Economic hitmen

Aisee hii mada ni very interesting, naona jeshi la watu watatu mnapambana, I'm just curious to see the end of this
 
wewe dada kuna siku niliwahi kukuambia humu upeo wako ni mdogo sana,na kama wewe ni msomi basi ni msomi TAHIRA labda uwe mwanafunzi wa kidato cha 4 au 6 ndo nitakuwa nimekuonea kwa kukuita hivyo.kuna vitu vingine havihitaji unazi wa vyama vya siasa. your more than imbecile.sijasoma comments za wengine kwa chini lakini najua watakuwa pamoja nami kuhusu wewe.
 
Not the matter of cooperating, those guys are evil! Look at China, all those who are found cooperating with economic hitman are sentenced to death, and there is no economic hitman in China.

Hapa sijakuelewa unavyosema not the matter of cooperating ilihali mifumo iliyopo sasa hivi wapo ndani tayari. Labda nikuulize tu, unazijua MNCs zilizofanya exploration ya gas na mafuta huko South? Unawajua real owners (Shareholders) wa kampuni zinavuna Gold kwenye migodi ya Lake Zone? Unajua ilifikaje mpaka Dowans ikawa Symbion na ghalfa akaja Hilary Clinton na baadae Obama akafika pale? Nadhani bado hujajaua opereshion mode ya hawa EHM. Hivyo unavyoona Magufuli hawezi ku cooperate naona hujawatambua hawa jamaa wapo vipi.
 
China is one of the strongest Economies mfano wako ni Invalid. Unataka EHMs waende kui sabotage Marekani?, Ulaya, China, etc wakati wanatoka huko huko???
China walikuwa ni socialist country ambayo ilikuwa na same philosophy na USSR wakati jamaa wanatekeleza policy ya EHM. Hawakuitarget kabisa. Focus yao kubwa Asia ilikuwa kuziteka nchi maskini za South Asia zisiwe influenced na China na USSR kuingia kwenye mfumo wa socialism. Ndo hapo wakaanza kuwaingia Indinesia, ili baadae watanuke ufilipino, Malaysia, Singapore na kwingine.
 
Na pia, China walishakuwa Socialist Country tangu miaka hiyo. US walikuwa hawana namna ya kupenya for idiological reasons na pia patner mkubwa wa China alikuwa USSR ambaye alikuwa hasimu mkuu wa US.
 
Ni kweli kbs, ukitaka kuprove hilo hakuna mji wowote tz ambao wazungu hawapo, ask yourself wanafanya nini
 

Jamaa kafanikiwa kueleza vizuri kuhusu economic hitman ilivyo but mkuu umekuja na kujaza ujinga wa kisiasa..hebu angalia kwa makini hapa..mikataba ya gas na mafuta ilipitishwa kwa haraka bila kujadiliwa kwa umakini na wabunge...hata hiyo mikataba fake ya migodi ya dhahanu na madini mengine mbona jpm hatoi msimamo wake ili ijadiliwe upya?..huoni kwamba economic hitmans tayari yashaiteka nchi..ref..ujio wa rais wa china..na pia mlolongo wa marais wote watatu yaani clinton..bush na obama?jpm hawezi fanya lolote mkuu the knee has been bent!hatuna jinsi!
 
kwanza,nchi za kiafrika ni masikini kwa sababu ya mifumo ya dunia iliyowekwa na USA na allies wake toka miaka ya 70 kwa kutengeneza maksudi matatizo ya kiuchumi kwa kupitia uhaba wa mafuta-nia ni ku control zile nchi zote zilizokuwa allies wa USSR na kwa hili wamefanikisha kwa 1000% kwa kutengeneza mfumo wa kibepari unao wabeba wao kumbuka huwezi kuwa strong kwa kuendelea na mfumo wa mwenzako ( socialism).sote tunajua mgogoro huo ulivyo weka nchi ambazo zilikuwa under USSR kwenye trap-vyombo kama IMF,WB vilipatia hapo nguvu.

kuna njia kuu 3 za kuondokana na hili
1.lazima usiwe tegemezi hasa ktk budget na misaada -ukiwa tegemezi tu lazima uingie kwenye trap:lazima kuhakikisha hamna nakisi ya budget

2.lazima kuwe na viongozi wasio kuwa na tamaa ya madaraka na mali,maana hata wao wanajua viongozi wa kiafrika huu ni mtego wao rahisi kuwakamata.e.g upate mtawala kama nyerere

3.Umoja na mshikamano,na hapa ndipo point kuu. maana unaweza ukawa na hivyo vyote hapo juu namba 3 huna panakuwa sawa na bure.e.g marehemu gadafi vyote 2 alikuwa navyo lakini hamna support kutoka nchi za kiafrika zingine.hii inatokana na viongozi wengi wa nchi kuingia kwenye mtego namba 1&2.

tutaendelea kuwa masikini mpaka siku nchi 3 au 4 zitakapoungana pamoja au bara lote la Afrika-na hili najua haliwezi kutokea maana nia ya mataifa ya magharibi ni kuona siku zote mnatengana.
kama hili litakwama tuna kete 1 kama itafanikiwa benki itakayo anzishwa na wanachama wa BRICS hii itawatoa watu IMF&WB kama watakopesha kwa mashariti nafuu-na hii kitu marekani anaipiga vita balaa ndo maana mpaka sasa utekelezaji wake wauleweki na siku ikifanikiwa hesabu moja kwa moja utawala wa USA kwenye hii dunia umefika kikomo.
 

Huyo Mudawote analeta siasa kwenye mada zisizohiyaji usiasa wowote. Hajui kama Bush ana share kubwa kwenye migodi yetu ya dhahabu...Clinton kaja na hatimaye RICHMOND>DOWANS>SYMBION ikazinduliwa na Obama juzi juzi

Hawa hawa jamaa juzi juzi wame sabotage HEP zetu kule mtera na kidatu ili wauze umeme wao wa Gesi.

We are already in the play.
 
Last edited by a moderator:
Nakukatalia kwa sababu sisi tumedili na wenye mbwa na siyo mbwa. Ndiyo maana nimesema economic hitman ni mfumo usio rasimi. China na US mikataba yao ni minono na inafaidisha nchi yetu. Sema akina lisu na wahuni wengine walitaka wapige hela kupitia hiyo mikataba na akina mengi walitaka share ili wafanye kama walivyozoea shamba la bibi. Nyie subirini muonenchi inavypoga mchaka mchaka
 
Mudawote embu andika vitu relevant basi na siyo hizo cheap politics zako.
 
Last edited by a moderator:
kaka mwaache huyo mwanamke,hajitambui alishindwa nyerere ku dili nao ataweza magufuli.
 
Hizo Western Financial Institutions ndizo tools wanazozitumia sana. Hawa ndio walioshauri nchi yetu ipunguze thamani yake dhidi ya Dola, pia walishauri serikali kufanya Redundance ya wafanyakazi wengi serikalini na wakashauri ubinafsishaji na soko huru. Waka infiltrate kwenye mfumo wetu wa kiuchumi hadi kupelekea kufa kwa NBC. Hata makampuni makubwa ya West yanayowekeza kwenye miradi mikubwa mikubwa huchota pesa huko kiulaini kabisa.

BRICS Bank (sina hakika na jina lake Rasmi) waliizundua kwa mtaji mnono sana sikumbuki ni dola Bilioni ngapi lakini huenda 2018 ikaanza kazi Rasmi na hii yaweza kuwa afadhali kwa mataifa machanga na Maskin kama TZ
 
anadhani clinton na Obama walikuaja kuangalia utamaduni na kuzindua obama drive!
 

Tatizo mkuu ni kwamba..acha siasa pembeni..tuzame kichumi..hizo kampuni kubwa zinazokuja huku na kupewa tenda hizo ndo huamua wamweke nani madarakani..ref..kwanini unadhani Obama ameshindwa kupiga marufuku umiliki wa silaha binafsi ingawa watu wanauwawa kila siku USA?kile chama cha silaha na masuppliers wa hizo silaha wananguvu kuliko Obama!..hapo mbwa wananguvu kuliko mwenye mbwa..hiyo slogan yako ya unaongea na mwenye mbwa ni applicable huku kwetu tu mkuu!wale jamaa wanajua kufanya lobbying mbaya kabisa!upande wa china..ujue kuwa ndo inatoka kwenye ujamaa na kukumbatia ubepari..they're hungry for raw materials and tenders.they're ready to do anything ili wazipate..wamewajengea makao makuu ya AU..pia kila nchi ya kiafrica imejengewa mijengo mikubwa bure kabisa eg Tz,malawi,msumbiji,zambia etc hiyo yote ni kubembeleza raw materials na tenda!hata wizi wa nyara za serikali..tusidanganyane..hakuna mikataba minono mkuu.tutaambulia mashimo ya migodi tu na hawatayafukia!so sad!
 
Mudawote embu andika vitu relevant basi na siyo hizo cheap politics zako.
Tatizo lenu nyie mmekalilishwa vibaya. Kama wewe umewahi kuishi nje ya nchi utanielewa, ila kama umekulia bongo tu basi utakuwa hunielewi. Mimi ninachomaanisha hapa ni hivi nchi ikiwa na umoja, na kiongozi/viongozi waadilifu economic hitman hawawezi kuharibu uchumi hata kidogo. Kinachotokea kt ya hizo financial institutions ni fair game tu. Hao economic hitman ni informal bodies that operate under the umbrella of those said financial institutions, lakini kikubwa lazima pawe na weakness ktk serikali, yaani serikali ijae wapiga dili kama akina lowasa. Mbona Rwanda wameweza? Mbona China wameweza? Mbona Ethiopia hao wameweza (tena kuongezea kuna jamaa zangu waethipia wao ukileta uanaharakati kama wa chadema wanakutupa mabwemapande), mbona wajapan wameweza? Hiyo mifano yenu ya amerika ya kusini haifanani na mazingira tuliyonayo kwa sasa, labda kama rais angekuwa lowasa hapo ningekubaliana na ninyi. Nchi nyingi za amerika ya kusini zinaongozwa na magenenge kama lile la lowasa (mfano mdogo tu, nina jamaa yangu ni mmexico anasema rais aliyepo sasa kaingizwa na watu wa madawa, na mpaka kipindi hiki serikali yake inakshfa kibao, na wao wanaendelea kulainisha mioyo ya watu kwa kuwapatia zawadi kam tv wananchi masikini, na mbinu aliyoingia nayo madarakani iko sawa kabisa na mbinu za lowasa alizotumia. In short mnahitaji kuuvaa utanzania ndiyo mtanielewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…