzi na upande wowote, ninachowaeleza hapa ni kwamba kuna unafiki, tumieni akili zenu.

Unasema '' Marehemu kaua wa Iran wengi sana '' nimeuliza ni takribani wangapi? Mwenzako kasema ni 30,000 , nikasema OK . Je wale wanaokufa Ghaza nani anawasemea? Mbona juzi jengo limeremeka wakauawa wanawake na watoto 106 on spot hatuwajawasiki ninyi watetezi wa haki za binadamu!

Unaposema kaua wa Iran wengi, nipe namba halafu nitakupa namba zingine dunia kutoka nchi za mgharibi zenyewe

Wamarekani wenyewe wanasema hivi, mabomu yanayotumika Ghaza hawawezi kuyatumia kwasababu hayana precision. Wamarekani wenyewe wanakubali kuna mbinu za kuzuia chakula ili watoto na Raia wengine wasio na hati wafe kwa njaa! hayo hamyaoni kama ni uhalifu , mnachoona ni cha Rais Rahisi tena akifanya nchi kwake.

Nikuulize swali lingine, kuna tatizo gani Rais wa Iran akiua watu wa Iran? Tuanzie hapa
 

Mkuu kila mtu anatumia akili zake! na kila mtu anaweza kuwa na narrative yake! Kwanza unaposema nani anawasemea wanaokufa Gaza, mbona wengi tu! Waliomeza narrative ya Wapelestina tunaowaona kila mahali, Ulaya, Marekani, Africa na mpaka ambayo wamekwenda Mahakama za kimataifa.

Vifo vya Gaza, Hamas wenyewe wanasema ni gharama ambayo inayolipwa katika mapambano yao! Unaweza kuichukia Hamas, lakini lazima uipe credit kwa kuweka agenda zake wazi, kuanzia kwenye Charter yao, na gharama ambayo wameamua kuilipa katika harakati zao.

Huwa sielewi kuona baadhi ya watu ambao wanaumizwa na idadi ya vifo Gaza! Wakati viongozi wa Hamas mara nyingi wamesema hiyo ni gharama ya lazima kulipa kwa kile wanachokidai! Na hutoa mfano wa Mapambano ya kudai uhuru Algeria! Na hata Wapelestina wenyewe (wengi) wameandaliwa kiimani kukubali vifo hivyo! Na Hamas imeonyesha kabisa kwa vitendo, kwa kujenga Mahandaki kwa ajili ya wapiganaji wake, wala sio kwa wanawake wao na watoto!

Narudia tena, nashangaa mno kuona mtu kama wewe unasema nani atawasemea wanaokufa Gaza! Wewe una huruma kuliko viongozi wa Hamas! Wao wanajua wanachokifanya! Kwangu mimi Hamas is a death cult!

Anyway, nitaendelea baadaye kuhusu huyu chinja chinja wa Iran, na kama unakiri unaijua historia, nitashangaa kama umeshindwa kuona kilichofanyika na Khomeni, na kundi lake, na huyu Marehemu kuanzia ujana wake walivyowamaliza Wairan kujenga huo utawala wa "Kimungu"
 
Ahaa hapo umemalizia na '' utawa wa Kimungu'' . Iran ni Taifa kama mengine, kama wanachotaka ni hicho kuna tatizo gani? Mbona hatuongelei kinachoendelea USA au UK! kuhusu tanaduni zao na mambo yao hata tusiyokubaliana nayo. Wenye dhima ya kupigania Iran ni Wa Iran, siyo Wamarekani au Wewe !

Unajua Shah wa Iran aliwekwa na nani? Unajua kwanini yalitokea ''mapinduzi' ya 1978 kumrudisha Khomeni?
Unajua watu wangapi walikufa kabla ya Shah hajatoroka kupitia tunnel? Unajua silaha za kuua Wanafunzi wa Iran waliompinga Shah zilitoka wapi?

Fikiria hivi, Marekani na Wewe mumeguswa sana na kifo cha Masah Amini yule Mwanaharakati wa Iran aliyefia mikononi mwa Polisi. Marekani hiyo hiyo haina uchungu na watu zaidi ya 5,000 waliouawa Haiti!

Nikuulize tena kwanini una uchungu sana na Vifo vilivyotokana na 'Rahisi' wa Iran?
Hili ni swali muhimu katika majadiliano.
 
Nawaza kwa Nini wasinunue chopa Urusi maana tech ya ndege iko juu sana Urusi au China
Au helicopter ziko US pekee na washirika wake!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…