Ebu leo Tukumbushane kuhusu maandiko ya Mungu

Ebu leo Tukumbushane kuhusu maandiko ya Mungu

Qur-an
SURA YA 4(Sura ya haki za wanawake)
36. Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na mpita njia, na walio milikiwa na mikono yenu ya kulia( yaai familia na watumishi wa ndani). Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wenye majivuno,
 
Naomba andiko kutoka kwenye bible or quruan unalolipenda na kulikumbuka mda wote
me naanza na
Mithali 1:10
Mwanangu wenye dhambi wakikushawishi wewe usikubali
maandiko yanasemaje kuhusu Corona?
 
ni andiko la kwanza nililolisoma ninavoanza kusoma biblia,ingawa lilikua kwa kingereza and nikaja kuelewa tafsiri baada ya mda kupita.

Naomba andiko kutoka kwenye bible or quruan unalolipenda na kulikumbuka mda wote
me naanza na
Mithali 1:10
Mwanangu wenye dhambi wakikushawishi wewe usikubali
 
1 yohana2:15>17
15 Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.

16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.

17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.
 
Isaya 41 : 10,
Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.

Cc; tokenring
 
Mhubiri7: 9
Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.
 
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِنَّمَا ٱلۡخَمۡرُ وَٱلۡمَيۡسِرُ وَٱلۡأَنصَابُ وَٱلۡأَزۡلَٰمُ رِجۡسٞ مِّنۡ عَمَلِ ٱلشَّيۡطَٰنِ فَٱجۡتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ

(Ali Muhsin Al-Barwani)
Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.

-Sura Al-Ma'idah, Ayah 90
 
Back
Top Bottom