Kwa hiyo haya yote yanahalalisha nini hasa kwa Mchinjaji wa Tehran??
my point is simple, kuna 'stereo type' inayosababishwa na western media katika ku manipulate akili za watu hasa third world ambako watu hawana access na information za kutosha wala hawana muda wa kujisomea magazeti au vitabu. Wananua bundle na kuangalia headlines za BBC na CNN tayari wanavamia keyboard
Ku-ua ni ku ua tu hakuna kua kuzuri au kubaya, midhali unaua wewe ni mhalifu tu uwe Mwarabu, Mzungu, Mchina au Mwafrika etc. Watu wetu wetu wafike mahali watumie akili na si kuendeshwa na vyombo vya habari vya magharibi.
Jana pekee jengo limepigwa na kuua Wapalestina 106! nani anaongelea hilo.
Wiki nzima tangu Israel ianze mashambulizi Rafah watu 800 wamekufa! nani anaongelea hilo! Hakuna
Ni kwasababu media za west hazionyeshi , kinachoonyeshwa ni kuhusu Rahisi Ebrahimu alivyokufa na ubaya wake
Huwezi kusema Rahisi Ebrahim kaua watu wengi kuliko 35,000 waliouawa katika miezi 6 ya vita Gaza na Israel.
Sihalalishi mauaji ninachokusudia kukuonyesha ni jinsi gani unavyoshindwa kutetea hoja kwasababu ya kumeza tu bila kufikiri.
Marekani ilitumia mwaka mzima kuzungumzia Mahsa Amini wa Iran aliyeuawa na Polisi.
Kwamba kuna ukiukwaji wa haki za Binadamu.
Wamareakani wenye uchungu sana na mtu mmoja wa Iran hawana uchungu na Watu waliopigwa risasa na Polisi wa Marekani wengi kuliko mtu mmoja. Chicago mtaa mmoja unazika watu 7 kila, haya hamuyaoni , mnaona ya Rahisi wa Iran
Israel inazuia chakula kisiingie Gaza watu wafe kwa njaa , hamuoni mnaona ya Ebrahim Rahis kwasababu ndivyo media zime tune akili zenu na hamuwezi kuangalia left or right.
Kwanini Vijana wa Tanzania hawana uwezo wa kufkikiri kama Wakenya au Zimbabwe. Huko kuna mijadala isiyoangalia upuuzi wa dini au rangi! watu wanachambua, sasa hapa kwetu maswali mawili mtu flat!
Hapa nimesoma watu wanazungumzia magaidi. Ukiwauliza Gaidi ni nani, nani anatoa hadhi ya ugaidi, nani anaondoa hadhi hiyo hawana jibu. Ni kwasababu wameaminishwa hivyo na media na hawana muda wa kutafuta info zingine
JokaKuu