Yofav
JF-Expert Member
- Mar 12, 2021
- 4,236
- 7,583
Naishi Hapa Dar mtaa fulani, Nina kama mwaka hivi sasa, Na mahali nilipopanga ni pana mazingira mzuri kiasi chake maana mwenye nyumba wetu ni mtu pia anaependa mali zake hivyo basi hayupo nyuma kutuhakikishia tunapata yale mahitaji ya msingi Kama maji kwa haraka zaidi na marekebisho ya dharura.
So, issue ipo hivi mtaro unaotumika kupitisha maji machafu katika eneo letu (namaanisha huu mtaro upo kwa nje ya geti ambapo umepakana na barabara) Ni mtaro unaotumika na watu wengi ikiwemo hata majirani zetu, So ni mtaro ambao unasaidi sana hapa kitaa maana unayatoa maji kuyaelekeza ulipo mto wa maji.
Mwenye nyumba wetu aliutengeneza mtaro na kuuweka wa kisasa zaidi pale yalipo mazingira yetu lakini kule maji yanapoelekea umbali kama hatua 100 hivi ni eneo wanaloishi watu wengine ila ni kidizain fulani kama hapajatengenezwa kisasa bali pako hovyo jambo linalofanya maji yale kushindwa ku-flow vizuri na kutuama.
Sasa jambo ambalo limenishangaza ambalo ninahitaji tulijadili hapa ni kwamba hii issue imefika serikalini according to mwenye nyumba so inavyodaiwa viongozi wa mtaa wamekaa kikao so sisi watu wote ambao tunahusika kutumia ule mtaro wanapaswa kuchanga pesa ule mtaro utengenezwe kisasa zaidi.
Sikupinga kupata taarifa hiyo maana jambo la kimaendeleo ni vizuri kushiirikiana ila taabu imekuwa kwenye gharama ambazo tunapaswa kuchangia, According to wao ni kwamba tunaotumia huo mtaro tupo 82 so ili tupate budget ya kuutengeneza huo mtaro basi kila mmpangaji anatakiwa kutoa sh.36,000/=, Jambo hili limeleta utata kwa kuwa baadhi ya wapangaji wanahoji kwamba wao wanapita tuu na walipanga nyumba na kufuata maelekezo ya mwenye nyumba wapi wamwage maji taka, So jukumu la masuala ya maji yataelekea wapi au mtaro una shida gani ni issue ambayo inamuhisisha mjenzi (mwenye nyumba)
Then kingine ni hiyo gharama ambayo inapaswa kuchangiwa, Imagine 36,000 kwa kila mpangaji kweli!!? Na hali hii?
Ebu wataalamu mnijuze kwa issue kama hii imekaaje na mimi nipate kuelewa, Hili jukumu ni la mpangaji au mwenye nyumba maana mwenye nyumba anasema yeye sio mmwagaji maji wanamwaga wapangaji, Na mpangaji anahoji kwamba inawezekanaje mjenzi ajenge nyumba asitengeneze mazingira yanayoeleweka ya kumwaga maji ikiwa kama jukumu lake?
Kwa mimi sijataka kupinga suala hili maana ni vizuri kusaidiana hata kama tunapita ila hiyo gharama kiukweli ni kubwa ni heri wangesema hata 10,000/= kwa kila mpangaji.
Uzi umeisha.