Ecuador: Waliofariki baada ya kutokea vurugu ndani ya magereza wafikia 27

Ecuador: Waliofariki baada ya kutokea vurugu ndani ya magereza wafikia 27

Sam Gidori

Senior Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
165
Reaction score
417
Idadi ya wafungwa waliofariki baada ya kutokea vurugu ndani ya gereza magereza mawili nchini Ecuador imefikia watu 27 huku serikali ya nchi hiyo ya pwani ya Magharibi mwa Amerika Kusini ikilazimika kutangaza hali ya hatari.

Rais wa Nchi hiyo, Guillermo Lasso ameagiza kutumia kila linalowezekana kurudisha hali ya usalama baada ya kutokea vurugu ndani ya magereza mawili siku ya Jumatano.

Mamlaka zimesema kuwa watu wengine 57 wamejeruhiwa, wakiwamo polisi wanane ambapo mmoja wao alibakwa. Mfungwa mmoja alinyongwa hadi kufa. Wafungwa wengine 86 waliotoroka wamekamatwa, lakini idadi ya wafungwa waliotoroka haijawekwa wazi.

Visa vya vurugu katika magereza ya Ecuador si vigeni kutokea; mwezi Februari mwaka huu, vurugu kati ya makundi hasimu ndani ya Gereza Kuu la nchi hiyo vilipelekea vifo vya wafungwa 79 ndani ya siku moja.

Magereza 60 ya Ecuador yana uwezo wa kuwahudumia wafungwa 29,000 lakini kuna idadi kubwa ya wafungwa kuliko inayoweza kuhudumiwa na mfumo. Mwaka 2020, wafungwa 103 walifariki kutokana na matukio ya vurugu magerezani.

Chanzo: Al Jazeera

1627110768039.png
 
Ni hatari aisee kama hawawezi kumiliki wafungwa wote hao kwann wanazalimisha kuwafunga wapendelee vifungo vya nje km uwezo mdogo
 
Hayo magereza ya huko hawana askari wa KMGM...?...🤣🤣....

Ghasia kwenye magereza huko ni kawaida sababu ya magenge ya wauza unga.
 
Back
Top Bottom